Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

Urafiki huja automatically tu mkuu na mnakuta mnashare interest au mnaviews za aina moja.

Ila kwa asilimia kubwa sana urafiki tulionao ni unafiki tu wa viwango vya juu, hakuna uhalisia, hao unaowaona watu wa karibu sana ndio maadui wa hatari mno. So ni kuwa makini tu na binadamu wote.

Ila sio vibaya kutafuta watu ambao mnashare interest mfano mnaweza kaa masaa kadhaa mkijadili mambo mbali mbali bila kuboreka na bado mkakutana tena wakati mwingine.
 
Mleta mada marafiki hawatafutwagi wanakujaga wenyewe,chamuhimu ni wewe kuhudhuria kwenye shughuli za majirani zako. Mfano misiba na sherehe au mambo ya kijamii halafu marafiki wa kweli utawapata kulingana na wewe ulivyo.
% kubwa ya marafiki wa mtaani huwa ni wanafki sana watakukera,we shirikiana nao kwenye mambo ya msingi.
 
Mleta mada marafiki hawatafutwagi wanakujaga wenyewe,chamuhimu ni wewe kuhudhuria kwenye shughuli za majirani zako. Mfano misiba na sherehe au mambo ya kijamii halafu marafiki wa kweli utawapata kulingana na wewe ulivyo.
% kubwa ya marafiki wa mtaani huwa ni wanafki sana watakukera,we shirikiana nao kwenye mambo ya msingi.
Huyu kajifanya nunda vile anajimudu sasa akili ndo zinamrudi afate huu ushauri utamfaa
 
Mi naona kama ndio yatakayonikuta mbeleni.
Napenda urafiki ila urafiki siuwezi.
Huwa nakuaga rafiki wa faida sana ila sasa unakuta mwenzangu nikimchunguza naona kama shobo zimezidi upande wangu.
Na hakuna kitu sikipendi kama kuwa faida anapata yeye/wao mimi faida sipati
Kingine watu wakikujua jua sana nalo ni tatizo! Heshima inaoungua sana
Kinachobaki unakua tu na wale watu ambao unafahamiana nao ila siku likikukuta jambo kwakweli hamna wa kukukimbilia.

Najiona ntakavyokua kama FINCH
Tatizo yaani watu wanapenda kufaidika wao tu...
Mimi ndo linalonishinda kwa kweli
Yaani ile mutual friendship sijawahi kukutana nayo..
Kuhusu shobo...mimi hainisumbui sanaa.
Napenda rafiki anaechangamka kunizidi..
Au tubalance shobo...yaani iwe equivalent flani hivi.
 
Huyu kajifanya nunda vile anajimudu sasa akili ndo zinamrudi afate huu ushauri utamfaa
Hamna sio ununda..
Unajua dunia ya sasa marafiki ni wachache haswaa marafiki wa kweli.
Iwe ndugu au majirani.
Watu wengi wanapenda kufaidika kwako laki ile urafiki wa kweliii ni nadra trust me.
Hivi unajua hata ndugu zako kama huna chochote hawakutafuti?
 
Good morning jf....
Tusio na marafiki tukutane hapa

Kuna hili swala nimekua nikijiuliza hivi karibuni, baada ya kuona sasa uzee umeanza kupiga hodi. Najiona umri umetangulia mbele halafu maisha ni kama nayaacha nyuma, ni kama naishi tofauti na umri wangu. Nimesogea umri wa kuozesha, kuondokewa na wapendwa (waliozeeka) na kukutana na mambo mengi ambayo nadhani yanahitaji watu....ila bahati mbaya sasa hao watu ndio sina.

Natamani kuwa na marafiki kuwa na watu, watu wa faida, watu ambao wanaweza kushare ramani za maisha, watu ambao tunaweza kupanga safari kwenda vituo vya wahitaji tukawape misaada, watu ambao nikihitaji kumwagilia moyo najua wapo, watu ambao nikikwama najua watakuwepo, kina mama wenzangu huwa wana vyama umuhimu wa vyama naujua ila mi hata chama sijawahi kuwa nacho....naishi mwenyewe mwenyewe tu hadi nawaza si nitakosa wa kunizika mie mwisho nizikwe na manispaa.

Wenye marafiki mnawapataje???
 
Mimi nimehamia mtaa mpya nimejenga huku cha kwanza nimeingia Jumuiya yani hii ndo kila kitu kwangu maana tunashirikiana kwny sala na mambo mengi ya kijamii, nimejiunga na chama cha ujirani, nimejiunga na chama cha watu wa kabila letu wa eneo ninaloishi.

Humo nimepata dada nimepata marafiki ambao we can share nimepata mama watu wazima wenye hekima n.k so nimejenga rafiki na watu karibu yangu achilia wale wengine kibaoo tulomaliza nao shule, maana wote hao tuna magroup yetu kuanzia shule ya msingi, o level a level hadi chuo so hao wote ni marafiki. Humo lazima kuna close friends wawepo. Jaribu kujichanganya maisha ni kujichanganya na watu ndo mtaji.
 
Yan just like me, marafiki zangu nlonao n wale nlomaliza nao chuo, hatunaga story Zaid ya kuview status, huku mtaani Nako Sina rafiki n mm na kazi zangu basi hata ikitokea shughuli Sina wakuongozana nae, ni tabu kweli kweli nawaza hata siku nikiwa nshughuli nani atanisaidia so sad, and I don't know how to get out this
 
Kuna kitu tunaita "network building" mara nyingi uandaliwa na balozi za nchi za kigeni kama USA, Denmark, Sweden,Japan,Canada, Japan, France & Germany etc japo baadhi unalipia around $30, 40,50 japo nyingine ni bure mara nyingi zinafanyikia Serena, Southern Sun Hotel,Four Season, Kempinsky na Cape Town fish market muda wa jioni baada ya kazi hasa ijumaa/alhamisi zinachukua lisaa 1 mpaka 2 hii utoa fursa ya wageni kupata marafiki na wenyeji kubadilisha mawazo.

Uwa zinaambatana na bites na vinywaji laini ni network building ambazo hamjuani unaenda kwa ajili ya kujuana na watu wapya, ni nzuri na zinakupa exposure kwakuwa hutaki marafiki wasioleweka zinakufaa, ikiwa utafeli/kuogopa kwenda kuna hizi nyingine ila nzuri kwa vijana zaidi hizi balozi za Nordic Countries,UK,France,Swiss,Germany etc huwa zinaandaa cinema kila alhamisi na huzialika balozi nyingine ni free entrance kwa wale wapenda wazungu zinawafaa kwasababu whites wanakuwa wengi mno na wanapenda watu weusi hapo ujanja wako tu wa kupata rafiki au hata mpenzi pia.
Nimehudhuria sana nimejifunza mengi.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mdada huwa napenda ile life style, weekends hupost status wapo kwenye coaster wanaenda kutembelea yatima yani wanavibe hao, usiku wapo pengine wanamwagilia moyo....napenda kwakweli ila mi sina
The way unavyoongea iyo "napenda kwakweli Ila mi Sina"😂

Nimemkumbuka My Young Sister na kile kisauti chake kipindi kile anakuwa Daah!! Aliwaona wenzie wamependeza akapenda gauni la mmoja wao ndo akaniambia Ivo Ile gauni naipenda Kaka Ila me Sina😍😍

Ila suala la kuwa na marafiki ni the way unavyojiweka, inaonekana ww ni mgumu kuchangamana na watu. Sio mwepesi kujenga mazoea na watu.

Mwenzio kila weekend nakaribishwa kwa watu. Hakuna kitu kizuri Kama kuishi vizuri na jamii inayokuzunguka.

Mie nilitengeneza marafiki kutokana na kuwahudumia wateja vizuri kazini, achana na staff wa kazini maana wale wakikuzoea Sana heshima inashuka.

Nilikuwa najitahidi kutoa huduma vizuri, wengi hushukuru ndo mwanzo wa kufahamiana na kualikana.
 
Back
Top Bottom