Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,853
121,988
Wanabodi,
Leo asubuhi hii waheshimiwa wabunge wetu, wataujadili mkataba wa IGA ( Intergovernmental Agreement), na baada ya hapo ndipo HGA ( Host Government Agreement) zitaingiwa kati ya TPA na DPW baada ya IGA kupitishwa.

IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai, kuruhusu kampuni ya DP World ya Dubai, kutuboreshea Bandari zetu.

Huku mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kumeisha anza kuibuka makundi sogozi yanayoleta uhayawani wa sentiments za kibaguzi, Mwarabu wa Oman anataka kumpa Bandari yetu Mwarabu wa Dubai hivyo Watanzania Wazalendo tusikubali!. Hawa ni muflis!.

Kule nyuma nilipopandisha pandisha bandiko hili Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu waliteswa, hasiwa, bakwa, na kuuawa kinyama nilitoa angalizo hili
Wanabodi,
Lengo la uzi huu sio ubaguzi, au kuwakumbusha machungu ya Waarabu, bali ni kujikumbusha tuu historia na kuwaelimisha baadhi ya wenzetu, wasiowajua hawa Waarabu wa Unguja na Pemba waliwafanya nini mababu zetu!.

Ila pia naomba kutoa Maangalizo muhimu yafuatayo:

1. Tuwe makini sana na watu waliofilisika kiakili ambao watachanganya Uarabu na dini ya Kiislam simply because, Dini ya Kiislamu inatumia lugha ya Kiarabu!. Masikini muflisi hawa, hawajui kuwa hata Ukiristo umeanzia Arabuni. Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismail, aliyezaa na mjakazi wa ki Misri, na Wakristo ni uzao wa Isaka aliyezaa na mkewe Sara. Hata Yesu Kristo, licha ya kuzaliwa Israel, alikulia Misri na alizungumza lugha ya Kiarabu!. Hapa mimi nazungumzia udhalimu wa Waarabu kama jamii na sio dini ya Kiislamu.

Udhalimu ni udhalimu tuu hauna dini, wala kabila, wala jamii, kwa sababu kwenye udhalimu sio Waarabu tuu peke yao ndio madhalimu, watu wa mataifa mbalimbali wamefanya udhalimu kwa watu wa mataifa mengine, na mfano mzuri ni udhalimu wa Wajerumani kwa Mayahudi chini ya Hitler ulioitwa Halocust ambapo Hitler aliwaua Wayahudi zaidi ya milioni 6 kwa ukatili wa ajabu!, ila kwenye biashara ya Utumwa Unguja, Pemba, na Arabuni, watumwa hawa walihasiwa hivyo kufanyiwa genoside na wahusika sii wengine bali ndugu hawa hawa ndugu zetu Waarabu ambao leo tunakula nao, tunakunywa nao na kufurahi nao kwa vile tumeisha samehe na tumeishasahau, yaliyopita sii ndwele.

Hawa Waarabu wa leo, ni vizalia vya Waarabu wale wale, ila hawa wa sasa, ni Waarabu wema, wastaarabu kama Waarabu wa sasa, wenye roho nzuri, sio wakatili, sio wadhalimu na wanawapenda watu weusi na kuwaoa kwa mapenzi, huku wanawake wao, wakiwapenda weusi na wakiolewa nao japo mwanzo ilikuwa ni kwa kulazimishwa na Karume, hivyo nashauri, kwa siku zijazo, hata Waarabu hawa, ama machotaa wao, wakishiriki tena uchaguzi, wakashinda kwenye uchaguzi huru na wa haki, wapewe tuu nchi watawale kwa sababu Waarabu hawa sii wale, wasinyimwe kutawala eti kwa sababu tuu ni Waarabu.

Waarabu wa enzi za utumwa, walikuwa madhalimu, hivyo kuendelea kudhani hata hawa wazaliwa wao pia ni lazima watakuwa ni madhalimu!, kwa kanuni ya mwana wa nyoka ni nyoka!, hivyo wanashinda uchaguzi lakini hawapewi, sio kuwatendea haki.

Japo mwana wa nyoka nyoka lakini si lazima kila mwana wa nyoka awe ni nyoka mwenye sumu kali, nyoka wengine ni kama joka la mdimu, halina madhara, hivyo Waarabu hawa wa leo wamebadilika, kwa sababu hata shetani mwanzo alikuwa malaika, hivyo Waarabu hawa wa sasa ni Waarabu wema, ni wenzetu na ni sehemu yetu, ukifanyika uchaguzi tena, wakishinda, wapewe tu nchi.

Paskali
Angalizo hili ni muhimu sana kwenye mjadala wa leo mule Bungeni kwetu. Tunawategemea kuwasikia waheshimiwa wabunge wetu wakitanguliza mbele maslahi ya taifa letu katika kulijadili hili la DP World. Hatutarajii kabisa kutokea mbunge mmoja yoyote muflis kuipinga DP World kwa Uarabu wao, kwa hoja za kibaguzi za Mwarabu ni Mwarabu tuu, awe ni Mwarabu wa Oman, Mwarabu wa Dubai, Mwarabu wa Arabuni, Mwarabu wa Zanzibar, Mwarabu ni Mwarabu tuu ni wale wale na mambo yao ni yale yale..., watu wa type hii ni ma hayawani!, hatutegemei kabisa uhayawani huu ukaibuka kwenye mjadala huu!.

Naendelea kusisitiza, ikitokea wewe huwezi jambo fulani, lazima utasaidiwa tuu!, utake kusaidiwa, utasaidiwa, usitake kusaidiwa, utasaidiwa!, mpaka pale utakapoweza kujisaidia! Watanzania tujifunze kujikubali kuwa kuna vitu hauwezi, na tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Nawatakia waheshimiwa wabunge wetu mjadala na majadiliano mema kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Paskali
Update
Nimefuatilia mjadala huu mwanzo mwisho, Bunge limeridhia, japo maslahi ya taifa yamezingatiwa, lakini we should have done more,
  1. Watanzania tupatiwe a due diligence report ya DP World ni kampuni ya nani?.
  2. Tanzania ni nchi sovereign, Dubai sio sovereign, Government inawezaje kuingia mkataba wa kiserikali na taasisi isiyo sovereign?. Nchi ni UAE na sio Dubai!.
  3. Serikali yetu inawezaje kuingia mkataba na kampuni binafsi ya DP World na kujifanya ni serikali ya Dubai?.
  4. Tungeweza kufanya as PPP na sio at governmental level!.
  5. Something fishy!.
Sasa ndio naelewa madudu ya ajabu ajabu huwa yanapita vipi hadi Bungeni mwetu zikiwemo sheria batili na hadi kuchomekewa ndani ya katiba yetu!.

Hongera Bunge letu kusupport kila kitu cha serikali, hata madudu!.
Hongera Wabunge wetu kujadili mlicholetewa kwenye karatasi bila kufanya homework yoyote!.
Hongera Spika Dr. Tulia, Mwanasheria mbobezi mbobevu kuruhusu Inter Governmental Agreement na kampuni inayojifanya ni serikali ya Dubai bila Bunge letu kufanya a due diligence report!.

Namalizia kwa kusisitiza, Mama ana nia Njema ila lazima asaidiwe asiingizwe chaka!.

P
 
Wanabodi,
Leo asubuhi hii waheshimiwa wabunge wetu, wataujadili mkataba wa HGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai, kuruhusu kampuni ya DP World ya Dubai, kutuboreshea Bandari zetu.

Huku mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kumeisha anza kuibuka makundi sogozi yanayoleta uhayawani wa sentiments za kibaguzi, Mwarabu wa Oman anataka kumpa Bandari yetu Mwarabu wa Dubai hivyo Watanzania Wazalendo tusikubali!. Hawa ni muflis!.

Kule nyuma nilipopandisha pandisha bandiko hili, nilitoa angalizo hili



Nawatakia waheshimiwa wabunge wetu mjadala mwema.

Paskali
Watanzania tumegawanyika......!!
 
Wanabodi,
Leo asubuhi hii waheshimiwa wabunge wetu, wataujadili mkataba wa HGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai, kuruhusu kampuni ya DP World ya Dubai, kutuboreshea Bandari zetu.
Watu tulisheherekea kuuwawa/kuuliwa kwa demokrasia ya kweli na kufufuliwa demokrasia ya uongo sasa matunda tunayavuna wote pasipokujalisha wakijani/wabluu/wanjano/zambarao au mweusi,Chawa au sio chawa.Sasa tumeipata kazi,na sasa kazi kwetu😂
 
Wanabodi,
Leo asubuhi hii waheshimiwa wabunge wetu, wataujadili mkataba wa HGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai, kuruhusu kampuni ya DP World ya Dubai, kutuboreshea Bandari zetu.
atu wa type hii ni ma hayawani!, hatutegemei kabisa uhayawani huu ukaibuka kwenye mjadala huu!.

Naendelea kusisitiza, ikitokea wewe huwezi jambo fulani, lazima utasaidiwa tuu!, utake kusaidiwa, utasaidiwa, usitake kusaidiwa, utasaidiwa!, mpaka pale utakapoweza kujisaidia! Watanzania tujifunze kujikubali kuwa kuna vitu hauwezi, na tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Nawatakia waheshimiwa wabunge wetu mjadala na majadiliano mema kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Paskali
"Ukitaka kula lazima na wewe uliwe kidogo". By JK
 
Moja na vitu muhimu kabisa kwenye nchi yetu ni Bandari, kwa hiyo Wabunge wa CCM mkithubutu kuiuza bandari yetu kwa waarabu aisee hapatatosha, pelekeni ujumbe huu kwa Mwenyekiti na Katibu wenu mkuu wa chama mapemaa kwamba kinakwenda kunuka.

Suala la kisingizio cha ufanisi ni la kitoto, yaani mnashindwa kuendesha bandari kweli? kweli ? sasa kama Bandari inawashinda je hii nchi mtaifikisha wapi?
 
Kuwaamulia wabunge nini waongee na nini wasiongee huoni kuwa huo nao ni Uhayawani?

Nchi Si mafungu ya nyanya kwamba anunue Dar na kupewa NYONGEZA bandari zote zilizobaki!!!

Ilani ya Uchaguzi ya 2020 ya CCM haikuwapa ruksa sa100 na Magu kuuza bandari bila UKOMO.

KATIBA hii hii pia haimpi ruksa kiongozi kuuza Nchi. Tunao Watanzania wanaoweza wakiwezeshwa.
 
Tunawategemea kuwasikia waheshimiwa wabunge wetu wakitanguliza mbele maslahi ya taifa letu
Hii kitu ni lini walitekeleza? Tuongee tu ukwel kbs bila unafiki, wabunge wa CCM wao ni kanyaga twende!! Ukiletwa muswada bungeni wa chap chap wao ni kupitisha kwa kishindo!! Hilo la kuwaasa kuweka maslahi ya Taifa mbele liondoe. Ng'wizukulu Mayala!!
 
Moja na vitu muhimu kabisa kwenye nchi yetu ni Bandari, kwa hiyo Wabunge wa CCM mkithubutu kuiuza bandari yetu kwa waarabu aisee hapatatosha, pelekeni ujumbe huu kwa Mwenyekiti na Katibu wenu mkuu wa chama mapemaa kwamba kinakwenda kunuka.

Suala la kisingizio cha ufanisi ni la kitoto, yaani mnashindwa kuendesha bandari kweli? kweli ? sasa kama Bandari inawashinda hii nchi je utaifikisha wapi?
Acha mikwara ,bandari itauzwa na hakuna wakuleta fyoko.
 
Nimemsikiliza bwana msigwa anasema eti ili kuiendeleza bandari inabidi wakope zaidi ya trilioni 6 sijui, hawawezi fanya hivyo sababu kuna mengi wanapaswa kufanya, ujenzi wa mashule, mabarabara, umeme kusambazwa.

Nikawaza sasa kama wanajiona hivyo hawawezi, si waachie ngazi, wenye uwezo waisogeze tanzania mbele.. miaka 60 ya uhuru tunajisifia kujenga zahanati, unacheka na kusikitika kwa pamoja.
 
Hapo uliposema mwarabu ni mwarabu tu, awe wa Oman, Tanzania, au Dubai, wote ni waarabu tu, mambo yao ni yale yale, na wote ni wale wale mahayawani!. nimepaelewa zaidi.

Wale wabunge leo wakiridhia tukaingizwa kwenye huo uhayawani walaaniwe wote watakaounga mkono, na vizazi vyao mpaka cha saba.
 
Back
Top Bottom