Hamas yakubali pendekezo la kusitisha mapigano, wananchi wa Rifah washangilia

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
51,839
23,274
Gaza kumekucha huko wananchi wanazurura mitaani wakiimba na kumshukuru Mungu baada ya Hamas kukubali masharti ya Israel muda huu.

Kwakweli Mungu ni mwema anajibu wamekufa wengi sana na sasa tuseme imetosha waliobakia waendelee na maisha ila adabu wamekipata walichokitafuta.

======
Kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh ametuma neno la kundi hilo kukubali pendekezo la wapatanishi, Qatar na Misri kusitisha mapigano.
  • Maelfu ya watu wamekimbia mashariki mwa Rafah baada ya Israel kuwataka kuondoka ikijiandaa na mpango wa mashambulizi kwenye mji huo
  • Hamas imesema mashambulizi ya Majeshi ya Israel haitakuwa 'Picnic' na imejiandaa kuwalinda raia wa Palestina.
Chanzo ndani ya Jeshi la Israel kimenukuliwa na Reuters kikisema Hamas wamekubali pendekezo laini la Misri ambalo halikubaliki kwa Israel. Vyombo vya habari vya Israel pia vimesema Serikali ya Israel havijakubali mpango huo.
 
1. Hapa hii ni habari mpya:

IMG_20240506_194849.jpg

2. Kutokea hapa Israel atokee mlango upi?

3. Ni vifijo na vigele gele Gaza, ngoja tuone.

4. Pana simu ya beberu tokea jumba jeupe na mazaga zaga yake imetinga jioni hii Tell Aviv.

5. Si haba hayapo marefu yasiyokuwa na tija.

6. Ikumbukwe msimamo wa HAMAS umekuwa kusimamisha mapigano maana yake, mwishonwa vita!
 
pole mwali ashakubali na bwana kapelekewa taarifa sasa haijulikani kama atabeba zigo au vipi la ila mwali ashamkubali bwana yule

1. Kwani Israel anasema je?

2. Si HAMAS ilihitaji guarantee tokea USA? Guarantee imepatikana? Hii ni mwisho wa vita?

3. Si Israel ilisema dili halikubaliki?

4. Je dili limebadilika au ni lile lile?

5. Mchumba bado hajajulikana.
 
Aibarikiye Israel atabarikiwa 😂😂🌟
Wakristo wenzangu kwenye hili ndio natofautiana na nyie, huwezi ua watoto na watu wasio na hatia then useme israel taifa teule, huyo Mungu gani? Labda ni Mungu kichaa huyo, ndio maana hizi dini naziona ni vyama vya kisiasa vya kale, uongo ongo mtupu, ila ndio ivyo sunday school na madrasa zimewaminisha na nyie mmekalili
 
Ukristo unaingiaje hapo Bwashee? 🐼
 
1. Kwani Israel anasema je?

2. Si HAMAS ilihitaji guarantee tokea USA? Guarantee imepatikana? Hii ni mwisho wa vita?

3. Si Israel ilisema dili halikubaliki?

4. Je dili limebadilika au ni lile lile?

5. Mchumba b do hajajulikana.
andika yoooote unayoweza ila Ismail Haniyah kakubali peupeeee hivyo bwana Israel anasubiriwa kama atabeba zigo au hatobeba Qatar na Egypt wanamlilia bwana Israel achukue zigo maana wameshamchoka bint palestina
 
Wakristo wenzangu kwenye hili ndio natofautiana na nyie, huwezi ua watoto na watu wasio na hatia then useme israel taifa teule, huyo Mungu gani? Labda ni Mungu kichaa huyo, ndio maana hizi dini naziona ni vyama vya kisiasa vya kale, uongo ongo mtupu, ila ndio ivyo sunday school na madrasa zimewaminisha na nyie mmekalili

1. Tofautisha wakristo na wafia Ukristo.

2. Wafia Ukristo ni sawa na wafia Uislam tu. Wote hao ni wafia dini wale wale mbele wameweka ushabiki kama Simba na Yanga tu.

3. Wafia dini na sense of reasoning wapi na wapi?
 
andika yoooote unayoweza ila Ismail Haniyah kakubali peupeeee hivyo bwana Israel anasubiriwa kama atabeba zigo au hatobeba Qatar na Egypt wanamlilia bwana Israel achukue zigo maana wameshamchoka bint palestina

1. Tuliza mpira tujue kwanza:

"Contents za dili, Israel anakubali au ana komaa."

2. Mchumba mbona atajulikana?
 
Si biblia imesema israel ni taifa teule, na aibarikiye israel amebarikiwa? Yaani israel hii iliyochokozwa na kikundi hamas alafu inafanya collective punshment imebarikiwa? Reall? Inazuia hadi gari zenye vyakula ili watu 2milion wafe kwa njaa na kiu, huyo Mungu aliyebariki israel ni kichaa
Bible ni mkusanyiko wa vitabu na nyaraka tofauti tofauti 😄😄
 
1. Kwani Israel anasema je?

2. Si HAMAS ilihitaji guarantee tokea USA? Guarantee imepatikana? Hii ni mwisho wa vita?

3. Si Israel ilisema dili halikubaliki?

4. Je dili limebadilika au ni lile lile?

5. Mchumba bado hajajulikana.
Ismail Haniyah na wenzake walioko Qatar wamewazaaa wakaona dah Rafah inaenda fumuliwa na magaidi wenzao kibao ndo wamejificha hapo Rafah hivyo watauliwa kibudu wakaona basi kinyooooonge bora wakubali yaishe maana wapalestina wenzao wamewageuka kwa kuanza kuondoka rafah na hivyo ngao hazipo tena
 
Walibaki pekee yao wakitumika kama vikaragosi vya Iran , nchi za kiArabu waliwatenga waPalestina na kuunga mkono mahusiano yao ya Israel na nchi za kiungwana za kiarabu kupitia makubaliano ya Abraham Accord :

Maktaba:
SAUDI ARABIA NA JORDAN, WATUNGUA MAKOMBORA YALIYOVYATULIWA YEMEN KUELEKEA ISRAEL

Saudia Arabia moja ya nchi ya kiarabu kusaini makubaliano ya Abraham Accord (normalisation) na Taifa la Israel. Hivyo Saudia walivyoona makombora yanakatiza anga lao toka kwa wa Houthi wa Yemen , wakafanya wajibu wao kuyatungua ingawa yalikuwa amelengwa kuipiga nchi ya Israel. Jordan nayo watungua makombora yaliyokatiza nchini kwao kuelekea Israel toka kwa vikaragosi wa Iran waliopo kama mgambo ktk nchi za Iraq na Syria.

Pia manowari za Marekani katika bahari Nyekundu Red Sea watungua makombora yaliyofyatuliwa Yemen kuelekezwa Israel. Marekani ni rafiki wa kweli wa Saudia, Jordan, UAE na mmoja ya wadau waliofanikisha Abraham Accord kuleta utulivu na amani Mashariki ya Kati.

Mataifa ya Egypt, Jordan na Saudia Arabia ni nchi za mfano zilizo wauungwana kusimamia makubaliano ya Abraham Accord bila kusukumwa na viongozi wa magaidi wa HAMAS wanaotumbua maisha ya kifahari ktk hoteli za Qatar. kuendekeza jazba, mihemuko au imani kupitia shindikizo la magaidi wavunje makubaliano haya ya kihistoria.

Tanzania nayo haitakiwi kukurupuka kufuata mkumbo wa wahafidhina wenye chuki, mihemuko, kukosa kufikiri kwa kina na kulaani haki ya taifa la Israel kujilinda uwepo wake na usalama wa maisha raia wake.

The Times of Israel
https://www.timesofisrael.com › mis...
Missile from Yemen downed over Saudi Arabia -- report

5 days ago — The interception allegedly occurs in the northwest of the country, near its border with Jordan. Yemen's Houthi rebels have
U.S. Department of State (.gov)
www.state.gov
At the One Year Anniversary of the Abraham Accords: Normalization ...

17 Sept 2021 — Normalization leads to greater stability, more cooperation, mutual progress – all things the region and the world need very badly right now ...
 
Back
Top Bottom