SoC01 Vijana kutumia ardhi kubwa tuliyonayo kwa Kilimo

Stories of Change - 2021 Competition

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,589
Habari JF,

Tanzania kama zilivyo nchi nyingine tatizo la ajira limekua sugu kwa vijana . Takwimu zinaonyesha kundi la vijana linaongezeka; kutakuwa na ongezeko la vijana kufikia million 15 kufikia mwaka 2030 tofauti na sasa ambapo idadi ni million 11. Hili ongezeko la vijana linaweza kuwa na athari nyingi kama halitakuwa limewekezwa vizuri na jamii (invested)., kutojithamini(confidence/low self esteem),na kukosa uwezo wa kujihudumia kwa vitu muhimu na kuingia kwenye uhalifu. Hizi ni baadhi ya athari zinazoweza kuonekana kwa vijana. Huu ni mzigo ambao jamii itaubeba kwa gharama kubwa, kupunguza mzigo kwa jamii na kuboresha Maisha ya vijana (livelihoods) nchi yetu inahitaji mikakati mipya wa kupambana na tatizo la ajira.

Ningependa kupendekeza nchi yetu iwekeze kuwapa ajira vijana kupitia Kilimo. Kilimo ni uti wa mgongo na asilimia 76 ya watanzania tunategemea kilimo na kinachangia sana kwenye pato la taifa hivyo ni eneo lenye potential kuongeza ‘income’ kwa mtu mmoja mmoja na kwa nchi yetu. Nimeona pia mahali tuna Ardhi ya rutuba (Arable land) ambayo ni kubwa sana (44millions hectares) ambayo matumizi yake kwa sasa ni madogo (33% only),tunaweza ku ‘optimize’ matumizi yetu ya ardhi kufikia at least 90% na tutaona maendeleo.

Bandiko hili naomba tushirikiane njia za ku ‘optimize’ matumizi ya ardhi yetu kwenye kuwapatia vijana ajira. Mimi ningependakwanza kushauri kubadilisha ‘attitude’ ama ‘mind set’ za vijana wa sasa kuhusu kilimo,wengi wanaona kilimo ni cha kwa waliofeli, na ‘hakilipi’.. Mimi sio mchumi ila nahisi serikali ikiweka muundo mzuri wa kununua mazao kutoka kwa wakulima,au kutafuta masoko ya wakulima ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kununua mazao hayo labda itasaidia vijana kuingia kwenye kilimo. Namaanisha serikali ifanye ku ‘deal’ na manunuzi ya mazao na vijana wa deal only na kulima, yaani kuwe na security fulani mtu akilima ajue atamuuzia nani na wapi….kukiwa na hiii 'security' ya masoko ndivyo watu/vijana watajiingiza kwenye kilimo bila kuogopa kuwa kilimo hakilipi.

Pia ikiwekwa kama ‘policy’ au utaratibu maalumu kwa vijana labda kwa umri wa miaka 16-27 wanaotaka kuingia kwenye kilimo wafanye hivyo, kama vile jeshini watu wanaingia wakimaliza secondary hivyo hivyo iwe ni utaratibu kwa vijana wanaotaka kuingia kwenye kilimo wawezeshwe na criteria iwe UMRI tu!! hii itasaidia kuvuta kundi kubwa la vijana wanaotaka kujiunga na kilimo ambao wana different ‘characteristics’ or ‘backgrounds’ rich/poor,educated/non educated etc hii itaondoa stigma kuwa kilimo ni cha kwa waliofeli.


Mapendekezo yangu nini kifanyike kuwasaidia vijana waingie kwenye kilimo;

Vijana wengi wanapungukiwa na fedha kumudu gharama za kununua mashamba na kulima, kwa hili naishauri serikali ifanye utaratibu wa kuwagaia viwanja vijana mashamba, tuna ardhi ya kutosha kwa kila kijana hesabu (44 millions hectares/ 11 millions young people) . Micro loans pia zinaweza kusaidia vijana kulipa gharama za kulima.

Kuwe na team maalumu wizara ya kilimo itakayo-deal na ku explore wanunuzi wa mazao ndani na nje, sasa hivi wizara inafanya kazi kijumla sana, inabidi kitengo kigawanywe ndani ya wizara kudeal na manunuzi ya mazao.

Mafunzo kwa vijana kufanya kilimo cha kiwango kikubwa (large scale), tutoke mahali tulipo sasa ambapo wengi tunafanya ‘small scale farming’ ambayo saa nyingine ni ngumu ku ‘survive’ na pia mafunzo kutumia ‘technology’ kulima.

Kuwe na utaratibu wa kuhakikisha vijana wanabaki kwenye kilimo kwa mfano ruzuku (subsidy), ‘vouchers’ za bei rahisi ( discounted fee rates) za kununua mbegu, mbolea ambazo zimelenga au mahususi kwa vijana pekee wanaojishughulisha na kilimo.

Nyingine nawakaribisha kujazia
 
Umeandika vizuri.. ila kweli kama una lengo la kushinda hizo milioni tano inabidi upitie upya spelling zako na kuchanganya maneno ya kizungu na kiswahili

Asante kwa ushauri, i hope sitahesabiwa kwa uandishi pekee, ;)
 
Code mixing nyingi sana, kama ni kiswahili kinatakiwa kiwe kiswahili sanifu mwanzo mwisho na kama ni kiingereza basi pia kiwe kiingereza mwanzo mwisho.

Mindset = Fikra
Policy =Sera
Stigma = Dhana
Hayo ni baadhi
Hongera kwa mawazo mazuri.
 
Umeandika vizuri.. ila kweli kama una lengo la kushinda hizo milioni tano inabidi upitie upya spelling zako na kuchanganya maneno ya kizungu na kiswahili
Mkuu,hivi kwenye hili shindano huruhusiwi kuchanganya lugha?
Naomba kueleweshwa.
 
Kama hauna ulazima wa kuchanganya lugha, usichanganye.. milioni 5 ni kubwa Mkuu.. inahitaji umakini mkubwa kuipata.. labda kama unaandika andika tu huitaki hiyo hela 😁

Acha kunichomea utambi basi 🤣
 
Mikopo midogo midogo ni muhimu sana kwa vijana wanaotaka kujiajili katika kilimo au ufugaji. Tatizo naloliona mimi ni namna ya kupata hiyo mikopo. Utakutana na vikwazo vifuatavyo
1. Dhamana. Hapo kijana uliyemaliza chuo unakaa kwa mzazi wako kupata dhamana ni ngumu sana
2. Mikopo mingi wanasema wanatoa kwa kupitia vikundi. Imagine mtaani wewe ndo umepata idea nzuri ya kuanzisha kilimo au ufugaji ukitaka mkopo unaambiwa mpaka muwe kikundi sasa hao wengine unawatoa wapi

NB
Hizi benk za kilimo kwangu mm naona ni kwa ajili ya wakulima wakubwa sidhani kama ni mkombozi kwa wakulima wadogo wadogo wanaoanza
Serikali tengenezeni utaratibu wa kuwainua wakulima wachanga na kuwatia moyo kama ilivyo kwa wamachinga basi tuwe na kundi la wamachinga wa kilimo hawa watasaidia sana kuinua uchumi wa Taifa
 
Mkuu, hongera kwa kushusha uzi fikirishi, but...

Serikali tayari leo tarehe 15 july 2021, tayari imesha pandisha kodi kwenye pembejeo za kilimo. So mambo kama hayo yanaendeleza kudumaza sekta hiyo na kuonekana wanaoifanya watu wafanyao kwa ajili ya kula tu sio kilimo biashara.

But, kwenye suala la mikopo, bado napo ni changamoto maana vijana wengi hawaaminiki kabisa kulingana na maisha walio lelewa katika mambo ya pesa, lakini wenda tukibadilisha baadhi ya mambo katika elimu yetu tunaweza kutengeneza uwajibikaji na uaminifu mkubwa.
 
Mkuu, hongera kwa kushusha uzi fikirishi, but...

Serikali tayari leo tarehe 15 july 2021, tayari imesha pandisha kodi kwenye pembejeo za kilimo. So mambo kama hayo yanaendeleza kudumaza sekta hiyo na kuonekana wanaoifanya watu wafanyao kwa ajili ya kula tu sio kilimo biashara.

But, kwenye suala la mikopo, bado napo ni changamoto maana vijana wengi hawaaminiki kabisa kulingana na maisha walio lelewa katika mambo ya pesa, lakini wenda tukibadilisha baadhi ya mambo katika elimu yetu tunaweza kutengeneza uwajibikaji na uaminifu mkubwa.

Serikali zetu zinafanya kazi kwa kubutua tu,hakuna kuangalia athari za matendo yao sasa hivi na baadae...so sad
 
Takwimu kutoka Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa asilimia 28 ya watu duniani wanajihusisha na kilimo.
Hii imepungua kutoka asilimia 44 mwaka 1991.

Je, huoni kuwa kuwa na asilimia nyingi ya watu wanaojihusisha na kilimo, kunapunguza maendeleo? Nchi nyingi kama siyo zote zilizoendelea duniani zimefanya hivyo kwa kupunguza idadi ya watu wanaojihusisha na kilimo na kuwahamisha kwenye viwanda.

Naomba maoni yako kuhusu hili.
 
Hakuna ulichoandika hapo, kabla hujafikria kufanya kilimo biashara ni lazima ufikrie mlaji mkuu ni nani na anahitaji kwa kiasi gani na ubora gani na kwa wakati gani.

Watu wengi hukimbilia kuwezeshwa kifedha ili kujiingiza kwenye kilimo,mtazika hela bure, kufanya kilimo biashara ni shughuli pevu,tunaofanya tunaelewa.LEO UNAWEZESHA VIJANA LET SAY IDADI YS VIJANA MILIONI 5 ,hawa wote wakifanya uzalishaji ulioseriuos masoko ya ndani hayamudu.
 
Takwimu kutoka Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa asilimia 28 ya watu duniani wanajihusisha na kilimo.
Hii imepungua kutoka asilimia 44 mwaka 1991.
Je, huoni kuwa kuwa na asilimia nyingi ya watu wanaojihusisha na kilimo, kunapunguza maendeleo? Nchi nyingi kama siyo zote zilizoendelea duniani zimefanya hivyo kwa kupunguza idadi ya watu wanaojihusisha na kilimo na kuwahamisha kwenye viwanda.
Naomba maoni yako kuhusu hili.
Mkuu, kupungua kwa watu wanaojihusisha na kilimo katika nchi zilizo endelea ni green light kwetu. Maana hivyo viwanda vyao vinahitaji raw materials ambazo kwa Kiwango kikubwa ni kutokana na kilimo.

Na kingine nafikiri labda ni kujikita katika kuzalisha zao fulani ( to be specific ) kutasaidia sana kuliko kutaka kulima kila kitu.kwa mfano ni israel na kilimo cha matunda na Singapore kwenye mchele....
 
Mkuu, kupungua kwa watu wanaojihusisha na kilimo katika nchi zilizo endelea ni green light kwetu. Maana hivyo viwanda vyao vinahitaji low materials ambazo kwa Kiwango kikubwa ni kutokana na kilimo.

Na kingine nafikiri labda ni kujikita katika kuzalisha zao fulani ( to be specific ) kutasaidia sana kuliko kutaka kulima kila kitu.kwa mfano ni israel na kilimo cha matunda na Singapore kwenye mchele....
Kwa mfano sasa hivi Kuna upungufu wa zao gani ambalo ni raw material ya viwanda gani tunaloweza kulima na kuwauzia?
Nchi ipi hiyo?
 
Back
Top Bottom