Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere akisoma ripoti ya ofisi yake ya Mwaka 2024/2025, Machi 30, 2026 amesema alibaini upungufu katika mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Arusha, ambapo ulikadiriwa kugharimu Tsh. Bilioni 187 lakini mkataba ukasainiwa kwa Tsh. Bilioni 338.
Uwanja huo unatarajiwa kutumika katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, itakayofanyika kwa pamoja Kenya, Tanzania, na Uganda kati ya Juni 19 hadi Julai 18, 2027.