Arusha: Mtoto adaiwa ‘kupooza’ mkono baada ya adhabu ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Miririni Wilaya ya Meru

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,326
5,499
MTOTO APOOZA MKONO.jpg
Mwalimu anayefahamika kwa jina la Nkya mtumishi katika Shule ya Msingi Miririni iliyopo Wilayani Meru Mkoani Arusha anatuhumiwa kufanya ukatili kwa Mwanafunzi ambao umesababisha mkono wa kulia wa mtoto 'kupooza' hasa sehemu ya vidole.

Mwanafunzi aliyejeruhiwa ametambuliwa kwa jina la Milcah Zakaria Mbise, kwa sasa anasoma darasa la 4, alifanyika ukatili huo mwishoni mwa Mwaka 2022.

Mama mzazi wa Milcah, Elimkunde amesema tukio hilo lilitokea Novemba 2022 na hadi sasa hali ya mwanaye haijatengemaa.

Mzazi huyo anasema hata alipoenda kushtaki kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Miririni hakupata msaada dhidi ya Mwalimu Nkya.

Mama mtu anasema “Siku ya tukio niliona watu wanamleta mwanagu akiwa hajitambui, alikuwa ameumia na afya yake ikaonekana kutokuwa sawa.

"Mtoto aliumia wakati amepewa adhabu na mwalimu wake shuleni, tukampaleka hospitali akapewa dawa ya kuchua tu, lakini tangu wakati huo hakuweza kufanya kazi kwa kutumia mkono huo kwa kuwa haukuwa na nguvu tena.

“Akashindwa kwenda shule kwa miezi mitatu, Walimu walipoona haonekani shuleni, wakanifuata na kutaka kunipeleka Polisi wakiamini nimemzuia mtoto kwenda shule, nikawaambia anaumwa na mkono tangu alipoumizwa na Mwalimu haufanyi kazi na hata vidole haviwezi kushika kalamu.

“Walimu wakalazimisha aendelee na shule akitumia mkono wa kushoto, anafanya hivyo lakini hawezi kuandika.”

Serikali za Mtaa
Kuhusu kama amefikisha suala lake Serikali za mtaa, mama mtu amesema “Balozi naye mtoto wake alipigwa shuleni akaharisha na kukojoa damu, Mwalimu aliyempiga mtoto wa Balozi amekimbia na hajarudi mpaka leo.”

Diwani
Diwani wa Miririni Kata ya Leguruki, Nathanael Sikawa amekiri kuifahamu shule husika na kudai kuwa hana taarifa juu ya tukio hilo.

UPDATES...
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima ameandika kwenye komenti za Instagram kupitia ukurasa wa JamiiForums kuwa anafuatilia suala hilo kwa ukaribu.
 
Ila walimu sometimes wanatoa adhabu kupitiliza kiwango, hatukatai ila kuna wakati wanazidisha mnoo.

Nimekumbuka O level, nikiwa 4m 3 kuna mwanafunzi alipigwa na makamu wa shule hadi mkono ulikua unalegea kwenye kiungio cha mkono, na hadi let yule mkono hauko vizuri km mwanzoo.

Walimu wapunguze adhabu kuzidi kiwango.
 
Kuna walimu makatili sana
 
Stress zao wanazihamishia kwa watoto
Wenyewe wanakuambia tz wasanii,watu wa mipira wanathaminiwa kuliko wao walimu

Ova
 
Back
Top Bottom