Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam

Karne ya 21 TRA mnafanya kazi za kuviziana tena usiku kukamata /kufuatilia so called magari yaliyokwepa Kodi ? Mtu atajuaje kama ni TRA au Majambazi ?

Gari mnazo namba na mmiliki jina mnalo na sio kwamba gari linapita hewani bali barabarani hivi kweli mlishindwa kuwasiliana na Polisi / Traffic na kuipiga gari fulani wanted kwamba ikipita sehemu / ikionekana Traffic waweze kuhoji na kumfahamisha Dereva kwamba nyaraka zinatakiwa au kuwaambia wapeleke nyaraka mamlaka husika?

Tatizo hii nchi hizo ni fursa za watu kutafuta milungula jambo ambalo linakuwa harassment kwa mlipa Kodi na mara nyingi Pesa nyingi zinaishia mikononi mwa watu na sio serikalini...
 
Hii ni ngeni kwako? Fatilia vizuri hao jamaa wana operations zao, wapelelezi, intelejensia yao na wanakamata vilevile, haijalishi siku wala masaa.
Unajua watu wengi wanajua TRA ni makadirio tu ya biashara, saa 12 jioni wamefunga ofisi.

Kumbe kuna upande mwingine wana deal hadi na magendo na wanakesha, ila kwa escort ya vyombo vya usalama. Kama hawakuwa na polisi basi wamejitakia, pole yao.
 
mna mamlaka ya kumfuatilia

Tanzania ina tatizo kubwa majeshi mengi - TRA task force, misitu, uvuvi, mapori tengefu, TANAPA, mgambo, polisi shirikishi bila kusahau majeshi ya usalama yaliyo DCEA, Zimamoto, Uhamiaji na Polisi.

Traffic police walikuwa na mashine viganjani kwa ajili ya kutoza faini, kufuatilia faini ambazo hazijalipwa. Pia traffic police wanafuatilia insurance kama zimelipwa n.k

Kwanini TRA wasiripoti taarifa hizo za BMW kwa jeshi la police traffic ili lishughulikiwe kipolisi badala ya TRA kukimbizana mabarabarani na gari shukiwa ambalo linadaiwa halijalipiwa kodi zote ?

TRA inafanye kazi kwa kisasa zaidi na kuhusisha traffic police kukazia sheria za kodi za magari.

Majeshi ya TRA task force, misitu, uvuvi, mapori tengefu, TANAPA, mgambo, polisi shirikishi hayajulikani yanadhibitiwa kwa kanuni gani za kikazi, nidhamu na mamlaka yao yanaishia wapi .
 
Sina Neno la kusema ila nisisahau kusema nimefurahi sana kusikia wamepigwa kipigo Cha umbwa Koko
🤗🤗🤣🤣😆😆
20240707_094520.jpg
 
Kama gari mnaijua na ina usajili kwanini msimuite mwenye nayo atoe nyaraka za gari yake? Inakuwaje mnaanza kufuatilia mtu tena usiku?

Nyie ni polisi?
Je mna mamlaka ya kumfuatilia mtu na kumkamata au kukamata mali yake bila kushirikisha vyombo vya ulinzi?

Hayo yote mmeyataka kwakuwa hali ya usalama wa raia nchini imedhoofu kiasi kwamba sasa raia ni lazima kuwa vigilant la sivyo ni kutekwa na kuuwawa tu.

Wafanyakazi wenu mnatakiwa muwape barua ya onyo kwa kuwa negligent. Wameshindwa kusoma alama za nyakati.
Maandazi ya Mungu yanauma nyie usiombee upigwe kitofali cha uso sijui wana hali gani huko walipo muda huu wanajuta kwanini waliifuata hio gari, next time gari itapigwa moto wawe makini
 
Tanzania ina tatizo kubwa majeshi mengi - TRA task force, misitu, uvuvi, mapori tengefu, TANAPA, mgambo, polisi shirikishi bila kusahau majeshi ya usalama yaliyo DCEA, Zimamoto, Uhamiaji na Polisi.

Traffic police walikuwa na mashine viganjani kwa ajili ya kutoza faini, kufuatilia faini ambazo hazijalipwa. Pia traffic police wanafuatilia insurance kama zimelipwa n.k

Kwanini TRA wasiripoti taarifa hizo za BMW kwa jeshi la police traffic ili lishughulikiwe kipolisi badala ya TRA kukimbizana mabarabarani na gari shukiwa ambalo linadaiwa halijalipiwa kodi zote ?

TRA inafanye kazi kwa kisasa zaidi na kuhusisha traffic police kukazia sheria za kodi za magari.

Majeshi ya TRA task force, misitu, uvuvi, mapori tengefu, TANAPA, mgambo, polisi shirikishi hayajulikani yanadhibitiwa kwa kanuni gani za kikazi, nidhamu na mamlaka yao yanaishia wapi .
Ni hatari sana, ndio maana tunaitaka katiba mpya maana ya sasa ina matundu kama nyavu ya samaki. Mtu anaamka tu anaamua kuanzisha anachokijua na kukipa mamlaka anayotaka kwa maslahi yake.
 
Back
Top Bottom