Barua ya wazi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kandongu

New Member
Mar 5, 2018
2
2
RAIS shikamoo,

Pole na Hongera sana kwa majukumu mazito ya kusukuma gurudumu la taifa letu. Mheshimiwa RAIS naandika BARUA hii nikiwa na majonzi mazito sana moyoni mwangu. Mheshimiwa RAIS nitajikita katika wizara ya TAMISEMI hususan katika SEKTA ya ELIMU kwani ndiyo sekta nyeti sana katika nchi yetu. Naomba majibu ya hoja zangu zifuatazo
:-
1. AJIRA 12,000+ KATIKA SEKTA YA ELIMU HAIAKISI MAHITAJI YA WALIMU YALIYOPO.Tarehe 17.04.2023 Mheshimiwa waziri wa utumishi akiwa bungeni amesema umetoa kibali cha kuajiri walimu zaidi ya elfu 12. Lakini Mheshimiwa RAIS idadi hii ni ndogo sana kulingana na MAHITAJI yaliyopo kutokana na vitu vifuatavyo:

(a) Zaidi ya shule mpya elfu moja za msingi na SEKONDARI zimeanzishwa hivyo shule hizi zinahitaji zipate walimu wakutosha ili shule hizi zifunguliwe.

(b) Shule nyingi sana zina uhaba wa walimu hususan za vijijini.Mfano shule za msingi za pembezoni mwa nchi kwenye mikoa ya Ruvuma,Mtwara,Rukwa ,Kigoman.k nyingi zina walimu 3-5

(c) Uanzishwaji wa michepuo mipya kama vile ya (dini,uchumi,michezo na Sanaa). TAMISEMI imeabzisha michepuo mipya lakini ikumbukwe kuwa masomo haya hayana walimu kabisa. .kwani mfano masomo ya dini yalikuwa yakifundishwa kwenye shule za binafsi tuu hususan za makanisa au Islamic schools. Vilevile masomo ya michezo na uchumi yalikuwa yakifundishwa kwenye shule chache sana na mahitaji ya walimu wa masomo uchumi na michezo ni makubwa sana.

(d) Uanzishwaji wa madarasa ya awali katika shule za msingi. Serikali imejenga madarasa ya awali ya mfano katika shule nyingi sana lakini wanafunzi waliopo kwenye shule hizi hawana walimu kabisaaa wakuwafundisha.

2. WALIMU WA KUJITOLEA
Wabunge wengi sana wamekuwa wakipiga kelele kuhusu kuwapa kipaumbele walimu WA KUJITOLEA. Mheshimiwa RAIS litizame jambo hili kwa makini sana. Kwani Kuna idadi kubwa sana ya walimu waliokuwa wakijitolea kwenye shule za umma lakini wakaaacha kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuthaminiwa na wakuu wa shule na walimu wakuu, serikali kutokuwatambua,kufundisha katika mazingira magumu( hususan bila kupata posho).Je walimu Hawa nao wanawekwa kwenye kundi gani? Na wao wazingatiwe kwani walifanya kazini hii kwa muda mrefu.

ILI KUTATUA MTAMBUKA HUU NAOMBA MHESHIMIWA RAIS KUPITIA OFISI YAKO YA TAMISEMI FANYA MAMBO YAFUATAYO:
1. Kuongeza idadi ya ajira hizi kutoka elfu 12 mpka elfu 30 angalau ili kupunguza uhaba huu wa walimu mashuleni kwani mahitaji ya walimu ni makubwa mno kuliko KADA nyingine yeyote ile.

2. Kuajiri walimu wa masomo ya michezo,dini na uchumi kwa wingi ili michepuo hii mipya ikapatwe kufundishwa kwenye shule zilizopendekezwa.

3. Walimu wa ELIMU ya awali nao wapewe kipaumbele.

4. Natoa rai pia kwako ikimpendeza Mwenyezi Mungu na kama bajeti inaruhusu walimu waliohitimu Miaka ya 2015-2018 wangeajiriwa kwa mkupuo.

Nitashukuru endapo ombi langu litapokelewa.
Wako katika ujenzi wa Taifa
RAIS WA WALIMU WASIO NA AJIRA TANZANIA
 
Kila kitu kinaendana na bajeti, huwezi kuchukua walimu wengi wakati uwezo wa kuwalipa huna, kumbuka serikali ina mambo mengi, kwa uwezo wa sasa ni kuajiri walimu 12,000+. Hata wewe ukiwa kwako, huwezi kuchukua watu wengi ukaishi nao wakati huna uwezo wa kuwalisha chakula kla siku. Hao walimu wanapaswa kulipwa kila mwezi hadi wanapostaafu, wakiajiriwa walimu wote maana yake serikali isimamishe shughuli zingine zote halafu iajiri walimu peke yake, maana yake kusiwepo na jeshi, kusiwepo na huduma za afya, kusiwepo na huduma zingine zote pamoja na kusimamisha miradi ya maendeleo. Changamoto ulizosema kweli zipo lakini huwezi kutatua zote kwa wakati mmoja, unatatua kidogokidogo kadili uwezo unavyoruhusu. Kwa sasa uwezo wake ndio huo. Kama wewe ni Mwalimu basi kuwa mvumilivu, utaajiriwa intake nyingine baada ya hii na Mungu atakufungulia milango.
 
Back
Top Bottom