Uzinduzi wa Ndege za ATCL: Kutoka Uwanja wa JNIA eneo la Tanzania Government Flight Agency

Mkuu wameruhusiwa sasa....Raia wanamwagika kwa wingi sana kuingia ndani
Mbona Nape hajaagiza watu wafanye kazi badala ya kuangalia ndege "zikizinduriwa". Au wananchi walioshiriki watapata ujira... Haahaaàaaaaasssh
 
Tukinununua Boeing tutapewa mapumziko ya wiki! Zidumu fikira sahihi za m/kiti wa chama!!!
 
Eti nazo zinazinduliwa? Sasa siku tukileta Air Bus nafikiri kutakuwa na mapumziko ya mwezi mzima.
Wee huoni foleni hiyo ya Abiria wenye LPO washajipanga hawajali mvua... hapo kweli tutapona ?
AnyHow tunaomba Wahusika wawe makini na undugu~nization au infant fares katika ticketing !!
security guard Ahsante hope siku za mbele AIRBUS sita (6) zizinduliwe hapo hapo JNIA !!
 
Pia tunaomba Mungu afanye wepesi tufike katika hizi mapema kabla ya 2020

Mkuu hebu ipake rangi na hii.........

house-colors-airbus-A350-1000%20XWB-fsx2.jpg
 
Hatimaye ile siku imewadia,leo ndio uzinduzi rasmi wa ndege mbili za TGFA zitakazokodiwa na ATCL kwa ajili ya matumizi ya usafiri wa ndani na nje ya nchi.Zaidi ya ndani ya mipaka ya Tanzania,ndege mpya za ATCL zinatazamiwa kuwa na "route" ya kuelekea Hahaya-Commor ambapo imekuwa na soko la uhakika hata wakati ikiwa na ndege moja tu.

Uzinduzi huo unategemewa kufanywa na Rais wa JMT Mh.John P. Magufuli.Eneo la ufunguzi litakuwa ni eneo la maegesho ya Wakala wa Ndege za Serikali(Tanzania Gvt Flight Agency)maandalizi ya uzinduzi huo yanaendelea na tayari ndege hizo zimetolewa eneo la "Apron" ya JWTZ-Air Wing na kuletwa TGFA.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari,wafanyakazi wa taasisi mbalimbali zinazofanya kazi uwanja wa ndege kama TAA,TGFA,TCAA,Swissport,Precision,ATCL,Police,State Security,JWTZ-Airwing na TMA watawakilisha raia wengine.

Kwa sbb za kiusalama na unyeti wa eneo,itakuwa ngumu kwa raia wengi kutoka nje bila kibali na vitambulisho kuingia moja kwa moja.Mpaka sasa utepe na eneo la kufanyia uzinduzi lipo tayari....Tutaendelea!!!

===== ======. =========
Hatimaye agizo limetoka na Raia wameruhusiwa kuingia na tayari kwa kumsubiri Rais anayetarajiwa kufika saa nne na nusu
vip JPM hatatoa tamko angalau watu tusafiri bure kwa muda fulani kama ilivyo kwa magari ya mwendokasi?
 
Naona Burudani Toka Kundi la Ngoma za Asili la Muungano Ndio Linaendelea Hapa!
Magufuli Anachekaaa!
Wanamwaga Sifa Sio Za Kitoto!
Wachezaji wa Ngoma Wanatokea Ruvuma!
Magufuli,Cheko Lake Linabip na Kukata Badala ya Kujipiga Usoni!
Ahahaha
 
vip JPM hatatoa tamko angalau watu tusafiri bure kwa muda fulani kama ilivyo kwa magari ya mwendokasi?
Bado,Ndio Kwanza Yupo Anaangalia Viuno Mauno!
Kuna Dada Yuko Uku Upande wa Wangu wa Kushoto Anamwaga Mauno Huyo!
Naona Magufuli Anaangalia,Jicho Kodo!
 
Naona Kundi la JKT,Wameleta Ngoma Yetu ya Gobogobo toka Kwa Watani Zangu Basukuma!
Naye Anamwaga Masifa na Anasema Tumsamehe kwa Kumwaga Kisukuma!
Upanf Wangu wa Kushoto Kuna Haka Kadada Kamisi Kanacheza Vizuri!
Mlioko Majumbani Mnakosa Mengi!
 
Back
Top Bottom