Kesho ijumaa kuu kwa wakristo kula nyama ni mwiko je nikila samaki vipi hapo?

Kwanza inabidi ujue hiyo ni amri ya kanisa sio ya Yesu au Mungu lakini pia kinachokatazwa ni nyama sio samaki lakini akili za kuambiwa changanya na zako kwani usipokula vyote samaki na nyama ukala zako tembele kwa siku moja utapata shida gani? Imarisha Imani yako
Hakuna sehem yyte kwenye bibilia inayakataza mtu kula nyama, hizo ni tamaduni za kipagani za babeli ya kale,

Roma catholic wameziingiza kwa Siri kwenye ibada zao
 
Hii kutokula nyama siku ya ijumaa kuu sio agizo la YESU hata kwenye biblia hamna "
Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi" isaya 8:20
Wamejipatia wapi hili jambo?"Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa" kama kweli ingekua ni mwili wa Yesu tulipaswa kula maana Yesu alisema "aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima" sasa leo watu wanazuiliwa. Mkate na divai ambayo huitwa mwili wa kristo na damu yake mbona tunakula???

Tukubali kuongozwa na biblia, kwenye biblia mitume hawakuaadhimisha icho kitu, sasa kimetoka wapi "
Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu." Mathayo 15:9

Kama biblia inatosha!! Kanuni za kanisa za nini hili kosa walifanya Israel "
Wakaziendea sheria za mataifa, ambao Bwana aliwafukuza mbele ya wana wa Israeli, na sheria za wafalme wa Israeli walizozifanya." 1wafalme 17:8

Ondoka na hii: kama nyama za kesho zinaashiria YESU basi zilipaswa kuliwa maana "
Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake."Yohana 6:56
 
Back
Top Bottom