Nimegundua matajiri wengi hapa Tanzania hawajasoma

dr namugari

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
9,474
16,037
Ikiamuacha MO dewji ambae amerithi Mali za wazazi wake hakuna tajiri mwingine mwenye degree wala diploma wengi wao wameishia darasa la Saba au darasa la nne, kule Arusha matajiri wa darasa la nne wako wengi sana tena ni watu maarufu sana wameliteka jiji kwa biashara za utalii, madini ya tanzanite na biashara za mifuko.

Jana nilikutana na tajiri mmoja hapa Dodoma aliishia darasa la saba nikamuambia kama siyo shule imenipotezea muda leo ningekuwa mbali mno tena tungekuwa tunakula sahani Moja na wewe alichekaa sana ndipo akasamema yeye angepata hata robo ya elimu yangu hata diploma tu angekuwa billionaire had sasa hivi, nikaona kabisa anatamani elimu yangu na mimi natamani biashara yake.

Akasema laiti angeishia hata fom four au diploma angepasua sana na madili kibao angepiga.

Akanimbia elimu ni Bora sana kama una akili za maisha ila ni mbaya sana kama unashindwa kutimia elimu yako kupata kipato.

Mwisho akasema yeye sasa hivi anahakiksha watoto wake wanapata elimu Bora wote wamesoma St Constantine arusha huko ada milion 15.

Mzee huyu ni mfanyabisha mdogo sana wa pembejeo za kilimo na viuatilifu

Imagine ni matajiri wangapi wamesoma Wana elimu kubwa una wafahamu? Mzee Mengi marehemu ana Diploma ya Uhasibu the rest ni la saba au form four failures!
 
Kuwa tajiri huwa haitgemei umesoma au haujasoma

Maana kufanikiwa katika maisha hutegemea na MTU Kuwa na Elimu ya kujitambua "the sense of who you are"

Hivyo MTU anayefanikiwa kujitambua akajua udhaifu wake na uimara wake ulipo anaweza kutoboa ktk maisha hata Kama hajasoma.

Hapa duniani ukiwa unajitambua to the fullest kuna speed unakuwa nayo katika kuelekea kufanikiwa.
 
Elimu ni muhimu maishani..Pia kingine Tambua Kila mtu ana njia yake ya kutoboa usilinganishe matajiri hao wachache ambao hawakufika mbali kielimu .

Kuna jambo amegusia hapo anapenda watoto wake wafike mbali kielimu bado anapenda kujifunza manake vitabu,majarida n.k wanapitia Sana watu wa dizaini hii(matajiri) maana kuna mbinu nyiiingi za kutoboa
 
Katika Mazingira yetu ya Kiswahili' utajiri Kwa maana ukiyoitumia hapa ... Unategemea mambo mengi sana. Mojawapo ni Bahati .. hayo mengine ni mchanganyiko wa saikolojia , Mila na Utamadini. Mambo haya Ndio yanawafanya Std Seven na Nne waendelee kuongoza! Hujajiukiza ni Kwa Nini huyo wa tajiri wa Dodoma anatamani Elimu! ? Alipitia njia niliyoileleza hapo juu .. na asijokijua ni kuwa pengine asingeweza fanikiwa kwa vile anavyowqza Sasa!
 
Hujasoma, unapambana mpaka unakua tajiri halafu unawasomesha watoto wanakua na elimu ya darasani hawana elimu ya maisha, ukifa ule utajiri nao unapotea. Hili ni tatizo kubwa sana kwenye jamii zetu, watoto wanaishia kurithi nyumba na viwanja ila ile akili ya mzee iliyoleta mali hawana.

Tusomeshe watoto ila tusisahau kuwa kuna elimu muhimu zaidi ya vyeti, elimu ya maisha.
 
Ikiamuacha MO dewji ambae amerithi Mali za wazazi wake hkuna tajiri mwingine mweny degree Wala diploma wengi wao Ni darasa la Saba au darasa la nne, kule Arusha matajiri wa darsa la nne wako wengi sana tena ni watu maarufu sana wameliteka jiji kwa biashara za utalii, madini ya tanzanite na biashara za mifuko.

Janaa nilikutana na tajiri mmoja hapa dodoma aliishia darasa la saba nikamuambia kama siyo shule imenipotezea muda leo ningekuwa mbali mno tena tungekuwa tunakula sahani Moja na wewe alichekaa sna nndipo akasamema yey Angepata hata robo ya elimu yangu hata diploma tu angekuwa billionaire had SAS hv ,nikaona kabsa anatamani elimu yangu na mimi natamani biashara yake.

Akasema laiti angeishia hata fom four au diploma angepasua sna na madili kibao angepiga.

Akanimbia elimu ni Bora sana kama una akili za maisha ila ni mbaya sana kama unashindwa kutimia elimu yako kupata kipato.

Mwisho akasema yeye sasa hivi anahakiksha watoto wake wanapata elimu Bora wote wamesoma St Constantine arusha huko ada milion 15.

Mzee huyu Ni mfanyabisha mdogo sana wa pembejeo za kilimo na viuatilifu

Imagine Ni matajiri wangapi wamesoma Wana elimu kubwa una wafahamu? Mzee Mengi marehemu ana Diploma ya Uhasibu the rest ni la saba au form four failures!
Mi ni Tajiri zaidi yao kwa afya na amani ya rohoni, hutaki andamana maana Mungu amenineemesha katika hilo.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
FB_IMG_17110489395627561.jpg



Wasomi wengi wanapenda kuparemba sana sehemu ya kulala wakati watafutaji wa kweli wanaweza kulala popote hata bila kuoga
 
Hujasoma, unapambana mpaka unakua tajiri halafu unawasomesha watoto wanakua na elimu ya darasani hawana elimu ya maisha, ukifa ule utajiri nao unapotea. Hili ni tatizo kubwa sana kwenye jamii zetu, watoto wanaishia kurithi nyumba na viwanja ila ile akili ya mzee iliyoleta mali hawana.

Tusomeshe watoto ila tusisahau kuwa kuna elimu muhimu zaidi ya vyeti, elimu ya maisha.
Sahhuh kbsa
 
Kuwa tajiri huwa haitgemei umesoma au haujasoma

Maana kufanikiwa katika maisha hutegemea na MTU Kuwa na Elimu ya kujitambua "the sense of who you are"

Hivyo MTU anayefanikiwa kujitambua akajua udhaifu wake na uimara wake ulipo anaweza kutoboa ktk maisha hata Kama hajasoma.

Hapa duniani ukiwa unajitambua to the fullest kuna speed unakuwa nayo katika kuelekea kufanikiwa.
Kujitambua tu haiwezi kukufanya uwe tajiri
 
Hakuna uhusiano (wa moja kwa moja) kati ya elimu na utajiri. Na ukweli huu unasimama karibu dunia nzima. Ni Tanzania (au niseme Afrika) ambako elimu imevishwa jukumu lisilo lake la kuwatajirisha waipatayo. Na hiki ni kichochezi kimojawapo kikubwa cha ufisadi huu wa kihayawani tunaoushuhudia huku kwa mtu mweusi. Nitashangaa sana kumkuta eti profesa wa Marekani ametajirika. Atapata wapi muda wa kufanya biashara wakati jukumu lake kuu ni kufanya utafiti na kurithisha maarifa na uzoefu wake kwa kizazi kipya?

Kama unataka mtoto wako awe tajiri basi elimu ya kidato cha 4 au 6 inamtosha sana. Ajabu sasa hata akija kutajirika bado atahitaji walimu ili wamsomeshee watoto wake. Bado akiumwa atahitaji madaktari. Akitaka kujenga maghorofa yake atahitaji wasanifu wa majengo. Na Range Rover lake jipya litahitaji mainjinia wa barabara...na mengineyo.

Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba elimu inahitajika ili kujenga fani ambazo zinahitajika katika jamii iliyostaarabika; na jukumu lake kuu siyo kuwatajirisha wenye nayo. After all, mifumo ya uchumi jinsi ilivyosukwa, kamwe haiwezeshi watu wengi kutajirika. Ndiyo maana katika serikali/jamii zinazojitambua jukumu kuu la serikali huwa ni kuinua maisha ya watu wote kwa kuhakikisha kuwa wanapata mahitaji yao ya msingi na kuishi maisha yanayoridhisha maana kusema eti wote/wengi wawe matajiri haiwezekani.

Hii obsession ya kwamba eti wasomi (wengi/wote) wanapaswa kutajirika kwa vile tu wamesoma ni kiinimacho tu ambacho hakina uhalisia katika kanuni za kiuchumi na uhalisia wa maisha.
 
Back
Top Bottom