TEC, CCT, CPCT Kemeeni yanayoendelea Zanzibar ili kuwalinda Wakristo waishio Zanzibar

Kwanini msielezee kwa kina zaidi kuhusu hii sheria yao ya kukamata wanaokula hadharani?
Je ni waislamu pekee kwa kutizama ID zao n.k.
Au ni katazo la kula hadharani kwa watu wote n.k
Adhabu yake ipoje?

Hili jambo msilichochee zaidi.
Mnachofanya ni kama kuonyesha wakristo wanakandamizwa na waislamu hapo Zanzibar, na matokeo yake si mazuri.
Kuuawa padri ndani ya kanisa akiendesha misa kulikofanyika Mwanakwerekwe haudhani kuwa ni tukio baya sana kwa nchi na wananchi wake?
 
zingatia table manners hakuna atakae sumbuka na wewe 🐒

kubugia bugia na kufakamia mavyakula hovyo hovyo hadharani bila bila aibiu wala utaratibu ni mazoea na ni tabia mbaya.
Ni malezi ya hovyo sana 🐒

Pika au nunua Chakula chako kaa ndani kwa utulivu kula maliza, jiunge na wenzako kijiweni kwa stori na porojo, safiii, nani atababaika na wew?

sasa wewe unajua kabisa sis tumefunga, wengine hatujafunga na tuna njaa kweli kweli na mfukoni hatuna jambo lolote, halafu wewe unanua biriani au chips yenye mapochopocho kama yote, halafu unakuja kuungana nasi kijiweni huku ukifakamia hilo pilau......

huo sio ungwana na wala sio ustaarabu.
unatibua saumu za wengine lakini pia unatibua na kuvuruga zaidi njaa wengine kwa tamaa zako. Tutakushughulikia kimoyomoyo wale wenye roho ngumu, lakini wenye roho nyepesi hawatakuacha salama 🐒
Mpumbavu sana wewe.. kila sehemu una paste huu ujinga..
 
Kwa taarifa yako wapo waliokamatwa wakipika chakula mchana! Tetea na hili kwa nguvu zako zote.
sitetei chochote kwa yeyote 🐒

ustaarabu na kuheshiimiana ni muhimu zaid kwenye mambo haya.
wapikaji na walaji ni vizuri kuzingatia ustaarabu, hali na utaratibu wa wengine 🐒

kuzingatia faida na wateja pekeyake bila kuzingatia mazingira na hali za wengine ni kujitafutia hasara na pengine usumbufu kwao na kwa wateja woa🐒

Kumbuka,
hao wapika vyakula pengine wameibua, wamechochea na kuamsha hasira za ndugu zao wa damu kabisa, kwamba why hawa ndugu zetu wanaharibu utaratibu wa imani ya dini na utamaduni wa familia yetu 🐒

Muheshimu anae kuheshimu, asie kuheshimu usimjali 🐒
 
kumbe kufunga ni utamaduni sio swala la dini
Mkuu Unajua maana ya Tamaduni???
Tamaduni Ni ile hali ya kufanya Jambo mara kwa mara kwa kulizoea..

Kwa mfano Tamaduni ya wakristo wengi ni kwenda Kusali Siku ya Jumapili..
So ukisema wakasali siku ya Jumatano unavunja Tamaduni yao..
Umenielewa??

Tamaduni=Tradition

2 Wathesalonike 2:15

Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.

Therefore, brethren, stand fast, and hold the traditions which ye have been taught, whether by word, or our epistle.
 
Ukristu uliingia Zanzibar rasmi mwaka 1879 ulipokamilika ujenzi wa kanisa la Anglikana, na wakiristu wamekua wakiishi vizuri mpaka miaka hii ya 2000 ambapo tulishuhudia padri akipigwa risasi ndani ya kanisa ambapo tukio hilo lilionekana kuwa la kawaida japo angepigwa risasi shehe dunia nzima ingejua Tanzania ilipo kwenye ramani.
Ok sawa Ila Usisahau uislamu Zanzibar ulikuwepo Miaka ya 844..
Na tangu hapo.ulikuwa chini ya Sultanate..
Yaani Ilikuwa ni nchi ya Kiislamu...
Hata hivyo iliisdhinishwa kuwa muslimu society mwenye miaka ya 1800s-1964..


Vasco.da gama aliwahi kusema alipofika zanzibar 1400s Alikuta ni nchi huru yenye Jamii ya Waislamu weusi..

Kasome Viitabu kuna kitabu kimoja kutoka historia ya East Africa Colon cha Uingereza kinasema

"The Portuguese arrived in East Africa in 1498, where they found several independent towns on the coast "Zenjibar" with Muslim Arabic-speaking elites. While the Portuguese travellers describe them as "black Muslim",
 
Kwanini msielezee kwa kina zaidi kuhusu hii sheria yao ya kukamata wanaokula hadharani?
Je ni waislamu pekee kwa kutizama ID zao n.k.
Au ni katazo la kula hadharani kwa watu wote n.k
Adhabu yake ipoje?

Hili jambo msilichochee zaidi.
Mnachofanya ni kama kuonyesha wakristo wanakandamizwa na waislamu hapo Zanzibar, na matokeo yake si mazuri.

Na kwanini wakataze wakati zanzibar sio nchi ya kiislam? Kuna maana gani ya muungano?
 
Huo utamaduni haukubaliki, ni wa kupingwa kwa nguvu zote, watanganyika waingie huko kwa wingi na wakale mchana tuone kama watawakamata wote na kuwasweka ndani. Mbona bara watu wanakula mchana na hawabughudhiwi? Tena wanakula malangoni mwa misikiti yenye migahawa kwenye fremu zao

Na hivi pasaka inakuja wakati wa ramadhani. Hao watanganyika waliokuwepo huko watateseka sana
 
Huyu uongo mwingine wa kijinga sana eti toka 1400......
Tafuta Hii Journal mkuu

Imeandikwa na Prestholdt, Jeremy. "Portuguese Conceptual Categories the 'Other' Encounter on the Swahili Coast." Journal of Asian.American Studies, Volume 36, Issue 4, PP 390..

inasema hivi..."The Portuguese arrived in East Africa in 1498, where they found several independent towns on the coast, "Zinjibar" (Zanguabar) with Muslim Arabic-speaking elites.
While the Portuguese travellers describe them as "black Muslim",


Rejea neno Independent towns
 
Back
Top Bottom