Uber has officially launched in Dar es Salaam, Tanzania!

Lakini tukiangalia kwa jicho la tatu Uber italeta matatizo ya kipato kwa madereva wengi wa hivyo vyombo.

Hiyo ni kwasababu madereva hao ndio watakaoendelea kugharamia ada za leseni zao za biashara, makato ya kodi kupitia TIN zao na bima za vyombo vyao.

Uber inaendeshwa kwa kutumia internet hivyo kuwa vigumu kwa vyombo vya sheria kuifuatilia hasa utunzaji wa usiri wa taarifa za wateja "privacy" na usalama wa wateja kwa ujumla.
 
Marekani [na nadhani ni kwa majimbo yote] huhitaji 'business license' kuendesha Uber.

Unachohitaji ni gari linalokidhi vigezo vyao, leseni halali [maana wana verify na DOTs], bima ya gari, taarifa zako za benki, na kusubiri wao wakufanyie background check, basi.

Huhitaji leseni mahsusi ya biashara.

Mfano ni mji wa San Fransisco ambako kuna legislation kabisa inayosema kwamba ni lazima dereva awe na business licence.
 
Mkuu fafanua vizuri ni kitu gani hicho wengine hatujui
Niliwahi kusema huku kuna watu hawasomi habari wala vitabu wala hawajishughulishi Kujua vitu ila utawakuta wana uwezo wa kuchangia mada sasa huwa najiuliza wanachangia kwa upeo gani? Hapa nimekupata mmoja mkuu! Kampuni kubwa namna hii duniani huijui? Kweli wewe ni KIBOKO
 
Mfano ni mji wa San Fransisco ambako kuna legislation kabisa inayosema kwamba ni lazima dereva awe na business licence.

Okay, basi nadhani inategemea na mji na mji na jimbo na jimbo.

Sehemu zingine Marekani huhitaji leseni ya biashara.
 
Vipi kuhusu abiria wasio waaminifu? Kwa bongo ni changamoto balaa. Mtu anaweza kuita cab impeleke sehemu, kumbe nae ni kibakana mwizi wa magari, usalama wa gari na dereva uko wapi hapo?
 
June 15, 2016

Serikali inabidi iwaelemishe Bodaboda na MaTax divers yasijekuwa yale ya wahuni wa Noirobi.
Ni usafiri mzuri sana na ni wakwenda mbele kwa mbele. Poleni san Matax drives Wapigaji wa JNIA. Tutawasahau tafutn kaziingine.
 
Hapa sheria za TAXI imekuaje?
Maana UBER inamruhusu mtu yoyote mwenye gari kufanya biashara ya TAXI bila kibali chochote zaidi ya driving license yake, kwa Tanzania tunajua kuwa TAXI bubu haziruhusiwi so UBER wamelizunguka vipi hilo?

sawli la akili sana hilo mkuu, maana tusijefikishana tena kuleeeeee,,,,, kwa waheshimiwa!!
 
Ni mtazamo tu nimetoa kuhusu malipo.

Mji gani katika nchi ya Marekani dereva hahitaji kusajili chochote?

Business licence ni lazima na madereva wanakuwa wanajukikana kama independent contractors.

Kama LA (How to drive with Uber in Los Angeles | Uber) hakuna business lincese yoyote, Independent Contractor maana yake ni kuwa umejiajiri mwenyewe hii Uber wanaitumia kukwepa wajibu wao kama mwajiri, so ukiwa unafanya Uber hauna haki za kawaida za mfanyakazi.

San Francisco nao ndo wanataka waanze kuweka license SF to require Lyft, Uber drivers to obtain business licenses

Austin, Texas walipitisha sheria kuwa lazima upate leseni na ufanyiwe fingerprinting Uber wakafungu biashara yao kabisa kwenye mji huo.

Ili kampuni ya Uber iweze kupata faida na ifikie valuation yao ya $68 BILLION ni lazima wasiwe na wafanyakazi yaani madereva wawe indipendent contractors ili wasiwe na gharama za wafanyakazi, ndo maana always wanapinga uandikishaji wa aina yoyote.
 
Ni hivi...kwa mfano mimi ninakuwa na ki Alteza changu.

Halafu nina download Uber partner App kwenye smart phone yangu. Nikishapewa rukhsa na Uber ya kuanza kuendesha, watu ambao nao wamepakua Uber rider App wakiomba niwafuate na kuwapeleka sehemu watakazo kwenda, naenda kuwachukua na kuwapeleka. Hizo Apps ndo zinatuunganisha.

Kwa hiyo, ni huduma ya teksi lakini ambayo inatumia zaidi teknolojia kuunganisha madereva na abiria.

Na madereza wanakuwa wanatumia gari zao ambazo hazina alama yoyote ile kama ambavyo zilivyo teksi.

Na malipo yote ni electronic...yaani hakuna cha kubadilishana pesa taslimu kama ilivyo kwenye teksi.

Rider anapojisaliji anaweka credit au debit card information zake kwenye system na akiomba ride....ride ikija na kukamilika...basi gharama atakuwa charged automatically kupitia card yake.
Kazi ipo ! Maana hapa changamoto ya elimu ina nafasi yake , sasa kiukweli madereva wengi wa Taxi wa nchi hii ni wale waliofeli shule ama wale wasiosoma kabisaaaa .
 
Vipi kuhusu abiria wasio waaminifu? Kwa bongo ni changamoto balaa. Mtu anaweza kuita cab impeleke sehemu, kumbe nae ni kibakana mwizi wa magari, usalama wa gari na dereva uko wapi hapo?

Yup..na hao wapo mbona.

Marekani kuna matukio kadhaa ambapo abiria wamewahi kupora magari ya madereva wa Uber.
 
Duh, kweli mkuu Consigliere wazo lako ni fikirishi kwa hakika.
Nilivyofuatilia operations za hawa jamaa ni wazi wanahitaji walau 80% ya miji iliyopimwa na maeneo yametambuliwa kimitaa bila kusahau miundombinu mizuri. Niliwaza mwanzo kuwa pamoja na ugumu watakaokutana nao, huenda wakaishia kuhudumia chini ya 10% ya mji!
Hakika umeielewa doubt yangu, maana kwa hali ya miundo mbinu na makaazi ilivyo sijui kama maeneo tuishiyo yatakua yanafikika. Ukiangalia huku uswahilini ndanindani kila kituo au mtaa unaitwa either msikitini, kwa mangi, kanisani n.k. Kwa kifupi mitaa haijawa mapped kabisa kiasi cha kutoelekezeka
 
Kazi ipo ! Maana hapa changamoto ya elimu ina nafasi yake , sasa kiukweli madereva wengi wa Taxi wa nchi hii ni wale waliofeli shule ama wale wasiosoma kabisaaaa .

Serikazi lazima ilinde fursa za kazi kwa vilaz*.

Madereva wazawe waende wakasome IT ama sinyo hawatawezasoma GPS or digita maps.
 
Back
Top Bottom