Mjanja M1
JF-Expert Member
- Oct 7, 2018
- 4,023
- 14,177
MADAKTARI wawili ambao ni Dk. Obote Casto na Dk. Deus Chacha wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kumtoa mimba mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kazi zao.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme wakati akizungumza na watumishi wa idara ya afya kutoka Halmashauri za Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama kama sehemu ya kuwakumbusha wajibu wao na kuagiza wale wanaobainika kwenda kinyume na misingi ya kazi zao wawajibishwe kisheria na siyo vinginevyo.
Chanzo: Nipashe