Akaninunulia Konyagi, nilipolewa akatembea na mke wangu. Nikazinduka na kumkuta jamaa kiunoni

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
3,511
5,887
Huyu rafiki yangu nilimtembelea nyumbani kwake Dar es salaam. Mimi nilikuwa nafanya kazi Mtwara na nilikuja Dar ili niunganishe usafiri wa kwenda kwetu Musoma.

Nyumbani kwa rafiki yangu tulipokelewa vizuri sana mimi na mke wangu. Bahati mbaya tulikuta mke wa jamaa kaenda kwao kwa ajili ya kujifungua. Jamaa akatuandalia dinner maridhawa, nyama choma na pombe za kutosha

Mimi huwa sinywi konyagi, nimezoea Smirnoff, lakini nikanywa kwa heshima ya mshikaji. Kumbe muda wote tukila na kunywa jamaa anamchombeza mke wangu

Ukafika muda wa kwenda kulala, tukaingia chumbani mimi na mke wangu, tukalala

Katikati ya usiku nikashtuka mke hayupo, chumbani ni self contained, nikaangalia chooni, kuna giza taa haijawashwa.
Nikawasha taa sikumkuta, nikaanza kunyata kuelekea chumbani kwa mshikaji.

Nikasikia sauti ya mke wangu akilalamika kwa mahaba, nikafungua mlango kwa nguvu na kuwakuta wakiivunja amri ya USIZINI.

Nikawainua wote wawili na kuanza kuwapiga, nilimpiga sana mshikaji hadi nikamuumua jicho na kumng'oa jino.

Nikamuacha mke wangu hapo, nikabeba bag langu na kuhamia guest. Asubuhi nikapanda ndege na kuelekea Mwanza.

Wito wangu kwenu wana JamiiForums, ukiwa na mkeo usifikie kwa mshikaji wala ndugu, fikieni hotelini.

Mshikaji kavunja ndoa yangu.
 
Mhh!!
tapatalk_1571512207895.jpeg
 
Back
Top Bottom