Tuwe wazi, kupata mtoto mwenye ulemavu au magonjwa ya kuwa tegemezi maisha yake yote ni zawadi kutoka kwa Mungu?

Awali ya yote kulipokea swala la kupata mtoto mwenye changamoto mfano waulizozitaja ni ngumu tena sana na hata ukiweza kulipokea kuna wakati utapitia cha maumivu.
Kwa uzoefu tu, nilipopata kijana wangu wa kwanza alipata utindio wa ubongo, haoni, na nitegemezi kwa kila kitu. Kwa nyakati hizo tuliumia kama familia lakini ilifika wakati ikabidi kukubaliana na hiyo shida. Kama familia tulikubaliana kuwa na ratiba nzuri za kazi zetu ilikuweza kumsaidia kwa mazoezi.
Yote kwa Yote najivunia kuwa naye kwa sasa ametimiza miaka saba.
Lakini nilicho jifunza ni kuwa kwa kiasi kikubwa inapotokea shida kama hii katika familia sisi wanaume huwa tuna wakimbia kina au kuwapelekea lawa.
 
Back
Top Bottom