Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,326
- 11,173
Side,
Naungana na pointi zako hapo juu, kuhusu hayo matamko ya sisiemu na watu wake. Kwa mtu anayedai kwamba nchi ilipatikana kwa mapanga, na hivyo anayeitaka naye apite njia hiyo hiyo nadhani haitakii mema Zanzibar na watu wake na ni mwehu! Kama hakutaka nchi ipatikane kwa "MAKARATASI" (kura) nadhani wangeondoa kabisa suala la uchaguzi, ambao aghalabu huwa wa tiktak ama mazingaombwe. Ndio yale yale ya kura za maruhani.
Suala la wizi wa kura kwa chaguzi za visiwani huwa si la kujadiliwa ama kuumiza vichwa sana, kwani linatambulika. Na mpaka kesho sijajua wale jamaa waliokimbia na maboksi ya kura mwaka 2000 na kwenda kubadili matokeo porini wamechukuliwa hatua gani!
Tungepata ufumbuzi wa hili suala tata nadhani tungekuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuchambua suala hili. Mlio na taarifa za suala hili tunaziomba.