CHADEMA imetuangusha, Ni wakati sasa wa Mbowe kuachia ngazi!

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Kutokana na trend ya maendeleo ya chama ya siku za hivi karibuni, kuanzia kwenye uchaguzi wa madiwani, nashawishika kwamba huu ni wakati mzuri sasa wa Mbowe kuondoka.

Ni dhahiri kwamba Mbowe ameshindwa kukiongoza chama au anazeeka kama mwenzake Lipumba kiasi cha kukifanya chama kianze kupoteza mwelekeo na watu wengi kuanza kurudisha imani kwa CCM. Sikutegemea kabisa kwamba Kalenga tungeshindwa vibaya kiasi hiki, despite resources tulizotumia kwenye kampeni. Na kwa matokeo haya ya Kalenga, ni dhahiri kule Chalinze hata kura 5000 hatutafikisha.

Hata NCCR na CUF walianza kuporomoka polepole hivi hivi na mwisho wa siku wakapotea kabisa. Naanza kuona dalili za CHADEMA kupoteza mwelekeo siku za hivi karibuni.

Chini ya utawala wa Mbowe naona hatuwezi kuwa na jipya kwa sasa kama chama. Amefanya kazi kubwa na nzuri sana ya kukiwezesha CHADEMA kukuwa na kufikia kuwa chama kikuu cha upinzani, lakini kwa sasa mbinu zake zimeexpire! Matumizi makubwa ya fedha za chama yasiyokuwa na matunda mazuri kwa kweli yafikie mwisho.

Tunataka kuona returns za kile tunachospend. Naamini Mbowe atajitathimini na kuamua kwa nia njema kabisa kutogombea katika kinyang'anyiro cha mwenyekiti wa chama kwenye uchaguzi wa chama ujao.
dala dala said:
Wengi wetu tulijiwekea matumaini makubwa sana kuwa CDM kuwa itatupeleka hatua moja au zaidi mbele katika kuipeleka Tanzania/Tanganyika kwenye mafanikio ya kiuchumi, kijamii, kisiasa nk. Bahati mbaya sana kama alivyotabiri Mzee Wassira kwamba CDM imara haitakuwepo 2015, naona dalili zote za kauli hii kutimia. Kilichobaki sasa ni Mwaga Ugali, Nimwage Mboga.

Kwa watu makini wataelewa kuwa mahali kilipofika Chama chetu hiki kipenzi cha walala hoi sipo penyewe. Nilishauri awali kuwa mgogoro kama huu ungetafutiwa suluhu ya ndani kwa ndani lakini pengine kwa kukosa uvumilivu au busara yanatokea haya mambo ya aibu. Pengine kuna mengi ambayo Watanzania hatukuyajua nyuma ya pazia sasa yatawekwa wazi. Binafsi nimesikitishwa sana na hali hii na pia naona Demokrasia haipo kama baadhi ya watu wanavyodiliki kusema.

Pengine tuendelee kumsubiria Masia mwingine huyu tuliyedhani ndiye ni kama siye. Kwa muda gani? How soon? Hamjachelewa sana, rekebisheni haya mambo na jaribuni kujipanga upya. It is obvious the party has lost its credibility. No one to trust, Neither Mbowe Nor Kabwe they are all corrupted. Then, who else to revive our hopes??

----------------------------
Jan 07, 2014:
Kwa miezi kadhaa tumesikia fukuto nyingi zikikikumba chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema. Kwa werevu, kuitazama hali iliyopo ndani ya chama hiki kikuu utaweza kung'amua mapungufu kadhaa.

1. Kukosa washauri
2. Kuamini wasioaminika
3. Kutoweza kutatua changamoto
4. Kutokukubali changamoto

Duniani, hakuna taasisi isiyokuwa na changamoto. Uimara wa taasisi huwa ni kwa namna gani mnaweza kutatua changamoto pasipo kuathiri majority yanayowategemea na mnaowategemea.

Jaribuni sana kutoegemea pande zozote mnazoaminishana, bali jengeni mabaraza ya wazee kuwashauri na tendeni haki. Leo mnagombana, hamuwasikii akina Mwigulu, hamjui sakata la Kapuya lilipoishia, hamuongelei serikali inaendaje na mnamshauri vipi rais katika kuteua mawaziri wapya, hamuongelei juu ya uchumi.

Leo mpo busy na Zitto na wenzake, hampigii kelele mauaji ya leo ya mtu mmoja kule mgodini Geita, hamuongelei mauaji ya watu 4 mgodi wa North Mara jana na leo. Mnajisahau au ndio mparanganyiko.

NAWASHAURI: Punguzeni washauri warika la vijana, na ongezeni washauri wazee. Wazee watawavusheni.

Kesi ya Zitto imehitimishwa leo, ni aibu kuburuzana mahakamani huku mawakili wote (mshindi na mshindwa) wakiwa ni wanachama wenu, jambo linaloashiria ipo shida kubwa ndani ya chama. Je, naye Albert Msando mtamuita msaliti, mamluki, snitch au katumwa?

Msitoe majibu mepesi ya ujana, pimeni na tazameni kila neno mnenalo linafikisha ujumbe gani na nini athari ya kesho. Wazee ni muhimu kwenu.

Katibu Mkuu alihamaki na kwenda Kigoma, Zitto nae akafuatia kujibu mapigo. Leo Dar mmeiona ilivyoshamiri kwa makundi mawili, je mpo tayari kupoteza uimara wenu?

HEKIMA NA BUSARA ni tunu bora zaidi maishani.

Jipangeni na MSIKURUPE kama mfanyavyo, taasisi yenu imekua sana na inaweza kuporomoka mkiangalia. Jiepusheni na historia kujirudia kutoka NCCR-MAGEUZI, CUF nanyi mkafuatia. Hapana.

Jipangeni.
Jan 09, 2014:
Ndugu zangu wana JF, Kwa moyo wa UJASIRI KABISA napenda ku-declare interest kwamba, mimi ni mwanachama mtiifu wa CDM kwa miaka 9 sasa, ninaimani na chama changu na nina imani na viongozi wangu wa chama kuanzia tawi mpaka taifa, ila leo nataka kuzungumzia yafuatayo:-

1. Kwa miaka kadhaa iliyopita chama changu kimefanikiwa kwa dhati kabisa kujenga uaminifu mbele ya kundi kubwa la vijana, sasa badala ya kuendeleza malumbano, KAMATI KUU ilitakiwa kupanga mkakati mahususi wa jinsi ya kuteka hisia na kujenga UAMINIFU KWA KUNDI LA WAZEE, badala ya kuendeleza chuki, visasi na malumbano kama ilivyo sasa.

2.Kuwa mjumbe wa kamati kuu inamaanisha uwakilishi sahihi kimaamzi, kwa kuzingatia WEREDI, HEKIMA,BUSARA, MTAZAMO CHANYA na pia UVIMILIVU WA KISIASA, sasa sijui kama viongozi wangu wanayazingatia hayo wakati wote linapofikia swala la kutoa MAAMZI. Mathalani, swala la ZITTO lilistahili kufanyiwa kazi kwa kuzingatia ALAMA ZA NYAKATI, Kama swala ni usaliti BUSARA, HEKIMA na MISINGI HURU YA KIKATIBA ingetuwezesha kumaliza swala la ZITTO pasipo makovu yoyote kama hali ya mambo ilivyo sasa.

3. Mwisho viongozi wangu wa chama wanatakiwa kutambua kwamba WANANCHI WAMEWAAMINI CHADEMA kwa sababu wanaonyesha nia ya dhati ya kusimamia haki, usawa na maendeleo ya watanzania maskini kwa vitendo, sasa vivyo hivyo wananchi wataondoa imani kwa chama changu iwapo viongozi wangu watashindwa kuonyesha DALILI YA KUSIMAMIA KATIBA NA MISINGI YA UTAWALA BORA,

*Kilio changu kwa kamati kuu, "Tusiendekeze VISASI, UBABE, CHUKI, UMWINYI na HISIA, ukomavu wa kisiasa hutoa nafasi kwa kiongozi wa juu kuzingatia MISINGI ya utawala bora.

*Tukumbuke, makovu yaliyowapata wenzetu NCCR kwa mkasa wa KAFULILA au CUF kwa Mkasa wa HAMAD RASHID MOHAMED, Mbowe mwenyekiti wangu huku kwetu TABORA wananchi wameshajenga IMANI na CDM toka enzi za uchaguzi Mdogo IGUNGA
Aprili 07, 2014

Naipenda CHADEMA, napenda uongozi wa mbowe na DR Slaa lakini nahisi chama kilipofika kinahitaji mabadiliko mapya ya kiuongozi. Mabadiliko ninayoyapenda ni ngazi ya juu hasa nafasi ya mwenyekiti cha chama.

Ninaposema hivyo sina imani na Zitto kabwe kuchukua nafasi hiyo ila nahitaji kiongozi mpya ambaye atakitoa chama katika mfumo na mtazamo wa sasa wa watanzania kuingia katika mtazamo mpya.

Kiongozi huyu mpya atambuwe kabisa kwamba mbowe amefanya kazi kubwa sana kukifikisha chama katika nafasi ya juu kama kilivyo pale. Lakini kwa sasa nahisi mbinu zake zimefikia kikomo.

Mbowe amefaulu kukipandisha chama kwa kutumia matukio. Wananchi walifuatwa katika kila walilolifanya CCM. Akitumia uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja pamoja na jopo lake aliweza kuwakamata CCM hadi wananchi wakamuelewa, wakamuamini wakakiamini chama.

Msimao huu ulikuwa ukienda sambamba na sura ya ubabe ambapo serikali ya CCM nayo ilikuwa ikipotea na kujiingiza katika mapambano na watu waliokuwa wakitafuta hoja. Mwisho wa ubabe wa serikali na Chadema uliishia kukijenga chama huku wananchi wakipewa tafsiri ya manyanyaso kwa upinzani.

Kwa hapa tulipofika ukichanganya na upepo wa Zitto pamoja na tasiri inayoingia mpya kwamba Chadema kimekuwa kikitengeneza matukio haramu ikiwa ni pamoja na Movie ya Rwakatare, nahisi kwa sasa chama kinahitaji mtu ambaye yuko Moderate.
Mtu ambaye anaweza kujenga hoja, akaipaka CCM, akawahamasiha wananchi kuichukua CCM na Serikali yake lakini akiepuka kuonekana mbabe zaidi.

Kiongozi mpya huyu asisahau kabisa kwamba Mbowe bado atakuwa ni mtu mhimu sana kuifanya Chadema iendelee kuwa chadema. Mbowe ana fedha, ana media ambayo ndiyo Mouth-peace ya Chadema, ni mtu mwenya kujituma sana katika harakati. BADO ATAKUWA NI MTU MUHIMU SANA CHADEMA.

Katika hili namuengua Zitto kwa sababu hisia za kwamba Zitto ana ndoa na CCM zina ishara za ukweli. Hata hivyo ZItto hafai kwa sababu katika uongozi wa chama kwa ngazi ya juu kama hiyo lazima uwe na element za unafiki lakini unafiki wa zitto unakuwa ubinafsi zaidi.

Unafiki tunaousema hapa ni pale ambapo mmesema, mkaamua kwamba tunafanya hivi ndani ya chama. Hata kama wewe hutaki, kwa vile ni maamuzi ya chama huna budi kupanda jukwaani ukajifanya kama vile wewe ndio mdau mkubwa wa wazo hilo. Kama mmesema tunasusia, usijifanye wewe mstaarabu zaidi, wewe ndio uwe wa kwanza kunyanyuka huku ukitoa kauri ambayo inaashiria kweli kwamba hujaridhishwa.

Wengine ambao siwaafika katika nafasi hii ni Tundu Lissu, pamoja na Lema. Hawa wanaujua unafiki lakini ubabe utakuwa paleplae kama kiongozi anayeondoka. Wajumbe wanaweza wakaja na majina mbalimbali wanayoyaona. Hilo ndilo wazo na mtazamo wangu mimi kama mpenda CHADEMA. Mimi sina jina mpaka sasa.

November 23, 2017

Kuna watu wanafikiri tatizo la wanachadema kukichoka chama chao ni ujio wa Lowassa, la hasha bali Mwenyekiti Mbowe uwezo wake wa ubunifu umefikia kikomo.

Hakuna asiyejua kwamba Lowassa ni bepari na CHADEMA ndio chama cha mabepari " uchwara" hapa Tanzania sasa uwepo wake katika chama chenye itikadi anayoiamini kuna ubaya gani?

Ukiangalia utendaji wa Mbowe katika nafasi zote mbili ile ya Mwenyekiti na KUB ni dhahiri anahitaji kusaidiwa. Na ni lazima sasa nafasi ya Mwenyekiti apatikane kidemokrasia na si kusubiri mwongozo wa familia fulani hakika chama kitakufa, wanachadema wa leo sio kina Mdee wa juzi. Nawasilisha!!
 
kupokea pesa hata kwa ccm si kosa kosa ni unazichuku kwa sababu gani "mbowe"ila imeonyesha ni kweli na yeye huwa anapokea kutoka ccm ila anazichukua ili atafune tu teeeeh teeeeh teeeeh teeeh chezea wahafidhina wewe watakukutanicha na chacha wangwe soon walikompeleka
 
Bahati yenu mnaoandika hata utumbo, post zenu zinakua hewani ila tu nikua mmechemka tayali vibalaka wenu out.
 
Wengi wetu tulijiwekea matumaini makubwa sana kuwa CDM kuwa itatupeleka hatua moja au zaidi mbele katika kuipeleka Tanzania/Tanganyika kwenye mafanikio ya kiuchumi, kijamii, kisiasa nk. Bahati mbaya sana kama alivyotabiri Mzee Wassira kwamba CDM imara haitakuwepo 2015, naona dalili zote za kauli hii kutimia. Kilichobaki sasa ni Mwaga Ugali, Nimwage Mboga. Kwa watu makini wataelewa kuwa mahali kilipofika Chama chetu hiki kipenzi cha walala hoi sipo penyewe. Nilishauri awali kuwa mgogoro kama huu ungetafutiwa suluhu ya ndani kwa ndani lakini pengine kwa kukosa uvumilivu au busara yanatokea haya mambo ya aibu. Pengine kuna mengi ambayo Watanzania hatukuyajua nyuma ya pazia sasa yatawekwa wazi. Binafsi nimesikitishwa sana na hali hii na pia naona Demokrasia haipo kama baadhi ya watu wanavyodiliki kusema.

Pengine tuendelee kumsubiria Masia mwingine huyu tuliyedhani ndiye ni kama siye. Kwa muda gani? How soon? Hamjachelewa sana, rekebisheni haya mambo na jaribuni kujipanga upya. It is obvious the party has lost its credibility. No one to trust, Neither Mbowe Nor Kabwe they are all corrupted. Then, who else to revive our hopes??

usitumie "hast generalization" utaharibu maana nzima ya topic yako. Ukisema "no one...." unakosea sana jizungumzie wewe kama wewe. Wapo wengi sana wenywe imani na cdm mpaka sasa. Na pili: inaonekana huu mgogoro umeanza kuusikia kwenye media hivi punde ndio maana hujitambui. Walio karibu na cdm wanaufahamu huu mzozo kitambo. Busara ilishatumika zaidi ya Mara Mia moja ikashindikana. Walibembeleza sana, walimsihi sana,mpaka Joseph Butiku japo yupo ccm alimshauri Zzk akamwambia ili asipotee kisiasa lazima ajitathmini sana "kwanini upendwe sana na maadui wa chama chako?". Aliongea mengi kumshauri zzk lakini yatosha kusema kuwa zzk amevumiliwa sana sana sana. Hata ccm wanalifahamu
 
Kama imani yako ilikuwa kwa watu nakupa pole...wengine imani iko kwa taasisi kama taasisi
 
Kama imani yako ilikuwa kwa watu nakupa pole...wengine imani iko kwa taasisi kama taasisi

Kumbuka taasis haiundwi na mawe, inaundwa na watu. Watu safi huunda taasis safi. Ni vigumu kutenganisha watu na taasis. Taasis sio kitu cha kufikirika bali kinaundwa na watu kama mimi na wewe, sasa watu wakipoteza credibility wanaiharibu hiyo institution.
 
usitumie "hast generalization" utaharibu maana nzima ya topic yako. Ukisema "no one...." unakosea sana jizungumzie wewe kama wewe. Wapo wengi sana wenywe imani na cdm mpaka sasa. Na pili: inaonekana huu mgogoro umeanza kuusikia kwenye media hivi punde ndio maana hujitambui. Walio karibu na cdm wanaufahamu huu mzozo kitambo. Busara ilishatumika zaidi ya Mara Mia moja ikashindikana. Walibembeleza sana, walimsihi sana,mpaka Joseph Butiku japo yupo ccm alimshauri Zzk akamwambia ili asipotee kisiasa lazima ajitathmini sana "kwanini upendwe sana na maadui wa chama chako?". Aliongea mengi kumshauri zzk lakini yatosha kusema kuwa zzk amevumiliwa sana sana sana. Hata ccm wanalifahamu
Butiku yupo CCM kutokana kimaslahi zaidi. Lakini hana chembe ya uccm hata kidogo
 
Ukiwa na akil kwenye wajinga unaonekana adui,...mnakumbuka stori ya odili samaru
 
usitumie "hast generalization" utaharibu maana nzima ya topic yako. Ukisema "no one...." unakosea sana jizungumzie wewe kama wewe. Wapo wengi sana wenywe imani na cdm mpaka sasa. Na pili: inaonekana huu mgogoro umeanza kuusikia kwenye media hivi punde ndio maana hujitambui. Walio karibu na cdm wanaufahamu huu mzozo kitambo. Busara ilishatumika zaidi ya Mara Mia moja ikashindikana. Walibembeleza sana, walimsihi sana,mpaka Joseph Butiku japo yupo ccm alimshauri Zzk akamwambia ili asipotee kisiasa lazima ajitathmini sana "kwanini upendwe sana na maadui wa chama chako?". Aliongea mengi kumshauri zzk lakini yatosha kusema kuwa zzk amevumiliwa sana sana sana. Hata ccm wanalifahamu

Wewe moja kwa moja ni mchaga na Ndiyo maana unamtetea Mbowe.

Lakini mbona inajulikana kabisa kwamba Mbowe uwezo wake ni mdogo sana hana analojua zaidi ya kupiga Disco ni mwanaharakati siasa hajui

Mbinafsi fisadi mwizi wa wake za watu mkabila lakini pia ni chama cha ukabila na ukoo ukaskazini mweee mbona wengi waisha shituka kama kubaki umebaki wewe peke yako POLE
 
Tatizo lenu ni shule ndogo nothing more. You cant reason and argue your case .
Utumbo uleule, hivi unadhani mtu aliyesoma utamjua kwa yeye kuchanganya lugha ya kizungu na kiswahili wakati wa kuongea au kuandika?
 
Ukiwa
na akil kwenye wajinga unaonekana adui,...mnakumbuka stori ya odili
samaru
Uongo mtupu kwanza sio ukiwa na akili kwani kila mtu anahakili kasolo
wale ambao wanamatatizo nadhani unazungumzia wenye uelewa kuliko wenzao
sio? sasa kama ndivyo unafikili Zito alikua na uelewa kuliko wenzake?
acha ujinga chama kina hadi Maprofesa ujinga wako peleka CCM, sawa?
 
Binafsi ameniumiza sana zitto, kupiga kelele kote kule kuhusu uswis, kumbe anagawana mamilioni na mafisadi! Duh..
 
Huruma ya Maccm juu ya Zitto inaongeza shaka juu ya mashtaka ya usaliti.
 
Back
Top Bottom