Chaguzi za CHADEMA zaingiliwa na rushwa kama za CCM

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
5,376
8,104
Sasa wananchi tukimbilie chama gani?

20240503_093649.jpg



View: https://twitter.com/Tanzaniawall/status/1786251731120058804?s=19
 
Ndiyo maana huwa nawambia wananchi wasiendeshwe sana na maneno ya wanasiasa.

Kama CHADEMA wanagawa rushwa ili kupata uongozi, ni kwa namna gani wataweza kuikosoa Serikali ya CCM kwenye mambo ya rushwa?
 
JF wataifuta hii ila wajue Mungu anaona na kesha ona
 
Ndiyo maana huwa nawambia wananchi wasiendeshwe sana na maneno ya wanasiasa.

Kama CHADEMA wanagawa rushwa ili kupata uongozi, ni kwa namna gani wataweza kuikosoa Serikali ya CCM kwenye mambo ya rushwa?

..anayehonga ni Mama Abduli.

..Na anatumia fedha za umma.

..suluhisho ni Katiba Mpya itakayozuia upuuzi wa aina hiyo.
 
Hamkani si shwari tena.

..hili ni tatizo baya sana.

..hatuwezi kuwa na siasa za aina hiyo.

..tutasababisha wananchi wakose imani na mifumo yetu ya uchaguzi.

..Ni hatari kwa usalama wa nchi kama wananchi watakuwa imani na mfumo wa uchaguzi wa viongozi.
 
Wanasiasa wote lao moja, usije ukawaamini hata sekunde moja kwa kuhadaika na namna mishipa inavyowatoka wakihutubia majukwaani
 
Uchaguzi ndani ya Chadema ni sawa na kumchinja nyati mbele ya kundi la watu wenye uchu wa nyamapori, kila mtu anammezea mate. CCM na maajenti wake wanatumia kila njia waweze kufanikiwa kuingiza watu wao watakao kidhoofisha chama.
Kama kinaweza kudhoofika basi hiki siyo chama tena anymore bali ni kundi la wajasiriamali wa siasa.
 
Back
Top Bottom