Uongozi wa kanisa KKKT utoe tamko haraka kuhusu yaliyojiri Jana Kimara

Salam,

Kwa Muda wa zaidi ya wiki mbili huku mitandaoni kumekuwa na mjadala mrefu unaozungumzia utata wa elimu ya mkuu wa mkoa wa Dar. Ninaamini hichi ndicho kilichopelekea mkuu huyo kusimama jukwaa la kanisa la KKKT Kimara katika jitihada za kujinasua kwenye shutuma hizo ambazo mwisho wake sio mzuri endapo itabainika kuwa ni kweli.
Sisemi kuwa shutuma hizi ni za kweli na wala binafsi sina ushahidi wa uhakika sana juu Hilo.

HOJA YANGU:
Naomba uongozi wa kanisa langu KKKT waliopo pale Luther house Dar wanifafanulie uhalali wa kutumia madhababu ya kanisa katika jitihada za kujisafisha kisiasa. Kwenye hili saga tumeshaona baadhi ya viongozi wengine wa kidini wakijitoa kusema wazi kuwa shutuma hizi za mkuu wa mkoa ni za kweli kabisa. Je, aliyempa mamlaka mchungaji wa Kimara kumsimamisha mkuu wa mkoa ili ajisafishe ni nani?? Ninalijua vizuri kanisa langu kuwa Lina uongozi makini na sio rahisi kwa mtu yeyote Kufanya Chochote kanisani bila uongozi husika kujua..... Na hasa mtu mkubwa Kama mkuu wa mkoa. Swali langu, je uongozi wa kanisa unahusika kwenye hili?
Kama hauusiki tafadhali naomba uongozi utoe tamko mapema sana. Kwa sababu ikiwa muhusika ataanguka inaweza ikaathiri heshima ya kanisa kwa namna moja au nyingine.

Ni Hilo tu.
Mimi muumini wa KKKT mwenye Kadi namba 881.
Makanisa haya makubwa RC,kkkT ndiyo yanayoongoza kwa ss kuwa sehem ya ukandamizaji na kuunga mkono mabaya ya viongozi wetu na wao hukimbilia huko kwani huko imani ya ki MUNGU hakuna tena hawa watu ni wafia dini maana yake waseme kweli hata mauti lkn kwa ss ni kinyume mfano swala la wana wa bukoba,njaa na mengine mengi tu hata huyo ametafuta wp pa kusemea akapata hapo,amezunguka miskitini lkn kwakuwa huko hakuna mashiko akaona huko akilia hapatakuwa na mashiko amepata pa kulilia ndo hivyo ,mh vita hiyo ya madawa ni sawa lkn kibaya ni kuianzisha na kukamata watu ambao hata chembe hawana hawa utawasafisha vp?ni mapambano mazuri lkn kuna watu umewapeleka sio, muombe sana MUNGU akupe moyo wa hekima.
 
Sisi wengine tunafarijika sanaa kwa namna mchungaji anavyoendesha ibada hapa kanisani. Ni ibada inayotubariki ndiyo maana mpaka sasa tupo hapa. Wewe kama ibada au mchungaji anakukera kwa namna ibada inabyoendeshwa nakushauri uende kwenye usharika mwingine. Hakuna sababu ya kukereka kwa jambo unaloweza kuzuia.
Ninachokijua Mimi ni kwamba kuna miongozo na taratibu za namna ya kuendesha Ibada za KKKT, na Kama wewe ni muumini wa kanisa hili huwezi kusema kuwa mtu ahame usharika Wakati utaratibu ni mmoja..... Hilo linaifanya hiyo hoja hapo juu kuwa huyo mchungaji ni unique iwe na mashiko.

Kanisa Lina taratibu, zikivunjwa ni kupanda mbegu ya makanisa ya kimapokeo kwenye kanisa kongwe Kama KKKT.
 
Wewe ndio Malasusa au? Lutheran limejengwa na misingi imara tangu enzi ndio maana umeliona liko imara hadi leo

Utaratibu wa Ibada mapokea ya kikanisa pamoja na Liturijia hivi ndivyo vimeitofatisha Lutheran na Madhehebu mengine

Sasa uyo maslai nani ajeuze misingi imara ya KKKT

Na wasiwasi na wewe ni moja ya wale waumini chokoraa hujui misingi ya dhehebu yako

Soma história ya Martin Luther ndio ujue KKKT sio chombo cha mchezo mchezo kama huo unaoufagilia waulize RC wanajua nani baba wa injili
 
WANALI CHAFUA HEKALU LA BWANA
KKKT Sio sehem ya wanasiasa sijui kujisafisha kwa kuhubiri
YAani Hadhi Ya KKKT inaanza polomoka uwezi ona mambo kama haya RC
Kutoa salam fupi hatukatai lkn mtu sijui ni kuhubiri sasa si aende kusomea uchungaji kuliko kubadili sauti (kinyonga Bashite) kama Mwl Mwakasege
Hahahaha kwanini asingeita waandishi wa habari kama kawaida yake ajielezee huko ingekua nzuri zaidi
 
Ndugu muumini, yule aliyesema kuwa ni zamu ya sisi walutheri kutoa Rais akiwa madhabahuni mbona haukutaka wanisa litoe ufafanuzi? Au kwa kuwa huyu wa sasa humpendi? Huu ni unafiki wa kiwango cha uprofesa.
Ndugu muumini, unajijua sana??? Una uhakika kuwa sikulisemea Hilo swala??? Au na wewe ni Kihiyo Bashite.
 
Asubuhi asubuhi badala ya kuwaza kazi mnawaza vyeti vya makonda, mnadhani vyeti vyake vitawaondolea ugumu wa maisha yenu
Karibu, pole kwa kule ulikokuwa umewekwa tulikosa ubuyu wako kwa kiasi fulani warumi
 
Ninachokijua Mimi ni kwamba kuna miongozo na taratibu za namna ya kuendesha Ibada za KKKT, na Kama wewe ni muumini wa kanisa hili huwezi kusema kuwa mtu ahame usharika Wakati utaratibu ni mmoja..... Hilo linaifanya hiyo hoja hapo juu kuwa huyo mchungaji ni unique iwe na mashiko.

Kanisa Lina taratibu, zikivunjwa ni kupanda mbegu ya makanisa ya kimapokeo kwenye kanisa kongwe Kama KKKT.
Mkuu, mtoa hoja anasema kuwa mchungaji yupo kama "brazamen". Huu ni udhalilishaji kwa kiongozi wetu. Hivyo, naona mtoa pamoja na mambo mengine ya utaratibu wa ibada lakini hampendi/ hamweshimu kiongozi wetu. Sasa kama hapendi huu utaratibu na huyu "brazameni" anamkera, ni bora ahamie kwingine kulinda imani yake.
 
DAUDI BASHITE Inaendelea ameanzia Msikitini, akaja Kanisani, Baadaye wapi kwa kalumanzila (Huyo ni bomu ambalo halijaelekezwa pa kutua) linaweza likalipukia sehemu yoyote: Onyo kwa makanisa Bomu hili linaweza kulipukia sehemu yoyote OPERATION 81 MZIZIMA
 
WANALI CHAFUA HEKALU LA BWANA
KKKT Sio sehem ya wanasiasa sijui kujisafisha kwa kuhubiri
YAani Hadhi Ya KKKT inaanza polomoka uwezi ona mambo kama haya RC
Kutoa salam fupi hatukatai lkn mtu sijui ni kuhubiri sasa si aende kusomea uchungaji kuliko kubadili sauti (kinyonga Bashite) kama Mwl Mwakasege
cha ajabu ninachoshangaa akina mama wanapiga vigelegele, yaani daah!!
 
Kkkt mna mambo sana. Huku Arusha mko bize kufufua hoteli ya Corridor. Dar mnamsafisha Mako. Msimu wa uchaguzi mkampa Lowasa madhabahu ajinadi.

Mnaendesha minada makanisani wakati hata Yesu alikataa nyumba ya baba yake kuwa pango la wanyang'anyi.

Hilo dhehebu kuna wapiga dili wengi sana. Mnapaswa mjitafakari kwa kweli kama bado mpo kwenye misingi ya Martin Luther.
 
Mkuu, mtoa hoja anasema kuwa mchungaji yupo kama "brazamen". Huu ni udhalilishaji kwa kiongozi wetu. Hivyo, naona mtoa pamoja na mambo mengine ya utaratibu wa ibada lakini hampendi/ hamweshimu kiongozi wetu. Sasa kama hapendi huu utaratibu na huyu "brazameni" anamkera, ni bora ahamie kwingine kulinda imani yake.
Nina amini ni lugha tu imetofautiana Kati yako na huyo unamuita mtoa mada.... Labda ametumia neno ambalo wewe kwa umri wako hulielewi. Ulitaka aseme mtanashati ok, weka neno mtanashati hapo kwenye brazamen ila haitoi maana ya sisi tulivyomuelewa aliyekuambia Hilo neno. Tunahoji utaratibu binafsi wa huyo kiongozi kuendesha Ibada kinyume na utaratibu kongwe wa kanisa....

All in all, turudi kwenye mada.
 
Kkkt mna mambo sana. Huku Arusha mko bize kufufua hoteli ya Corridor. Dar mnamsafisha Mako. Msimu wa uchaguzi mkampa Lowasa madhabahu ajinadi.

Mnaendesha minada makanisani wakati hata Yesu alikataa nyumba ya baba yake kuwa pango la wanyang'anyi.

Hilo dhehebu kuna wapiga dili wengi sana. Mnapaswa mjitafakari kwa kweli kama bado mpo kwenye misingi ya Martin Luther.
Hili swala la minada, Nadhani umepotoka kidogo. Rudi kwenye hoja ya kushinikiza uongozi utoe tamko.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Salam,

Kwa Muda wa zaidi ya wiki mbili huku mitandaoni kumekuwa na mjadala mrefu unaozungumzia utata wa elimu ya mkuu wa mkoa wa Dar. Ninaamini hichi ndicho kilichopelekea mkuu huyo kusimama jukwaa la kanisa la KKKT Kimara katika jitihada za kujinasua kwenye shutuma hizo ambazo mwisho wake sio mzuri endapo itabainika kuwa ni kweli.
Sisemi kuwa shutuma hizi ni za kweli na wala binafsi sina ushahidi wa uhakika sana juu Hilo.

HOJA YANGU:
Naomba uongozi wa kanisa langu KKKT waliopo pale Luther house Dar wanifafanulie uhalali wa kutumia madhababu ya kanisa katika jitihada za kujisafisha kisiasa. Kwenye hili saga tumeshaona baadhi ya viongozi wengine wa kidini wakijitoa kusema wazi kuwa shutuma hizi za mkuu wa mkoa ni za kweli kabisa. Je, aliyempa mamlaka mchungaji wa Kimara kumsimamisha mkuu wa mkoa ili ajisafishe ni nani?? Ninalijua vizuri kanisa langu kuwa Lina uongozi makini na sio rahisi kwa mtu yeyote Kufanya Chochote kanisani bila uongozi husika kujua..... Na hasa mtu mkubwa Kama mkuu wa mkoa. Swali langu, je uongozi wa kanisa unahusika kwenye hili?
Kama hauusiki tafadhali naomba uongozi utoe tamko mapema sana. Kwa sababu ikiwa muhusika ataanguka inaweza ikaathiri heshima ya kanisa kwa namna moja au nyingine.

Ni Hilo tu.
Mimi muumini wa KKKT mwenye Kadi namba 881.
Kanisani ni kimbilio kwa sisi wenye dhambi.
Suala la elimu ya mtu halina uhusiano na cheo/mafanikio.
Hata Mwl.Nyerere alikuwa na wakuu wa Mikoa,wenye Elimu ya kiwango cha chini kushinda Mh.Makonda.
 
Asubuhi asubuhi badala ya kuwaza kazi mnawaza vyeti vya makonda, mnadhani vyeti vyake vitawaondolea ugumu wa maisha yenu
Ugumu wamaisha unaletwa na Daudi bashite.

Kwakua mimi mwenye vyeti original nazunguka mitaani mwaka wa 3 sina kazi ila makonda anavyeti feki kachukua nafasi zetu

b6084552d2b8315a16c91e73d451dd91.jpg
yangu
 
ndugu zangu tusimhukumu ndugu yetu toba zote zinapatikana mbele ya altare ya bwana binadam wote niwadhaifu na hata mungu anajua ..... hapo mlipo kuna mtu
ambayo siimdhaifu?.... altare ya bwana ndo inayofuta madhaifu yetu....kweli wengi mmechukia bcoz amepeleka vitu vya kisiasa pale....madhabahu yale angeenda kujitakasa yeye kama yeye si kwa cheo cha RC
KWANI wewe halijakuchukiza? Hivi angeenda pale madhabahuni apige tu magoti aombe kuombewa (hata kama angefanya siri sababu ya kuombewa), pangekuwa na sababu ya kuchukia?

Ndugu usijaribu kuwa mnafiki, tunayo sababu ya kuchukia, na Tunayo haki ya kupaza sauti viongozi wa Kanisa wasikie. Tena ni hivi karibuni tu, Mkuu wetu wa KKKT Askofu Shoo alitoa tamko kuwa wanasiasa wasitumie madhabahu ili kutimiza malengo yao ya kisiasa. Kanisa linapaswa kujilinda na chachu za namna mbalimbali. Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi. (1 Tim. 5:22)

Kosa linaweza kutokea kama ajali. Ila hatua zitakazofuata ndizo zinaweza kuonesha ukomavu wa Kanisa (au taasisi yoyote) katika swala lililoleta shida. Iliwahi kutokea miaka michache iliyopita, Rostam Aziz alialikwa kwenye harambee ya kwaya moja pale Kinondoni. Pamoja na kutoa mchango wa Jenereta na ahadi ya fedha taslim, pia alitumia nafasi hiyo kujisafisha kisiasa. Uongozi wa Kanisa wa wakati ule ulibaini tatizo na ukaiagiza hiyo kwaya kurejesha hiyo michango, na upepo ukaendelea kuvuma katika hali ya kawaida.

Hivyo tunaendelea kupasa sauti zetu, viongozi wa Kanisa wasikie, na hatua mwafaka zichukuliwe!
 
Back
Top Bottom