SoC04 Uwekezaji katika nyumba janja za wageni

Tanzania Tuitakayo competition threads
Jun 25, 2023
45
31
Utangulizi
Nchini Tanzania, tumekuwa na nyumba nyingi sana za kupokea wageni; nyumba za kitalii, nyumba za kawaida na hata nyumba za asili kwa ajili ya kuwapa huduma mbalimbali wageni wetu mara tu wawasilipo nchini.

Nyumba hizi za wageni zimekuwa zikijengwa zaidi katika Majiji ya Dar es Salaam, Arusha na Visiwani Zanzibar kwani ndiko ambako takwimu zinaonesha na wengi huamini kuwa wageni ni wengi zaidi watembeleao maeneo haya.

Lakini sasa, ukweli ni kwamba haijalishi ni eneo lipi wageni hufikia zaidi au vyovyote vile, lakini Mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya ni mikoa ambayo hali yake ya hewa, rutuba ya ardhi isababishayo ukijani wa mazingira, mito na mibubujiko ya maji (waterfalls), misitu yenye miti mirefu na ya kijani pamoja na miinuko na milima ya hapa na pale; ndiyo mikoa inayoongoza kwa mandhari nzuri zaidi zinazowavutia wageni; hivyo ndiyo mikoa inayofaa sana kujenga nyumba janja (Smart Villas) na zenye hadhi kwa ajili ya wageni wanaokuja kujihusisha na shughuli mbalimbali za muda mfupi, muda mrefu au muda wa kati nchini Tanzania.

Hii ndiyo mikoa inayoongoza kwa kilimo nchini Tanzania, japo ndiyo mikoa ambayo pia inaongoza kwa udumavu kutokana na kukosekana kwa food security na chakula chote kinacholimwa kusafirishwa kwenda mikoa maarufu kama vile Dar es Salaam na Dodoma ili kujipatia kipato, hivyo wakulima na wenyeji hujisahau wao na watoto wao katika suala zima la lishe.

Katika sifa yake ya kuongoza kwenye kilimo, mikoa hii ya Morogoro, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya; tafsiri yake ni kuwa ndiyo mikoa yenye ardhi iliyo na rutuba, ukijani na iliyonawiri vizuri hivyo mandhari yake kuwavutia zaidi wageni.

Sifa za nyumba janja za wageni
Nyumba janja za wageni zinapaswa kuwa na sifa kadhaa ambapo sifa ya kwanza kabisa ni mandhari yenye maji yatoayo sauti kama vile mito na maporomoko (waterfalls), mandhari ya ukijani inayohusisha miti na misitu mikubwa, midogo na ya kati ya hapa na pale pamoja na milima na miinuko midogo, mikubwa na ya kati.

Kwa sifa hizi; mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya; inaingia katika orodha ya mikoa inayofaa sana katika ujenzi wa nyumba janja za wageni; kwani ni mikoa yenye mito mingi na maporomoko mengi ya maji. Sambamba na mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya; Pwani, Tanga pamoja na Kilimanjaro pia inaingia katika orodha ya mikoa inayofaa sana katika ujenzi wa nyumba janja za wageni kwani nayo ina mandhari yenye maji yatoayo sauti kama vile mito na maporomoko (waterfalls), mandhari ya ukijani inayohusisha miti na misitu mikubwa, midogo na ya kati ya hapa na pale pamoja na milima na miinuko midogo, mikubwa na ya kati.

Sifa ya pili ya nyumba janja za wageni ni utulivu. Utulivu huu unahusisha utulivu wa asili na utulivu unaohusisha umbali na shughuli za kibinadamu. Hali ya utulivu hupatikana zaidi katika maeneo yenye milima na miinuko midogo, mikubwa na ya kati, misitu yenye miti midogo mikubwa na ya kati pamoja na maeneo yenye mito, maporomoko ya maji na yenye mazingira asilia zaidi kuliko jirani na makazi ya watu au maeneo yaliyo tambarare na jangwani; kwani shughuli nyingi za watu na makazi ya watu huendelea zaidi katika maeneo haya.

Sifa ya tatu ya nyumba janja za wageni ni mionekano ya nyumba hizi, kuanzia nje mpaka ndani. Kwa mwonekano wa nje, jambo la kwanza la kuzingatia ni ubunifu wa landscape pamoja na miundombinu ya barabara kuelekea nyumba hizi za wageni.

Hapa ubunifu unahitajika sana, kwani linahitajika eneo kubwa la nje, lililo kuanzia umbali wa mita angalau mia tano mbali na barabara za kijamii, makazi ya watu, shughuli za watu na ghasia za hapa na pale; ili kumpa mgeni utulivu lakini pia kumpa uwanja na nafasi ya kucheza michezo mbalimbali, kupumzika, kufaidi upepo mzuri wa nje pamoja na kumfanya kuwa huru kutembea huku na huko.

Hapa ubunifu mkubwa sana unahitajika, kwa kuhakikisha nyumba janja za wageni zina viwanja vya michezo, zina barabara nzuri za kupitika kwa miguu na magari, parking nzuri za magari, mawasiliano mazuri, Wi-Fi huru, na zina mandhari za kuvutia; zenye mapambo asilia yanayohusisha mawe, kokoto, lami, mifumo ya maji safi yatoayo sauti, miti na nyasi asilia (Natural Exterior Planning & Designing)

IMG_20240504_183304.jpg

(Chanzo Picha: Pinterest)

IMG_20240504_183001.jpg

(Chanzo Picha: Pinterest)

IMG_20240504_183137.jpg

(Chanzo Picha: Freepik)

Baada ya mandhari hayo ya nje, mandhari ya ndani pia ni jambo muhimu mno la kuzingatia. Mandhari ya ndani yanahitaji ubunifu mkubwa ambao utamfanya mgeni anogewe kuendelea kubaki nchini Tanzania.

Nyumba janja za wageni si maghorofa marefu, mafupi wala ya kati, bali ni nyumba za kawaida zenye vyumba viwili au vitatu tu, lakini vyumba hivi vinatakiwa kuwa 'self-contained' yaani kila chumba kimtosheleze ipasavyo mgeni anayefikia katika chumba hicho.

Kila chumba kinapaswa kuwa na mahali pa kulala na kukaa, choo, bafu, jiko pamoja na studio ya uandishi, uchoraji, muziki na/au filamu vilivyobuniwa na kutengenezwa kwa sanaa na ubunifu wa hali ya juu.

Tukianza na mwonekano wa chumba, chumba kinapaswa kuwa na kuta, paa na sakafu za LED pamoja na rangi au picha zinazobadilikabadilika;

zilizochorwa kwa kutumia sanaa yakinifu (immersive art), ambayo humfanya mgeni awapo chumbani ajihisi kama yupo Bustani ya Edeni.

Ifuatayo ni mifano ya vyumba na sehemu za ndani za majengo zilizotengenezwa kwa kutumia Sanaa Yakinifu (Immersive Art) kwenye kuta, paa pamoja na sakafu za LED.

IMG_20240504_182720.jpg

(Chanzo Picha: CBC)

IMG_20240504_183227.jpg

(Chanzo Picha: Dynamo LED Displays)

IMG_20240504_182617.jpg

(Chanzo Picha: Basa Studio)

Chumba hakipaswi kuwa na mambo mengi zaidi ya dirisha moja refu na la kisasa, mlango pamoja na kitanda janja chenye television na simu janja zilizounganishwa na king'amuzi na mtandao wenye kasi zaidi wa 5G na kuendelea.

IMG_20240504_182842.jpg

(Chanzo Picha: Hospitality Technology)

Ufuatao ni mfano wa mwonekano kwa ujumla, wa chumba Janja (Smart Room)

Choo na Bafu

IMG_20240504_183435.jpg

(Chanzo Picha: DHL Bathroom Supplies Limited)


Jiko

IMG_20240504_183340.jpg

(Chanzo Picha: Media Licdn)


Kitanda

IMG_20240504_183620.jpg

(Chanzo Picha: Hi Can, High Tech Smart Bed)


Hitimisho
Napenda kutumia nafasi hii, kuhamasisha wawekezaji, makampuni, taasisi, mashirika, serikali pamoja na watu binafsi kuwekeza zaidi katika Nyumba Janja kwa Wageni; kwenye mikoa niliyoitaja. Hii ni kwa ajili ya kuwavutia zaidi wageni kuja kufurahia maisha pamoja nasi nchini Tanzania.​
 
; hivyo ndiyo mikoa inayofaa sana kujenga nyumba janja (Smart Villas) na zenye hadhi kwa ajili ya wageni
Ntajifunza kitu hapa. Twende kazi🤔
Napenda kutumia nafasi hii, kuhamasisha wawekezaji, makampuni, taasisi, mashirika, serikali pamoja na watu binafsi kuwekeza zaidi katika Nyumba Janja kwa Wageni; kwenye mikoa niliyoitaja. Hii ni kwa ajili ya kuwavutia zaidi wageni kuja kufurahia maisha pamoja nasi nchini Tanzania.
Ebhana ahsante sana, nadhani umetuinspaya hata wenyeji kujitwalia baadhu ya 'feautures' za nyumba janja za wageni na kuziweka kwenye nyumba zetu hizihizi. Sio kuigana tu mapaa marefu, tutaiga na 'ujanja' wa nyumba. Saaaafi👏
 
Shukrani na Karibu sana
Ntajifunza kitu hapa. Twende kazi🤔

Ebhana ahsante sana, nadhani umetuinspaya hata wenyeji kujitwalia baadhu ya 'feautures' za nyumba janja za wageni na kuziweka kwenye nyumba zetu hizihizi. Sio kuigana tu mapaa marefu, tutaiga na 'ujanja' wa nyumba. Saaaafi👏
 
Back
Top Bottom