Anahitajika mtaalam wa Kutengeneza chakula cha mifugo.

 
Ukipata mtu Ali ye soma B.Sc Animal Science sua atakusaidia Zaidi
Sio kweli ,wewe umeongelea hivo Kwa ishu ya kujua animal nutrition,na hivo hata watu wa animal health and production ,Veterinary laboratory technology na hata biotechnology huwa wanasoma hio animal nutrition ,halafu kujua animal nutrition sio tiketi ya kuonekana kama kazi mtu ataiweza,Kwa sababu chakula kikitoka kwenye production kabla hakijaenda kwenye market lazima kifanyiwe quality assurance Kwa ajili ya kucheki ubora pamoja na usalama wake,so hapo lazima laboratory tests zifanyike kulingana na aina ya chakula,so unadhani hao watu wa animal science hizo laboratory test wanazijulia wapi maana hata kama kusoma wanasoma Kwa uchache sana
 
Tuna tegemea kuwa na Kiwanda kidogo cha kuzalisha chakula cha mifugo aina mbalimbali, tunahitaji mwenye ujuzi na awe na uzoefu huo kwa kazi husika.

Kwa yeyote mwenye ujuzi huo namkaribisha
Pm
au email; godfreycyp@yahoo.com
Kwanza nikupongeze Kwa hatua kubwa unayotegemea kupiga,Cha kushauri kama ndo kwanza unaanza usitake kuingia gharama ya kutafuta sijui mtaalamu wenye ujuzi na uzoefu Kwa sababu ni ngumu kumpata na vile vile unaweza ukampata lakini usidumu nae Kwa muda mrefu,unajua Kwa nini ,ni Kwa sababu viwanda vingi vidogo vinakuwaga havina good working environment Kwa ajili ya shughuli za kitaalamu namaanisha quality assurance Kwa kukosekana vitu kama feed glinder,nir feed analyzer,hot air oven,analytical balance n.k
So moja Kwa moja ujanja wanaotumiaga wamiliki wa viwanda vichanga ni kulipa hela Kwa ajili ya kufanyiwa quality assurance ,mfano Kwa dar sample nyingi za feed hupelekwa pale vetenari kwenye ofisi za maabara ya taifa ya wanyama(Tanzania veterinary laboratory agency(TVLA)) hata pia viwanda vikubwa kama falcon,hill feed,nutrifeed,silverland,interchick nk Kuna baadhi ya test wao wenyewe hushindwa kufanya kutokana na ukosefu wa vifaa mfano test kama ya kupima soya so huingia ubia na kampuni nyingine au huwa wanapeleka pale tvla

Vile vile hii kazi ni ngumu Kwa upande wa quality assurance Kwa viwanda vichanga Kwa sababu ya ukosefu wa Standard Operating Procedure(sop) Kwa maana hii ndo huwa inamuongoza mtaalamu wa maabara kuhusu test husika inafanyika vipi Kwa hatua zipi ,Kwa muda Gani na Kwa kutumia vifaa Gani na kemikali zipi.

So kama unaona sijui interchick,falcon,hill feed,silverland nk mfano wanazalisha starter ya kuku ambayo ipo Bora ujue haitokei Kwa bahati mbaya lazima kuwe na good manufacturing practise(GMP) na good laboratory practice(GLP) ndo mambo kama hayo ya sop yapo humo humo ,so sop ikiwepo hata akichukuliwa mtu asiye na uzoefu kazi anaweza kufanya kutokana na sop huwa inatoa mwongozo Kwa vitu vingi kama aina ya test,hatua za kufanya test,muda wa kukamilisha test,materials za kufanyia test n.k

Vile vile jambo lingine ambaló ni changamoto Kwa viwanda vichanga ni ukosefu wa formula za kutengenezea aina mbalimbali za vyakula ,Kwa sababu hata Kwa viwanda vikubwa kuhusu formula huwa wanafanya Siri sana,Sasa unakuta mtu kamwajiri mtaalamu kwenye kiwanda chake ambacho ni kichanga ,na mtaalamu akasema apewe muda wa kufanya test mbalimbali Ili apate formula sahihi ,huwa inashindikana Kwa sababu ya wamiliki kukosa uvumilivu na kutaka matokeo ya haraka
 
Mimi nahitaji kufungu duka la dawa za mifugo na chakula cha mifugo, nimfugaji wa muda mrefu wa kuku na bata na kuku katika small scale.
Nilikuwa naomba muongozo kuanzia kwenye Vibali, experience, changamoto, na mbinu.
Nipo dar
 
Sio kweli ,wewe umeongelea hivo Kwa ishu ya kujua animal nutrition,na hivo hata watu wa animal health and production ,Veterinary laboratory technology na hata biotechnology huwa wanasoma hio animal nutrition ,halafu kujua animal nutrition sio tiketi ya kuonekana kama kazi mtu ataiweza,Kwa sababu chakula kikitoka kwenye production kabla hakijaenda kwenye market lazima kifanyiwe quality assurance Kwa ajili ya kucheki ubora pamoja na usalama wake,so hapo lazima laboratory tests zifanyike kulingana na aina ya chakula,so unadhani hao watu wa animal science hizo laboratory test wanazijulia wapi maana hata kama kusoma wanasoma Kwa uchache sana
Haya umejionea au kuna mtu amekusimulia? Animal science wanaijua sana hiyo proximate analysis
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom