Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili ndio utauvunja Muungano

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,615
113,833
Wanabodi,

Sisi wengine wenu humu, japo tuna vyama toka ndani ya mioyo yetu, CCM kimeoza kwa rushwa na ufisadi, from top to bottom, left, right and center hadi kwenye shina lake!, huku hakuna upinzani wowote wa maana!, watu wanacheza makida makida na wengine hadi kuchezea shilingi chooni!, hivyo, 2015 ni CCM tena!, kilichobaki ni kuikomalia tuu hii hii CCM kwenye hili la Katiba Mpya, CCM angalau ifanye "the right thing!", "at the right time!", a to "do it right!", hivyo kazi yetu sisi tunaotanguliza maslahi ya taifa mbele, imebaki ni kubanana na huyu huyu aliyeshika mpini!, na sii mwingine bali Mheshimiwa sana, Rais wetu Mpendwa, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete!.

Ninachokisema leo, ni kumuomba Rais Jakaya Kikwete, aunusuru huu Muungano wetu adhimu!, yeye kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, he must do the right thing, at the right time, and do it right!, kwa kwanza yeye mwenyewe kukaa chini na kutafakari "what is right!", akiisha ujua ukweli, aamue to do the right thing, muda wewe ni sasa!, kwa kukishauri Chama chake, Cha Mapinduzi, kiachane kabisa na msimamo wake wa kutaka ku force serikali mbili!, kiiukubali ukweli halisi wa rasimu ya Tume ya Warioba iliyopendekeza serikali tatu sio tuu ili kuudumisha muungano bali angalau kuunusuru muungano, na kujinusuru yenyewe!, vinginevyo msimamo wa CCM kupigia chapuo hoja ya serikali mbili, sio tuu kutapelekea huu muungano wetu adhimu, kumvunjikia Rais Jakaya Kikwete mikononi mwake!, bali hata hiyo CCM inatoongoza kwa kupiga makele mule kwenye bunge maalum, nayo pia mtamfia mikononi mwake!.

Wengi wetu kwa sasa wanaliangalia tuu bunge la Maalum kwa macho ya juu juu tuu na kuishia kwenye kufikiria "the end justifies the means!", kwamba kwa vile CCM ndio wako wengi mule Bunge Maalum, wakiamua ni serikali mbili, then katiba mpya ni lazima iwe ya serikali mbili, hivyo katiba hiyo mpya ya serikali mbili, hata ikipigiwa kura ikakataliwa, then tutabakiwa na katiba ya sasa ya serikali mbili, hivyo wana CCM kujifariji kuwa vyovyote itakavyo kuwa, mshindi atakuwa ni CCM!, bila kufikiri over and above beyond katiba mpya kukataliwa Zanzibar, what will happen next?!.


  1. Bunge Maalum lime-open the "Pandora Box" la Muungano, hivyo Wanzanzibari, wakiwemo Wanzanzibari wa CCM Zanzibar na wale makada wao ndani ya kundi la 201, waliomo ndani ya Bunge Maalum, watapiga kura za wazi kuunga mkono serikali mbili, kisha kule Zanzibar watapiga kura za siri kuikataa katiba mpya ya serikali mbili!.
  2. Kwa hali ilivyo, na watu wanavyofunguliwa macho na masikio kuhusu hiki "kiini macho cha muungano!", there is no way!, no way at all, katiba mpya ya CCM ya serikali mbili, inaweza kupata theluthi mbili ya kura za Wanzibari hata kama katiba hiyo iboreshwe vipi!, itakataliwa tuu, kwa sababu hoja ya Warioba kupendekeza serikali 3 ni ili kuwa accomodate Wanzaibari!.
  3. Katiba Mpya ikiisha kataliwa, nchi itaendelea kuongozwa na katiba hii iliyopo yenye kero za muungano, zilizoshindikana kuisha kwa miaka 50 sasa!, hadi kupakwa siagi na jam ya asali kuwa hakuna kero za muungano, kilichopo sio kero bali ni changamoto tuu za muungano!. Katiba hii ikiendelea, itaamsha hasira za Wanzanzibari!.
  4. Uchaguzi Mkuu ujao, Wanzanzibari wote wa CCM na CUF, watakuwa na "hasira na CCM", hivyo wataipigia "CCM Kura za Chuki" kule visiwani Zanzibar!, hivyo CCM itaanguka rasmi Zanzibar, na serikali ya Zanzibar sasa itaongozwa na chama cha CUF!. Kuanguka kwa CCM Zanzibar, ndiko kutakuwa gharama ya kwanza ya CCM kulipia udhalimu wake wa kulazimisha serikali mbili, na huu ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa muungano huu adhimu uliodumu kwa miaka 50 na nashauri hizi sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano tunazokwenda kuzifanya mwezi huu, tuzifanye kubwa kweli kweli!, kwa sababu, kama CCM itashikilia msimamo wake, wa serikali mbili, then huenda sherehe za mwaka huu, zikawa ndizo sherehe za mwisho kabisa za Maadhimisho ya sikukuu ya Muungano!.
  5. Waziri wa Sheria wa Zanzibar, Mhe. Aboubakar Khamis Bakari, ndie ataendelea kuwa waziri wa sheria wa serikali ya CUF, na ndiye huyu huyu aliyetoa hoja binafsi ya serikali ya SUK na ndiye aliyeyasuka yale marekebisho ya katiba ya Zanzibar ya 2010 kuuita Zanzibar ni nchi, na ndiye aliyepenyeza kile kipengele cja "kura ya maoni" Zanzibar, hivyo kazi ya kwanza ya serikali mpya ya CUF, itakuwa ni kuitisha "kura ya Maoni" Zanzibar, kuwauliza Wanzanzibari kama wanautaka muungano au la!, jibu lake, najua kabisa Mhe. Rais Dr. Jakaya Kikwete, unalijua fika!, kila mtu anajua wazi, Wanzanzibari wakipewa fursa ya kupiga kura ya maoni kuhusu muungano, watajibu nini!.
  6. Sisi tuliojaaliwa jicho la ndani, tunajua kabisa, ndani ya moyo wako wewe rais JK, ulitaka serikali tatu!, ndio maana ukairuhusu rasimu ya Warioba kupita kama ilivyo!, ila wahafidhina wa ndani ya CCM!, haswa wale "wanga" wasiona na uwezo wa kuona mbali, wakakushika sikio ukabadili msimamo! na sio tuu kumgeuka Warioba bali kutugeuka Watanzania!. Na Sitta pia anajulikana wazi atataka serikali tatu!, hili la kuruhusu maoni ya wachache yasomwe mara mbili, sio duplication ya bahati mbaya, hata jana kitendo cha kuliahirisha bunge baada ya kusikia TBC wamemuhujumu Lissu hivyo kikao cha leo kuanza na Lissu, ni mbinu tuu za kuzibeba serikali 3!, ila kwa vile mule CCM ndio wengi na wengi wao ni wajinga wajinga, wakiutumia uwingi wao vibaya, wataipindua rasmu ya Warioba na kuyapindua maoni ya wananchi na badala yake wataunda rasmu mpya ya CCM ya serikali mbili!.
  7. At the moment Rais wetu, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, bado uko kwenye most bright prospects za kumaliza kipindi chako cha miaka 10 ya urais ukiwa ndie rais utakaye acha historia kubwa zaidi ya kutukuka ukiacha Nyerere aliyetuleta uhuru, wewe uliyetuletea katiba mpya ya wananchi, kama utaruhusu maoni ya wananchi waliopendekeza kwa Warioba, katiba ya serikali tatu ipite, hivyo sio tuu kuulinda muungano, bali kuudumisha muungano na kumaliza kabisa kero za muungano na wakati huo huo kukinusuru chama chako cha CCM kule Zanzibar!. Kwa Bara CCM sio kuwa ni imara sana!, no, bali kwa sababu hatuna any serious opposition, hivyo CCM kitaendelea kushinda kwa ulaini kabisa kwa miaka kadhaa ijayo!.
  8. Lakini kama JK, umekubali kuingizwa mkenge na hao wahafidhina wa CCM kwa kukudangana kuwa kwa vile wewe sio mgombea 2015, you have nothing to loose, hivyo endelea ku force, Tanzania tusipate katiba mpya ya wananchi ya serikali tatu, badala yake tupate katiba mpya ya CCM ya serikali mbili kwa kuwatumia wale wateule wako ndani ya kundi la 201 na uwingi wabunge wa chama chako, hivyo kujiaminisha utaacha katiba mpya yenye legacy ya jina lako!, ambalo litaandikwa kwa maandishi ya dhahabu!, ujue hilo litatokea ila litafuatiwa na hili..
  9. Kuanguka kwa CCM Zanzibar!, serikali ya CUF itaitisha kura ya maoni, Wanzanzibari wataukataa muungano, hivyo huu muungano wetu adhimu, uliodumu kwa miaka 50!, utakuvunjikia wewe, mikononi mwako!, na baada ya kuvunjika kwa muungano, hilo litaonekana kama dogo, kubwa zaidi litafuatia huku bara ni hili...
  10. Siku zote Watanzania walio wengi wameaminishwa kuwa chama kingine kikiingia madarakani, nchi itakuwa haitawaliki!, Watanzania Bara wakiona kumbe Zanzibar imewezekana!, next election ni zamu ya Bara, naamini unajua wazi kuwa siku zote CCM inashinda sio kwa sababu inapendwa sana!, CCM siku zote inashinda kwa "mbinu" na "taking advantage ya ignorance ya Watanzania" na "mazoea!", with CCM kama chama cha upinzani nchi ya Zanzibar, believe it or not, Watanzania waliokuwa wakiichagua CCM kwa mbinu, ignorance na mazoea!, wataamka!, na kukijitokeza chama serious cha upinzania, au kama Chadema kitaacha ujinga ujinga na upuuzi upuuzi wake kikawa serious, 2020 CCM kitawekwa pembeni!, na kazi kubwa ya kwanza ya setikali mpya ya Taifa la Tanganyika itakuwa ni kuipurura CCM kwa kutaifisha mali zake zote ilizopora wananchi wa Taifa hili tangu enzi za chama kimoja, na kuzigeuza ni mali za umma!, Mali pekee ya CCM itakayosalimika ni ile Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba!, na hala hala Wazee wake Maalim Mohamed Said, wale wa Gerezani wasije nao wakadai jengo lao waliloipa Tanu!. With that CCM will never make it again!.
Mhe. Rais wetu Mpendwa, Dr. Jakaya Kikwete, the choice is yours!. Namalizia kwa kukusisitizia kuyazingatia maneno ya mwana zuoni mmoja simtaji jina, alisema "Anajidhania anaipenda sana nafsi yake, ataiangamiza!, na anayeichukia nafsi yake, ataisalimisha!", Vivyo hivyo suala la serikali mbili ndani ya katiba, kama unadhani unaupenda sana huu Muungano wetu na unaipenda sana CCM, serikali mbili zitauangamiza na kuingamiza CCM!, na kama unadhani serikali tatu zitauvunja muungano, chakua serikali tatu, zitaiumiza CCM lakini ndio zitauimarisha muungano na kuinusuru CCM-Zanzibar, hivyo kuinusuru CCM bara kuendelea kuongoza japo with "a loot"
The End Justify the means!"

Mungu Mbariki JK auone ukweli maneno ya unabii wa uzi huu!.

Mungu Ibariki Tanzania!.

Pasco.
 
Bjpi5YNCEAA2kY6.jpg
 
Thank you Pasco... Great advise and i am sure JK needs to leave a 100 years legacy by doing the right thing now

We really need a serious katiba and NOT political katiba kama "tabaka tawala" linavyotaka, and I am sure JK hayuko kwenye "tabaka tawala" japo ni mtawala
 
Kwa nini miaka hamsini haujavunjika uje kuvunjika leo,watu wa cuf mnashida sana tunajua kuwa mmepanga kurudisha utawala wa kiarabu pemba hiyo mipango yenu sasa inajulikana.
 
Nadhani JK alikubali katiba iundwe upya akiamini kuwa mambo yatakuwa mepesi na kwenda kama chama chake kinavyotaka.
He was wrong. Absolutely wrong.
Wananchi wa sasa wana ufahamu sana.
Mkuu kosa la jk liko wapi kazi iko mezani wajumbe wanaendelea na kazi wao wanajukumu la kupima na kuamua kilicho chema wala siyo vinginevyo hayo mawazo yako ya kurushia watu lawama bila sababu hazina maana.
 
Kwa mtu yoyote makini hili jambo liko wazi kabisa.Hata kuna mdau aliandika hapa JF akionya uwezekano wa CCM kupoteza umaarufu wake Zanzibar na CHADEMA kujijengea umaarufu Zanzibar kwa kutetea serikali 3.Kwahiyo ni kweli kabisa,CCM itaanguka Zanzibar na upinzani(CHADEMA na CUF) utakubalika zaidi Zanzibar.

Nashawishika kusema kuwa Lissu leo hii ataonekana "lulu" ndani ya Zanzibar kwa hotuba yake na pia atakibeba chama chake visiwani kwa kiwango kikubwa mno.

Hata huku bara,watanganyika wengi ambao ni wafuasi wa CCM wanataka Tanganyika irudi na CCM wakiendelea ba msimamo wao wa serikali mbili,hata huku bara watapoteza mashabiki wengi na wengi wao wataikubali zaidi CHADEMA.Kwa sisi tunaolilia mabadiliko huu utakuwa ni mtaji mkubwa kwetu na utakuwa ni mwanzo wa ushindi katika chaguzi zijazo.

Ukweli ni kuwa wananchi wengi wa kawaida wanataka serikali 3 na isitoshe hawaoni hata faida ya huu muungano ila huu muungano unafaidisha zaidi watawala na bahati mbaya watawala wanashindwa kusoma alama za nyakati na kubadilika na ipo siku watakuja kujuta.

CCM badilikeni wenye nchi hawataki aina hii ya muungano hivyo mkilazimisha mnajiandalia anguko leno la kisiasa.

Hata hivyo,anguko la CCM ni ukombozi wa mtanzania hasa sisi wa huku bara.Hawa jamaa ni watu "dhalimu" sana na si vibaya wakaondoka madarakani kwa njia yoyote ile.
 
Ujumbe mzuri kwa JK ila m jst askin myself simple question kwamba hii rasimu maudhui yote ni kuhusu serikali mbili au tatu tu?.....

Hamna mambo mengne pia ya ku-highlight!...
 
Hoja zako zimeshiba hazina hata chembe ya shaka hata kidogo.kama ni kiongozi bora atalifanyia kazi andiko lako na kubadilisha msimamo wake na chama chake.kama atapuuza na sisi tutampuuza na kukipiga chini chama chake cha ccm.
 
Back
Top Bottom