Kwa sheria hii ya Uchaguzi na tume hii ni wazi kwamba uchaguzi itakumbwa na machafuko

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
62
1,246
๐—ž๐˜„๐—ฎ ๐˜€๐—ต๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ฎ ๐—ต๐—ถ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—จ๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ด๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐˜๐˜‚๐—บ๐—ฒ ๐—ต๐—ถ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—จ๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ด๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐—ป๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐˜‡๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ ๐˜‚๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ด๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐—บ๐—ธ๐˜‚๐˜‚ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฑ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐—ธ๐˜‚๐—บ๐—ฏ๐˜„๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ณ๐˜‚๐—ธ๐—ผ.

Nimemaliza kusoma sheria namba 02 ya mwaka 2024 inayoanzisha muundo wa Tume ya Uchaguzi; na nimemaliza kusoma sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani namba 01 ya mwaka 2024. Nilichokiona ni majanga matupu na hofu ya watawala.

1. Kwanza kabisa ukisoma sheria no.01/2024 inayounda Tume ya Uchaguzi inayodaiwa ni huru imeweka wazi kwamba Mwenyekiti wa tume, makamu wake, mkurugenzi wa tume watateuliwa na Rais ambaye ni mmoja wa wagombea katika uchaguzi utakaosimamiwa na hawa wateuliwa.

2. Wajumbe watano wanaounda tume hiyo nao watateuliwa na Rais ambaye ni mgombea kwenye uchaguzi ambao utasimamiwa na wajumbe hawa atakaowateuwa. Sijui kwanini waliingiza neno Tume Huru katika sheria hii wakati mmoja wa wagombea ndiye amepewa mamlaka ya kuteuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Ukiachana na sheria ya muundo wa tume ya uchaguzi bado kuna majanga mengine kwenye sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

1. Kifungu cha 36 cha sheria hiyo kinampa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kuweka pingamizi na kumuondoa mgombea yoyote anayeshiriki uchaguzi. Kumbuka kwamba kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa kifungu cha 4 na cha 5 kinachoainisha majukumu ya msajili wa vyama vya siasa hakuna sehemu hata moja inayompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kuondoa wagombea kwenye chaguzi isipokuwa kusajili vyama, kuvilea, kusimamia chaguzi za ndani, kugawa ruzuku n.k.

2. Kifungu cha 37 - (3) Kinampa mamlaka pia mwanasheria mkuu wa serikali kuweka pingamizi kwa mgombea yoyote na mgombea huyo akaondolewa. Sasa kama mnavyojua ni kwamba mwanasheria mkuu wa serikali ana maslahi ya moja kwa moja na mmoja wa wagombea Urais hasa Rais anayegombea kwa muhura wake wa pili, hivyo kuweka pingamizi kunaweza kutafsiriwa kama ametumwa na Rais kwa mlango wa nyuma.

3. Kifungu cha 54-(1),(2) na kifungu cha 38-(1),(2) kinaruhusu tume kuengua wagombea ambao wamewekewa mapingamizi na mwanasheria mkuu au msajili na tume ikabakiza mgombea mmoja na mgombea huyo mmoja akapigiwa kura za ndiyo au hapana kama wakati wa Nyerere na chama kimoja.

4. Kifungu cha 85-(2)-(m), kifungu cha 94 - (1)-(e), kifungu cha 103 -(1)-(h) na kifungu cha 104 - (1)-(h) kwa pamoja vifungu hivi vinaruhusu askari polisi kuwepo ndani ya vituo vya kupigia kura wakati wa zoezi la kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo. Kumbukeni hapo awali sheria ilikuwa hairuhusu askari kuwepo ndani ya chumba cha kupigia kura isipokuwa nje kwa ajili ya kuimalisha usalama. Lakini bado askari polisi wengi waliingia ndani ya vituo vya kupigia kura na kuingiza kura feki wakati mwingine kutoa mawakala wa upinzani. Sasa sheria hii imehalalisha wao kuwepo ndani ya vituo na sio nje tena kama mwanzo.

5.Kifungu cha 92 - (2) kinaipa mamlaka Tume ya Uchaguzi, Mkurugenzi wa Uchaguzi na msimamizi wa Uchaguzi kwenda kuhesabia kura mahali pengine endapo wataona kituo kilichotumika kupigia kura ni finyu au si salama. Mfano msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya anaweza kusema Mbeya si salama kuhesabia na kujumlishia kura na akaaamua kuhamishia kazi hiyo Dodoma.

Sasa kwa mazingira haya kuna uchaguzi huru na haki kuanzia muundo wa tume yenyewe mpaka sheria inayosimamia uchaguzi? Wananchi watakubali kuwa Mbuzi wa kafala kama walivyofanyiwa 2019 na 2020? Kwa mateso waliyopitia wananchi kwa hii miaka mitano watakubali tena kuchezewa sharubu na hawa vibaka walioko serikalini ambao wengi wao ndio viongozi?

Binafsi nayaona machafuko makubwa ambayo pengine serikali inaweza kuanguka. Naona sasa itakuwa zamu ya viongozi wa serikali kukimbia nchi badala ya wapinzani.

Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu
 
Attachments

  • Screenshot_20240401-113812_1.jpg
    Screenshot_20240401-113812_1.jpg
    86.9 KB · Views: 2
Mdude hatuna uchaguzi tanzania yaani wanafanya kiini macho ili kupata misaada ya wazungu!!!! Fikiria uchaguzi ni wa raia lakini polisi anaingia ndani ya chumba Cha upigaji kura kufanya nini? Mkwe wa rais ndie anayepa watu wa uchaguzi yaani ni uhuni tu
 
Naunga mkono hoja
 
Samia anaweza kuwa chanzo cha maafa makubwa yatakayoikumba Tanzania kwa kufanyia mzaha suala la katiba mpya! Atakuja gundua kuwa katiba si kitabu kama alivyosema bali ni uhai wa Taifa!
 
Yatachafuka makoti yako hayo mekundu kama mganga wa kienyeji
 
Samia anaweza kuwa chanzo cha maafa makubwa yatakayoikumba Tanzania kwa kufanyia mzaha suala la katiba mpya! Atakuja gundua kuwa katiba si kitabu kama alivyosema bali ni uhai wa Taifa!
Hawezi pitisha katiba mpya kabla hajaingia mikataba ya milele ambayo itamnufaisha mile na kizazi chake!!Katiba mpya itambana sana!
 
๐—ž๐˜„๐—ฎ ๐˜€๐—ต๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ฎ ๐—ต๐—ถ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—จ๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ด๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐˜๐˜‚๐—บ๐—ฒ ๐—ต๐—ถ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—จ๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ด๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐—ป๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐˜‡๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ ๐˜‚๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ด๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐—บ๐—ธ๐˜‚๐˜‚ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฑ ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐—ธ๐˜‚๐—บ๐—ฏ๐˜„๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ณ๐˜‚๐—ธ๐—ผ.

Nimemaliza kusoma sheria namba 02 ya mwaka 2024 inayoanzisha muundo wa Tume ya Uchaguzi; na nimemaliza kusoma sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani namba 01 ya mwaka 2024. Nilichokiona ni majanga matupu na hofu ya watawala.

1. Kwanza kabisa ukisoma sheria no.01/2024 inayounda Tume ya Uchaguzi inayodaiwa ni huru imeweka wazi kwamba Mwenyekiti wa tume, makamu wake, mkurugenzi wa tume watateuliwa na Rais ambaye ni mmoja wa wagombea katika uchaguzi utakaosimamiwa na hawa wateuliwa.

2. Wajumbe watano wanaounda tume hiyo nao watateuliwa na Rais ambaye ni mgombea kwenye uchaguzi ambao utasimamiwa na wajumbe hawa atakaowateuwa. Sijui kwanini waliingiza neno Tume Huru katika sheria hii wakati mmoja wa wagombea ndiye amepewa mamlaka ya kuteuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Ukiachana na sheria ya muundo wa tume ya uchaguzi bado kuna majanga mengine kwenye sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

1. Kifungu cha 36 cha sheria hiyo kinampa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kuweka pingamizi na kumuondoa mgombea yoyote anayeshiriki uchaguzi. Kumbuka kwamba kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa kifungu cha 4 na cha 5 kinachoainisha majukumu ya msajili wa vyama vya siasa hakuna sehemu hata moja inayompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kuondoa wagombea kwenye chaguzi isipokuwa kusajili vyama, kuvilea, kusimamia chaguzi za ndani, kugawa ruzuku n.k.

2. Kifungu cha 37 - (3) Kinampa mamlaka pia mwanasheria mkuu wa serikali kuweka pingamizi kwa mgombea yoyote na mgombea huyo akaondolewa. Sasa kama mnavyojua ni kwamba mwanasheria mkuu wa serikali ana maslahi ya moja kwa moja na mmoja wa wagombea Urais hasa Rais anayegombea kwa muhura wake wa pili, hivyo kuweka pingamizi kunaweza kutafsiriwa kama ametumwa na Rais kwa mlango wa nyuma.

3. Kifungu cha 54-(1),(2) na kifungu cha 38-(1),(2) kinaruhusu tume kuengua wagombea ambao wamewekewa mapingamizi na mwanasheria mkuu au msajili na tume ikabakiza mgombea mmoja na mgombea huyo mmoja akapigiwa kura za ndiyo au hapana kama wakati wa Nyerere na chama kimoja.

4. Kifungu cha 85-(2)-(m), kifungu cha 94 - (1)-(e), kifungu cha 103 -(1)-(h) na kifungu cha 104 - (1)-(h) kwa pamoja vifungu hivi vinaruhusu askari polisi kuwepo ndani ya vituo vya kupigia kura wakati wa zoezi la kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo. Kumbukeni hapo awali sheria ilikuwa hairuhusu askari kuwepo ndani ya chumba cha kupigia kura isipokuwa nje kwa ajili ya kuimalisha usalama. Lakini bado askari polisi wengi waliingia ndani ya vituo vya kupigia kura na kuingiza kura feki wakati mwingine kutoa mawakala wa upinzani. Sasa sheria hii imehalalisha wao kuwepo ndani ya vituo na sio nje tena kama mwanzo.

5.Kifungu cha 92 - (2) kinaipa mamlaka Tume ya Uchaguzi, Mkurugenzi wa Uchaguzi na msimamizi wa Uchaguzi kwenda kuhesabia kura mahali pengine endapo wataona kituo kilichotumika kupigia kura ni finyu au si salama. Mfano msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya anaweza kusema Mbeya si salama kuhesabia na kujumlishia kura na akaaamua kuhamishia kazi hiyo Dodoma.

Sasa kwa mazingira haya kuna uchaguzi huru na haki kuanzia muundo wa tume yenyewe mpaka sheria inayosimamia uchaguzi? Wananchi watakubali kuwa Mbuzi wa kafala kama walivyofanyiwa 2019 na 2020? Kwa mateso waliyopitia wananchi kwa hii miaka mitano watakubali tena kuchezewa sharubu na hawa vibaka walioko serikalini ambao wengi wao ndio viongozi?

Binafsi nayaona machafuko makubwa ambayo pengine serikali inaweza kuanguka. Naona sasa itakuwa zamu ya viongozi wa serikali kukimbia nchi badala ya wapinzani.

Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu
Mdude acheni porojo za kutafuta visingizio,,fanyeni kazi kuwaokoa watanzania walio wengi. Mpaka sasa wapinzani hawajui nani atagimbea Urais na mikakati haipo kabisa. Nchi hii itaendelea kutawaliwa na maccm mpaka YESU arudi. Machafuko hayawezi kutokea kama mpinzani hajapigiwa kura za kutosha na ikaonekana kweli kashinda
 
Back
Top Bottom