Uber has officially launched in Dar es Salaam, Tanzania!

Mk
Hapa sheria za TAXI imekuaje?
Maana UBER inamruhusu mtu yoyote mwenye gari kufanya biashara ya TAXI bila kibali chochote zaidi ya driving license yake, kwa Tanzania tunajua kuwa TAXI bubu haziruhusiwi so UBER wamelizunguka vipi hilo?

Mkuu ni Taxis tu zilizosajiliwa ndizo zinakuwa zinafanya hii biashara, isipokuwa UBER wanakuwa wanadhibiti mapato kwani mapato yanatozwa kwenye kadi ya mteja anapofanya bookings kupitia debit au credit kadi yake.

Kuna nchini zingine madereva wameruhusiwa kupewa tips na wateja na pia nchi zingine wanatumia mitandao ya simu kufanya malipo kama ule wa MPESA.
 
Ila kusema ukweli kwa Tanzania naona kutakuwa na changamoto sana na madereva watakuwa wanakula hasara tu mwisho wa siku.

Hicho ndicho ambacho mie ninakiona.. Mazingira na miundo mbinu sio rafiki kwa huduma hii.. Pia monitoring na vetting kwa ajili ya kuwapata wenye magari waaminifu ni ngumu kwa sasa hapa kwetu..
 
Wakati kuna baadhi ya watanzania wanabuni njia za kupata mapato mapana wengine wanaendelea kupiga kelele tu.

Nilishuhudia pale London na Hyderabad nchini India madereva wakichuana kati ya wale "established" na wale wapya.

Wale established wenye black cabs walidhani wamehodhi hiyo biashara pale central London lakini kumbe kunaweza kuja mtu akaweka uwiano wa customer base na kukawa na usawa.

Ni kwamba kinachoondolewa ni uwezo wa madereva kupata cash mkononi lakini mwisho wa siku anakuja kulipwa kipato chake mwisho wa mwezi.
 
June 15, 2016

Uber-app.png


Uber has officially launched its services in Dar es Salaam, Tanzania. This is the 9th African country and 475th city on Uber’s global network.

As usual, users in Dar es Salaam will enjoy six free rides for three days. The code is “MoveTanzania”.

Uber has been spreading across Africa this year so far. They launched in Ghana last week, and Uganda two weeks ago. Again, I’m wishing Uber the best in this new African country.

=======

Nini hatma ya Bodaboda, Bajaj na Taxi jijini Dar?

=======

Kwa wanaouliza kuhusu Uber:

Uber Technologies Inc. is an American multinational online transportation network company headquartered in San Francisco, California. It develops, markets and operates the Uber mobile app, which allows consumers with smartphones to submit a trip request which is then routed to Uber drivers who use their own cars.
SAAAFI
 
Hicho ndicho ambacho mie ninakiona.. Mazingira na miundo mbinu sio rafiki kwa huduma hii.. Pia monitoring na vetting kwa ajili ya kuwapata wenye magari waaminifu ni ngumu kwa sasa hapa kwetu..

Kwa mfano, watawezaje kufanya background checks za madereva ili kuweza kuhakikisha usalama wa abiria?
 
Kwa mfano, watawezaje kufanya background checks za madereva ili kuweza kuhakikisha usalawa wa abiria?

Dereva anafanya taratibu zote za kuwa dereva yaani leseni ya udereva, leseni ya biashara ya eneo analofanyia biashara kama ni Kinondoni au Ilala.

Dereva anakuwa independent na Taxis yake iwe inaonyesha kuwa ni taxi.

Uber watafanya verifications kwa dereva na pia katika hiyo apps kuna uwezo wa mteja kufuatilia mwenendo wa dereva mpaka pale anapomchukua.

Hivyo kwa upande wa usalama ni kwamba details zote za devera zinakuwa zimehifadhiwa mahala na pia mienendo yake.

Itabidi maderva wawe wameiva kwelikweli, kwani kuna changamoto ya madereva wasio na leseni, bima na elimu ya kutosha ya usafiri wa abiria.
 
Dereva anafanya taratibu zote za kuwa dereva yaani leseni ya udereva, leseni ya biashara ya eneo analofanyia biashara kama ni Kinondoni au Ilala.

Dereva anakuwa independent na Taxis yake iwe inaonyesha kuwa ni taxi.

Uber watafanya verifications kwa dereva na pia katika hiyo apps kuna uwezo wa mteja kufuatilia mwenendo wa dereva mpaka pale anapomchukua.

Hivyo kwa upande wa usalama ni kwamba details zote za devera zinakuwa zimehifadhiwa mahala na pia mienendo yake.

Itabidi maderva wawe wameiva kwelikweli.

Unajua maana ya background check?

Je kama dereva ni convicted felon? Je kama dereva ana historia ya ubakaji?

Uber watayajuaje hayo?

Nikupe mfano kwa Marekani, kabla mtu hujawa authorized kuwa Uber partner...kuna background check inayofanyika. Wanatumia jina lako, social security number yako, dob, na kadhalika.

Wanacheki kuona kama ushawahi kuwa na felonies zozote zile ambazo zinatoa mwanga wa tabia zako ambazo huenda zikaja kuhatarisha usalama wa abiria.

Kwa Tanzania watawezaje kuyafanya hayo?
 
Uber ni kampuni ya Kimarekani kama ilivyo Google, Yahoo, Coca-Cola, na zinginezo nyingi tu.

USA baby...


What about Uber's cousin LYFT, is it American too?
The name sounds like it's originated from Europe.
 
Mkuu fafanua vizuri ni kitu gani hicho wengine hatujui[/QUOTE
Kama una gari na una smart phone hivyo unakuwa tax driver na mnakutana na mteja kwa njia ya smart phone. Badala ya ku chat tu sasa unaweza kufanya biashara. You download an application and the potential customers also down load the app. Then through this uber app. You will be able to pick your customer and your customer will contact you fo
Utaratibu huu utasaidia sana uporaji uliokuwa unafanyika dhidi ya watalii waliokuwa wanaitembelea nchi yetu kwa nia njema wakati huo huo kuliingizia taifa letu fedha nyingi za kigeni. Lakini madereva wenye nia ya kujipatia kipato kwa njia isiyo halali wamekuwa wanashirikiana na watu wasio waaminifu kwa kuwapora mali za watalii hawa na wakati Fulani kuwatishia mpaka watoe namba za siri za kadi zao za benki hatimaye kufanikisha kutoa fedha zote kutoka kwenye account zao.

Uber itaongeza ujambazi sana hasa katika miji Kama Dar Es Salaam
 
Na gharama za car service,fuel n.k nani atakuwa anazigharamia?

Wewe mwenyewe. Ndo maana naona changamoto kwa Tanzania zitakuwa ni nyingi mno kiasi cha kufanya watu wasifanye hiyo biashara.

Uber ni business model ambayo inaweza kufanya kazi vizuri kwenye mazingira ya kueleweka.

Unless labda kila wanapoenda wanakuwa na tailored approach kulingana na sehemu yenyewe.
 
Back
Top Bottom