2025 patachimbika kwa moto huu, CHADEMA muwe na mipango hii ya kuingia Ikulu

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
349
951
Naona moto wa Chadema (Tundu Lissu) umewaka Tanzania nzima. Naona huu moto ni kama ule wa vijana wa Senegal Marais wa sasa (Rais na makamo wake) walivyo uwasha moto mpaka wakaingia ikulu ya Senegal.
Cha kufanya CHADEMA ni kutokulaza damu kuanzia sasa hivi mpaka uchaguzi mkuu 2025.

1. Maandamano yaendelee nchi nzima mkigawana mikoa.
2. Hoja ngumu ziendelee kutolewa mikutanoni na kwenye media mbalimbali hasa online TV kwa sababu hakuna TV iliyo huru kuwaunga mkono kwa kuogopa pini kutokana wizarani.

3. Mtangazie umma na polisi kwamba kura za uchaguzi wa wananchi zitalindwa na wananchi wenyewe kwa sababu katiba haijazuia wananchi kulinda kura zao.

4. Tume ihakikishe kila chumba cha kupigia kura kuna kuwa na wakala wa vyama kwa ajili ya kuhesabu kura na kuhakikisha usahihi wa kura zote halali.
Mizengwe kwa mawakala au ikijulikana kwamba kituo fulani hakukuwa na wakala wa chama, kura katika hicho kituo hazitatumbulika.

5. Kuwe na wenyeviti wa chama kuanzia ngazi ya mtaa, Tanzania nzima na mawasiliano yao yawe kwenye database makao makuu. Wenyeviti hawa watoe taarifa mara moja makao makuu kama kuna hujuma yoyote inatokea kwenye vituo vya kupigia kura ili viongozi makao makuu watoe tamko la kukemea kwa nguvu muda huo huo.

6. Mfungue kituo cha kuhesabu na kujumlisha kura zote kutoka kwenye kila kituo Tanzania nzima. Na muwatangazie Tume ya uchaguzi kwamba mahesabu yao yawe sawa na yenu kichume na hapo watakuwa wamechochea ukosefu wa amani katika nchi. Katiba haijazuia chama kuwa na tume yake kujumlisha kura zake kutoka kwa mawakala wao nchi nzima.

Hakuna muda mwepesi wa Upinzani kuingia ikulu kama 2025 endapo raisi aliyepo atagombea tena.
Tundu Lissu una kitu naona utatufaa Tanzania kupata unafuu kwenye masuala ya sheria kwa sababu wewe ni mbobevu kwenye upande huo wa sheria.

Sheria zetu ni mbovu zinazokandamiza raia wa kawaida huku wezi na wabadhirifu zikiwaacha pasipo kuwagusa. Tazama wezi wa ripoti za CAG bado wapo wanadunda huku wameiba pesa ambazo zingeweza kusaidia wananchi kupata hata mikopo banki kwa riba nafuu chini ya 10% wakaingiza kwenye biashara na kukuza uchumi wa nchi.

Sheria zetu ni mbovu zinawapa mamlaka wawekezaji uchwara wa kigeni kudai fidia ya mabilioni wanaposhindwa kufanya kazi.
 
Ahahahahaha! Mwaka 2024 CCM itashinda kwa kishindo Serikali za Mtaa na 2025 itashinda tena kwa kishindo Uchaguzi Mkuu. Tanzania hakuna chama cha Siasa zaidi ya CCM!
 
Mafisadi wanamuogopa sana huyu Lissu (zaid ya Magufuli) maana wanajua moto wake akiingia kule kwenye milango ya mahala patakatifu. Atakuwa ni moto wa kuotea mbali na Nchi itakuwa moto moto sana... sijui kama watawala wako tayari kuachia moto moto mdomoni ili hali sasa hivi hata kumeza maneno yake wanakwama
 
Chadema haiwezi kushinda japo mazingira yapo wazi kwa chama makini kushinda. Unahitaji muungano kama ule wa ukawa pia kuwahusisha CCM ambao hawapendezwi nchi inavyoendeshwa, kanda ya ziwa na mashabiki wa JPM. Washabiki wa JPM ndio walio wengi wa Watanzania inabidi kuwafikia na kuwaweka karibu ili kushinda.

Sio kila siku kumkandia JPM. Hiyo sera haitawasaidia CDM. Watashinda viti vya ubunge labda 30 hadi 60, kura labda milioni 4, 5, 6. Hawatashinda kuchukua serikali unless wafanye kama Ruto coalition of the willing, wakiweka chuki binafsi pembeni na kushirikiana na Watanzania wote kuiondoa CCM madarakani.
 
Ahahahahaha! Mwaka 2024 CCM itashinda kwa kishindo Serikali za Mtaa na 2025 itashinda tena kwa kishindo Uchaguzi Mkuu. Tanzania hakuna chama cha Siasa zaidi ya CCM!
Akili mgando pamoja na uozo wote huu bado unashabikia CCM kweli? Au nawe ni sehemu ya wanufaika msiokuwa hata na chembe ya aibu.
 
Ahahahahaha! Mwaka 2024 CCM itashinda kwa kishindo Serikali za Mtaa na 2025 itashinda tena kwa kishindo Uchaguzi Mkuu. Tanzania hakuna chama cha Siasa zaidi ya CCM!
Nafikiri iwapo wapinzani wataendelea kupewa uhuru ulio katika sheria zinazoongoza siasa kama kuandamana na kunadi sera zao majukwaani kwa uhuru, kashfa na matusi basi kuna viti vya ubunge watapata iwapo kura hazitaibwa. Raia wengi wana hali ngumu na kuna hoja zingine za wapinzani zitawaingia na wataona bora wawajaribu kwenye ubunge ili kupata nafuu ya maisha.

Ila katika uchaguzi wa Rais, muda wa Rais kutoka upinzani bado haujafika sababu watanzania wanaamini zaidi katika usalama,utulivu na amani kuliko maendeleo, ni kama wamekubali maisha ya kuwa maskini bila kujua sirikali ina effect katika maisha wanayoishi. Mfano, raia wa Tanzania wanaweza kutajirika haraka sana iwapo mikoa yote itaunganishwa kwa usafiri rahisi wa reli na kuwepo umeme usiokatika mwaka mzima, this is a reality in Europe.
 
Back
Top Bottom