Blinken aitolea wito Hamas ikubali 'pendekezo la kusitisha vita Ghaza

LINGWAMBA

JF-Expert Member
Sep 30, 2023
458
1,072

Blinken aitolea wito Hamas ikubali 'pendekezo barabara sana' la kusitisha vita Ghaza​

Screenshot_20240501-201942.jpg

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameitolea wito Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ikubali pendekezo la makubaliano ya kusitisha mapigano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Blinken ametoa wito huo leo alipokuwa akizungumza na familia za mateka wa Israel wanaoshikiliwa huko Ghaza kufuatia mkutano wake na Rais wa utawala wa Kizayuni Isaac Herzog, na kudai kwamba: "kuna pendekezo barabara sana mezani sasa hivi. Hamas inahitaji kusema 'sawa'."

Harakati ya Hamas bado haijatoa maoni yoyote kuhusu kauli hiyo ya Blinken.

Alipokutana na kufanya mazungumzo na Herzog, waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani alisema, Washington "imedhamiria" kufanikisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na harakati ya Hamas.

Aidha, Blinken amerudia tena kuelekeza lawama kwa harakati ya Hamas iwapo makubaliano ya kusitisha mapigano hayatafikiwa, akisema: "na sababu pekee ambayo italifanya hilo lisifikiwe ni Hamas".
Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani aliwasili Tel Aviv jana Jumanne katika kituo cha tatu cha ziara yake anayofanya katika eneo la Asia Magharibi baada ya kuzitembelea Saudi Arabia na Jordan, kwa lengo la kufanya mazungumzo na mashauriano kwa ajili ya kutafuta mwafaka wa kusitishwa vita huko Ghaza.

Harakati ya Hamas, ambayo inaaminika kuwa inawashikilia karibu mateka 130 wa Israel, inataka kukomeshwa mashambulizi ya kinyama na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Ghaza kabla ya kufikia makubaliano yoyote na utawala huo ya kubadilishana mateka.

Makubaliano ya awali ya mwezi Novemba mwaka jana yalishuhudia kuachiliwa kwa Waisraeli 81 na wageni 24 mkabala na Wapalestina 240, wakiwemo wanawake 71 na watoto 169.../
 
Sasa Netanyahu upande mwingine anasema haijalishi HAMAS itaachia au haitaachia mateka Israel itaendelea kuua raia Rafah, hapo kwa nini HAMAS wasione kuwa kuachia mateka ni biashara kichaa?
 
Uzuri Israel imesema hata Mateka wakiachiwa vita ya kuwamaliza ipo pale pale hadi Hamas wadhoofike kabisa
 
Israel hahitaji huruma za USA yeye anaangalia baada ya vita kusitishwa na kupata hayo mateka kitu gani kitaendelea? Mateka 130 huku Israel imeshapoteza askari zaidi ya 150 mwenye vita na raia 1000 kwenye yale mashambulizi ya 7 October, inaonekana hao mateka 130 si kitu kwa future ya Israel. Vita uishe tumechoka
 
Mwanzo walisema vita haiishi mpk hamas ifutike sasa hv wanahangaika kupeleka mapendekezo tu halafu Hamas wanayasoma wanarudishiwa kafanyeni marekebisho mrudi hz dharau
We huoni gaza ishafutika wavaa vipedo na watoto wao wanakwisha
 
We huoni gaza ishafutika wavaa vipedo na watoto wao wanakwisha
Ww kweli akili huna kwani malengo ya israel ilikuwa kubomoa majengo au kuifuta hamas na kuokoa mateka? Israel wamebomoa nyumba, hospitals na mashule lakini hamas wapo na mateka hakuna mliyookoa sana sana mnaunajisi mji wa watu mmejazana mashoga tu mnatifuana mitalo tu
 
Back
Top Bottom