Wazo zuri sanaMkuu, wewe juzi juzi si ulikuwa unauliza ni wapi wanachukua walinzi ili na wewe upeleke form ya kuomba kazi ya ulinzi?
Hii biashara ya ufuta umeianza lini?, kama ina faida kwa nini utake kuomba kazi ya ulinzi?. Angalia usimuingize choo cha kike mdogo wetu.
Oya mdogo wangu, hapo juu kuna watu wamekupa ushauri mzuri sana. Hiyo hela yako kwa sasa tafuta sehemu uitunze kwanza, usiingize kwenye biashara yoyote ile. Tafuta mtu ambaye anafanya biashara ya nafaka, muombe awe mentor wako(Omba hata kujitolea kumsaidia kazi zake) mpaka pale ambapo utaielewa hiyo biashara vizuri. Siku ukitaka kuanza kufanya biashara rasmi, chukua robo ya hela yako (2M) anza kununua mzigo kidogo kidogo. Ukishaanza kupata wateja wa kutosha ongeza robo ya hela (Hapo utakuwa umeingiza nusu ya hela yako kwenye biashara). Nusu ya hela inayobaki itunze kama back-up capital.