Adhabu ya viboko kidato cha tano na sita ifutwe

Ni kwamba hawawezi jiongoza au hawajaelekezwa?
Hawawezi jiongoza, Kwamba Ukiingia darasani achana na Simu sikiliza lecture kama huwezi toka nje hii haihitaji kuelekezwa.

Ukiwa kazini Basi fanya kazi sio usubiri due date uanze kuomba msaada au kutoa kazi mbovu.
Huko ni kushindwa kujiongoza, sio kutokuelekezwa.
 
Pole sana aisee,, nakumbuka mwishoni ilibidi nifake cheti cha hospitali kwamba nina matatizo ya mifupa ili nisichapwe, bila hivyo ningerudi home mikono imevunjika
Pole sana maana hiyo yenu ilikuwa imezidi Ila safi sana kwa kujiongeza 👏🏾👏🏾

Ila waalimu wa shule zetu hiziiiii sijui ni stress za kipato. Ila tumekua na ishabaki story na hilo ndilo la msingi
 
Tulifungiwa kwenye fizikia praki so Kuna Wana walitoka wakaenda town kufuata hela kwa emo mie nilizunguka zunguka hapo hapo school Mana hatukuwekewa mlinzi.jamaawa town ikabidi apige c wakati b ilikuwa simple
🤓🤓🤓🤓🤓🤓 daaah nidhamu ni muhimu mkuu oooh
 
Tatizo malezi yetu na yao tofauti,wao wanatambua umuhimu wa shule, elimu.
Sisi hatujui umuhimu au faida ya elimu na shule
Na kweli, ndio maana unakuta mtoto nyumbani anapigwa badala ya kufundishwa mema, halafu shule nayo hivyo hivyo
Ulaya pia watoto watukutu lakini wana jela zao kama wakiharibu zaidi
Ila shule hawapigwi wakiwashinda kabisa hufukuzwa
 
😁😁😁 hapana mkuu

Nilikuwa moja ya wale wanafunzi ambapo zisipotokea fimbo za jumla, ningeweza kukaa hata wiki tatu bila kuadhibiwa . Ila mwalimu akitaka kunionea lazma nimbadilikie.

Uzuri hata yeye akiingia na mimi staff lazma watu wamshangae kuwa huyu jombaa kafanyaje. Hiyo pia ilinisaidia kupata utetezi wa waalimu 😁
Toka hapo uliwahi kumbishia mwalimu..
Bado ulikua na karoho ka uhuni mkuu.
Unajua mwanafunzi kama ukiwa vizuri class basi zarau zinazidi sasa hiyo haitakiwi mkuu 🤓🤓🤓🙌🙌🙌🙌
 
Na kweli, ndio maana unakuta mtoto nyumbani anapigwa badala ya kufundishwa mema, halafu shule nayo hivyo hivyo
Ulaya pia watoto watukutu lakini wana jela zao kama wakiharibu zaidi
Ila shule hawapigwi wakiwashinda kabisa hufukuzwa
Tatizo la Tanzania na Afrika ni umasikini uliovuka mipaka ya ubinadamu.
 
Pole sana maana hiyo yenu ilikuwa imezidi Ila safi sana kwa kujiongeza 👏🏾👏🏾

Ila waalimu wa shule zetu hiziiiii sijui ni stress za kipato. Ila tumekua na ishabaki story na hilo ndilo la msingi
Ilo ndo la msingi
 
Pole sana maana hiyo yenu ilikuwa imezidi Ila safi sana kwa kujiongeza

Ila waalimu wa shule zetu hiziiiii sijui ni stress za kipato. Ila tumekua na ishabaki story na hilo ndilo la msingi
Hizo stori inabidi kizazi kijacho wasisimulie stori za kufanyiwa ukatili shuleni

Tangu miaka ya 70 tunachapana viboko mpaka leo hatushtuki tuu
 
Prof Mkenda unapofanya mabadiliko ya mitaala na mambo mengineyo basi na adhabu ya viboko kwa kidato cha tano na sita ifutwe maana wale ni watu wazima.

Haiwezekani wanamaliza form iv pamoja, mmoja anaenda chuo cha kati (anaachana na mambo ya viboko) mwezake wa umri ule ule anayeenda form five anaenda kukutana na viboko.

Viboko ni adhabu ya kizamani sana hasa kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.

Wanafunzi wa Vi ni watu wanaojitambua na kujua ni nini wanafanya kama ilivyo wanafunzi wa vyuo vya kati ambao hawachapwi viboko.

Na nyie walimu, ingia darasani fundisha achana na kuchapa viboko watu wazima wa form v$vi, fanyeni kama walimu wa vyuo vya kati

Wazo zuri sana ILA muhimu zaidi ni kujua kuwa, adhabu hutokana na tabia au matendo ya muhusika
Kama hao A- Level wata achana na tabia za kufanya mambo ya hovyo kama vile wanafunzi wa darasa la saba au form one wala hakutakuwa na mtu wa kufikiria kuwapa hizo adhabu.
Pamoja kuwa siungi mkono hiyo adhabu ILA hao wanafunzi nao wanatakiwa wajitafakari!
 
Hizo stori inabidi kizazi kijacho wasisimulie stori za kufanyiwa ukatili shuleni

Tangu miaka ya 70 tunachapana viboko mpaka leo hatushtuki tuu
Tupo enzi za manamba mkuu bola kiboko hatuendi. Ni aibu sana
 
Mtu mzima ukiwa hueleweki uchapwe tu hata kama una midevu mingi kama savimbi ona jela wanavyofyatua viboko
 
Nashauri profesa Mkenda apeleke viboko hadi vyuo vikuuu

Kure watu ni wajinga sana
Nashauri yeye mwenyewe na maprofesa wenzake wafungiwe mahali wale fimbo za uhakika na washike masikio na warushwe kichura kila siku mpaka pale watakapovumbua vitu 100

Wanajiita wataalamu hata valve hawawezi kutengeneza
Watoto wanapigwa na hatuoni wanachofanya hata wakikua huoni mzazi anajisifia kuwa mtoto wangu katengeneza hiki zaidi ya kutengeneza Ugali
 
Viboko tunavyo tangu zamani ila havisaidii kitu zaidi ya ukatili tuu na kutengenezeana chuki
 
Wazo zuri sana ILA muhimu zaidi ni kujua kuwa, adhabu hutokana na tabia au matendo ya muhusika
Kama hao A- Level wata achana na tabia za kufanya mambo ya hovyo kama vile wanafunzi wa darasa la saba au form one wala hakutakuwa na mtu wa kufikiria kuwapa hizo adhabu.
Pamoja kuwa siungi mkono hiyo adhabu ILA hao wanafunzi nao wanatakiwa wajitafakari!
Basi tungeweka sasa, wafanyakazi ukichelewa kazini upigwe viboko, mkeo akikosea umpige viboko nk sasa kwanini viboko viwe kwa wanafunzi tuu
 
kuna mwalimu alinipiga form six, ati nimechelewa kufika assemble, nilikuwa mtu maarufu shuleni, mwenye akili darasani, kiongozi wa wenzangu, akaamua kunidhalilisha mbele ya wanafunzi, alinichapa fimbo kali sana. nimekuja kukutana naye amestaafu amechoka balaa.

Sitarudisha baya ila sikumpa tip yeyote. though hata yeye hakuomba na alikumbuka kuwa alinipiga vibaya hivyo hakutegemea chochote. waalimu mue makini, imagine hapo ningekuwa mtu mbaya, nikawa boss, mtoto wake akaja kuomba kazi kwangu au akawa chini yangu, nisingelipiza kisasi kwa mtoto wake?

Na wanafunzi huwa wanakumbuka zaidi mabaya waliyofanyiwa na waalimu wao kuliko waalimu kukumbuka mambaya waliyowafanyia wanafunzi wao.
Hukukosea au ulikosea?
 
Mtoto wako wa 17yrs unampiga viboko?
Haki hata wa 30yrs namtandika. Ushindwe kujisimamia halafu useme you have grown past childish age. Huoni ndivyo viongozi wetu wanafanya upumbavu kwasababu wanasema they have grown past the normal citizens au the law. Utachapwa bila kosa.
 
Back
Top Bottom