Dar es salaam: Uzuri uliojificha

greater than

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
886
1,383
Arusha,Zanzibar,Kilimanjaro,Mara na Mbeya ni moja kati ya sehemu ambazo zimekuwa ukipata sifa lukuki juu ya uzuri wa maeneo ndani ya mikoa hiyo.

Uzi huu ni maalum kwa ajili ya kuonesha uzuri wa Dar,Jiji ambalo mamillion ya watu pamekuwa nyumbani....Kuna maeneo mengi mazuri na vivutio vingi ndani ya mkoa huu ambavyo wengi hawavijui tu.
Tutaanza kwa kuangazia Vivutio vilivyopo Wilaya ya Kinondoni.

MBEZI BEACH : I
Fukwe za Mbezi,
Kata : Kawe
Wilaya : Kinondoni
Utafaidi:
  • Kuogelea kwenye fukwe na swimming pool
  • Upepo mzuri wa Fukwe
  • Chakula kizuri na Vinywaji
  • Michezo ya kwenye maji
  • Kuendesha boti ndogo
Eneo lenye uzuri wa kipekee ambalo lina mchanganyiko wa Mazingira ya asili pamoja na yale ya Kujengwa na binadamu.
  • Mazingira hayo ya asili ni ufuko wenye mchanga mweupe,Uoto wa mikoko pamoja Bahari.
  • Mazingira ya Kujengwa ni Hoteli kubwa zilizopo maeneo hayo pamoja na sehemu za michezo ya kuogelea.
  • Hotel:Jangwani,Landmark,White Sands
  • Water world

95a5570c-city-34738-16567f2e874.jpg
Hii ni picha iliyopigwa kwa juu​

images (5).jpeg

images (4).jpeg

unafikaje :
Panda gari/bajaji/bodaboda hadi ufike kituo cha basi cha Mbezi Afrikana..ulizia wenyeji Fukwe ya Africana ilipo

Gharama : Nauli kutokea Africana,haizidi 1,000 kwa Bajaj
Kwa huduma za Hotel,Migahawa uwe na takribani 20,000 tsh

Usalama : 90 %

wajuze wenzio
 
PORI LA AKIBA LA PANDE : II
20240416_143439.jpg
Kata: Mabwe Pande
Wilaya : Kinondoni
Historia : Ndiyo pori peke ndani ya mkoa wa Dar es Salaam,lilipata hadhi ya kuwa pori la akiba 1952
Utafaidi :
  • Utumbeze kwenye msitu wa Asili
  • Picnics
  • Kujionea ndege hadimu
  • Kuendesha baiskeli katika pori
  • Kuona wanyama kama Ngedele,nyani,Galagos/Bushbaby,Sungura,Nguchiro,Nguruwe pori,chatu na nyooka wengine.
images-108.jpeg

Unaweka makazi japo kwa masaa

images-107.jpeg

Dar yenye Ukaribu na misitu

images-105.jpeg

Hii siyo Iringa au Morogoro

images-106.jpeg

eneo tulivu
20240416_143439.jpg



Unafikaje :
  • Mbezi stendi, Unapanda gari za Msakuzi,shuka mwisho wa gari...
  • Bunju B, barabara ya vumbi kwenda Mbezi: weka google map, itakufikisha
Gharama :
  • Nauli ...2,000 kwenda na 2,000 kurudi,ukitokea Mbezi.
  • Kiingilio ....Wakubwa 11,000 na Watoto 8000
Usalama : 100%
Waambie wenzio
 
MAGOFU YA MJI WA KALE WA KUNDUCHI : III
Kata : Kunduchi
Wilaya : Kinondoni
Historia: Haya ni magofu ya mji wa kale wa Kunduchi uliokuwepo kuanzia karne ya 10 hadi karne ya 15.
Utafaidi :
  • Masalia ya Msikiti wa kale
  • Utajifunza juu ya historia ya watu wa kale wa mji wa Kunduchi
  • Rekodi ya maneno ya kwanza ya Kiswahili
  • Makaburi ya kale
  • Ushahidi wa biashara kati ya watu wa Kunduchi na uchina...
    img_4_1713377942825.jpg
img_5_1713377976522.jpg

images (7).jpeg

Makaburi ya kale

img_1_1713377884069.jpg

Msikiti wa kale

Unafikaje : Kutokea Makumbusho,Panda gari ya Kwenda Kunduchi...fika Kunduchi mwisho, Panda Boda kufika hapo.

Gharama :
  • Nauli...3,000 kutokea Makumbusho
  • Kiingilio .....7,000
Usalama : 85 %
Waambie wenzio.
 
KISIWA CHA MBUDYA : IV
Kata : Kunduchi
Wilaya: Kinondoni
Taarifa :
  • Ni mojawapo kati ya vilivyopo ndani ya Mkoa wa Dar,Hakina makazi ya watu.​
  • Unaenda na kurudi siku hiyo hiyo...
  • Kipo umbali wa km 3 kutoka Pwani ya Dar es salaa.
  • Ndiyo sehemu pekee duniani yenye kiumbe Metacirolana mbudya.
Utafaidi:
  • Kuogelea kwenye maji safi ya bahari
  • Matembezi kwenye Fukwe safi za mchanga mweupe
  • Picnic
  • Chakula cha viumbe bahari mbalimbali
  • Snorkeling / Kuzamia ndani ya kina kirefu
images (8).jpeg

images (11).jpeg

images (9).jpeg
images (10).jpeg

Unafikaje : Fika hotel ya Jangwani sea Breeze au WhiteSands Kuna huduma ya Boti ya kukupereka huko.
Gharama : 25,000Tsh kwenda na kurudi.

Usalama : 98 %

Waambie wenzio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom