UZUSHI BAKITA waonya kuhusu maneno Famasiala, Fautani

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Nimeona mtandaoni barua ikizunguka kuwa BAKITA wameonya kuhusu matumizi ya maneno kama Famasiala, Famchezo, Fautani nk

BAKITA J.jpg

 
Tunachokijua
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni Taasisi ya Umma chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo inasimamia shughuli za ukuzaji wa Kiswahili nchini na kuratibu maendeleo yake nchi za nje. Baraza liliundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 27 ya Mwaka 1967 na kufanyiwa marekebisho Mwaka 1983.

Famasiala, Famchezo, Fautani ni maneno ya misimu ambayo yamevumishwa na kutumiwa jamii.Maneno haya yameundwa yameundwa kwa ufupisho wa sentensi ambapo Famasiala ikisisima badala ya unafanya masihara?, Famchezo ikisimama badala ya unafanya mchecho?, na fautani ikisimama badala ya unafanya utani?

Baada ya kuwapo kwa uvumi kuwa BAKITA imeonya matumizi ya maneno Famasiala, famchezo na fautani, Jamiiforums ilifanya mazungumzo na BAKITA kupitia Mhariri mwandamizi wa baraza hilo, Oni Sihala ili kupata ukweli wa barua hiyo.

Akizungumzia barua hiyo, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Oni Sigala amesema

“Barua si ya kwetu BAKITA na hatukatai lugha za misimu kwa kuwa kwetu zina mchango katika ukuaji wa lugha.

“Hatujawahi kukataa wala kutoa onyo ikitokea kuna lugha za msimu zinazozungumzwa, watu wanaotengeneza barua za aina hiyo hatuwezi kuwashauri waache kwa kuwa wapo wanaofanya ili kujiongezea wafuasi kwenye kurasa zao.

“Ninachoweza kusema ni kuwa kama wanataka ufafanuzi wa lugha au maneno waje Baraza tutawapokea na kuwapa ushirikiano mzuri."


Hivyo kutokana na ufafanuzi huo kutokea BAKITA barua hiyo iliyosambaa katika mitandao mbalimbali ni uzushi
Hahahahaa ningeshangaa sana Kaoneka,Consolata na Oni sigala kupoteza muda kwa vitu vya kipuuzi.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom