Umeongea la maana sana ni kweli wanaume tunalinga sana tukipendwa na mademu wa kawaidaWanaume mara zote tunashauriwa kuoa au kuingia kwenye mahusiano na wanawake wanaotupenda, shida inakuja mwanamke anakupenda ila kwa kuwa hana sura nzuri ya kuvutia au hajajaliwa tako basi tunaamua kuwatolea nje, matokeo yake tunaishia kuwapenda wanawake tunaowapenda lakini wao hawatupendi.
Ndio hao kila kukicha wanatupiga mizinga na vituko havikomi maana wanajua tumeshapenda hatuna cha kufanya zaidi ya kutimiza yale wanayoyataka wao.
Mwanamke anayekupenda kwa dhati hata mia yako hatahangaika nayo labda wewe kama mwanaume uwajibike kama mwanaume lakini hawezi kukupiga mizinga isiyoeleweka , mwanamke asiyekupenda hawezi kuacha kukupiga mzinga na utakuta mwanamke huyohuyo anayekupiga mzinga ana mwanaume anayempenda na hamuombi hata mia.