Mtu mwenyewe anavyoongea tu unamuona kabisa kwamba ameshindwa hata kabla hajaanza hiyo safari yenyewe. Tena wanatakiwa wamrudishe haraka sana nyumbani maana inaonekana hata kazi yenywe ya udiplomasia haiwezi kwa jinsi anavyobwabwaja!
mie naona apewe tu hiyo haki yake ya kugombea wazanzibari si hewallah bwana, labda akaangukie kwa mkapa maana nyerere waliomuangukia mwanzo ndio hayupo.
maana mama Fatuma alienda kulia kwa nyerere ili Amani apite.
la si hivyo kwa hizo bezo zake na kejeli ajue hapiti hata hapo Ofisi kuu kisiwandui seuze kuwa Rais wa Zanzibar.
Rais wa zanzibar kwa tiketi ya CCM ni sura mpya kabisa ambayo hakuna anayeweza kuibashiri leo
Mtu w pWANI,
Sura mpya itatoka wapi CCM? Hapo ni wale wale, mambo yale yale, ufisadi ule ule, ni Mwinyi vs Bilali.
kwani ile kanuni ya mwana ccm kutotangaza nia yake ya
kugombea uraisi kabla ya chama kutoa ruhusa haipo tena?
au sijaielewa vyema hiyo kanuni? nakumbuka sumaye
alipata dhoruba alipoeleza nia yake ya kugombea uraisi
kabla ya "wakati".
Quote"Msije mkafanya kosa kumchagua mtu mwenye sifa ya usomi, lakini kumbe kusomea kwenyewe ni kupiga kinanda au kwa mfano mtu kasomea kusonga ugali aje kuwa mgombea. Kwa nini asitafutwe mtu kama Balozi Karume aliyesomea Uchumi, Diplomasia na Utawala katika Biashara na kumpa nchi, kuliko kumtafuta dereva wa teksi," alibeza Karume.
"Msije mkafanya kosa kumchagua mtu mwenye sifa ya usomi, lakini kumbe kusomea kwenyewe ni kupiga kinanda au kwa mfano mtu kasomea kusonga ugali aje kuwa mgombea. Kwa nini asitafutwe mtu kama Balozi Karume aliyesomea Uchumi, Diplomasia na Utawala katika Biashara na kumpa nchi, kuliko kumtafuta dereva wa teksi,"
Hakuna vijana wasio walevi wanayoiweza hii kazi?