Uchambuzi wa Sheria ya Kanisa Katoliki ya kutokula nyama siku ya Ijumaa Kuu

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
3,136
2,472
Tumsifu Yesu Kristo

Kwa wakatoliki, leo siku ya Ijumaa kuu ni kumbukumbu ya mateso na kifo cha Yesu Kristo Msalabani.

"funga Jumatano ya majivu usile nyama siku ya Ijumaa kuu".. ni moja ya sheria ya kanisa katoliki.

KWANZA kabisa kabla ya kwenda mbali, lazima tujue kuwa, maana yetu ya msingi katika kutokula nyama, ni moja tu; ile ya KUFUNGA STAREHE.

Lazima tujue na kukubali ukweli kuwa, Ijumaa Kuu ni siku ya mateso na kifo cha Bwana Wetu Yesu Kristo.

Sisi tunafahamu kwamba, haya yote yaani mateso hadi kifo cha Yesu msalabani, yamempata kutokana na dhambi zetu hivyo, nasi tunakusudia kuacha starehe zetu na hivyo, tunafunga ili tujutie dhambi zetu.
Hii ni kusema kuwa, tunafunga ili tupate kuzitubia dhambi tulizozifanya na hivyo, katika kufunga Mungu atuonee huruma na atusamehe dhambi zetu na za wenzetu wengine ambao ni wadhambi kama sisi.

Kufunga huku, ni mapambano baina yetu na dhambi pamoja na mkuu wa dhambi yaani shetani.

Kristo anasema katika Injili ya Marko 6:26 kwamba, katika kesi na masuala fulanifulani, shetani hatoki pasipo sala na kufunga.
Basi, tunapaswa kutambua kuwa hayo tunayoyafanya ni juhudi zetu katika kujichomoa toka kwenye ufalme wa dhambi na mfalme wake yaani SHETANI, na kujiweka mikononi mwa Mfalme wa watakatifu yaani, MUNGU MWENYEZI.

Sasa, suali linakuja hivi, KWA NINI SISI WAKRISTO(WAKATOLIKI) tunaacha kula nyama katika siku hiyo ya Ijumaa Kuu? Nadhani kwetu, hili ndilo suala la msingi.

Ndugu msomaji, tutambue kuwa kuwa, katika suala la kufunga, inampasa mtu kuchagua kitu kizuri cha kukiacha. Kwa mfano, huwezi kufunga kitu kama kula ugali wa muhogo wakati ugali wa namna hiyo kwako ni shida, bali unafunga kitu kizuri kama labda kula wali na pilau. Huko ndiko kweli kufunga, kujikatalia na kujitesa kwa toba.

Ieleweke kuwa, tangu enzi zile za kale, huko ilikoanzia dini yetu na huko lilikoanzia zoezi la kufunga, waamini waliacha kula nyama na vitu vitokanavyo kama vile siagi na maziwa kwa vile vilikuwa ni vitu vinavyochukuliwa na kueleweka kuwa ni vya anasa na vile vilivyowakilisha anasa vilipopatikana.

Badala yake, watu katika sehemu na siku hizo, walipotakiwa kufunga, walikula vitu visivyo vya starehe kama vile samaki na mboga za majani.
Hilo, ndilo tulilolipokea kutoka kwa wamisionari kwamba, tunapofunga tuache kuvitumia vitu vya anasa na starehe; nyama ikiwa ikiwa kitu kimojawapo.

Hata hivyo ndugu msomaji, kwa vile vitu vya starehe sio nyama peke yake hapa duniani, sote tunaombwa, kila mmoja akague vitu vyake vya starehe na hivyo, aviache siku ya kufunga.

Ikiwa kwako sigara ni starehe na anasa, basi nia afadhali kuacha siku ile ya kufunga.
Na kama kwako kuogelea ni anasa na starehe, ni afadhali kuacha huko kuogelea siku ile ya kufunga.

Ikiwa ni kuenesha gari, ni afadhali kuacha siku ile ya kufunga. Na ikiwa ni kucheza disko au muziki, basi yafaa kuacha kwa ajili ya kufunga na kadhalika, na kadhalika ili mradi tu, hizo anasa tuziache kando nasi tupate muda wa kuhuzunika na dhambi zetu tukiomba toba kwa Bwana Wetu Yesu Kristo aliyesulibiwa kwa ajili ya dhambi zetu.

Kabla sijamalizia, napenda nikudokeze sababu mojawapo BINAFSI inayowafanya wengine wafunge nyama siku ya IJUMAA KUU.
Hii ni ile sababu ya kufananisha nyama ya kuliwa na mwili au nyama ya Bwana Wetu Yesu Kristo aliyepigwa mijeledi na kutobolewa na kuchubuliwa na kuachwa ikivuja damu nyingi.
Hii ni hali ambayo huwafanya wengine, washindwe kula nyama wakiona maiti ya mtu yeyote.

Nasisitiza kuwa, sababu hii nimeiita SABABU YA KIBINAFSI kwa sababu Kanisa linapowaomba watu wafunge kula nyama siku ya Ijumaa Kuu, lina hoja moja tu, ile ya kuacha starehe na KUFUNGA, siyo hiyo nyingine ya kuona nyama ya kuliwa kama kitu kinachofanana na nyama au mwili wa Bwana Wetu Yesu Kristo.
Basi hii ni sababu ya pili lakini, ni sababu ya waamini binafasi kuona hivyo na ndivyo wanavyosadiki.

Aidha, ndugu msomaji, tukumbuke kwamba, ikiwa kwetu nyama si starehe, au anasa, maaskofu wetu wanao uwezo wa wa kuturuhusu kuila, ikiwa tutaipata siku ya Ijumaa Kuu wakati kama haiwezekani kuitunza hadi kesho yake.

Kesi hii ni ya pekee vinginevyo, kama kwetu nyuma ni starehe pia, kama tunavyoipenda, basi katika siku ya Ijumaa Kuu, tufunge kuila na siku hiyo basi baada ya kuacha sterehe hiyo, tukumbuke dhambi zetu na kutubu toba ya dhati inayotoka ndani.

Mungu awabariki kwa Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Amina.

images (11).jpeg

images (10).jpeg
 
Sababu ipi inafanya nyama kuwa ni anasa?
Tuoneshe reference ya kifungu chochote cha Biblia kilichoelezea.

Je, dhana ya kuwa kula nyama ni sawa na kula mwili ya YESU Kristo imetoka wapi?
Tuoneshe au tutajie ni kifungu kipi cha Biblia limeelezea.

Sibishani ila ni kwa educational purposes.
 
16:116 - Wala msiseme uwongo kwa kuropokwa na ndimi zenu Hichi halali na hichi haramu, mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu.
Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.
 
Sababu ipi inafanya nyama kuwa ni anasa?
Tuoneshe reference ya kifungu chochote cha Biblia kilichoelezea.

Je, dhana ya kuwa kula nyama ni sawa na kula mwili ya YESU Kristo imetoka wapi?
Tuoneshe au tutajie ni kifungu kipi cha Biblia limeelezea.

Sibishani ila ni kwa educational purposes.
Mkuu jamaa hajasema kula nyama ni anasa.

Kama umemuelewa hilo neno kula nyama linajumuisha kufanya anasa.
Yaweza kua kulewa ndo kula nyama kwako
Kula pilau ndio kula nyama kwako..

Na pia hapo juu mleta uzi katolea ufafanuzi hiyo kula nyama imetoka wapi.
Ni kua hapo kale nyama na siagi ndo vilikua vyakula bora, pendwa na vitamu.
Hivyo basi mtu akifunga anaacha kula hivyo vitamu(nyama na siagi) badala yake anakula vile asivyovipenda kama mbogamboga na samaki.

Sasa basi unapofunga na ukaambiwa usile nyama siku ya ijumaa kuu, basi maana yake ni usifanye anasa.

Na akadokeza pia hiyo ya kuhusisha kula nyama na mwili wa Yesu ni nadharia binafsi ambazo zinafatwa na watu na kuheshimiwa pia.

Maelezo haya ni kutokana na nilivoelewa hii thread.

Nawasilisha.
 
Wakatoliki waumini hawaruhusiwi kula nyama siku ya ijumaa kuu. Kisa heti kula nyama siku ya Leo ni kama kushiriki mateso ya kristo kwa jinsi Alivyo jeruhiwa wakati wa mateso Yake.

Mimi nisemetu unaweza usile nyama kama mkatoliki lakini swali je! Matendo yako yana usafi kiasi gani?

Je ! Pombe na Anasa zingine sindio mbaya kuliko kula nyama siku ya ijumaa kuu?

Tuache nadharia za mapokeo tuwe na usafi wa moyo ndio Ibada Takatifu Mbele za Bwana.

Tena ukichunguza maandiko utagundua siku wana wa Israel wanatoka misri ndio siku Ambayo walikula nyama sana. Maana ndio siku kuu ya kutoka utumwani.
 
Ndugu msomaji, tutambue kuwa kuwa, katika suala la kufunga, inampasa mtu kuchagua kitu kizuri cha kukiacha. Kwa mfano, huwezi kufunga kitu kama kula ugali wa muhogo wakati ugali wa namna hiyo kwako ni shida, bali unafunga kitu kizuri kama labda kula wali na pilau. Huko ndiko kweli kufunga, kujikatalia na kujitesa kwa toba.
Je nyama kitu kizuri kwa kila mkatoliki au ilikuwa nzuri kwa aliyekuja na hilo wazo
 
Tumsifu Yesu Kristo

Kwa wakatoliki, leo siku ya Ijumaa kuu ni kumbukumbu ya mateso na kifo cha Yesu Kristo Msalabani.

"funga Jumatano ya majivu usile nyama siku ya Ijumaa kuu".. ni moja ya sheria ya kanisa katoliki.

KWANZA kabisa kabla ya kwenda mbali, lazima tujue kuwa, maana yetu ya msingi katika kutokula nyama, ni moja tu; ile ya KUFUNGA STAREHE.

Lazima tujue na kukubali ukweli kuwa, Ijumaa Kuu ni siku ya mateso na kifo cha Bwana Wetu Yesu Kristo.

Sisi tunafahamu kwamba, haya yote yaani mateso hadi kifo cha Yesu msalabani, yamempata kutokana na dhambi zetu hivyo, nasi tunakusudia kuacha starehe zetu na hivyo, tunafunga ili tujutie dhambi zetu.
Hii ni kusema kuwa, tunafunga ili tupate kuzitubia dhambi tulizozifanya na hivyo, katika kufunga Mungu atuonee huruma na atusamehe dhambi zetu na za wenzetu wengine ambao ni wadhambi kama sisi.

Kufunga huku, ni mapambano baina yetu na dhambi pamoja na mkuu wa dhambi yaani shetani.

Kristo anasema katika Injili ya Marko 6:26 kwamba, katika kesi na masuala fulanifulani, shetani hatoki pasipo sala na kufunga.
Basi, tunapaswa kutambua kuwa hayo tunayoyafanya ni juhudi zetu katika kujichomoa toka kwenye ufalme wa dhambi na mfalme wake yaani SHETANI, na kujiweka mikononi mwa Mfalme wa watakatifu yaani, MUNGU MWENYEZI.

Sasa, suali linakuja hivi, KWA NINI SISI WAKRISTO(WAKATOLIKI) tunaacha kula nyama katika siku hiyo ya Ijumaa Kuu? Nadhani kwetu, hili ndilo suala la msingi.

Ndugu msomaji, tutambue kuwa kuwa, katika suala la kufunga, inampasa mtu kuchagua kitu kizuri cha kukiacha. Kwa mfano, huwezi kufunga kitu kama kula ugali wa muhogo wakati ugali wa namna hiyo kwako ni shida, bali unafunga kitu kizuri kama labda kula wali na pilau. Huko ndiko kweli kufunga, kujikatalia na kujitesa kwa toba.

Ieleweke kuwa, tangu enzi zile za kale, huko ilikoanzia dini yetu na huko lilikoanzia zoezi la kufunga, waamini waliacha kula nyama na vitu vitokanavyo kama vile siagi na maziwa kwa vile vilikuwa ni vitu vinavyochukuliwa na kueleweka kuwa ni vya anasa na vile vilivyowakilisha anasa vilipopatikana.

Badala yake, watu katika sehemu na siku hizo, walipotakiwa kufunga, walikula vitu visivyo vya starehe kama vile samaki na mboga za majani.
Hilo, ndilo tulilolipokea kutoka kwa wamisionari kwamba, tunapofunga tuache kuvitumia vitu vya anasa na starehe; nyama ikiwa ikiwa kitu kimojawapo.

Hata hivyo ndugu msomaji, kwa vile vitu vya starehe sio nyama peke yake hapa duniani, sote tunaombwa, kila mmoja akague vitu vyake vya starehe na hivyo, aviache siku ya kufunga.

Ikiwa kwako sigara ni starehe na anasa, basi nia afadhali kuacha siku ile ya kufunga.
Na kama kwako kuogelea ni anasa na starehe, ni afadhali kuacha huko kuogelea siku ile ya kufunga.

Ikiwa ni kuenesha gari, ni afadhali kuacha siku ile ya kufunga. Na ikiwa ni kucheza disko au muziki, basi yafaa kuacha kwa ajili ya kufunga na kadhalika, na kadhalika ili mradi tu, hizo anasa tuziache kando nasi tupate muda wa kuhuzunika na dhambi zetu tukiomba toba kwa Bwana Wetu Yesu Kristo aliyesulibiwa kwa ajili ya dhambi zetu.

Kabla sijamalizia, napenda nikudokeze sababu mojawapo BINAFSI inayowafanya wengine wafunge nyama siku ya IJUMAA KUU.
Hii ni ile sababu ya kufananisha nyama ya kuliwa na mwili au nyama ya Bwana Wetu Yesu Kristo aliyepigwa mijeledi na kutobolewa na kuchubuliwa na kuachwa ikivuja damu nyingi.
Hii ni hali ambayo huwafanya wengine, washindwe kula nyama wakiona maiti ya mtu yeyote.

Nasisitiza kuwa, sababu hii nimeiita SABABU YA KIBINAFSI kwa sababu Kanisa linapowaomba watu wafunge kula nyama siku ya Ijumaa Kuu, lina hoja moja tu, ile ya kuacha starehe na KUFUNGA, siyo hiyo nyingine ya kuona nyama ya kuliwa kama kitu kinachofanana na nyama au mwili wa Bwana Wetu Yesu Kristo.
Basi hii ni sababu ya pili lakini, ni sababu ya waamini binafasi kuona hivyo na ndivyo wanavyosadiki.

Aidha, ndugu msomaji, tukumbuke kwamba, ikiwa kwetu nyama si starehe, au anasa, maaskofu wetu wanao uwezo wa wa kuturuhusu kuila, ikiwa tutaipata siku ya Ijumaa Kuu wakati kama haiwezekani kuitunza hadi kesho yake.

Kesi hii ni ya pekee vinginevyo, kama kwetu nyuma ni starehe pia, kama tunavyoipenda, basi katika siku ya Ijumaa Kuu, tufunge kuila na siku hiyo basi baada ya kuacha sterehe hiyo, tukumbuke dhambi zetu na kutubu toba ya dhati inayotoka ndani.

Mungu awabariki kwa Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Amina.

View attachment 2188233

View attachment 2188234
Hiyo sio sheria ya Kanisa Katoliki ni sheria ya kanisa katoliki la Tanzania. Sheria za Kanisa Katoliki zinapatikana ktk Codes Iuris Canonicis. Kwa kukusaidia Sheria ya Kanisa Katoliki inakataza kula nyama Ijumaa zote sio Ijumaa Kuu tu. Kanisa la Tanzania kutokana na mazingira ya watu ndio wakaweka hiyo ya Ijumaa Kuu.
 
Mimi nisemetu unaweza usile nyama kama mkatoliki lakini swali je! Matendo yako yana usafi kiasi gani?
Gujiakili guzitoooo!! km grease!!…..hata km matendo yake si masafi ndo maana tuliagizwa..''kesheni mkiomba maana hajui siku wala saa'' !! sasa unajuaje km amekuja humu baada ya kutubu na akasamehewa??
e ! Pombe na Anasa zingine sindio mbaya kuliko kula nyama siku ya ijumaa kuu?
Pombe ni anasa kwako cha pombe wewe!!….....kuna watu humu Duniani akisikia harufu tu ya pombe anatapika, anaugua, kichefu chefu, kifupi anakuwa mwehu!...usihukumu watu kwa jinsi unavooona weye!
 
Back
Top Bottom