Featured content

Jaji Chande: Tume imepokea ushahidi toka kwa Watu 63,603
Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025, Jaji Mohamed Chande Othman, amesema Tume hiyo imepokea ushahidi kutoka kwa Watanzania 63,603 kwa njia mbalimbali. Amesema ushahidi huo umepatikana kupitia mahojiano ya ana kwa ana na mashahidi 1,323, mashahidi wa viapo 553, na madodoso 4,891 yaliyokuwa na maswali bila majina ya wahusika.
Msigwa: Deni la Taifa linakua siyo kwa sababu tunatumia vibaya fedha
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa ongezeko la deni la taifa halitokani na matumizi mabaya ya fedha, bali ni matokeo ya uwekezaji mkubwa katika miradi ya kimkakati ya maendeleo inayolenga kuleta mapinduzi ya kiuchumi. Msigwa amefafanua kuwa fedha hizo zimeelekezwa katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa kama reli ya mwendokasi (SGR), upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam, uimarishaji wa shirika la ndege (ATCL), pamoja na kuboresha huduma za kijamii ikiwemo kusambaza umeme vijiji
Rais Samia: Mmeshuhudia siku tatu zile, hakukuwa na harusi wala mabaa, zilikuwa siku nzito
Rais Samia Suluhu amesema amani ni hazina ya shughuli zetu za kiuchumi na kijamii akisisitiza kwamba bila amani hakuna kujenga uchumi, hakuna shughuli za kijamii. Ameongeza kuwa, mmeshuhudia siku tatu zile (Oktoba 29) ambapo hakukuwa na shughuli za burudani, harusi, kitchen party, mikusanyiko ya kijamii, wala michezo yoyote. Amesema zilikuwa siku tatu nzito.
Msanii A.Y: Niwe mkweli suala la kutengeneza Mdundo wa Taifa, haliwezekani
Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya (AY), ameweka wazi msimamo wake kuhusu mjadala wa “mdundo wa taifa,” akisisitiza kuwa utambulisho wa muziki hauwezi kulazimishwa kupitia mipango ya mezani bali hujitengeneza wenyewe kadri muda unavyokwenda. Amesema muziki wa Bongo Fleva tayari una ladha yake inayotambulika kimataifa, akitoa mfano kuwa hata nchi kama Nigeria zilipitia hatua za kuiga kabla ya kufikia utambulisho wao wa sasa, hivyo wasanii wanapaswa kuthamini muziki wa nyumbani.
Waziri Nanauka: Serikali kuanzisha Benki ya Vijana
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amesema serikali inaendelea na utafiti wa kuanzisha Benki ya Vijana nchini ili kuondoa vikwazo vya mitaji na kutoa huduma za kifedha zinazoendana na mahitaji ya vijana wanaoanza shughuli za kiuchumi. Akiwasilishaji wa makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27, Nanauka amesema benki hiyo itakuwa chombo cha kimkakati cha kuchochea ubunifu, kuongeza ajira, na kuimarisha mchango wa vijana katika kukuza uchumi
Uchambuzi wa Hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu 2026/2027: Tusome katikati ya mistari
"Kama baba wa familia anasema 'tutajenga nyumba kubwa mwaka huu', unauliza maswali ya msingi: Bajeti iko wapi? Fundi ni nani? Nyenzo zimenunuliwa? Tutamaliza lini?" Vivyo hivyo, tunapaswa kuihoji Serikali. Zingatia: Tarehe mosi Aprili 2026, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb.) aliwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2026/2027. Hotuba ina kurasa 131. Watanzania wengi hawatapata muda wa kuisoma yote. Ipo hapa Muhimu...
Iran yafungua lango la Hormuz kupisha mazungumzo ya Israel na Lebanon
Serikali ya Iran, kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje Seyed Abbas Araghchi, imetangaza rasmi kufunguliwa kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz kwa meli zote za kibiashara kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku 10 kati ya Israel na Lebanon yaliyoanza Aprili 16, 2026.
Maelekezo ya Lissu "Futeni kesi zangu na za chama, nikiwa huru ndiyo tuzungumze"
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameeleza utayari wake wa kushiriki mazungumzo ikiwa tu atakuwa huru baada ya kufutwa kwa kesi zote zinazomkabili yeye pamoja na chama chake. Kupitia taarifa iliyotolewa Aprili 16, 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, imeeleza kuwa Lissu amesema kesi ya Uhaini inayomkabili inatokana na msimamo wake wa No Reforms, No Election.
Arusha: Watu 6 wakamatwa wakituhumiwa kumuua Askari kwa kudhani ni Mwizi
Jeshi la Polisi linawashikilia Watu 6 kwa kudaiwa kumuua Askari Polisi, Roland Mollel baada ya kumshambulia, tukio lililotokea katika Mtaa wa Mlimani, Kata ya Muriet, jana Aprili 15, 2026. Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Justine Masejo amesema Roland alikuwa katika shughuli zake binafsi baada ya kazi, kulitokea taharuki iliyotokana na kusambaa maneno ya kundi la Watu wakidai eneo lao kuna wezi, marehemu akapita akiwa amebebwa katika bodaboda, kundi la Watu likawashambulia huku wakiwakimbiza.
Rais wa FIFA: Nimeonana na Iran, itashiriki Kombe la Dunia 2026 Marekani
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino amewahakikishia mashabiki wa Soka Duniani kuwa timu ya taifa ya Iran itashiriki Kombe la Dunia 2026, licha ya mashaka yaliyotanda tangu Marekani na Israel zilipoingia katika vita na Iran. Amesema Iran imefuzu kihalali kushiriki Kombe la Dunia na wachezaji wake wana haki ya kucheza na kuiwakilisha nchi yao.
Mwigulu: Elimu ya msingi ya lazima kuwa miaka 10
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba ametangaza kuanza kwa utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu utakaofanya elimu ya msingi kuwa ya lazima kwa kipindi cha miaka kumi, akisema ni sehemu ya mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu. Akihitimisha hotuba ya bajeti bungeni, ameeleza kuwa mabadiliko hayo ni makubwa zaidi tangu yale ya mwaka 1967 yaliyoongeza elimu ya lazima kufikia darasa la saba.
Afrika Kusini: Kiongozi wa Upinzani Julius Malema ahukumiwa miaka 5 jela
Kiongozi wa Chama cha Upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF), Julius Malema amehukumiwa kifungo cha Miaka Mitano jela na kulipa faini baada ya kupatikana na hatia ya makosa matano ikiwemo kumiliki silaha kinyume cha Sheria na kuifyatua hadharani hali iliyohatarisha maisha ya Watu. Mwanasheria wake amesema watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo ili kuzuia kiongozi huyo kupelekwa gerezani.
Mahakama ya Rufani yairuhusu CHADEMA kuendelea na shughuli za Kisiasa nchini
Mahakama ya Rufani Kanda ya Dodoma, leo Aprili 15, 2026 imetengua maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyokizua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya shughuli za Siasa nchini, kufuatia kesi iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar), Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya chama hicho.
Korea Kusini: Raia kuanza kupewa Intaneti ya bure kama haki ya msingi sawa na maji na umeme
Korea Kusini imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza mpango wa kuwapatia wananchi Intaneti bure hata baada ya vifurushi kuisha, kwa kasi ya takriban 400 Kbps. Hatua hii inalenga kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu mtandaoni kama sehemu ya mkakati wa kuifanya Intaneti kuwa haki ya msingi, tofauti na nchi kama Ufilipino, Estonia na Costa Rica ambazo hutoa Wi-Fi ya bure katika maeneo ya umma.
Kakoso: Serikali iweke tozo kwenye mawasiliano ya simu kusaidia kujenga barabara
Mbunge wa Tanganyika (CCM), Selemani Kakoso, amependekeza kuongeza tozo ya shilingi 100 kwenye matumizi ya simu ili kusaidia kukarabati miundombinu. Ametoa hoja hiyo Aprili 13, 2026, Bungeni Dodoma akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Amesema iwapo litakubaliwa na wataalamu, linaweza kuingizia Serikali karibu Tsh. Trilioni 1 zitakazosaidia kutatua changamoto ya miundombinu.
Polisi: Mwanamtandao Ashlee Jenae alifia Hospitali baada ya kukutwa amejinyonga
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Unguja Kaskazini, Benedict Mapujira amesema Mwanamtandao Ashy Robinson (Ashlee Jenae), Raia wa Marekani alifia Hospitali alikowaishwa baada ya kukutwa na Mhudumu wa Hoteli akiwa amejinyonga katika chumba chake cha hoteli. Ameongeza kuwa Mwili wa Ashlee bado upo Zanzibar kama sio jana basi leo utakuwa umefanyiwa uchunguzi
Rais wa Djibouti ashinda muhula wa sita kwa 97.8%
Rais wa Djibouti, Ismael Omar Guelleh, ameshinda tena uchaguzi kwa asilimia 97.8 ya kura, na hivyo kujihakikishia muhula wa sita madarakani unaoongeza utawala wake kufikia miaka 27. Katika uchaguzi huo uliofanyika Aprili 10, 2026, alikabiliana na mgombea mmoja wa upinzani, Mohamed Samatar, huku vyama viwili vikuu vya upinzani vikisusia uchaguzi tangu Mwaka 2016 vikidai kukosekana kwa usawa katika mamlaka za uchaguzi. Ushiriki wa wapiga kura ulikuwa 80.4%
Mwabukusi: Tunahitaji ukweli waliotekwa wako wapi? Na wa 'Mauaji ya Halaiki' ya Oktoba 29, 2025?
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi amevitaka vyombo vya dola na taasisi za usimamizi wa uchaguzi kutoa majibu ya haraka kuhusu kile alichokiita “mauaji ya halaiki” na miili ya raia iliyopotezwa Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa taifa haliwezi kupona bila ukweli na uwajibikaji.
UTAFITI: Tanzania miongoni mwa nchi zenye Uhuru mdogo zaidi wa mtandao
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Cloudwards mwaka 2026, ulioshirikisha nchi 171 na kutathmini viwango vya udhibiti wa mtandao kwa kuzingatia vigezo kama matumizi ya majukwaa ya mitandao ya kijamii, upatikanaji wa maudhui ya kisiasa na kidini, kanuni zinazohusu matumizi ya VPN pamoja na maudhui ya kiuchumi na kijamii. Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoonesha kuwepo kwa udhibiti wa majukwaa ya mitandao ya kijamii, ikiwemo X, JamiiForums.com na Clubhouse, kwa kiwango cha 28%.
TG-MSG: Tume ya Matukio ya Oktoba 29 iache danadana, Watanzania wanahitaji Uwajibikaji
Mtandao wa Asasi za Kiraia nchini (CSOs) kupitia Kikundi Elekezi cha Wadau wa Utawala Tanzania (TG-MSG) umeitaka Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande kuacha kuchelewesha mchakato huo na badala yake kutoa ripoti kamili kwa umma. Tume hiyo ilisema Mamlaka ya Uteuzi imeridhia maombi yao ya muda wa ziada wa siku 21 ili kukamilisha kazi kabla au ifikapo Aprili 24, 2026.
Back
Top Bottom