Uongozi wa kanisa KKKT utoe tamko haraka kuhusu yaliyojiri Jana Kimara

Salam,

Kwa Muda wa zaidi ya wiki mbili huku mitandaoni kumekuwa na mjadala mrefu unaozungumzia utata wa elimu ya mkuu wa mkoa wa Dar. Ninaamini hichi ndicho kilichopelekea mkuu huyo kusimama jukwaa la kanisa la KKKT Kimara katika jitihada za kujinasua kwenye shutuma hizo ambazo mwisho wake sio mzuri endapo itabainika kuwa ni kweli.
Sisemi kuwa shutuma hizi ni za kweli na wala binafsi sina ushahidi wa uhakika sana juu Hilo.

HOJA YANGU:
Naomba uongozi wa kanisa langu KKKT waliopo pale Luther house Dar wanifafanulie uhalali wa kutumia madhababu ya kanisa katika jitihada za kujisafisha kisiasa. Kwenye hili saga tumeshaona baadhi ya viongozi wengine wa kidini wakijitoa kusema wazi kuwa shutuma hizi za mkuu wa mkoa ni za kweli kabisa. Je, aliyempa mamlaka mchungaji wa Kimara kumsimamisha mkuu wa mkoa ili ajisafishe ni nani?? Ninalijua vizuri kanisa langu kuwa Lina uongozi makini na sio rahisi kwa mtu yeyote Kufanya Chochote kanisani bila uongozi husika kujua..... Na hasa mtu mkubwa Kama mkuu wa mkoa. Swali langu, je uongozi wa kanisa unahusika kwenye hili?
Kama hauusiki tafadhali naomba uongozi utoe tamko mapema sana. Kwa sababu ikiwa muhusika ataanguka inaweza ikaathiri heshima ya kanisa kwa namna moja au nyingine.

Ni Hilo tu.
Mimi muumini wa KKKT mwenye Kadi namba 881.
Hii issue mimi mwenyewe kama muumini nimefadhaika sana aise.....KKKT tunakua kama tumeshanunuliwa na huyu bashite.

KKKT please ombeni radhi au toeni tamko fasta waumini tujue mlimaanisha nini au mmeanza siasa maji taka.

Ni mimi muumini wa usharika wa cathedral kadi namba 1134 dodoma.
 
ishawah tokea kama hii kwenye mbio za urais 2015 mbona hamkuomba matamko
Wewe ulikuwa wapi?kwanini hukulikemea hilo kama wewe uliliona?Mwache makonda ajibebe mzogo eake mwenye.kwanini hafuati sheria za nchi?Anatumia mamlaka yake kimabavu kama baba yake magu.Mungu anamuumbua Makonda anaiona nafsi yake kuwa ni ya kinafiki huku akijifanya mlokole.Huyo kamjaribu mungu,sasa mungu anamuumbua.kama angekuwa ni mcha mungu wa kweli.Mungu angemlinda .
Hiyo kadi unatoaga sadaka kwenye bahasha au ni urembo tu?
 
Akija RC nikiwepo akipewa fursa ya kuongea namfata namkaba nampa ngumi na mateke namtoa Nje , siwezi kukubali uijnga ujinga kama huo.
 
Wewe ndio Malasusa au? Lutheran limejengwa na misingi imara tangu enzi ndio maana umeliona liko imara hadi leo

Utaratibu wa Ibada mapokea ya kikanisa pamoja na Liturijia hivi ndivyo vimeitofatisha Lutheran na Madhehebu mengine

Sasa uyo maslai nani ajeuze misingi imara ya KKKT

Na wasiwasi na wewe ni moja ya wale waumini chokoraa hujui misingi ya dhehebu yako

Soma história ya Martin Luther ndio ujue KKKT sio chombo cha mchezo mchezo kama huo unaoufagilia waulize RC wanajua nani baba wa injili
Well said Mkuu.
 
KWANI wewe halijakuchukiza? Hivi angeenda pale madhabahuni apige tu magoti aombe kuombewa (hata kama angefanya siri sababu ya kuombewa), pangekuwa na sababu ya kuchukia?

Ndugu usijaribu kuwa mnafiki, tunayo sababu ya kuchukia, na Tunayo haki ya kupaza sauti viongozi wa Kanisa wasikie. Tena ni hivi karibuni tu, Mkuu wetu wa KKKT Askofu Shoo alitoa tamko kuwa wanasiasa wasitumie madhabahu ili kutimiza malengo yao ya kisiasa. Kanisa linapaswa kujilinda na chachu za namna mbalimbali. Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi. (1 Tim. 5:22)

Kosa linaweza kutokea kama ajali. Ila hatua zitakazofuata ndizo zinaweza kuonesha ukomavu wa Kanisa (au taasisi yoyote) katika swala lililoleta shida. Iliwahi kutokea miaka michache iliyopita, Rostam Aziz alialikwa kwenye harambee ya kwaya moja pale Kinondoni. Pamoja na kutoa mchango wa Jenereta na ahadi ya fedha taslim, pia alitumia nafasi hiyo kujisafisha kisiasa. Uongozi wa Kanisa wa wakati ule ulibaini tatizo na ukaiagiza hiyo kwaya kurejesha hiyo michango, na upepo ukaendelea kuvuma katika hali ya kawaida.

Hivyo tunaendelea kupasa sauti zetu, viongozi wa Kanisa wasikie, na hatua mwafaka zichukuliwe!
Word.
Wasiwasi wangu ni itakuwaje Kama akitumbuliwa??? Kanisa litajificha wapi??
 
Cjabarikiwa hata kidogo coz kanisa cyo xehemu ya mikutano ya viongozi wa kiserikali,ninashindwa kuelewa huyu ndugu David Bashite aliruhusiwa vp kupanda madhabahuni ambapo ni mahari patakatifu
 
Hili ni dhehebu langu bt honestly kuna tatizo kubwa sana na hii sio mara ya kwanza kwa wanasiasa kutumia KKKT katika mambo yao ya siasa
Mi nilichostaajabu na waumini wanashangilia ......
Hakuna shida km mtu atakuja kwa ajili ya ku-repent lkn sio kujisafisha kisiasa
Viongozi wa KKKT acheni kutumika kisiasa mnakwaza waumini wenu
 
Asubuhi asubuhi badala ya kuwaza kazi mnawaza vyeti vya makonda, mnadhani vyeti vyake vitawaondolea ugumu wa maisha yenu
we jamaa bhana,nenda celebrity forum kuleeee....ndo kwako,afu wew si nawe ndo zinakuwaga kazi zako kuleta mada kule za wema sepetu asubuhi saa11? warumi bhana.
 
Ni Upuuzi Wakiwango cha Juu Sana hiki Kilichofanyika "Mimbari " haiwezi kutumiwa ki holela na Wanasiasa.
 
Back
Top Bottom