Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Wakuu humu, heshima mbele. Nimefuga kuku kama 100 hivi wa kienyeji, na nawalisha pumba za mahindi mchanganyiko na mashudu, dagaa na madini. Wanaenda vizuri, ila shida ni kwenye utagaji, wanataga wachache na sio kila siku, anaweza kutaga leo, akaruka siku tatu ndio anataga tena. Nilikua naomba msaada humu, kwa wazoefu, namna ya kumfanya kuku wa kienyeji kutaga kwa mfululizo. Kuna majogoo 10 within.
Ahsante sana.
Mimi ni muuzaji wa vitabu vya ufugaji wa kuku wa kienyeji, nakushauri ununue kitabu kinaelezea kila kitu tuwasiliane kwa namba hii 0756462228
 
Chakula unachowapa mahindi na mashudu kina kiwango cha juu fat na protein. Kumbuka wakati wa utagaji kuku huongeza kiwango cha mafuta mwilini kwa hiyo inaathiri utumbo wa mayai.
Kingine labda una over feeding hao kuku hilo pia linaathiri kasi ya utagaji.
 
Ahsante sana mkuu. Hapo kwenye overfeed itakua inanihusu. Sasa mbadala wa pumba na mashudu ninini mheshimiwa?
 
Changanya pumba au chakula unachowapa na (layers) hicho ni chakula wanachopewa kuku wa mayai hakikisha layers na pumba zinakuwa na uwiano sawa laa sivo ukizidisha layers watataga sana bila kuatamia
 
Haya mayai yatakayo tagwa kwa kuwapa layers yataweza kuanguliwa kweli?
 
Wakuu humu, heshima mbele. Nimefuga kuku kama 100 hivi wa kienyeji, na nawalisha pumba za mahindi mchanganyiko na mashudu, dagaa na madini. Wanaenda vizuri, ila shida ni kwenye utagaji, wanataga wachache na sio kila siku, anaweza kutaga leo, akaruka siku tatu ndio anataga tena. Nilikua naomba msaada humu, kwa wazoefu, namna ya kumfanya kuku wa kienyeji kutaga kwa mfululizo. Kuna majogoo 10 within.
Ahsante sana.
Changanya layers mash watataga mfululizo
 
mkuu wewe umekulia New york? au Michigani? kwa sababu kama umekulia kijijini basi unajua fika tabia za kuku wa kienyeji.

Layers wenyewe hawatagi kila siku sembuse wa kienyeji? how come?
Sio kweli, kuku wa kienyeji anaweza kutaga hadi mayai 70 mfululizo japo anaweza kurusha siku moja. Mimi huwapa layers mash kidogo nachanganya na pumba
 
Back
Top Bottom