Tamko la Jukwaa la Wakristo mkoa wa Mbeya (TCF)

Status
Not open for further replies.

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Leo Mkoani Mbeya Umoja wa Maknisa Kupita Maaskofu na Wachungaji Wametoa tamko Katika mambo Yafuatayo:
1.Wameitaka serikali ya Kikwete kumukamata mara Moja Shehe Illunga Hassan Kampungu kwa Ushahidi wa Uchochozi Katika DVD unao toa maelekezo kwa Waislamu kupiga kuua Ma Padri, Wachungaji , Maaskofu N.K.
2.CCM na serikali yake Wameshindwa kuwalinda viongozi wa dini na hata wanapouawa hakuna hatua za dhati zinazochukuliwa dhidi ya Wauaji .Wamesistiza kuwa hakuna utawala wa Sheria
3.Wameitaka serikali ya kikwete kueleza kufafanua bayana tamko la Mhe Wassira juu ya kuwapa haki Waislamu Kuchinja Wanyama huku akiwakataza Wakristo kufanya hivyo. Wanataka kujua Wasira anaiwakilisha Serikali ya CCM?? Na ametumia Sheria gani Kuwakataza Wakristo kuchinja Wanyama??.
4.Ufafanuzi wa mambo hayo hapo juu umetakiwa kutolewa haraka na ikifika tarehe 25 Feb,2013 Watachukua hatua ya kuthibitisha kuwa Serikali ya CCM na Rais Kikwete wamejifungamanisha na dini ya Kiislamu hivyo , Watawataka wakristo wote kurudisha kadi za CCM na kuzichoma ili kulinda katiba ya nchi!!!!
Up date
MHESHIMIWA NDG. ABAS KANDORO,

KAMA MKUU WA MKOA NA MWAKILISHI WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE MKOA WA MBEYA, TUNAPENDA KUSOMA MBELE YAKO TAMKO RASMI LA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA (TCF).

NDUGU MKUU WA MKOA,

"HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU WOWOTE" (Mit. 14:34).

Katika mkutano wa jukwaa la Wakristo Tanzania mkoa wa mbeya ulionyika tarehe 12/02/2013 Jijini Mbeya, wajumbe tulitafakari kwa undani juu ya hali inayoendelea kujitokeza katika nchi yetu na hasa katika mahusiano baina ya dini mbili kuu UKRISTO NA UISLAMU.

Jukwaa hilo lilijumuisha taasisi zake kuu (yaani mabaraza ya Madhehebu ya Kikristo) Tanzania Episcopal Council (TEC), Christian Council of Tanzania (CCT) na Pentecostal Council of Tanzania (PCT).

Mbali na mambo yake ya kawaida jukwaa hilo lilitafakari utekelezaji wa Serikali juu ya tamko Rasmi la jukwaa la Wakristo kitaifa lililotolewa tarehe 06/12/2012 na kusomwa katika makanisa yote ya Kikristo nchini kwenye sikukuu ya Krismas tarehe 25/12/2012. Katika tafakari letu jukwaa la Wakristo wa Mkoa wa Mbeya tumeona kuwa kunabaadhi ya mienendo inayojitokeza katika nchi yetu ambayo kama isipodhibitiwa na kukomeshwa na Serikali italeta athali kubwa na hata kuondoa amani na uthabiti (Stability) wan chi.

Katika kutafakari kwa jukwaa juu ya athari zinazoweza kujitokeza, kumekuwepo na mambo yanayotendeka waziwazi yenye athri kubwa kwa amani na usitawi wan chi na wanchi wake kwa ujumla. Kwa mfano, uchochezi, kashfa, matusi na uchokozi wa wazi unaofanywa na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupitia vyombo vya habari vya kidini (rediona magazeti), mihadhara, kanda za video, CD na DVD pamoja na kauli zinazotolewa na viongozi wa dini hiyo kwenye baadhi ya nyumba zao za ibada(ushahidi upo kama vile uhamasishaji wa Sheikh Ilunga) pasipo serikali kuchukua hatua stahiki na badala yake kubaki kimya au kupambana na wanaofichua harakati hatarishi kwa utulivuwa nchi.

Miongoni mwa harakati hatarishi zinazosambazwa kwa njia ya CD na DVD za Sheikh Ilunga, kuhusu kuua Wachungaji, Mapadri na Maaskofu zimeanza kuwa matokeo mabaya; kwani Padri kule Zanzibar alipigwa risasi na watu walioitwa na serikali wahuni na sasa kifo.

Kimetokea na mchungaji Mathayo Kachila kule Buselesele Mkoani Geita na kikundi kinacho dhaminiwa ni wanaharakati hao wa kiislamu wenye jazba na gadhabu kali inayotokana na mvutano uliopo kati ya wakristo na waislamu kuhusu nani mwenye haki kisheria KUCHINJA WANYAMA. Hatua zinazochukuliwa na Serikali hazilizishi wala kukidhi matakwa ya wananchi wapenda amani.

Tuna mifano kadhaa ya matukio kama haya yaliyojitokeza kwa wanchi wenzetu moja ni ile ya wenzetu aliyepigwa risasi kule Rungwe Ndg. John Mwankenja (Mwenyekiti wa CCM Rungwe) aliyepigwa risasi kwa mambo yanayodhaniwa kuwa ni ya kisiasa) Serikali ichukuwe hatua madhubuti kwa kutuma wachunguzi kutoka Dar es salaam kwa swala hilo na wote tuliridhika kwa hatua hizo madhubuti. Hatua kama hizo mbona hazichukuliwi katika masuala haya ya kidini na badala yake Serikali inakaa kimya au ina chukua hatua ambazo kimsingi hazitatui tatizo ili wananchi waridhike na Seeikali yao? Je tuseme Serikali inaangalia haiba (Personality) za watu au aina ya vikundi? Swala la uchinjaji lilipo jitokeza kule Mwanza waziri wan chi ndg. Steven Wasira alienda na kutoa majibu mepesi katika swala zito je, tuseme aliyoyatamka huko yalikuwa ni KAULI YA SERIKALI au kauli yake mwenyewe? Na kama yake mwenyewe mbona Serikali haijakanusha waziwazi? Na kama ni kauli ya serikali hiyo haki ya kuchinja kwa waislamu inatokana na sheria zipi za nchi? Je huo ndio utawala wa sheria tuliyoahidiwa na serikali ya awamu ya nne kuwa itatenda kazi kwa kuzingatia utawala wa sheria.

Kupigwa risasi kwa Pdri na kuuwawa kwa mchungaji kunathibitisha hazma halamu na batili ya "Ua, chinja" mapadri, wachungaji na maaskofu iwe kwa siri au kwa wazi iliyohasisiwa na Sheikh Ilunga ambayo sio tu inahatarisha amani ya nchi lakini pia inavunja haki za kuishi za binadamu zilizoainishwa katika katiba ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Aidha harakati hizi zina muelekeo wa kudhoofisha ukristo Tanzania kama sio kuumaliza kabisa.

Pamoja na mambo mengine kinachosikitisha ni namna ambavyo serikali inavyoyashughulikia mambo mazito yanayotikisa amani na utulivu wan chi. Utasikia mala ikisema "Mtu haruhusiwi kujichukulia sheria mkononi" na ndipo kikundi Fulani kitaibuaka na kuvunja mabucha na kuchoma nyama iliyomo humo hapo tena utasikia serikali hiyohiyo ikitowa kauli kwamba "Mvumiliane" je tunakwenda wapi?

Kwa misingi hiyo kwanini tusite kusema kwamba serikali ya chama cha mapinduzi (CCM) inaibeba dini ya kiislamu? Kwakuwa jukumu la serikali ya chama cha mapinduzi ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Tanzania bila kujali dini zao, makabila yao na hata rangi zao wanaishi katika misingi ya uhuru, haki, udugu na amani kama raisin a watendaji wake walivyotoa kiapo mara baada ya kupewa dhamana ya kuiongoza nchi na wananchi wake kwa ujumla pasipo na ubaguzi wowote.

HITIMISHO: Ili wakristo wote nchini warudishe imani yao kwa serikali ya chama cha mapinduzi mambo ya fuatayo ni lazima yachukuliwe hatua za haraka iwezekanavyo:

Tunataka Serikali izingatie utawala washeria kulingana na ahadi yake katika kushughulikia maswala ya kijamii na sio vinginevyo. Kwa kuzingatia sheria maswala ya imani na dini yapo wazi kabisa kama zilivyoanishwa kwenye katiba ibara ya 19 (1), (2) (3) (4) na kufanya vinginevyo ni uvunjifu wa sheria.

Swala la kuua lisichukuliwe kama mazoea ya kawaida na inapotokea popote ni lazima Serikali ichukuwe hatua inayostahiki kwa kuzingatia utawala wa sheria kwakuwa wote wako sawa mbele ya sheria ibara ya 12, 13 (1) –(5).Usawa huo ni lazima uonekane katika swala la mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila na kama hatua zilivyochukuliwa katika mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri na mwenyekiti ya CCM Wilaya ya Rungwe Ndg. John A. Mwankenja. Hiyo ni haki ya msingi kkwa kila mtantania bila kuangali haiba (Personality) yake kama katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inavyoainisha haki xza kuishi, kulindwa na kushughuklikiwa kisheria katika ibara ya 14 na 15 pamoja na vifungu vyake viwili vidogo.

Tunataka Serikali itueleze ni ushahidi gain zaidi inayoutaka kuliko ule unaopatikana kwenye CD na DVD zilizotolewa na Sheikh Ilunga kama inazingatia utawala utawala wa sheria.

Tunataka Serikali iwajibike kutolea ufafanuzi kauli ya waziri wan chi Ndg. Steven Wasira inayohusu haki ya kuchicha kwa waislamu kama inatokana na sheria gain ya nchi?

Kama Serikali inatekeleza utawala wa sheria, tunataka wakristo tuwe na machinjio na bucha zetu kulingana na imani yetu.

Kama Serikali haitachukuwa hatua za makusudi katika kutekeleza madai yetu sisi kama viongovi wa dini ya kikristo tutachukua hatua ya kuwaambia waumini wetu kwamba Serikali ya chama cha mapinduzi inaibeba dini ya kiislamu na wao watajua la kufanya.

Pamoja na kutaka utekelezaji wa haraka kutoka kwa Serikali bado tunawaomba wakristo tuwe katika hali ya maombi na utulivu kwa wakati huu ambapo tumo katika vita vya kiroho ili Mungu akatuimarishie amani ambayo ni nguzo kuu ya Taifa letu. Tamko hili rasmi la jukwaa la wakristo Mbeya lisomwe katika makanisa yetu yote siku ya juma pili tarehe 24/02/2013.

Tunakuambatanishia na nakala ya Tamko Rasmi la TCF Taifa la tarehe 6/12/2012.

NDUGU MKUU WA MKOA NAWASILISHA.

Nakala kwa:

Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
Tanzania Christian Furum Taifa
Mwenyekiti wa the Tanganyika Law Society.
Vyombo vya habari TV, Redio na magazeti
 
Mi hilo la kuchinja waendelee nalo tu jamani, hawa ni wafanyakazi wetu, sisi ni watoto wa the Most High so sioni shaka suala la kuasidiwa kuchijna ila walinikera sana juzi walivyokataa kuchinja kitimoto peke yake kule Geita
 
Mmh haya mapya tena! Aisee hali kumbe ilisha haribika siku mingi.
 
Nlijua watakuja na tamko tu ! Bado wala wa TEC nao watamtaka JK kuwapisha Ikulu kama wauwaji wasipopatikana
 
Leo Mkoani Mbeya Umoja wa Maknisa Kupita Maaskofu na Wachungaji Wametoa tamko Katika mambo Yafuatayo:
1.Wameitaka serikali ya Kikwete kumukamata mara Moja Shehe Illunga Hassan Kampungu kwa Ushahidi wa Uchochozi Katika DVD unao toa maelekezo kwa Waislamu kupiga kuua Ma Padri, Wachungaji , Maaskofu N.K.
2.CCM na serikali yake Wameshindwa kuwalinda viongozi wa dini na hata wanapouawa hakuna hatua za dhati zinazochukuliwa dhidi ya Wauaji .Wamesistiza kuwa hakuna utawala wa Sheria
3.Wameitaka serikali ya kikwete kueleza kufafanua bayana tamko la Mhe Wassira juu ya kuwapa haki Waislamu Kuchinja Wanyama huku akiwakataza Wakristo kufanya hivyo. Wanataka kujua Wasira anaiwakilisha Serikali ya CCM?? Na ametumia Sheria gani Kuwakataza Wakristo kuchinja Wanyama??.
4.Ufafanuzi wa mambo hayo hapo juu umetakiwa kutolewa haraka na ikifika tarehe 25 Feb,2013 Watachukua hatua ya kuthibitisha kuwa Serikali ya CCM na Rais Kikwete wamejifungamanisha na dini ya Kiislamu hivyo , Watawataka wakristo wote kurudisha kadi za CCM na kuzichoma ili kulinda katiba ya nchi!!!!

kwani wanazo? si walichukua za chadema ? lol.....wasitudanganye kanisa haliwezi kujitoa ccm..lina faidi sana.....ila..ni chuki tu kwa kikwete ndo zina wasumbua...
kuhusu ilinga....alikua akisema kuhusu yallio tokea kenya......ammbapo viongozi ....wa ...kiislam zaidi ya 6 ...pamoja na mmoja kilema kipofu ...kuuliwa.....na kufurahiwa na mapadre..so....jino kwa jino....hajasema kuanza wao.....bali kulipa kisasi.....wakiuliwa na wao walipe....haya yote yanakuja ..kwani jamii haina haki....
 
hivi kutoa tamko la kuitaka serekali imkamate shekhe ama askofu ndio sherias inavyoeleza??!!!
kama si kutaka kuleta mzozano wa kidini zaidi kwa nini maaskofu msiende hatua kwa hatua kwa kuanza kufungua shitaka dhidi ya huyo mnaesema mchochezi katika kituo cha polisi kilichokaribu na nyinyi,tutangulize akili kabla ya kupenda kuwa katika vichwa vya khabari vya kila siku
 
Hiyo namba nne nzuri sana kwani sasa yametimia vita imeshaanza,halafu hii ya ccm+uislam inakujaje leo baada ya mfumo kristu toka zama za kale,natamaani sana tamko lisitolewe ili na wakristu tuwe na chama chetu cha kidini ambacho tutakitaja baada ya kuchoma kadi.
 
Kama yeye ni Jogoo si aende Kenya akaseme hayo? Aone wanaume watakavyomfanya.

Chezea Kenya wewe, mijitu Sura na Roho ni mbaya mno, ukileta za kuleta hawakuchelewi.

Nilishawahi kuona Wakenya wamempandishia Boss wao na walipoona ujinga, wakaondoka hapo hapo.

Sisi Mitanzania ndiyo mijitu ya kujipendekezapendekeza kama Juliana Shonza kwa pesa za CCM, Kudadadeki.
kwani wanazo? si walichukua za chadema ? lol.....wasitudanganye kanisa haliwezi kujitoa ccm..lina faidi sana.....ila..ni chuki tu kwa kikwete ndo zina wasumbua...
kuhusu ilinga....alikua akisema kuhusu yallio tokea kenya......ammbapo viongozi ....wa ...kiislam zaidi ya 6 ...pamoja na mmoja kilema kipofu ...kuuliwa.....na kufurahiwa na mapadre..so....jino kwa jino....hajasema kuanza wao.....bali kulipa kisasi.....wakiuliwa na wao walipe....haya yote yanakuja ..kwani jamii haina haki....
 
L
4.Ufafanuzi wa mambo hayo hapo juu umetakiwa kutolewa haraka na ikifika tarehe 25 Feb,2013 Watachukua hatua ya kuthibitisha kuwa Serikali ya CCM na Rais Kikwete wamejifungamanisha na dini ya Kiislamu hivyo , Watawataka wakristo wote kurudisha kadi za CCM na kuzichoma ili kulinda katiba ya nchi!!!!
Huu mstari na wenyewe ni sehemu ya hilo tamko? Ni maaskofu wa makanisa gani hao? Kama maaskofu nao wameamua kuwa wanasiasa, basi hatutapona kupigana mwaka huu. Hili ni tamko la kitoto kabisa kuweza kutolewa na maaskofu. Labda kama limetolewa na wainjilisiti? Hivi kweli askofu anaongelea habari za kuchoma kadi za CCM? Kama kweli hili ndilo tamko la maaskofu basi tatizo letu ni kubwa kuliko tunavyolidhani. Maana sasa hawana tofauti na huyo Shehe Illunga.
 
Wanajukwaa hebu tazameni hii nimeitoa huko kwenye wavuti ya mbeya yetu; Naamini mnajua kusoma.....

MHESHIMIWA NDG. ABAS KANDORO,

KAMA MKUU WA MKOA NA MWAKILISHI WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE MKOA WA MBEYA, TUNAPENDA KUSOMA MBELE YAKO TAMKO RASMI LA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA (TCF).

NDUGU MKUU WA MKOA,

"HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU WOWOTE" (Mit. 14:34).

Katika mkutano wa jukwaa la Wakristo Tanzania mkoa wa mbeya ulionyika tarehe 12/02/2013 Jijini Mbeya, wajumbe tulitafakari kwa undani juu ya hali inayoendelea kujitokeza katika nchi yetu na hasa katika mahusiano baina ya dini mbili kuu UKRISTO NA UISLAMU.

Jukwaa hilo lilijumuisha taasisi zake kuu (yaani mabaraza ya Madhehebu ya Kikristo) Tanzania Episcopal Council (TEC), Christian Council of Tanzania (CCT) na Pentecostal Council of Tanzania (PCT).

Mbali na mambo yake ya kawaida jukwaa hilo lilitafakari utekelezaji wa Serikali juu ya tamko Rasmi la jukwaa la Wakristo kitaifa lililotolewa tarehe 06/12/2012 na kusomwa katika makanisa yote ya Kikristo nchini kwenye sikukuu ya Krismas tarehe 25/12/2012. Katika tafakari letu jukwaa la Wakristo wa Mkoa wa Mbeya tumeona kuwa kunabaadhi ya mienendo inayojitokeza katika nchi yetu ambayo kama isipodhibitiwa na kukomeshwa na Serikali italeta athali kubwa na hata kuondoa amani na uthabiti (Stability) wan chi.

Katika kutafakari kwa jukwaa juu ya athari zinazoweza kujitokeza, kumekuwepo na mambo yanayotendeka waziwazi yenye athri kubwa kwa amani na usitawi wan chi na wanchi wake kwa ujumla. Kwa mfano, uchochezi, kashfa, matusi na uchokozi wa wazi unaofanywa na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupitia vyombo vya habari vya kidini (rediona magazeti), mihadhara, kanda za video, CD na DVD pamoja na kauli zinazotolewa na viongozi wa dini hiyo kwenye baadhi ya nyumba zao za ibada(ushahidi upo kama vile uhamasishaji wa Sheikh Ilunga) pasipo serikali kuchukua hatua stahiki na badala yake kubaki kimya au kupambana na wanaofichua harakati hatarishi kwa utulivuwa nchi.

Miongoni mwa harakati hatarishi zinazosambazwa kwa njia ya CD na DVD za Sheikh Ilunga, kuhusu kuua Wachungaji, Mapadri na Maaskofu zimeanza kuwa matokeo mabaya; kwani Padri kule Zanzibar alipigwa risasi na watu walioitwa na serikali wahuni na sasa kifo.

Kimetokea na mchungaji Mathayo Kachila kule Buselesele Mkoani Geita na kikundi kinacho dhaminiwa ni wanaharakati hao wa kiislamu wenye jazba na gadhabu kali inayotokana na mvutano uliopo kati ya wakristo na waislamu kuhusu nani mwenye haki kisheria KUCHINJA WANYAMA. Hatua zinazochukuliwa na Serikali hazilizishi wala kukidhi matakwa ya wananchi wapenda amani.

Tuna mifano kadhaa ya matukio kama haya yaliyojitokeza kwa wanchi wenzetu moja ni ile ya wenzetu aliyepigwa risasi kule Rungwe Ndg. John Mwankenja (Mwenyekiti wa CCM Rungwe) aliyepigwa risasi kwa mambo yanayodhaniwa kuwa ni ya kisiasa) Serikali ichukuwe hatua madhubuti kwa kutuma wachunguzi kutoka Dar es salaam kwa swala hilo na wote tuliridhika kwa hatua hizo madhubuti. Hatua kama hizo mbona hazichukuliwi katika masuala haya ya kidini na badala yake Serikali inakaa kimya au ina chukua hatua ambazo kimsingi hazitatui tatizo ili wananchi waridhike na Seeikali yao? Je tuseme Serikali inaangalia haiba (Personality) za watu au aina ya vikundi? Swala la uchinjaji lilipo jitokeza kule Mwanza waziri wan chi ndg. Steven Wasira alienda na kutoa majibu mepesi katika swala zito je, tuseme aliyoyatamka huko yalikuwa ni KAULI YA SERIKALI au kauli yake mwenyewe? Na kama yake mwenyewe mbona Serikali haijakanusha waziwazi? Na kama ni kauli ya serikali hiyo haki ya kuchinja kwa waislamu inatokana na sheria zipi za nchi? Je huo ndio utawala wa sheria tuliyoahidiwa na serikali ya awamu ya nne kuwa itatenda kazi kwa kuzingatia utawala wa sheria.

Kupigwa risasi kwa Pdri na kuuwawa kwa mchungaji kunathibitisha hazma halamu na batili ya "Ua, chinja" mapadri, wachungaji na maaskofu iwe kwa siri au kwa wazi iliyohasisiwa na Sheikh Ilunga ambayo sio tu inahatarisha amani ya nchi lakini pia inavunja haki za kuishi za binadamu zilizoainishwa katika katiba ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Aidha harakati hizi zina muelekeo wa kudhoofisha ukristo Tanzania kama sio kuumaliza kabisa.

Pamoja na mambo mengine kinachosikitisha ni namna ambavyo serikali inavyoyashughulikia mambo mazito yanayotikisa amani na utulivu wan chi. Utasikia mala ikisema "Mtu haruhusiwi kujichukulia sheria mkononi" na ndipo kikundi Fulani kitaibuaka na kuvunja mabucha na kuchoma nyama iliyomo humo hapo tena utasikia serikali hiyohiyo ikitowa kauli kwamba "Mvumiliane" je tunakwenda wapi?

Kwa misingi hiyo kwanini tusite kusema kwamba serikali ya chama cha mapinduzi (CCM) inaibeba dini ya kiislamu? Kwakuwa jukumu la serikali ya chama cha mapinduzi ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Tanzania bila kujali dini zao, makabila yao na hata rangi zao wanaishi katika misingi ya uhuru, haki, udugu na amani kama raisin a watendaji wake walivyotoa kiapo mara baada ya kupewa dhamana ya kuiongoza nchi na wananchi wake kwa ujumla pasipo na ubaguzi wowote.

HITIMISHO: Ili wakristo wote nchini warudishe imani yao kwa serikali ya chama cha mapinduzi mambo ya fuatayo ni lazima yachukuliwe hatua za haraka iwezekanavyo:

Tunataka Serikali izingatie utawala washeria kulingana na ahadi yake katika kushughulikia maswala ya kijamii na sio vinginevyo. Kwa kuzingatia sheria maswala ya imani na dini yapo wazi kabisa kama zilivyoanishwa kwenye katiba ibara ya 19 (1), (2) (3) (4) na kufanya vinginevyo ni uvunjifu wa sheria.

Swala la kuua lisichukuliwe kama mazoea ya kawaida na inapotokea popote ni lazima Serikali ichukuwe hatua inayostahiki kwa kuzingatia utawala wa sheria kwakuwa wote wako sawa mbele ya sheria ibara ya 12, 13 (1) –(5).Usawa huo ni lazima uonekane katika swala la mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila na kama hatua zilivyochukuliwa katika mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri na mwenyekiti ya CCM Wilaya ya Rungwe Ndg. John A. Mwankenja. Hiyo ni haki ya msingi kkwa kila mtantania bila kuangali haiba (Personality) yake kama katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inavyoainisha haki xza kuishi, kulindwa na kushughuklikiwa kisheria katika ibara ya 14 na 15 pamoja na vifungu vyake viwili vidogo.

Tunataka Serikali itueleze ni ushahidi gain zaidi inayoutaka kuliko ule unaopatikana kwenye CD na DVD zilizotolewa na Sheikh Ilunga kama inazingatia utawala utawala wa sheria.

Tunataka Serikali iwajibike kutolea ufafanuzi kauli ya waziri wan chi Ndg. Steven Wasira inayohusu haki ya kuchicha kwa waislamu kama inatokana na sheria gain ya nchi?

Kama Serikali inatekeleza utawala wa sheria, tunataka wakristo tuwe na machinjio na bucha zetu kulingana na imani yetu.

Kama Serikali haitachukuwa hatua za makusudi katika kutekeleza madai yetu sisi kama viongovi wa dini ya kikristo tutachukua hatua ya kuwaambia waumini wetu kwamba Serikali ya chama cha mapinduzi inaibeba dini ya kiislamu na wao watajua la kufanya.

Pamoja na kutaka utekelezaji wa haraka kutoka kwa Serikali bado tunawaomba wakristo tuwe katika hali ya maombi na utulivu kwa wakati huu ambapo tumo katika vita vya kiroho ili Mungu akatuimarishie amani ambayo ni nguzo kuu ya Taifa letu. Tamko hili rasmi la jukwaa la wakristo Mbeya lisomwe katika makanisa yetu yote siku ya juma pili tarehe 24/02/2013.

Tunakuambatanishia na nakala ya Tamko Rasmi la TCF Taifa la tarehe 6/12/2012.

NDUGU MKUU WA MKOA NAWASILISHA.

Nakala kwa:

Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
Tanzania Christian Furum Taifa
Mwenyekiti wa the Tanganyika Law Society.
Vyombo vya habari TV, Redio na magazeti
 
4.Ufafanuzi wa mambo hayo hapo juu umetakiwa kutolewa haraka na ikifika tarehe 25 Feb,2013 Watachukua hatua ya kuthibitisha kuwa Serikali ya CCM na Rais Kikwete wamejifungamanisha na dini ya Kiislamu hivyo , Watawataka wakristo wote kurudisha kadi za CCM na kuzichoma ili kulinda katiba ya nchi!!!!

???????????????????????????????????????
 
kumekucha kwa jambo hili hata CCM hampo salama , mtakwenda na maji, taifa huzaliwa, hukua na mwisho hufa ili lizaliwe upya nahisi tunaelekea kufa
 
Nafikiri kuna tatizo kubwa ndani ya jamii ya kitanzania kwa sasa. Kwanini udini ujitokeze kwa kasi namna hii kwa sasa? Tuamini kwamba mfumo wa usalama wa taifa umeshindwa kweli kufanya kazi? Jamani watanzania kama tunatumiwa inatubidi tuchange akili zetu vizuri tusije tukajenga himaya ya alqaida au bokoharam nchini mwetu.
 
haya machochezi ya waislamu hayawezi kukalipiwa na serikali kwa sababu ni mradi wa serikali ya Iran wa kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini. Hizi cd na DVD ni pesa kutoka Iran zinaletwa nchini kuhakikisha mkristu unatukanwa mpaka uone uislkamu ni bora kuliko dini yako. serikali haiwezi kufanya lolote hapo hata tulalamike vipi.
 
hivi kutoa tamko la kuitaka serekali imkamate shekhe ama askofu ndio sherias inavyoeleza??!!!
kama si kutaka kuleta mzozano wa kidini zaidi kwa nini maaskofu msiende hatua kwa hatua kwa kuanza kufungua shitaka dhidi ya huyo mnaesema mchochezi katika kituo cha polisi kilichokaribu na nyinyi,tutangulize akili kabla ya kupenda kuwa katika vichwa vya khabari vya kila siku
Tafuta kwanza DVD aliyotoa huyo shehe Illunga ndipo utakapojua maaskofu wanamaanisha nini,kama hujaiangalia na kuisikiliza hutaweza kuchangia kitu,at least auleze umma alikuwa na maana gani na nikwa vipi ataweza kujitenga na mauaji yanayoendelea kwa kuwa wauaji wanatekeleza maagizo yake?huenda ndo mratibu
 
Imani yangu mkristo nalipenda sana dhehebu langu katoliki ila kwa hili hata mafundisho ya ukipigwa kofi ugeuze na shavu lingine kwa nzia leo ntatofautiana na kanisa
 
Leo Mkoani Mbeya Umoja wa Maknisa Kupita Maaskofu na Wachungaji Wametoa tamko Katika mambo Yafuatayo:
1.Wameitaka serikali ya Kikwete kumukamata mara Moja Shehe Illunga Hassan Kampungu kwa Ushahidi wa Uchochozi Katika DVD unao toa maelekezo kwa Waislamu kupiga kuua Ma Padri, Wachungaji , Maaskofu N.K.
2.CCM na serikali yake Wameshindwa kuwalinda viongozi wa dini na hata wanapouawa hakuna hatua za dhati zinazochukuliwa dhidi ya Wauaji .Wamesistiza kuwa hakuna utawala wa Sheria
3.Wameitaka serikali ya kikwete kueleza kufafanua bayana tamko la Mhe Wassira juu ya kuwapa haki Waislamu Kuchinja Wanyama huku akiwakataza Wakristo kufanya hivyo. Wanataka kujua Wasira anaiwakilisha Serikali ya CCM?? Na ametumia Sheria gani Kuwakataza Wakristo kuchinja Wanyama??.
4.Ufafanuzi wa mambo hayo hapo juu umetakiwa kutolewa haraka na ikifika tarehe 25 Feb,2013 Watachukua hatua ya kuthibitisha kuwa Serikali ya CCM na Rais Kikwete wamejifungamanisha na dini ya Kiislamu hivyo , Watawataka wakristo wote kurudisha kadi za CCM na kuzichoma ili kulinda katiba ya nchi!!!!

Hapo ndipo ninapokuwa na wasiwasi na hawa wachungaji uchwara,wachungaji wa vichochoroni.Ukipima kauli zao kwa mwenye akili utagundua kuwa hawa ndio wanahusika na mauaji yanayoendelea nchini.Dhamira yao imeonekana.Kumbe wanataka sheikh Ilunga hasan kapungu akamatwe.Yani mko tayari muwauwe wenzenu ilimradi tu sheikh wetu akamatwe.

Ndio kusema hamtosheki tu,ponda yuko ndani,mukadam yuko ndani na pia viongozi wote wa uamsho wako ndani.Endeleeni tu lakini mkae mkijua mchezo wenu mauti yetu sote.Hapata kalika hapa Tanzania.
 
Ccm tunashukuru kwani tumeyaona hayo mliyokuwa mkiyaita maisha bora kwa kila mtanzania!
Kikwete wewe ni dhaifu na ulicho wahaidi waislam ipo siku utailipa damu ya wakristo inayo uliwa kila kukicha! Ila ccm bye bye
 
Yote haya ni dalili mbaya kwa ccm, huyu ndiye bundi wenu wala msimtafute kwingine kokote
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom