M
Maelezo ya mtoa mada si nadharia ni halisi,sijatenda ila nimeshuhudia kwa macho.Tunachokwama wengi wetu ni usimamizi.Kuku ufugaji wake ni sawa na mkulima wa bustani.Matokeo yenye tija kubwa yanategemea mno nidhamu ya usimamizi kuliko vitu vyote.
Narudia tena ni maelekezo halisi,ongeza nidhamu kwenye usimamizi.Ninatofautiana naye kidogo kwenye eneo la uwiano wa jogoo na mitetea.Kwa sasa wataalam wanashauri jogoo 1 mitetea 5,kwa mitetea 10 unahitaji jogoo 2 ili washindane.
Bahati mbaya, mahesabu na kinachoitwa maandiko ya miradi ya Ufugaji kibiashara mengi humu JF hayatoki kwa wafugaji. Kwa uzoefu wangu wa Ufugaji, hakuna Kuku utakayemnyang'anya vifaranga Leo halafu baada ya wiki 3 aanze kutaga,
Kuna wengine ni wazazi halisi wana uchungu wa kupoteza watoto kama binadamu. Kuku wangu baadhi ukiwanyang'anya watoto, wiki mbili hadi mwezi, hachangamani na wenzake, yuko mpweke, anakula kwa shida, akisikia sauti ya kifaranga tu, popote, anasimama. Huyo kuja kutaga tena, ni miezi 3.
Lakini pia, Kuku wa kienyeji huwezi piga mahesabu ya utagaji kwa siku 30 za mwezi na 365 za mwaka. Ukijaribu kuwa halisia kidogo, piga wastani wa mayai 15 kwa kila miezi 3. Najua kuna koo chache wanaoweza kutaga hadi mayai zaidi ya ishirini, lakini wapo pia ambao Fanya ujuavyo, hawazidishi 10. Hata Mimi ninao ambao hufikisha 18 hadi 23, lakini ninao ambao Mara zote hawavushi 8, hususani jamii ya kuchi. Hata kama unaondoa unabakiza moja moja, akifikia mwisho wake, hata kama umeyaondoa yote, anahatamia michanga tupu.