Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Mtoa mada nadhani unataka kuturudisha enzi zile za mzee wa kuota ndoto na kutabiri (Nyerere)

Katika rundo la picha ulizoweka kwanini kila picha inayoonyesha mateso ya Waarbu kwa mtu mweusi iwe ya kuchora? Hivi wakati huo kamera zilizokuwepo zilikuwa hazipigi picha za mateso bali za furaha tu?

Mada yako haina tofauti na hadithi za kusadikika wanazopewa wageni kila wakitembelea kanisa la mkunazini Unguja? Wagalatia wa kanisa lile na wengineo wamesahau kuwa aliewapa kiwanja cha kujenge kituo chao cha kuzalisha propaganda dhidi ya waarabu na uislamu ni Sultani wa Kiarabu ambae ndie aliekuwa mtawala wa zanzibar!!??

Suala la kujiuliza ikiwa soko la watumwa lilikuwepo pale penye kanisa la mkunazini na wao ndio wenye kanisa, jee niwakati gani soko lilikuwepo na baadae ikapatikana nafasi ya kujenga kanisa!!?

Akili za kuambiwa.
Kuna dini fulani kuitetea ni kazi sana
 
Ndugu katika Imaan wameguswa eeeeh!
Pole


Ndugu yako katika imani , akimaliza hapo anawaletea mipasho ya waarabu

1736671982836.jpeg
 
Mwana JF, Paskali, anakutakia wewe na familia yako HERI YA SIKUKUU YA MAPINDUZI MATUKUFU
YA ZANZIBAR!
Paskali


TUUSOME UKWELI HUU

Dondoo hizi zimechukuliwa kutoka kitabu cha Amani Thani Ferooz, Ukweli ni Huu, Mzanzibari na kiongozi wa Chama cha Wazalendo wa Zanzibar (Zanzibar Nationalist Party) katika miaka ya 1960. Sehemu hii inaelezea mateso waliyoyapata wafungwa wa kisiasa baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964, ambayo kwa maoni yake yalikuwa na mavamizi ya Tanganyika kwa Zanzibar.

MAHABUSU WA KISIASA WA MWALIMU NYERERE

Maalim Harun Ustadh
Maalim Mohammed Mattar
Seyyid Hassan Sheikh
Seyyid Mohammed Adnan
Mzee Mohammed Mbaba
Ahmed-Rashad Ali
Hashim Haji Abdalla
Seyyid Hashim Abdalla Baharun
Abdul-Latif Binbrek
Mohammed Shioni
Seyyid Mohammed Mattar
Mohammed Ali Abbas
Ali Abdalla (Admeri)
Ali Jaffer
Ali Khalifa Miskiry
Ali Manara (Mtu wa Tanganyika)
Aman Thani Fairooz

Baada ya kumaliza kutukhutubia, Mkuu wa Magereza, aliondoka na sisi kila mmoja alipe-wa kirago chake pamoja na shuka mbili na kopo la kunywiya maji na ndio hilo hilo la kutumia kwa kujisafishia baada ya kwenda haja kubwa na ndogo. Tulipomalizika sote kupewa vitu hivyo, tuliongozwa mpaka kwenye vyumba vya kulala mahabusi.
Siku ya pili, waliletwa wenzetu wawili wengine, mmoja alikuwa mwanamke, Bibi Mbarawa Bakari, yeye alipelekwa katika upande wa mahabusi wa kike na mwengine alikuwa Seyyid Harun Abdalla Baharun, yeye aliletwa upande wetu. Sote kwa jumla tukawa watu 19, mmoja mwanamke na 18 wanaume. Hawa wenzetu wawili, Bibi Mbarawa na Seyyid Harun wao walikamatwa hapo hapo Zanzibar. Mpaka wakati huo tulikuwa bado hatujaweza kufahamu sababu zilizope-lekea kukamatwa na kuletwa gerezani.

Baada ya kiasi cha mwezi mmoja tokea kuletwa gerezani, Rais Karume pamoja na kikosi chake cha ‘Baraza la Mavamizi’ walikuja na Karume alitukhutubia kwa kutumia ma-neno kama haya: “Nyinyi mmeletwa kwetu kutokana na ukorofi mnaoufanya huko Dar-es-Salaam. Mwalimu Nyerere ametoa amri muondolewe na mrejeshwe makwenu. Mpaka sasa bado hatujaletewa ripoti yenu kamili. Tutapoipata na baada ya kuichun-guza, tutatoa uamuzi wetu. Ikiwa kukuachilieni huru au kukupelekeni mbele ya mahakama. Lakini mjue kuwa mahakama yenyewe ni ya kijeshi. Ikiwa mutaonekana na kosa, basi adabu yenu itakuwa KIFO”. Baada ya kusema hivyo, alianza kutu-tukana na ku-tutisha kwa kutumia lugha za ukali na za vitisho na alielekeza ma-tusi yake na vitisho vyake zaidi kwa ndugu zetu wenye asili za Kingazija kwa vile ilitokea katika hilo kundi letu, jamaa wa Kingazija walikuwa wakionekana ni wengi. Kutokana na vitisho hivyo, ndugu yetu mmoja aliingiwa na khofu hata ali-tokwa na haja ndogo bila ya kuweza kujizuwia. Karume na kikosi chake walipomuona katika hali hiyo, badala ya kuamrisha aon-dolewe kwa kusitiriwa, waliangua vicheko wakamcheka na kum-fanyia istihizai. Sisi tuliinamisha nyuso zetu chini utadhani wanawari wa ki-zamani. Ilikuwa ni siku hiyo na pahala kama hapo, gerezani, ndipo Rais wa nchi, Abeid Amani Karume alipotoa amri ikawa ndio sheria ya kuwa Wangazija wote si raia wa Zanzibar kuanzia siku hiyo na wakati huo. Mngazija yoyote mwenye kutaka uraia wa Zanzibar basi lazima afanye maombi ya Tajnis. Hapo hapo alimtaka Al-Haj Aboud Jumbe awaite waandishi wa magazeti siku ya pili na awape khabari hizo. Mzalia wa Zaire anamwambia mzalia wa Tanganyika atangaze kuwa wazalia wa Zanzibar si Wazanzibari ati kwa kuwa asili ya wazee wao ni Comoro! Hii ndiyo haki?

Jambo la kustaajabisha na kuhuzunisha ni kuwa wakati huo alipokuwa Karume akipasisha sheria hiyo ya “kifashist”, hao ndugu zetu wajii-tao “progressives” walikuwepo na sio kuwa walinyamaza kimya kwa kuwafik hayo, bali walifurahikia na kupigia makofi na huku wakisema, “Sawa Mzee! Sawa Mzee”! Ikiwa u”progressive” wenyewe ndio hali yake kama hiyo, basi hatujui huo u”reactionary” utakuwa hali gani! Dikteta anatoa amri, amri inakuwa sheria ya nchi, bila ya hata kushauriana na hilo gengi lake la wauwaji, isitoshe, wanaojiita “progressives” wanasherehekea!! Baada ya hapo Karume na kikosi chake waliondoka na walituacha sisi katika khofu na ya wasi wasi kwa kufikiria yepi yatayotutokea, kwani yeye ndio keshatowa ruhusa tutendewe maovu wapendavyo hao aliowaachia nafsi zetu kwao. Serikali ya ‘mavamizi’ haikuwa ikiendeshwa kwa njia za haki, mwendo wake ni wa kinguvu-nguvu na kibaba-baba tu. Mfunge! Mnyonge! Mchinje! Ndio sheria zilizokuwepo. Kwahivyo tulikuwa katika hali mbaya sana baada ya siku hiyo.

Kiasi cha miezi miwili kutoka siku hi-yo aliyokuja Karume gerezani, natumai ilikuwa taarikh 14 Ramadhan, Disemba 1968, kiasi cha saa 12 za magharibi muda mchache kabla ya kulia kwa kin’gora, alitujia sajini wa magereza na alitutaka tu-chukue futari zetu tumfuate kwani wakati huo tulikuwa tu-mesha letewa mapande yetu ya muhogo wa kutokosa na majani mapevu ya kisamvu. Tulichukua na tu-limfuata mpaka katika uwanja wa ‘kotagadi’ alituambia tukae hapo. Kiasi cha muda mdogo, kin’gora kililia na tu-liruhusiwa kwenda kut-awadha na kusali, tulifuturu na kiasi cha kumaliza tu, taa zote za ‘kotagadi’ zilizimwa kumekuwa kiza to-to-roo! Mara lango la gereza lilifunguliwa na gari la magereza lika-ingia ndani kinyume nyume. Roho zilitubakuka, vinywa vilijaa mate, mradi kila mmoja hajijui, hajitambui.

Muda si muda, tuliam-biwa tuingie katika hiyo gari. Msafara wetu haukuwa mkubwa sana kwani ulimalizikia kwenye gereza la kwa “Ba Mkwe” au kwa jina lengine, “Mlango wa Nyuma”. Wakati huo, wenzetu wawili, Ahmed-Rashad Ali na Ali Manara, wao walikwisha achiliwa huru.

Hili gereza la “Kwa Ba Mkwe” limean-zishwa na Serikali ya Mavamizi muda mchache tu baada ya kukamata kutawala. Makusudio makubwa ya kuanzishwa gereza hilo ni la kuwatesea wananchi ili wawe na khofu wasithubutu kutoa fikra zao na maoni yao kukhusu mwendo wa serikali. Wananchi wengi sana wamepotezewa roho zao katika gereza hilo. Gereza hilo lilikuwa chini ya uangalizi wa Idara ya Usalama (Security Department) na mkub-wa wa Idara hiyo alikuwa Ibrahim Makungu, na mkuu wa gereza hilo, alikuwa Hassan Reihan (Hassan Mandera) au kwa jina lengine alikuwa aki-julikana “ZIRAILI” na kweli alikuwa ziraili. Kwani mtu yoyote afikae mikononi mwake basi kurejea yuhai ni miujiza. Ponapona, utamalizikia gerezani kwa kifungo cha miaka kumi baada ya kufikishiwa kila aina ya mateso.

Tulifika kwa “Ba Mkwe” kiasi cha saa moja unusu za usiku na tulimkuta mwenyewe Mandera na watu wake wanatusubiri. Tulianza kuandikwa majina yetu mmoja mmoja, na kila anayemaliza kuandikwa akipelekwa kwenye vyumba vya gereza hilo. Tuligawanywa ka-tika vyumba mbali mbali. Kwa wakati huo hapana ali-yeweza kujua kuwa fulani yuko katika chum-ba fulani au yupo pamoja na fulani. Mimi niliba-hatika kutiwa chumba kimoja pamoja na Shariff Mohammed Mattar, katika chumba hicho tuli-wakuta watu wane weshakuwa wenyeji zamani. Wenzetu hao walitukaribisha na mmoja kati yao, alitwita kwa majina yetu. Yeye aliweza kututambua bali sisi tulishindwa kumtambua mpaka alipotujuul-isha yeye mwenyewe.

Hali zao zilikuwa zikitisha kwani wote walikuwa wamejifunga matambara na ma-gunia viunoni kuwa ndio nguo zao za kujisitiri, matumbo wazi. Manywele timtimu na yamesokotana, madevu na masharubu yameziba vinywa. Chumba ki-nafuka moto, chumba chenyewe ni urefu futi 10 na upana futi 10, kina dirisha moja nalo liko juu hata ukichupa huwezi kulipata. Yule mzee aliyetwita kwa majina yetu alituuliza, “Jee, mnaweza kunitambua mimi nani?” Tulimjibu laa, hatujaku-tambua”. Alisema, “Najua kuwa hamku-weza kunitambua. Jina langu ni Abbas Othman kwa jina la umaarufu naitwa Mzee Kenyatta”. Alipotutajia jina hilo la Kenyatta, hapo hapo tuliweza kumfahamu. Hakika alikuwa amebadilika sana. Mzee Kenyatta alituambia kama hivi:-
“Ndugu zangu, lazima nikuelezeni kukhusu mambo yaliopo katika gereza hili. Katika gereza hili, watu hawapewi virago vya kulalia, ndio kama mnavyoona hivi tulivyo tunalala na tunakaa juu ya sakafu kavu.

Kadiri ya nguo ulizokuja nazo ndizo hizo hizo utazoishi nazo kwa muda utaokuwepo katika gereza hili. Hata ukiumwa basi hupelekwi kwa daktari, ukibahatika, unaweza ukaletewa vichembe viwili vya asprin, lakini si katika kawaida. Milango ya vyumba hivi inafungwa saa ishirini na nne. Kufunguliwa kwake ni kwa muda maalumu tu, tena haifunguliwi yote kwa wakati mmoja. Ukifunguliwa mlango wa chumba kimoja, vilivyo baki vyote huwa vimefungwa mpaka warejee waliyotolewa kutoka katika chumba hicho, ndiyo kifunguliwe chengine.

Yaani musiweza kukutana wa chumba hiki na chumba hiki. Nyakati zenyewe za kawaida za kufunguliwa milango ni alfajiri kiasi cha saa 11 hivi. Wakati huo ndio hutoa ndoo ya uchafu wa choo, na wakati huo ndio tunautumia kwa haraka haraka kujitia maji mwilini, bila ya sabuni; na kusugua meno kwa kidole na kutumia udongo, hata kijiti cha msuwaki huachiliwa kuwa nacho hapa. Baada ya hapo hufunguliwa tena kiasi cha saa moja ya asubuhi kwa kwenda kuchukuwa kifunguwa kinywa. Na baada ya hapo, hufunguliwa tena kiasi cha saa tano za mchana kwa ajili ya kuzitoa nje sahani za chai ya asubuhi.

Na hufunguliwa tena kiasi cha saa nane za mchana kwa ajili ya kuchukuwa chakula cha mchana. Kisha baada ya hapo hufunguliwa tena kwa mara ya mwisho kwa siku hiyo kiasi cha saa 11 za jioni kwa ajili ya kuzitoa sahani za chakula cha mchana na kwa kuchukuwa maji. Muda wa kufunguliwa na kurejeshwa ndani hauzidi dakika kumi. Si ajabu tukaona hivi sasa, ukafunguliwa mlango na akatolewa yoyote kati yetu na ikawa ndio basi tusimuone tena, au baada ya muda wautakao wenyewe ndio wakamrejesha. Akitolewa mtu ndani ya chumba huwa kwa ajili ya mambo mane ndio khasa! Imma hutolewa kwa kubadilishwa chumba au kwa kwenda kuteswa, au kwa kwenda kuuliwa, au kwa kwenda katika gereza kuu kwa kufungwa. Amma kutolewa humu kwa kuachiliwa huru, hilo ni jambo la matokeo makubwa sana.”

Mzee Kenyatta alimaliza kwa kusema, “Haya niliyo kuelezeni ni mambo ya kawaida ya gereza hilii. Lakini vituko vinavyotokea katika gereza hili mara kwa mara ni vingi sana na vinaweza kututokea katika wakati wowote si mchana, si usiku. Kwa vile mpo, mtayaona wenyewe”.

Wakati huo, ulikuwa kiasi cha saa nne za usiku, tulita-funa vipande vyetu vya muhogo tulivyo vibakisha vikiwa ndio daku letu, na tulipiga kopo la maji kisha tulipangusa pangusa mchanga, na tulijitupa katika sakafu kavu, na kuutafuta us-ingizi. Wapi! Usingizi haukukubali kuja. Kucha tulizifungua TV za moyoni ikimalizika, chanal hii tukifungua nyengine; mpaka tuliposali Alfajiri jicho halikukubali kufun-ga hata dakika.

Kiasi cha kumaliza tu kin’gora cha asubuhi cha kuingia makazini, mlango wa chumba chetu ulifun-guliwa na nilimuona kijana mmoja amesimama na alikuwa akitutizama kwa uso wa kijeuri uliyo chan-ganyika na ujinga. Kijana huyo aliuliza kwa sauti ya ki-jeuri kabisa, “Nani Aman Thani hapa?” Nilimjibu, “Mimi hapa”. Aliuliza tena, “Wewe ndiye uliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbu”? Nilimwambia, “Naam, ndiye mimi”. Aliniuliza tena, “Na wewe ndiye sasa Katibu Mkuu wa chama chenu cha siri cha Kiislamu huko Dar-es-Salaam?” Nilimjibu, “Chama hicho cha siri mimi sikijui, wala sijapata kukisikia, wala mimi siye Katibu Mkuu wa Chama hicho ikiwa kipo”. Aliniambia, “Baada ya muda mdogo, utakijua. Wengi kama wewe walipoletwa hapa, kila walichokuwa wakiulizwa wakisema, hatujui. Lakini baada ya kukutana na vijana wa kazi, kila walilosema hawalijui, waliliju-wa wenyewe. Basi na wewe baada ya muda mdogo utayajuwa yote, subiri tu”.

Alipomaliza kusema hivyo, aliufunga mlango kwa kijeuri. Alipoondoka huyo kijana niliwauliza wenzangu, “Huyu ndiye nani”? Mzee Abbas Kenyatta aliniambia, “Huyu anaitwa Musa Makwega. Inasemekana kuwa ni mtoto wa ndugu yake Simba Makwega”.
Naam, haukupita muda ila mlango wa chumba chetu ulifunguliwa tena na safari hii alikuja kijana mwengine. Kijana huyo alikuwa amevaa chupi tu, hakuwa na nguo nyengine yoyote katika mwili wake. Alipofika alisema, “Aman Thani na atoke nje”. Nilitoka na niliongozwa mpaka kwenye chum-ba kimoja kikubwa na huko nilimkuta Mandera na Juma Musa. Hawa wawili nilikuwa nikiwajua tokea zamani. Pia walikuwepo na wengine ambao baadae niliwajuwa majina yao. Mmoja akiitwa Ame Fidia na mwengine, Haji kwa umaarufu akiitwa Haji Kifupi, na yule aliyekuja kunichukuwa akiitwa Mzee. Haji na Mzee wote wawili walikuwa ni vi-jana wa Bumbwini, Unguja, na Ame Fidia alikuwa kijana wa Tumbatu, na Juma Musa alikuwa kijana wa ki-Unguja katika sehemu za mashamba, sikupata kujuwa shamba gani kwao.
Katika chumba hicho, kulikuwemo meza moja kubwa na viti viwili. Juu ya meza hiyo, kulikuwepo bastola moja na pembezoni mwa ukuta, kulikuwepo na mizigo kwa mizigo ya fimbo za mipera. Chini ya hiyo meza kulikuwepo kamba ya kitani iliyoku-wa nene kidogo ambayo katika ncha yake moja ilikuwa na kitanzi. Kuta za chumba hicho na sakafu yake, vyote vilikuwa vimejaa mabaka mabaka ya damu iliyokaukia. Mandera aliniambia. “Aman, mimi na wewe tuna-juana zamani sana. Hatujapata kukwaana hata mara moja, bali lazima nikuambie kuwa hapa katika gereza hili, hapana udugu, wala ubaba, wala urafiki, wala hapana kujuwana. Katika gereza hili, yapo mateso ya kila namna na tuna haki ya kumtesa mtu yoyote kwa mateso ya aina yoyote, maadamu atajifanya mkaidi wa kutwambia ukweli juu ya mambo tuyatakayo kutoka kwake. Na ikiwa atatwambia ukweli, basi hatoteswa na hatokaa humu kwa muda mkubwa ila ata-tolewa, na kwenda zake nje na kuendelea na maisha yake. Basi nakwambia na wewe ikiwa utataka uteswe basi utateswa; ikiwa utajaribu kuuficha ukweli, sisi tunazo khabari zote, lakini tu-nataka tuyakinishe kutokana na vinywa vyenu wenyewe.”

Aliendelea kwa kusema, “Tunalolitaka utwambie, ni nini makusudio ya kuunda hicho chama chenu cha siri cha Kiislamu, na ni nani wakuu wenu wenye kukiendesha chama hicho kwa kifedha? Tunajua kuwa nyie ni wenye kutumiliwa kwa kutekeleza madhumuni ya hao wakuu wenu. Nakuahidi, ikiwa utatwambia ukweli, basi hutokaa humu hata wiki, utatolewa na utarejeshwa Dar-esSalaam kuendelea na maisha yako”.
Hakika nilisangazwa na masuali hayo kwani licha mimi kuwemo na kutokuwemo katika chama hicho, bali hata kupata kukisikia sijapata kukisikia maisha yangu. Nilimjibu kuwa, “Mimi sikijui, wala hao wakubwa wa chama hicho ikiwa wapo, mimi siwa-jui”. Kiasi ya kumwambia hayo tu, nilimuona Mandera amebadilika sura yake na alianza kutumia lugha za ukali na matusi na mwisho aliniambia, “Ikiwa unataka kutuonesha uhodari kwa kukataa kusema kweli, basi na sisi tutakuonesha nini tutakufanya sasa hivi. Utatuambia ukweli au vipi?”

Nilimwambia, “Ikiwa un-autaka ukweli, huo niliyo kwambia ndio ukweli wala sina ukweli zaidi kuliko huo”, “yote haya uyasemayo miye sijui lolote juu yake”. Allah Akbar! Alinipiga kibao cha ghafla, kilinitupa mpaka chini. Hapo, aliamrisha nilazwe juu ya meza, sikuwahi hata kupepesa, nilijisitukia nimesha bwag-wa juu ya meza kama gunia la chumvi na ni-melazwa kifudifudi.

Naam, Mandera hakupoteza wakati, alianza kunicharaza kwa fimbo za mipera na huku akinitukana kwa matusi mabaya mabaya. Nilikuwa siwezi hata kufurukuta kwani hao wasaidizi wake walinidhibiti mikono na miguu, mradi nilikuwa taaban! Tokea nilikuwa nikihisi maumivu ya kupigwa mpaka mwili ulikufa ganzi nik-awa sihisi chochote. Tokea nikiweza kupiga makelele na kuyayatika mpaka nilikuwa siwezi hata kuguna. Alipochoka mwenyewe, ndipo na mimi nilipopata afuweni. Lakini, wakati huo nilikuwa chordo! Chumba chote nikikiona kinazun-guka na watu nikiwaona wanazunguka.

Niliachwa katika hali hiyo kiasi cha muda mdogo, kisha Mandera aliniambia niinuke kwenye meza nikae katika kiti. Nilipojaribu kujizowa-zowa, miguu ilishindwa kukanyaga chini kwani bakora zilifika mpaka nyayoni na pia miguu ilikuwa ikinitetemeka. Nilikamatwa huku na huku na kuwek-wa juu ya kiti. Mandera aliniuliza, “Umefunga wewe leo?” (kwani siku hiyo ilikuwa Ramadhani ya kumi na tano) Nilimjibu, “Naam, nimefunga!” Aliniambia, ” Basi leo, utafuturu mikwaju”. Wakati huo roho ilikuwa kavu, mate yamenikauka, jasho likinitoka kila sehemu ya mwili. Matako yametutumka na ku-pasuka pasuka. Kiti kilikuwa hakikaliki kwani kilikuwa kikinitonesha. Kwa hakika, nilikuwa katika hali mbaya sana. Baada ya Mandera kupumua kidogo, alirejea tena kuniuliza masuali yake yale yale aliyoniuliza mara ya mwanzo. Na mimi, nilimjibu kama nilivyomjibu mwanzo.

Hapo, Mandera aliamrisha nitiwe ile kamba ya kitanzi na nikatiwa nayo shingoni. Baada ya ku-tiwa, ilichukuliwa ncha moja ikapitishwa dirishani. Dirisha hilo lilikuwa juu sana hata huyo aliyekuwa akipenyeza hiyo kamba ilim-bidi apande juu ya meza kuitupia. Wakati huo mimi nilikuwa nimekaa juu ya kiti na shingoni mwangu nimevalishwa hicho ki-tanzi cha kamba ya kitani. Wote walitoka nje, isipokuwa Mandera tu alibakia pamoja na mimi na kitanzi changu shin-goni mwangu. Utafikiri n’gombe mkali wa kuchezwa. Wale wali-yokuwa wametoka nje, kazi yao ilikuwa kuivuta ile kamba mfano wa mtu anapovuta ndoo ya maji kutoka kisimani kwa kutumia roda. Nilianza kunyanyuka, si kwa khiyari, bali kwa kule kuvutwa mpaka nilikiwa-cha kiti ikawa nafuata kule ninako vutwa. Mandera kazi yake ilikuwa ni kuamrisha, “Vuta! Wacha!” Akisema vuta, huvutwa na akisema wacha huachiliwa.

Na ilipokuwa ikiachiwa, nilikuwa nikishindwa kujizuwia kwahivyo nikianguka kama nanga ibwatikavyo ba-harini. Mandera alikuwa akinipiga kwa fimbo za mipera na huku akiniambia, “Simama!”. Mradi kazi ilikuwa kama hivyo, mpaka walipotaka wenyewe, waliniachia na walinitoa hicho kitanzi. Mandera alitoka nje ya hicho chumba na aliniacha mimi na hao wasaidizi wake. Juma Musa aliniam-bia, “Sikiliza Aman! Wacha ushupavu wako utakuja kujidhuru mwenyewe. Hapa ni pahala pabaya sana. Matokeo ya gereza hili hutoyaweza wewe, kwani ni ya khatari sana na mwisho ni kuuliwa. Basi mimi nakuomba useme kweli wa hicho chama chenu upate kujinusuru na mateso”.

Mimi nilinyamaza kimya sikumjibu chochote, kwani nilielewa kuwa anatumia lugha alizofundishwa katika kazi yake hii. Juma Musa alipoona hakupata chochote kwangu, na yeye alitoka katika hicho chumba na kuniacha mimi na hao wasaidizi wao wengine. Baada ya muda, Mandera na Juma Musa walirejea katika chumba, Mandera ali-wauli-za hao watu wake kama nimesema chochote na Juma Musa alimwambia Mandera kuwa, “Anajifanya hodari, hataki kutwambia ukweli. Mimi nimejaribu kumnasihi, hata hakuonesha ku-wa ananibali kitu”. Mandera alisema, “Kwa nini hatu-muuwi, kwani patakuwa kitu gani tukimuuwa? Lete ile bastola!” Kijana mmoja katika wasaidizi wake akiitwa Mzee, aliruka kuileta hiyo bastola. Mandera aliniambia, “Unaiona hii basto-la, basi towa shahada kabisa. Leo utafuturu kabur-ini”.

Aliamrisha nifungwe kitambaa cha uso. Makame Fidia ndiye aliyenifunga hicho kitambaa. Nilitoa shahada. Hapo sikuweza kujuwa yalipitish-wa mazingaombwe gani kwani nilisikia mlio mkub-wa wa risasi lakini haikunigusa wala haikuniuwa, lakini kwa khofu nilizokuwa nazo, nilianguka mpaka chini. Nilipoanguka, niliwasikia wakicheka kwa tafrija na istihizai, na huku Mandera akisema, “Nyoo! Si unajitia uho-dari wewe, mbona unaogopa kufa. Hii ya leo ni trai tu mchezo bado”.

Mandera aliamrisha nifunguliwe hicho kitambaa cha uso na baada ya kufunguliwa, aliniambia, “Leo tutakuachia ukapumzike na ukazidi kufikiri mpaka kesho. Utakapoletwa hapa uweumesha kata shauri juu ya kusema kweli au kuendelea na kuuficha ukweli. Lakini, nakwambia kuwa kesho ukitufanyia mchezo kama huu uliyoufanya leo, basi tutaanza kwa kukutoa kucha za vidole vya mikono, kisha tukutowe na vya miguu, na tutakupaka hina ya pili pili ho-ho. Sasa mrejesheni kwa wenzake. Wakati huo kin’gora cha saa nane unusu cha kutoka watu makazini kilikuwa kikilia. Mchezo ulianza tokea saa mbili za as-ubuhi mpaka wakati huo wa saa nane unusu ndipo ulipomalizika.

Nilikuwa katika hali mbaya sana hata nilishindwa kwenda bila ya kusaidiwa kwa kukamatwa mkono utadhani mtoto mdogo anafundishwa kwenda tata.
Nilipofika katika chumba wenzangu waliponiona hali hiyo niliyokuwa wakati huo, jambo la mwanzo, walininasihi nisiendelee na sau-mu, na mimi nilihisi hivyo hivyo, kwani roho yangu ilikuwa kavu, midomo mikavu hata mate ya-linikauka.

Hapakuwepo na cha kukila kwa wakati huo, isipokuwa maji na hata kingekuwepo, basi nisingeweza kukila. Hayo maji nayo yalikuwa yakipita kwa shida. Mwili wangu ulikuwa umejaa mitutumko tutumko, na mipasuko pasuko ya bakora za Mandera hata nilikuwa na taabu kwa muda wa siku kadhaa kuweza kulala; bali hata kukaa kitako ilikuwa taabu. Ilipofika laasiri, nilipata homa kubwa sana na wenzangu walijaribu kuwaita wachungaji wa gereza hilo kwa kuwagongea mlango ili wapate kuniombea dawa.

Hapana aliyekuja. Kwa bahati Mzee Kenyatta alikuwa na akiba ya vidonge vya aspirin, aliweza kunigaia vidonge viwili, si haba viliweza kidogo kunisaidia. Usiku kucha nilikesha kwa maumivu niliyokuwa nayo na kwa khofu nilizokuwa nazo kwa kufikiria hayo yaliyokuwa yakiningojea patapo kucha. Mandera nilikuwa nikimuona amenisi-mamia ma-choni mwangu. Kulipokucha homa ilinizidi kwani ilikuwa kila dakika ipitayo, nilikuwa sasa hivi au khala-fu ni-takuja kuchukuliwa. Al-Hamdulillahi, nilishinda kut-wa na kucha bila ya hata kuulizwa. Na ilikuwa ndio basi, hawakunichukua tena baada ya siku hiyo moja.

Tulikaa katika gereza hilo la “Kwa Ba Mkwe” tokea Disemba 1968 mpaka taarikhi 3 Mei, 1969 tulipotolewa na kupelekwa katika Makao Makuu ya Magereza. Kupelekwa kwetu huko kulikuwa kwa ajili ya kufungwa gerezani. Tulipofika ‘kotagadi’, ilikuwa kiasi cha saa 11 za jioni. Kila mmoja alipewa viroba vyake, na shuka moja, na kirago cha kulalia pamoja na kopo la kunywiya maji. Tulizivua nguo zetu na tulivivaa viroba vya kifungwa. (Viroba ni shati lisilokuwa na ukosi na suruali kipande, kaputura).

Tulipoona tumepewa viroba vya wafungwa, kila mmoja alipigwa na msangao na machozi yalikuwa ya kimlengalenga. Tulijikaza kidume na tulikuwa tukipeyana moyo wenyewe kwa wenyewe. Waliyokuwa wakitusikitisha zaidi ni wale wenzetu waliyokuwa wazee kwa umri wao kama Seyyid Hassan Sheikh, Maalim Harun Ustaadh, na mare-hemu Maalim Mohammed Mattar. Wote hao walikuwa umri wao ni baina ya miaka 60 na 70 na hawakuwa na siha nzuri kutokana na maradhi waliyokuwa nayo, ya Presha, Sukari na maradhi ya ukongwe. Tuliweza kuelewa kuwa tumesha kuwa wafungwa lakini hatujui kifungo chetu ni cha muda gani. Juu ya hayo, kwa vile kuwa tumetoka katika gereza la “Kwa Ba Mkwe”, tukiwa na uhay wetu. Ingawa baadhi yetu tulikutana na mateso lakini tumetoka bila ya vilema na kuwa an-galau tutaweza kwenda huku na huku kuliko kukaa ki-tako kimoja usiku na mchana, bila ya harakati zo zote, tuliona siku hiyo kama tumeachiliwa huru.

Kabla ya kuondoka hapo ‘kotagadi’, tuliwaona wen-zetu wengine nao wameletwa na kupewa viroba vyao. Miongoni mwao, walikuwemo, Bwana Abdul-Aziz Twala ambaye alikuwa Waziri katika Serikali hiyo ya Mavamizi, Bwana Jaha Ubwa, ambaye alikuwa, Mkuu wa Jimbo (Area Commissioner), Bwana Mdungi Usi, am-baye alikuwa, Katibu wa Baraza la Mji (Town Clerk), Bwana Aboud Nadhif, ambaye, alikuwa Mkuu wa Idara ya Muawana (Co-operative Society), Bwana Juma Maulid (Jimmy Ringo) ambaye alikuwa, Kamisari (Commissar). Pia miongoni mwao walikuwemo, Mzee Abbas (Kenyatta) na Ali Ngwenge, wote hao wawili ni katika wakereketwa wa Afro-Shirazi.

Vile vile waliyoletwa kufungwa siku hiyo kutoka huko huko gerezani “Kwa Ba Mkwe”, alikuwa ndugu yetu, Sheikh Saleh Ali Nasser (Saleh Master). Ndugu yetu huyu Saleh Ali Nasser (Master) ni mmoja kati ya wananchi waliyoteswa vibaya sana katika gereza hilo la “Kwa Ba Mkwe”. Kwani siku hiyo tuliyoletwa Makao Makuu ya Magereza kwa ki-fungo, mwenzetu huyo alikuwa hata hakuweza kwenda sawa sawa kwa miguu yake.

Tulipomaliza sote tulipelekwa kwenye vyumba vya kulala mahabusi na kulipokucha baada ya kufungua vinywa kwa vipande vya muhogo mchungu wa kutokosa na uji wa sembe, tulipangwa na kun-yolewa nywele mmoja mmoja kwa nyembe zilizokuwa butu kweli kweli. Kila mmoja alikuwa akichu-rurika damu kich-wani kwa kuparuzwa paruzwa. Baada ya hapo, tulipelekwa kwa Mkuu wa Magereza kwa kutia vidole vyetu katika Daftari la kuwekewa majina ya wafungwa. Kama kawaida, tuliyakuta yameandikwa yale yale ya kutia choko choko, kuhukumiwa na mkuu wa jeshi la Taifa katika mahakama ya Kijeshi.

Mradi uwongo na unafiki mtupu. Tulipofika kwa Mkuu wa Magereza, Bwana Adam Taib, ndipo tulipoambiwa kuwa tumefungwa miaka 10 kwa kila mmoja. Baada ya kuondoka hapo kwa Mkuu wa Magereza, nilimwambia Jaha Ubwa, kwa uchungu kwani ukishakuwa mfungwa huna tena unachokiogopa. Nilimwambia, Jaha, “Unaiona Serikali yako hii inavyosema uwongo hivi!? Jaji gani huyo aliyetuhukumu sisi, au mahakama gani hayo tuliyohukumiwa? Au nyinyi wenzetu, mlipelekwa?” Jaha masikini, alishindwa hata kunijibu. Alibakia akipuma tu na kunitumbulia ma-cho. Neno alilolisema ni, “Mungu atatulipa”. Yeye na wenziwe ndio hapo Mungu anawalipa kwa waliyoyatenda kuipindua nchi na kuunga mkono mauwaji ya ASP. Baada ya chakula cha mchana, tuliondolewa na kupelekwa gereza la Langoni (shamba).

MATESO YA “KWA BA MKWE”

Wananchi wengi wa Unguja na Pemba wameteswa mateso mabaya mabaya katika gereza hilo la “Kwa Ba Mkwe”. Wengi wamepoteza roho zao kwa mateso hayo na wengi wametoka humo na vilema katika viwiliwili vyao. Licha ya kuteswa kwa kupigwa kwa bakora bali baadhi ya wananchi wamefika kuchomwa moto wa sigireti katika tupu zao mpaka wakawa-chwa na madonda bila ya kupe-wa dawa ya namna yoyote. Wengine wamefukizwa pilipili hoho na huku wamefunikwa shuka.

Wakifukizwa mpaka chini ya tupu zao. Wapo waliyokuwa wameteswa kwa kumwagiwa mafuta ya petroli kisha wak-awashwa moto. Wapo walion’golewa kucha za mikono na miguu na kutiwa rojo la pilipili hoho. Wapo walioteswa kwa kutiwa mpira katika tundu zao za kwendea haja kubwa na kisha wakamiminiwa maji mfano wa mtu anapopigwa bomba kabla kufanyiwa op-ereshini au kwa dawa fulani hospitali. Hufanyiwa hivyo, mpaka matumbo yakawajaa maji yakawa yanatokea mdo-moni. Wapo walioingiliwa nyuma.

Nathubutu kusema kuwa mateso waliyokuwa wakiteswa wananchi wa Unguja na Pemba katika gereza hilo la “Kwa Ba Mkwe”, hata huko Afrika ya Kusini wakati wa Rais Botha au Haiti wakati wa utawala wa Papadok, haya-jawahi kufanyika kama hayo yaliyofanyika Zanzibar wakati wa Utawala wa Karume na Al-Haj Aboud Jumbe. Lakini ulimwengu kwa sababu wazijuazo wenyewe, ulinyamaza kimya kama kwamba hakukuwa likitokea lolote. Lakini, ulim-wengu si huu tu, utakuja ulimwengu mwengine na huko tutakutana na Hakimu mwenye kuyajuwa ya dhahiri na ya siri yaliyokuwa yametendeka. Hakimu mjuzi wa kuadhibu kama istahikivyo, bali sio Mandera, mateso ya Mandera hayawezi kulin-gana na hata chembe ya mchanga ya malipo ya Hakimu wa Kesho. Na tujiweke tayari, na hayo hayako mbali bali yako karibu kweli kweli. Ni kufunga pumzi tu!

MAISHA YA GEREZA LANGO

Hali ya maisha ya magereza katika wakati huo(1968) yalikuwa mabaya zaidi kuliko yale ya wakati ule wa mwanzo nilipokuwa nimefungwa (1964 – 1967). Shida za kila kitu zilikuwa kubwa. Chakula walichokuwa wakipewa wafungwa kiliku-wa hakitoshi kulin-gana na ugumu wa kazi walizokuwa wakifany-ishwa. Kwa jinsi ya wananchi walivyokuwa waki-fungwa kwa wingi, ilifika mpaka magereza ku-wa hayana nguo wala virago vya kuwapa wafungwa wepya, licha ya chakula. Wafungwa wapya walifika kupewa vipande vya magunia kuvaa viunoni na ku-lala juu ya upande wa gunia. Ilikuwa wanapomaliza baadhi ya wafungwa vi-fungo vyao, viroba vyao ndio hupewa wa-fungwa wengine bila ya hata kufuliwa.

Katika mwaka wa 1970 na 1971, magereza yakinuka njaa na uchafu kwani kulikuwa hakuna chakula chochote baada ya muhogo mchungu asubuhi na mchana kwa majani mapevu ya kisamvu. Wafungwa walikuwa wakikiita chakula hicho, “full suit” kwa kuwa chakula ni muhogo na kitoweo chake ni majani ya muhogo. Muhogo wenyewe ulitokea kuwa mchungu na zaidi ya mambo chumvi nayo ilikuwa imeadimika kwahivyo, mambo yalizidi kuwa magumu. Wafungwa walikuwa wakiponea makoroma ya nazi wakati wanapokuwepo katika kazi za nje, makondeni na vichakani.

Jua lilikuwa kali sana hata mito mingi na visima, vilikauka vikawa havina hata tone moja la maji. Wafungwa walikuwa wakinuka kama fungo. Mwenyezi Mungu alijaalia kisima kimo-ja kiliopo karibu na gereza la Langoni kilikuwa kikitoka maji. Lakini, watu wakitoka Kizimbani Sakafuni kuja kuteka maji hapo, na kisha wakiya-pakia kwa mapipa na madebe katika magari ya n’gombe. Mradi dhiki ilikuwa kubwa sana. Kwa jinsi ya wafungwa walivyokuwa wengi, ulifika wakati tulikuwa tukilala wafungwa 70 mpaka 80 katika banda moja ambalo lililokusudiwa kulazwa wafungwa si zaidi ya 30 mpaka 40 kwa wingi.

Wananchi walikuwa wakifungwa ovyo bila ya makosa yoyote. Ikiwa Mheshimiwa anamtaka mke wa mtu na hampati kwa sababu wewe unamuhifadhi na kutoka ovyo ovyo, basi utasitukia unakumbwa na Mandera bila ya kulijua kosa ulilolitenda. Kwanza ut-awekwa katika hilo gereza lake la “Kwa Ba Mkwe” na mwisho utapelekwa katika gereza kuu kwa kifun-go cha kuanzia miaka mine mpaka miaka 10! Hujahukumiwa wala hujaambiwa umefanya nini.

NYAKATI ZA KUFANYISHWA KAZI “WAFUNGWA WA SISASA”

Kengele ya kuamshwa wafungwa ilikuwa ikipigwa saa 11 za alfajiri. Likifunguliwa tu banda wengine tulikuwa tukikimbilia vyooni, na wengine walikuwa wakikimbilia kuchukua kifungua kinywa. Saa 12 barabara tulikuwa tukitolewa kwenye kambi na kupelekwa sehemu za kufanyishwa kazi. Kiasi ya saa moja asubuhi tukianza kufanyishwa kazi ikiwa za kulima au za kun’goa minazi au za namna yoyote mpaka saa tisa za alaasiri ndipo inapo simamishwa kazi na kure-jeshwa kambini kwa wale waliyokuwa wameweza kumaliza kazi zao. Ama kwa wale waliyokuwa hawakuweza kumaliza mpaka kufika wakati wa kusimamishwa kazi, wao walikuwa wakiachwa hapo hapo kuendelea na kazi wamalize sehemu zao.

Wafungwa wanaorejeshwa kambini wakiwa wamemaliza kazi zao kwa wakati, wao baada ya kula chakula na kupumzika kidogo, walikuwa wakichukuliwa tena kwa kufanyishwa kazi ndogo ndogo kama vile, kukata majani, kwenda kuokota kuni, kupalilia matuta na hata wakati mwengine kupalilia mpunga na kulima. Kazi ya wakati huo ilikuwa ikiitwa “fatiki”. Ikianza saa 11 mpaka saa 12 za magharibi. Baada ya hapo ndio tukiachiliwa kiasi cha nusu saa ku-koga ikiwa maji yapo.

Katika wakati wa kikoloni, wafungwa walikuwa wakifanyishwa kazi kuanzia saa moja ya asubuhi mpaka saa saba za mchana, na walikuwa hawafanyishwi kazi siku za Jumapili, wala siku za mapumziko mengine ya Serikali, wala walikuwa hawafanyishwi hiyo “FATIKI”. Lakini wakati wa Serikali ya wenyewe, wenye kujiita, “waleta usawa na waondoa dhulma kwa wananchi wan-yonge”, ndio wakati ilipofanyika dhulma ya daraja ya juu na ndio wakati waliyoku-wa wamedhulumiwa hao wanyonge. Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam walipofanya maandamano na kusema bora mkoloni Mwalimu Nyerere alihamaki na kukifunga chuo hicho kwa muda! Kweli chungu.

UFUNGWA WA KARUME NI ZAIDI YA UTUMWA

Mara nyingi Mwalimu Nyerere na viongozi wa Serikali ya Mavamizi ya Zanzibar husema juu ya ubaya wa utumwa uliyokuwepo visiwani Zanzibar. Hatusemi kuwa utumwa ulikuwa ni kitu kizuri, hashaa! Kumnunua binaadamu mwenzio na kummiliki upendavyo ni jambo baya sana na wala hapana binaadamu mwema awezaye kulikubali au kulikubalisha jambo kama hilo. Kwa kufahamu ubaya na idhlali za mtu kunyimwa uhuru wake wa maumbile Zanzibar ilikuwa miongoni mwa wa mwanzoni kuharamisha utumwa. Utumwa umeondolewa rasmi Zanzibar tokea mwaka 1897, ni kiasi cha miaka 67 mpaka hapo yalipofany-ika hayo ‘mavamizi’, ka-tika 1964.

Idadi kubwa sana ya wananchi wa Unguja na Pemba hawajui huo utumwa namna ulivyokuwa, lililokuwepo ni kusikia tu. Juu ya hivyo, iwapo tutachunguza kwa kutumia akili zetu kwa njia za insafu, na tuk-aweka upande chuki zetu binafsi, tutafahamu kuwa utumwa uliokuwepo katika visiwa vya Zanzibar, haukuwa wenye mateso kama ilivyokuwa katika nchi ya Kimarekani na nchi zenginezo ulimwenguni. Kwani lau ingalikuwa watumwa katika Zanzibar walikuwa wakiteswa kama wadaivyo akina Nyerere na wenziwe, basi, wakati ulipopigwa marufuku huo utumwa, asingetokea hata mmoja kukataa kuondoka katika nyumba ya huyo aliyekuwa bwana wake. Katika kitabu “Short History of East Africa”, Dr. Hollingsworth ameandika miezi mitatu baada ya kutoka sheria ya kuwa mwenye kutaka uhuru wake akabadilishe basi ni watu 120 tu waliokwenda jiandikisha.

Anasema Hollingsworth, “Ni jambo la kweli kuwa watumwa wengi wakiangaliwa vizuri na bwana zao”. Mpaka hivi leo wapo vilembwe vya hao waliyokuwa watumwa wanaishi pamoja na vilembwe vya hao waliyokuwa mabwana. Si kama wanaishi tu, bali wazee wao wamezaliwa katika majumba hayo na wao wenyewe wamezaliwa katika majumba hayo hayo. Na wanaishi kama ni ndugu na wajomba.

Katika huo wakati wa utumwa tunavyosikia kutokana na wazee ni kuwa watumwa walikuwa wakipewa pahala pao pakulala, wakipewa chakula kizuri, wakiozwa wake na wanawake wakiozwa waume na wengine walikuwa wakiolewa na hao mabwana zao na vizazi vingalipo hadi hivi leo. Watumwa walikuwa hawafanyishwi kazi siku za Ijumaa wala siku za Sikukuu na walikuwa hawaad-hibiwi kwa kupigwa labda ikiwa wamefanya makosa yaliyokuwa makubwa. Watumwa waliandikiwa mashamba na majumba na bwana zao.

Haya, natuwatizame hao watumwa wa Karume waliyokuwa wakiitwa, “wafungwa wa kisiasa”, ilikuwa kabla ya kupelekwa katika mateso ya ku-fanyishwa kazi, kwanza waliku-wa wakipe-lekwa kwa Mandera wakateswe kwa kila namna ya mateso. Watakao bahatika kubakia na uhai kutokana na mateso hayo ndio tena hupelekwa magerezani kwa ku-fanyishwa kazi ngumu zenye mateso makubwa makubwa. Watumwa hao wa Karume walikuwa wakifanyishwa kazi kutoka saa moja ya asubuhi mpaka saa 12 za magharibi na walikuwa hawapewi chakula zaidi ya muhogo na majani mapevu ya muhogo.

Walikuwa hawaachiliwi kupumzika laa Ijumaa walaa Jumaapili walaa siku za Sikukuu. Wakiumwa walikuwa wakiachwa hivyo hivyo na maradhi yao mpaka wapone kwa kudra za Mwenyezi Mungu na wengine wameondoka duniani kwa kutoku-pata matibabu yenye kufaa. Kwa jumla watumwa wa Karume khasa tulioku-wa wakiitwa, “wafungwa wa kisiasa”, tulikuwa haturuhusiwi kuja kutizamwa na watu wetu bali, hata ku-waandikia barua tulikuwa haturuhusiwi.

Kwa wingi na shida ya mateso tuliyokuwa tukiyapata, katika ku-fanyishwa kazi, wawili kati ya kundi letu la watu 16 tuliyoletwa na Nyerere kutoka Dar-es-Salaam walikufa gerezani. Nao ni Mzee Mohammed Mbaba na Maalim Harun Ustadh. Wote hao wawili waliumwa na waliachwa wakiatilika na maradhi bila ya kupewa matibabu, ingawa Bwana Mganga wa gereza la Langoni, alitoa amri ya kutaka wapelekwe wakaonane na Daktari mkuu katika hospitali kuu ya mjini. Lakini aliyekuwa mkuu wa magereza ya Langoni na Kinu Moshi, Muhidin Khamis Kwangwati alikataa kuwapeleka na aliwaacha hapo hapo gerezani mpaka walipokuwa karibu na kukata roho, ndipo alipo waondoa na kuwapeleka kwenye kihospitali kidogo cha gereza kiliopo katika Makao Makuu ya Magereza Kiinua Miguu, na huko hawakukaa muda illa waliiaga dunia. Tuliishi katika hali kama hizo za dhiki na shida pamoja na mateso ya kila namna kwa muda wa siku 1110 yaani miaka mitatu na siku.
 
Back
Top Bottom