Mbabaishaji
Member
- Nov 13, 2018
- 71
- 133
UBUNTU BOTHO
Sababu kumi (10) ambazo zaipasa serikali kuhamisha ujenzi wa uwanja wa mpira jijini Arusha kwenda jiji Mwanza .
1)Fidia za eneo au viwanja, gharama za eneo au kiwanja Arusha ni kubwa sana ukilinganisha na Mwanza. Huenda ndio sababu mmoja wapo wa uwanja huo kuwa ghari.
2)Uchache wa mashabiki wa mpira wa miguu Arusha ukilinganisha na Mwanza, Arusha kuna mashabiki wachache sana wa mpira wa miguu na hata mikoa ya jirani kama Manyara na Kilimanjaro (ukitoa wilaya ya Moshi) kutokana na kuwa na jamii kubwa ni ya wafugaji wakuhamahama (waishio porini) ambao wengi si wapenzi wa mpira. Pia tabia na sifa ya ubahiri wa makabila ya watu wa ukanda huo.
3)Hakuna timu inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara kutokea Arusha, na hata timu zinazoshiriki mashindano ya ligi daraja la kwanza hazijazi uwanja hivyo kutapelekea hasara za kimapato.
4) Migogoro, chuki , fitina kutoka kwa viongozi na wasimamizi wa mpira jijini Arusha ambao wengi wao ni wamiliki wa timu zinazoshiriki ligi daraja mbali mbali mkoa humo. Je viongozi hao wataweza kusimamia uwanja huo.
( Habari zaidi utaipata kutoka gazeti la Mwananchi online la j.tatu, Januari 04,2016 ukurasa wa spoti_mikiki.)
5) Uchache wa vipaji na utayari wa vijana wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuutumia uwanja huo. Kwa miaka ya hivi karibu tumeona jinsi soka la Arusha lilivyo poromoka na timu ya mwisho kushiriki ligi kuu ilikua timu ya kitaasi ya maafande JKT Oljoro iliyoshuka daraja mwaka 2013/2014 na mpaka sasa hakuna timu ya jamii au ya kampuni au ya mtu binafsi inayoshiriki ligi kuu Tanzania wala ligi daraja la kwanza ukilinganisha na timu kanda ya ziwa.
6)Utunzaji wa uwanja wa mpira kwenye maeneo au ukanda wenye unyevunyevu mwingi kama Arusha ni gharama. Vyuma na na nati huwa vinawahi kuota kutu na marekebisho huchukua mda mrefu kufanyika kutokana na mapato machache mfano uwanja wa Benjamin mkapa.
7) Hasara ya uwekezaji katika ujenzi wa uwanja huo endapo utajengwa Arusha. kutokuwepo kwa mashabiki wengi wa mpira jijini Arusha kutapelekea kuwepo kwa hasara kutokana na mapato madogo yatakayo kusanywa, pia utaongezea serikali gharama za utunzaji na uendeshaji wa uwanja huo.
8)Umbali na gharama za nauli kwa timu na mashabiki wa mikoa jirani kama Singida Fountain gate na Coastal union ya Tanga zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara endapo zitahitaji kuutumia uwanja huo katika mechi kubwa, nauli:-
Singida - Arusha = 22,000/
Tanga - Arusha= 25,000/
Wakati ukijengwa Kwanza gharama zitakua nafuu kiasi kwa timu na mashabiki wa mikoa jirani kama Geita gold na Kagera sugar, nauli :-
Geita - Mwanza= 8000/
Kagera(Bukoba) - Mwanza = 24,000/
9)ikiwa lengo la ujenzi wa uwanja huo ni kwaajili ya AFCON na ukuzaji wa utalii, basi ulipaswa ujengwe Mbeya ili kusogeza karibu kwa mashabiki kutoka maeneo ya mbali na viwanja ambavyo michuano hiyo itafanyika, mfano mashabiki wa Arusha wako jirani na Nairobi hivyo wao ni rahisi kwenda kuangalia mashindano hayo wakati mashabiki kutoka sehemu nyingine kama Mbeya, Katavi, Ruvuma, Iringa, Kigoma Kagera na Mwanza na mikoa ambayo mashindano hayo yatafanyika, pia itasaidia kufungua nchi kwaajili ya maeneo mapya ya utalii.
10) Utayari wa wakazi wa Arusha juu ya ujenzi wa uwanja huo uko chini, hii ni kutokana na wakazi wengi kutokuwa wapenzi wa soka ukilinganisha Mwanza ambako tayari kuna mwamko wa soka.