Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,272
- 35,639
Huenda kuna mambo yamenipita, nimeona niulize hapa.
Ninakumbuka takribani miaka mitano iliyopita kulitokea ujio wa Mfalme wa Morocco hapa Tanzania wakati wa kipindi cha utawala wa Magufuli na ulikwenda sambamba na utiaji wa saini wa mikataba zaidi ya 10 (ambayo hatukuambia kwa kina kila mkataba unahusu nini) na mfalme yule kwa furaha akaahidi kutujengea mara moja msikiti mkubwa sana na uwanja wa kisasa sana pale Dodoma, tena bure!
Sasa muda umepita, kuna ukimya mzito, ahadi ya ujenzi wa uwanja upo kimya mnoo. Nini kinaendelea?
Mfalme wa Morocco ametutapeli kwa maneno? Mfalme katoa pesa na wajanja wa kijani wamezitafuna gizani?
NOTE: Tanzania (kwa kushirikiana na Kenya na Uganda) tunataka kuwa wenyeji wa AFCON 2027, na mkakati ni kuwa na viwanja vitatu, Uwanja wa Mkapa upo tayari unahitaji marekebisho machache), Zanzibar tayari wanarekebisha uwanja wao, hivyo kunabakia upungufu wa uwanja mmoja, na sasa tumesikia serikali imeanza mpango wa kujenga uwanja mpya Arusha, hivyo mabilioni ya pesa yatabidi kutengwa kwa kazi hiyo.