Achana na uongo wa kujifunza kwa waliofeli, jifunze kwa waliofaulu kihalali tu

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,718
15,695
Hepuka ushauri na kujifunza kwa watu ambao wanafeli mfululizo na muda wote wanapambana kifedha bila mafanikio.

Jifunze kwa watu wanaofaulu kihalali, watu wambao wamejijengea mifumo yenye kuleta ufaulu hata kama hawajasoma. Jifunze nidhamu zao, lugha zao za mwili, namna wanavyoendesha mambo, angalia mifumo yao iige kwa haraka.

Kwa waliofeli kwa consistency ( kimuendelezo) labda ujifunze jinsi ya kuwakwepa na kuepuka mifumo na tabia zao.


Ni hayo tu.
 
Kama issue ni kujifunza, nadhani pande zote mbili wana mengi ya kukufundisha.
Ni njia ndefu sana. Hapa namaanisha mwenye mwendelezo wa kufeli, sio mwenye historia ya kufeli na kuinuka.

Kuna watu wao kila wanachofanya kinafeli. Hawa ndio nawazungumzia, ukiiga haww unaweza kujikuta umeiga pattern ambayo itakusababishia kuchelewa kufaulu.
 
Ni njia ndefu sana. Hapa namaanisha mwenye mwendelezo wa kufeli, sio mwenye historia ya kufeli na kuinuka.

Kuna watu wao kila wanachofanya kinafeli. Hawa ndio nawazungumzia, ukiiga haww unaweza kujikuta umeiga pattern ambayo itakusababishia kuchelewa kufaulu.
Ulichokiongea nakuelewa, ila umaliziaji wako ndio naukataa.

Kujifunza na kuiga ni vitu viwili tofauti (learning and copying). Anayeiga maana yake hajajifunza chochote, na huyo kupotea ni sio jambo la ajabu. Kama lengo ni kuwa Bora, basi sharti tujifunze. Na kwenye kujifunza, tunahitaji pande zote mbili failures na waliofanikiwa.
 
Siri ya mafanikio ya mtu ni kiza kinene wengine wakikuambia nini kafanya kufika pale unaweza kusema hivi shetani tunae mkemea misikitini na makanisani kumbe ni huyu.Mm sitakagi kujifunza walifanya nn wakatoboa mm napenda mtu wa kunipa deal napambana kIvyangu nitoboe
 
Wewe fanikiwa tu mkuu, mambo ya kusema sijui kihalali hayo waachie wapiga projo!
Cha msingi ni kufanikiwa tu basi
 
Ili uwe imara ni muhimu ujifunze kutoka kwa pande zote.Ni muhimu ujifunze kwanini watu fulani hawafanikiwi na wengine wanafanikiwa ili uweze kufanya kinachostahili.

Kujifunza kutoka upande mmoja pekeake ni rahisi kutopata mafanikio thabiti.
 
Back
Top Bottom