SoC04 Kilimo ni sekta mama hapa nchini haya yafanyike kwa maendeleo ya taifa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Arnold peter

Member
May 2, 2024
6
3
UTANGULIZI.
Pamoja na jitihada za serekali katika kuimarisha sekta ya kilimo lakini bado Kuna changamoto nyingi ambazo ni vifaa duni,ukosefu wa mitaji,ukosefu wa elimu,kukosekana Kwa masoko ya uhakika, bidhaa kukosa ubora unaotakiwa sokoni na kukosa namna bora ya kuhifadhi mazao Yao n.k

Hivyo basi serekali inaweza ikapunguza na kutatua Moja Kwa Moja matatizo haya Kwa mbinu zifuatazo;

1. Serekali ijenge na kuanzisha madarasa ya kutolea elimu ya kilimo ngazi ya vijiji au katani.
Kutokana na ukosefu wa elimu bora ya kilimo Kwa wanachi serekali haina budi kuanzisha madarasa haya, maana idadi kubwa ya wananchi waishio vijijini ni wakulima wadogo wadogo na wasio na elimu ya kutosha juu ya kilimo Cha kisasa.Tunahitaji eneo dogo tupate mazao mengi na hii itaondoa umaskini miongoni mwao na kuleta mzunguko mzuri wa Fedha hivyo elimu na usimamizi wa karibu unahitajika na njia pekee ni kuwa na madarasa haya ya pamoja.

2. Serekali ianzishe maafisa kilimo ngazi ya jamii; Hii Itasaidia sana katika kushauri na ufuatiliaji wa ubora wa elimu ya kilimo inayotolewa na utendeaji kazi wake Kwa mtu mmoja mmoja maana matokeo yataonekana dhahiri pia hawa maafisa ngazi jamii watasaidia katika utoaji wa taarifa za mkulima mmoja mmoja changamoto anazo pitia na namna bora ya kuzitatua Kwa wakati na kupelekea kupata mazao bora yenye tija Kwa kuwa maafisa hawa wanatoka katika jamii Yao hivyo serekali itapunguza gharama za kiuendeshaji na kuweza kuisaidia jamii kuondokana na umaskini.

3. Serekali ijaribu kuondoa Kodi kwenye vifaa vya kilimo.
Hii Itasaidia wakulima wadogo wadogo ambao ndio wengi nchini kupata vifaa hivi na kuvitumia katika kuboresha uzalishaji wao na Kutoa ajira itokanayo na mazao bora ya shamba, pia vifaa hivi vinaweza kukopeshwa Kwa bei nafuu katika vikundi au mtu mmoja mmoja chini ya usimamizi wa madarasa Yao ngazi ya Kijiji au kata.

4. Serekali ianzishe vijiji vya kiuwekezaji sekta ya kilimo kulingana na mazao ya kimkakati.
Hapa lazima serekali ipaangalie vizuri Kwa kuangalia Yale mazao ambayo yanatuletea Fedha za kigeni basi kuanzisha vijiji ambavyo watawaweka vijana jukumu lao kubwa ni uzalishaji tu ila wao ni kuandaa mazingira rafiki ikiwemo miundo mbinu wezeshi na mikopo ya bei nafuu hivyo itakuwa imesaidia ajira na Fedha za kigeni tutazipata kiulaini kabisa.

5. Serekali ianzishe mfumo wa kidigital wa uuzaji na ununuliwaji wa mazao ya wakulima.
Hapa wasajiliwe wanunuzi wote wa mazao ya wakulima na taarifa zao ziwe kidigital na washindane bei kidigital ila mkulima akitaka kujua bei ya bidhaa yake akiingia kwenye mfumo ajue HAMIS AU JOHN ananunua gunia la mahindi kwa Laki 7 hii itapelekea wakulima kulifaidi jasho lao pia serekali jukumu lake ni Kutoa miongozo ya bei ya ukomo.

6. Serekali ijaribu kupima ardhi zote na iweke wazi hali ya udongo ya eneo husika katika madarasa haya ya ngazi ya kata au vijiji hii Itasaidia namna bora ya kuchagua mbegu na mbolea katika hatua za ukuzaji wa zao husika.

7. Serekali ishirikiane na sekta binafsi katika kuandaa viwanda vidogo vidogo ngazi ya vijiji au kata Ili kuchakata mazao ghafi ya wakulima na kuyapandishia thamani Ili yatakapofika Kwa mlaji angalau bei iwe bora zaidi hii itaongeza Ajira na kipato pia Kwa mkulima.

8. Serekali ianzishe Kila shule ya msingi na sekondar i kuwa na mashamba Darasa.
Hii Itasaidia sana Watoto hawa kujifunza namna bora ya kilimo ambacho Cha manufaa hii itawafanya wanafunzi wajue umuhimu wa kilimo na manufaa yake pamoja na faida zake Kwa vitendo.Tusisubiri mpaka mtoto huyo awe mtu mzima.

HITIMISHO
Endapo mambo hayo yatafanyiwa kazi Kwa vitendo basi hali yetu ya kilimo itaimarika na Kutoa ajira Kwa vijana na kuongeza uzalishaji mali wenye tija Kwa MAENDELEO makubwa ya kiuchumi miaka 10 ijayo.
 
5. Serekali ianzishe mfumo wa kidigital wa uuzaji na ununuliwaji wa mazao ya wakulima.
Hapa wasajiliwe wanunuzi wote wa mazao ya wakulima na taarifa zao ziwe kidigital na washindane bei kidigital ila mkulima akitaka kujua bei ya bidhaa yake akiingia kwenye mfumo ajue HAMIS AU JOHN ananunua gunia la mahindi kwa Laki 7 hii itapelekea wakulima kulifaidi jasho lao pia serekali jukumu lake ni Kutoa miongozo ya bei ya ukomo.
Nakazia kwenye hili, lakini pointi zote ulizoongelea ni nzuri mno.

Mawazo ya kujenga hasaaa.
4. Serekali ianzishe vijiji vya kiuwekezaji sekta ya kilimo kulingana na mazao ya kimkakati.
Hapa lazima serekali ipaangalie vizuri Kwa kuangalia Yale mazao ambayo yanatuletea Fedha za kigeni basi kuanzisha vijiji ambavyo watawaweka vijana jukumu lao kubwa ni uzalishaji tu ila wao ni kuandaa mazingira rafiki ikiwemo miundo mbinu wezeshi na mikopo ya bei nafuu hivyo itakuwa imesaidia ajira na Fedha za kigeni tutazipata kiulaini kabisa.
Yas mtu anayetamani fursa fulani, ahamie kijiji fursa hiyo inakotekelezwa saaf. Hii inawezekana ikiwa kila kijiji kinafikika na soko lenye bei za kiujumla za kidijitali.

Kama tumeweza kwenye bei za petroli kujua bei ya jumla hadi ya rejareja, inashindikana vipi mazao na bidhaa za kijasiriamali?
 
Back
Top Bottom