Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Wanabodi,

Katika karibu kila jambo, kuna mazuri na mabaya yake, kama ilivyo kwa ukoloni, japo wakoloni walitunyonya, pia kuna mazuri, walituachia, ikiwepo elimu ya kisasa, walileta maendeleo mbambali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii vikiwemo viwanda, miundombinu, maendeleo ya kilimo, ila pia walituletea dini za Kikristo, vivyo hivyo pamoja na mazuri ya Waarabu kuvivamia visiwa vya Zanzibar na Pemba na kuvitwaa kama mali yao, miongoni mwa mazuri waliyoyaleta Waarabu hawa, ni pamoja na kilimo cha karafuu, miundombinu ya ma kasri, pia Waarabu walileta dini ya Kiislamu visiwani Zanzibar.

Lakini pamoja na mazuri yote haya, sio vibaya tukakumbushana tuu baadhi ya maovu ya Waarabu hawa kwa kuyajua baadhi ya madhila yaliyowakuta ndugu zetu Wamatumbi, chini ya mikono ya Waarabu wakati wa utawala dhalimu wa Sultani wa Zanzibae kwenye visiwa vya Unguja na Pemba.

Naomba kukiri, nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kutoka na mada hii:

Sultani gani aliye na shutuma za mauaji Zanzibar ya Mkuu MaalimMohamed Said

Yenye lengo la kuonyesha kuwa yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ndio pekee yaliyosababisha mauaji ya genocide Zanzibar, as if ukiondoa Mapinduzi ya Zanzibar, hakujawahi kutokea genocide nyingine yoyote Zanzibar, simply because aliyeuwawa kwenye Mapinduzi yale, ni Mwarabu, yaani Mwarabu tuu ndio binadamu, lakini Wamatumbi mamia kwa maelfu wote waliouwawa vifo vya kikatili sana chini ya mikono ya Waarabu, wao sii kitu!, not worth mentioned!.



Mkuu Maalim Mohamed Said, kwa heshma na taadhima, nakuomba kwanza acha chuki zako dhidi ya wamisionari, usifikirie mabaya tu ya wamishionari bali ufikirie na wema wao ukiwemo kukusomesheni kwenye shule zao ukiwemo wewe!.

Pili, hata kama lengo lako ni kuutetea Uislamu, lakini mara moja moja kuwa mkweli toka ndani ya nafsi yako, kwa sababu naamini kabisa unayajua fika madhila yaliyowapata ndugu zetu Wamatumbi wakati wa kipindi chote cha utumwa chini ya utawala dhalimu wa wavamizi Waarabu kwenye visiwa vyetu vya Zanzibar na Pemba.

Hizo picha hapa chini sii za kuchorwa, ni picha halisi za kupigwa na kamera za wazungu, zikionyesha kidogo tuu ila kiukweli kilichowapata mababu zetu, kikubwa na kibaya kuliko hata hicho kilichoweza kupigwa picha chini ya mikono ya utawala dhalimu wa Waarabu, watumwa wote wanaume walihasiwa!, lengo la kuwahasi wanaume ni ili kuzuia wasizaliane, kitendo cha mwanamke kubeba ujauzito miezi 9 kisha kuzaa mtoto na kumsubiri hadi akue, itakuwa ni hasara, kwa kupunguza kasi ya mahitaji ya watumwa wapya!

Watumwa wa soko la Zanzibar waliouzwa Arabuni na Bara Hindi, ambapo baada ya kufika kule, wanaume wote walifanyiwa ukatili wa ajabu kwa kuhasiwa ili wasizaliane, na walifanyishwa kazi za shokoa.

Wanawake walifanywa wajakazi, kazi za wajakazi zinajulikana, wenye bahati zao, walifanywa masuria, wasio na bahati waliuliwa na wengine kujifia, ndio maana hakuna kizazi cha watu weusi India na Arabuni, hao machotara, ni kwa baadhi ya Waarabu wenye utu na roho nzuri, lakini the rest ni unyama unyama tu.

Idadi kubwa kizazi chotara cha machotara wa Zanzibar, Pemba na Arabuni, kulitokana na wanaume dhalimu wa Kiarabu, kuwaingilia kwa nguvu watumwa wa kike ambao walinunuliwa mahsusi kama wajakazi, na pale mjakazi waliposhika ujauzito, wenye bahati walichange status kutoka kuwa watumwa na kugeuka masuriya wa wamiliki, ila wamiliki, walikuwa huru, kuwafanya chochote watumwa wao, ikiwepo kuwatesa, kuwapiga hadi kuwaua kwa ukatili wa hali ya juu! Mtumwa mwanamke baada ya kuingiliwa ki nguvu, yaani kubakwa, ikitokea akashika ujauzito, mwanamke yule kama ni mjakazi, ilitegemea imani ya wake wa bwana wao, wake wenye bahati, walikomboka na utumwa na kugeuka masuriya na ndio wamama wa machotara wote!, wasio na bahati, waliuwawa kwa kutobolewa tumbo, kutoa, kiumbe ambacho ndicho kilizikwa kama binadamu si ridhki, na mwili wa mtumwa ulifukiwa tuu kama mzoga!.

Je, wajua kuwa hata baada ya kupigwa marufuku kwa biashara haramu ya watumwa duniani kote, biashara hii iliendelea kufanyika Zanzibar kwa siri na kificho?!. Jee wajua kuna njia za chini kwa chini zimechimbwa Bagamoyo na Zanzibar ambapo watumwa walifichwa kwenye mapango na kupitishwa chini kwa chini hadi baharini?.

Je, ulikuwa unajua kuwa kila Sultani, wake zao na watoto zao, walipokufa, walizikwa na watumwa hai?!. Jee wajua mapokeo ya kwenye jengo la Beit Al Ajab, kwenye kila milingoti hapo, ndani walimuweka mtumwa hai mwanamume?!.

Je, wajua waliofanikisha kukomesha biashaa ya Utumwa Zanzibar ni akina nani? Kwa kusaidia tu, waliokomesha biashara hii dhalimu ya utumwa Zanzibar ni Wamisionari, ambao waliingia mkatataba na Sultani dhalimu wa Zanzibar, ndipo ikukubaliwa kuwa watumwa wote wenye kutaka kuwa huru, lazima wagombolewe kwa wale matajii wao kufidiwa kwa kulipwa fedha, ambapo hao wamisionari, waliwalipia fedha kuwagomboa watumwa, na ndipo wakaanzisha kanisa la kwanza kabisa Afrika Mashariki, lilianzia Zanzibar, na waumini wa kwanza, ni watumwa waliogombolewa!. Mahali kanisa lilipo ndipo lilipokuwepo soko la watumwa.

Jee wajua kitu walichofanyiwa Waarabu dhalimu hawa baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ilikuwa ni katika kujibu tuu au payback ya "what goes around, comes around?!", ila hapa naomba kukiri wazi, kuwa sio Waarabu wote kabisa walikuwa madhalimu kwa kuwatenda vibaya watumwa wao!, wako baadhi ya Waarabu ambao waliwatendea wema watumwa wao, na Wamisionari walipotaka kuwagomboa, watumwa hao walikataa kwa ridhaa zao, hivyo wakaendelea kubaki utumwani kwa ridhaa zao wenyewe!.

Wako Waarabu, waliwapenda watumwa wa kike, japo waliwanunua kama vijakazi kwa ajili ya kuwafanya watumwa wa mapenzi, lakini wapo waliotokea kuwapenda kwa mapenzi ya dhati vijakazi hao, wengine wakawaoa na kuwa masuria, na wakawazalia watoto!. Namfahamu mmoja wa watoto wa Sultani ambaye alizaliwa na suria, na yungalipo hai hadi leo!

Hii ni Ripoti ya aliyetumwa na utawala wa Waingereza kufuatilia kilichokuwa kinafanywa na serikali dhalimu ya Sultan, baada ya kupigwa marufuku biashara ya utumwa.

Pitia hapa: A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba ...

Na kwa vile wengi wetu ni wavivu, hatupendi kusoma kujiongezea maarifa bali tunapenda kupikiwa, kupakuliwa, kulishwa, kutafuniwa, sisi kazi yetu ibaki ni kumeza tuu, hivyo na mimi nitawatafunia sehemu chache chache za ripoti hii na kuzitafasiri kwa ajili ya wale wenzangu na mimi.

"They complained that the Arabs treated them harshly", yaani Waarabu wanawatesa.

In Zanzibar a good many people had been telling me how slaves were suffering in the hands of Arabs!. At Chaki Chaki I walked into a tumble-down I found a number of slaves male and female, heavily chained and fettered". Nilikuta makundi ya watumwa wake kwa waume wamefungwa minyororo!"


img-20160417-wa0025-jpg.339723

winterton_image_large.jpg


f1cfd5c8c022ec081b501e137cd76f48.jpg

0d422469a7bfe49699e19d8d898530d7.jpg
East-African-Slave-Trade.jpg


6ea26ffb39629355ebf88004858ec924.jpg
images
images
Slavezanzibar2.JPG
Servant_or_slave_woman_in_Mogadishu.jpg
8193f522fd2fbf34063d4baf59dfcced.jpg
Hizi picha wajemeni sio picha ya kuchorwa, ni picha za kweli na halisi zilizopigwa na kamera za wadhungu na sii lazima ziwe zimepigwa Zanzibar.

Lengo la uzi huu sio ubaguzi, au kuwakumbusha machungu ya Waarabu, bali ni kujikumbusha tuu historia na kuwaelimisha baadhi ya wenzetu, wasiowajua hawa Waarabu wa Unguja na Pemba waliwafanya nini mababu zetu!.

Ila pia naomba kutoa Maangalizo muhimu yafuatayo:

1. Tuwe makini sana na watu waliofilisika kiakili ambao watachanganya Uarabu na dini ya Kiislam simply because, Dini ya Kiislamu inatumia lugha ya Kiarabu!. Masikini muflisi hawa, hawajui kuwa hata Ukiristo umeanzia Arabuni. Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismail, aliyezaa na mjakazi wa ki Misri, na Wakristo ni uzao wa Isaka aliyezaa na mkewe Sara. Hata Yesu Kristo, licha ya kuzaliwa Israel, alikulia Misri na alizungumza lugha ya Kiarabu!. Hapa mimi nazungumzia udhalimu wa Waarabu kama jamii na sio dini ya Kiislamu.

Udhalimu ni udhalimu tuu hauna dini, wala kabila, wala jamii, kwa sababu kwenye udhalimu sio Waarabu tuu peke yao ndio madhalimu, watu wa mataifa mbalimbali wamefanya udhalimu kwa watu wa mataifa mengine, na mfano mzuri ni udhalimu wa Wajerumani kwa Mayahudi chini ya Hitler ulioitwa Halocust ambapo Hitler aliwaua Wayahudi zaidi ya milioni 6 kwa ukatili wa ajabu!, ila kwenye biashara ya Utumwa Unguja, Pemba, na Arabuni, watumwa hawa walihasiwa hivyo kufanyiwa genoside na wahusika sii wengine bali ndugu hawa hawa ndugu zetu Waarabu ambao leo tunakula nao, tunakunywa nao na kufurahi nao kwa vile tumeisha samehe na tumeishasahau, yaliyopita sii ndwele.

2. Kwenye biashara ya utumwa, waliokuwa wakikamata watumwa, sio Waarabu, Waarabu wao walikuwa ni wafanyabiashara ya watumwa kwenye soko kuu la watumwa la Zanzibar, wakitokea Bagamoyo, na wanunuzi wakuu wa watumwa toka soko la Zanzibar kwa ajili ya kuwasafirisha kuwauza Uarabuni na India, ambako kote huko baada ya kufika, watumwa wanaume walihasiwa!. Waarabu pia ndio walikuwa wamiliki wa watumwa katika mashamba ya Zanzibar na`Pemba, ambapo nako watumwa wanaume walihasiwa, wanawake walifanywa vijakazi na ndio wazazi wa machotara wa Zanzibar na Pemba, wengi ni baba Mwarabu, mama uzao wa watumwa wanawake wenye bahati, ambao hawakutumbuliwa mimba za Waarabu!

Upatikanaji wa watumwa kutoka bara pia ulihusisha baadhi ya watawala wetu wa asili wakiwemo machifu ambapo baadhi ya wahalifu waliostahili adhabu za vifo katika jamii zao, badala ya kuuliwa na kuwa hasara jumla, waliuzwa, utumwani, lakini watumwa wengi ni watu tuu wa kawaida wasio na hatia yoyote ambao waliwamiwa na kukamatwa kwa nguvu, wakiwemo wanawake na watoto!. Zoezi la ukamataji watumwa pia lilihusisha vitendo vya ukatili, ambapo wengi watumwa hawa, waliuawawa katika purukushani, na wengine wengi walifia njiani na miili yao kuachwa ikioza, miili yenye bahati ilifanywa vitoweo vya wanyama wa porini.

Kwenye misafara hiyo, ndugu zetu waliteswa sana mateso ambayo hayazungumziki walioishiwa nguvu, walipigwa hadi kifo ila hakukuwepo na kamera ya mzungu wa kutupigia picha kuja kutuleta humu!.

3. Waarabu ninaowazungumza hapa, ni wale Waarabu madhalimu na makatili wa enzi zile za utumwa ambao wengi wao, mwaka 1964, walifurushwa kutoka Unguja kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964!, ila waliofurushwa ni wale tuu waliokuwa Zanzibar tu, lakini waliokuwa Pemba hawakuguswa.

Hawa Waarabu wa leo, ni vizalia vya Waarabu wale wale, ila hawa wa sasa, ni Waarabu wema, wastaarabu kama Waarabu wa sasa, wenye roho nzuri, sio wakatili, sio wadhalimu na wanawapenda watu weusi na kuwaoa kwa mapenzi, huku wanawake wao, wakiwapenda weusi na wakiolewa nao japo mwanzo ilikuwa ni kwa kulazimishwa na Karume, hivyo nashauri, kwa siku zijazo, hata Waarabu hawa, ama machotaa wao, wakishiriki tena uchaguzi, wakashinda kwenye uchaguzi huru na wa haki, wapewe tuu nchi watawale kwa sababu Waarabu hawa sii wale, wasinyimwe kutawala eti kwa sababu tuu ni Waarabu.

Waarabu wa enzi za utumwa, walikuwa madhalimu, hivyo kuendelea kudhani hata hawa wazaliwa wao pia ni lazima watakuwa ni madhalimu!, kwa kanuni ya mwana wa nyoka ni nyoka!, hivyo wanashinda uchaguzi lakini hawapewi, sio kuwatendea haki.

Japo mwana wa nyoka nyoka lakini si lazima kila mwana wa nyoka awe ni nyoka mwenye sumu kali, nyoka wengine ni kama joka la mdimu, halina madhara, hivyo Waarabu hawa wa leo wamebadilika, kwa sababu hata shetani mwanzo alikuwa malaika, hivyo Waarabu hawa wa sasa ni Waarabu wema, ni wenzetu na ni sehemu yetu, ukifanyika uchaguzi tena, wakishinda, wapewe tu nchi.

Paskali

A number of African kings and merchants took part in the trading of enslaved people from 1440 to about 1833. For each captive, the African rulers would receive a variety of goods from Europe. These included guns, ammunition, alcohol, indigo dyed Indian textiles, and other factory-made goods.
 
A number of African kings and merchants took part in the trading of enslaved people from 1440 to about 1833. For each captive, the African rulers would receive a variety of goods from Europe. These included guns, ammunition, alcohol, indigo dyed Indian textiles, and other factory-made goods.
Hizo chain unyamwezi saaana. Warudi tuzivae
 
Wanabodi,

Katika karibu kila jambo, kuna mazuri na mabaya yake, kama ilivyo kwa ukoloni, japo wakoloni walitunyonya, pia kuna mazuri, walituachia, ikiwepo elimu ya kisasa, walileta maendeleo mbambali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii vikiwemo viwanda, miundombinu, maendeleo ya kilimo, ila pia walituletea dini za Kikristo, vivyo hivyo pamoja na mazuri ya Waarabu kuvivamia visiwa vya Zanzibar na Pemba na kuvitwaa kama mali yao, miongoni mwa mazuri waliyoyaleta Waarabu hawa, ni pamoja na kilimo cha karafuu, miundombinu ya ma kasri, pia Waarabu walileta dini ya Kiislamu visiwani Zanzibar.
Pascal hueleweki, si ni wewe tumekusikia ukimkaribisha na kumfurahia Sultani humu!!
 
Mada inaongelea udhalimu wa Waarabu dhidi ya Babu zetu.

Wachangiaji badala ya kuchangia Mada husika wanakuja na maswala ya Dini, Wazungu na jazba.

Kwani Waarabu ni miungu isiyotenda uovu ?

Mwingine aje na Mada ya Wazungu walivyo tesa babu zetu tutachangia pia juu ya hiyo mada.

Ukienda pale Bagamoyo utakuta ushahidi wa namna Waarabu walivyotesa na kufanya Biashara ya Watumwa weusi na jinsi walivyo watesa.

Watu wanahamishia Mada kwenye Dini.
Mjifunze kuzielewa Mada na kuchangia maudhui za hizo Mada.

Udini unawatoa kwenye ukweli.
Na mnabaki kuonekana kama vichekesho tu.
 
Mwana JF, Paskali, anakutakia wewe na familia yako HERI YA SIKUKUU YA MAPINDUZI MATUKUFU
YA ZANZIBAR!
Paskali
 
Mada inaongelea udhalimu wa Waarabu dhidi ya Babu zetu.

Wachangiaji badala ya kuchangia Mada husika wanakuja na maswala ya Dini, Wazungu na jazba.

Kwani Waarabu ni miungu isiyotenda uovu ?

Mwingine aje na Mada ya Wazungu walivyo tesa babu zetu tutachangia pia juu ya hiyo mada.

Ukienda pale Bagamoyo utakuta ushahidi wa namna Waarabu walivyotesa na kufanya Biashara ya Watumwa weusi na jinsi walivyo watesa.

Watu wanahamishia Mada kwenye Dini.
Mjifunze kuzielewa Mada na kuchangia maudhui za hizo Mada.

Udini unawatoa kwenye ukweli.
Na mnabaki kuonekana kama vichekesho tu.

Kwani babu yako yupi alifanyiwa uovu na mwarabu ?? Lete jina lake tupeleke kesi mahakamani
 
Back
Top Bottom