SoC04 Tuwajenge vijana wa elimu ya juu kujitegemea zaidi kwa kuanzisha kozi za ufundi stadi na ujasiliamali vyuoni

Tanzania Tuitakayo competition threads

Angyelile99

Member
Oct 9, 2023
26
24
Tanzania ni moja ya nchi za kiafrika zenye a idadi kubwa ya wasomi ambao wamekua wakiishi kwa kutegemea kuajiriwa. Hii imekua ni desturi sasa tangu kupata uhuru miaka ya 1961, ni kwasababu ya uwepo wa mfumo wa elimu ya kikoloni unao ruhusu utegemezi zaidi.

Pamoja na uwepo wa jitihada kubwa za serikali katika kuajiri watumishi wapya ambao ni wahitimu wa elimu ya juu kutoka vyuo mbali mbali hapa nchini rakini bado suala la ajira imebaki kua janga la taifa.

Mpaka sasa selikali imekua ikiangaria ni kwajinsi gani nchi yetu inaweza kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana haswa wanao hitimu elimu ya juu. Tatizo hili limekua sugu sasa. Kwani idadi ya wahitimu wa ngazi ya vyuo vya kati na vya juu inaongezeka kila mwaka, wakati huo huo kumekua na ufinyu wa hali ya juu wa ajira katika sekta mbalimbali serikalini.

Sasa binafsi nadhani ili kuondokana na janga hili la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi. Ni pamoja na kuanzisha mfuno elekezi kwa vyuo vyetu hapa nchini utakao wawezasha vijana kupata alimu mama ambayo imekua ikitolewa mala zote sambamba na elimu ya ufundi stadi pamoja na ujasiliamalii.

Kupitia mpango huu wa uanzishwaji wa kozi hizi za ufundi stadi na ujasiliamali kwa vyuo vyetu hapa nchini itakua na faida mbali mbali zitakazo punguza janga la tatizo la ajira kwa vijana na kuwatengeneza kujitegemea zaidi.

Faida hizo ni kama ifuatavyo;

1. Kuondoa dhana ya kusoma ili niajiliwe. Kupitia mpango huu wa uwepo wa kozi za ufundi satadi na ujasiliamali. Utasaidia kujenga kundi la vijana wanao weza kuishi kwa kuto kutegemea ajira pekeake bari ni kuwa na uwezo wa kuishi kwa kujitegemea zaidi.

2. Kuongeza uwezo na ujuzi wa wanafunzi: Kozi hizi zitawezesha wanafunzi kupata maarifa na stadi muhimu katika fani za ufundi na ujasiliamali, kuimarisha uwezo wao wa kiufundi na ujasiliamali. Hii itawaweka kua tayari kwa soko la ajira, ikiwasaidia kupata ajira au kuanzisha biashara zao wenyewe

3. Kuongeza ajira na fursa za kazi: Wanafunzi wanaohitimu kozi hizi watakuwa na ujuzi na sifa zinazohitajika katika soko la ajira, hivyo kuongeza fursa zao za kupata ajira. Kwasababu kozi hizi huundwa kwa ushirikiano na sekta binafsi na wadau wa soko la ajira. Hii huwezesha kuunda mitendaji na mafunzo yanayolenga mahitaji halisi ya soko.

4. Kusaidia katika maendeleo ya kiuchumi: Kozi hizi zitasaidia katika kuandaa vijana wenye ujuzi na ubunifu wa kutosha kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi, pia kwa kuongeza vipato na ustawi wa wanafunzi na jamii kwa jumla.

5. Kuimarisha mahusiano baina ya vyuo vikuu na sekta binafsi: Uanzishaji wa kozi hizi utawezesha kuimarisha ushirikiano na mahusiano baina ya vyuo vikuu na sekta binafsi, jambo ambalo litasaidia kuwezesha mikakati kadhaa ya maendeleo.

6. Kusaidia katika kutatua changamoto za kiutaalamu: Kozi hizi zitasaidia kuandaa wataalamu wenye ujuzi wa kutosha katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili nchi. Kwa mfano wanafunzi wanao soma masuala ya uwalimu, mala tu watakapo anza kozi hizi za ziada. Itasaidia wao kuja kutumika katika kufundisha elimu hii ya ujasiliamali na ufundi stadi kwa shule za msingi ma sekondari.

7. Kuongeza fursa za utafiti na ubunifu: Kozi hizi zitawezesha wanafunzi kuzamia katika tafiti na ubunifu wa teknolojia na mbinu mpya zinazohitajika katika sekta mbalimbali.zinazo weza kuendana na kazi ya teknologia ya sasa.

8. Kuimarisha uwezo wa ushindani katika soko la kimataifa: Wanafunzi wanaohitimu kozi hizi watakuwa na sifa zinazohitajika kujiunga na masoko ya kimataifa. Hivo itasaidia kua na idadi kubwa ya watu wanao weza kupata fursa mbali mbali nje ya nchi.

9. Kusaidia katika kuimarisha sera na mipango ya maendeleo: Taarifa na maoni yanayotolewa na wataalamu walioandaliwa na kozi hizi zitasaidia katika kuandaa na kutekeleza sera na mipango bora ya maendeleo. Ikiwemo suala la vijana ma maendeleo kupitia mpango wa kujiajiri.

10. Kuongeza hadhi na sifa ya vyuo vikuu: Uanzishaji wa kozi hizi utaongeza hadhi na sifa ya vyuo vikuu katika kutoa elimu ya staha na kuandaa vijana wenye ujuzi na uwezo wa kuchangia katika maendeleo ya nchi.
Kwa ujumla, uanzishwaji wa kozi hizi katika vyuo vikuu nchini Tanzania unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kupunguza tatizo la ajira kwa wanafunzi wanao maliza masomo yao. Hii itasaidia kuimarisha ustawi wa kibinafsi na wa taifa kwa jumla. Pia itasaidia kuondokana na uwepo wa wingi kubwa la wahitimu wa elimu ya juu wanao subiri kuajiliwa to.
 
Sasa binafsi nadhani ili kuondokana na janga hili la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi. Ni pamoja na kuanzisha mfuno elekezi kwa vyuo vyetu hapa nchini utakao wawezasha vijana kupata alimu mama ambayo imekua ikitolewa mala zote sambamba na elimu ya ufundi stad qmoja na ujasiliamalii.

Kupitia mpango huu wa uanzishwaji wa kozi hizi za ufundi stadi na ujasiliamali kwa vyuo vyetu hapa nchini itakua na faida mbali mbali zitakazo punguza janga la tatizo la ajira kwa vijana na kuwatengeneza kujitegemea zaidi.
Pamoja na kuwa huo ufundi stadi umekaa poa kimaendeleo ya kitaifa, na kuwaingiza wasomi huko kutatupatia mafundi wenye akili kwelikweli lakini lipo tatizo kwenye cha kuwavutia huko.

Watu wenye akili wanavutiwa na maeneo ya kazi yanayolipa vizuri, tena maeneo yasiyohitaji hadi umdanganye unayemhudumia ndiyo ulipwe vizuri (mwenue akili, hasa anayeelekeana na ujiniazi haendani na utapelitapeli).

Ukiangalia hata sasa kuna kauli za 'ooooh, wasomi bongo mmegundua nini? Mmeshindwa kutengeneza hata toothpick, sijui redio'. Hizo ni shughuli za kiufundi stadi na ninaamini wasomi wapo wengi tu wanaoziweza. Swali ni je? Wakiingia huko itawalipa zaidi ya wanavyolipwa wakiwa kwenye siasa? Ajira? Ufundi stadi unalipa kiujumla? Soko lake lipoje?

Tukitaka wasomi waingie wengi kwenye ukinyozi itabidi maslahi yawe kama kinyozi wa ulaya, (naskiaga ulaya kunyoa ni gharama sana)
Tukitaka wasomi waingie kwa wingi ufundi magari, itabidi ukipeleka gari yako gereji ya mtaaani ya fundi msomi ulipie kama tunavyolipia tukipeleka gereji za brand kama SCANIA, FORD, TOYOTA, LAND R....... nk

Maslahi yakivutia mahala popote, akili kubwa zitakuwa za kwanza kuvutika huko kiotomati. Ndiyo maana sasa hivi ni rahisi kukuta msomi anatafuta mtaji achuuze biashara kutoka nje sababu ya maslahi angalau. Maslahi.
 
Nchi za afrika kwa sasa zimekua ma wasomi ambao ni machinga wamekubari kuzunguka mtaani kutafta mia mia ilibkupata mlo wa siku. Elimu hii ya ufundi stadi na ujasiliamali sio kwamba itakua kama baseline ya maisha yake. Bali ni kumsaidia kwamba wakati nasubir kazi ya taaluma yake nafasi itakapo patikana basi awe tayari anakitu cha kuanzia. Kwa mfano mimi nimemaliza degree ya education wakati nasubiri kuajiliwa siku moja basi tayari lile boom nililo kua napata nanunua vifaa vya kutototleshea mayai kulingana na kozi ya ziada niliopata nikiwa chuo ya ufugaji. Kisha narudi nyumbni ma kuanza kufuga kuku wa nyama. Itanisaidia mim familia yangu na kulipa kodi kwa ajiri ya uchumi wa taifa pia. Kuliko kukaa to kusubir kazi
 
Mpaka sasa tumekwisha kujifunza haiitaji tena kua na chakuwavutia. Kitendo to chakuona kundi kubwa la wasomi wanamaliza na hamna ajira kitafanya vijana wa vyuo kujikitaa pia katika elimu hii ya ufundi na ujasiliamali wakiwa vyuoni ili kuepuka kua wazurulaji wakisha hitimu na uzuri mtaji upo ambao ni boom wanalo pata. Sasa hivi mama anawalipa 600000. Me nakumbuka nilisave 1700000 baada ya kumaliza chuo na ilikua ni 500000 kwa miezi miwilibyani siku 60 lakini kwasababu sina elimu ya ujasiliamalii nikashindwa nini nifanyie hii pesa.
 
Back
Top Bottom