Tuseme: Makonda, Haya hapa Majina ya Wauzaji Madawa ya Kulevya wakubwa

WANACHEZA NA AKILI ZETU TU HAO KAMA SHERIA KAMA ILE YA DUTERTE HAIJALETWA HAMNA KITACHOENDELEA.
HAWA JAMAA NI WA KUCHOMA MOTO HADHARANI ILI IWE ONYO KWA WENGINE MAANA FAIDA YAKE NI KUBWA AJABU
 
Tatizo ni kwamba sisi wa uraiani stori hua nyingi lakini ushahidi ni tatizo, kuna jamaa miaka miwili nyuma hapa Dar alikua ananunua sana nyumba za watu wakadai ni dealer, na ana ubarikio wa mtoto wa raisi.
Yule jamaa akaja kutajwa na Mange Kimambi kua ni dealer lakini sisi wa uraiani na Miss Kimambi what we have in common (I think) ni kwamba hatuna ushahidi kama jamaa ni dealer kweli ni stori za mtaani ndiyo tunazitumia.

Polisi au mamlaka zinazohusika zinatakiwa zi-deal na hizo tuhuma,
simple example ni kama unapoibiwa mathalani simu ofisi au nyumbani na kuna mtu ambaye kwa namna mazingira au jinsi tukio lilivyotokea unaweza kumuhisi na baadae polisi wakatumia hisia zako kufanya upelelezi,
Je polisi wamefanya upelelezi wakabaini hausiki au ndo wanapigiwa simu wakajazwe vumbi la pesa na upelelezi kuisha kama muziki kwa style ya fade out!
 
Makonda kwa hapa kachemka akate mizizi kabisa asifiche fiche vitu mbona mizizi inajulikana kabisa hapo anadil na retails wakati ukimbana wholesale unamaliza kila kitu
 
Kwangu Mimi aliye kamatwa na ngozi ndiye mla nyama! Kila mtu anasema hawa ni dagaa basi wewe tutajie huyo papa ni nani?
Kama wala nyama walishapewa warning, kweli utaacha kuiteketeza au kuificha. Niambie tofauti ya askari anayemtonya muuzaji na alichokifanya mh. Na yeye amehakikisha hao watu wanajipanga. Wengi hili hamlioni.
 
Hebu jaribu kua mwanaume mwenye msimamo kama ni mwanaume kwel,Mara tunawajua Mara akitajia asitangaze,mara wapo kino Mara mbezi sasa tushike lipi tuache lipi? Unadhan kuna MTU anaweza pambana na serikali ikiamua? Hajazaliwa MTU hyo bado na hatatokea, mi nadhan ungesema makonda majina ya hawa jamaa mapapa ni fulan fulan na fulan,lakin unajitokeza kifua mbele kua wanajulikana mbona sasa wote hamuwataji? Sawa watto wa vigogo akina nan? Taja mmoja tujue kwel unawajua na utupe na ushahidi.. Mteja km chid Benz atasema tu anaponunua,then atafuatwa baadae chein yte inafuatwa inayojihusisha... Labda nikuulize kwa nn watu wanadhan makonda anakose?au unadhan kwamba hawa watu hawasthil kufuatwa au labda wataogopwa mpka mwisho?

Na kuhakikishia tusihukum kabla Ila tujipe muda kuna MTU atageuka shujaa
 
Miaka ya 80 mwishoni na 90 mkoa wa Mbeya kulikuwa na Jambazi mmoja maarufu sana alikuwa anafahamika kwa jina la Jombi. Alikuwa maarufu na tajiri. Yeye alikuwa na mtandao mkubwa sana na inasemekana Polisi wengi wakubwa walikuwa kwnye payroll yake kwa njia moja au nyingine pamoja na wanasiasa. Huyu bwana alikuwa akiiba magari TZ anaenda kuuza SA au Zambia na akiiba huko analeta TZ.

Pia alikuwa akifanya Ujambazi mwingine wa humu humu ndani kwa umakini mkubwa sana. Ilikuwa ikitokea anatakiwa akamatwe kuhojiwa anapigiwa simu aende kituoni au anaambiwa kesho kuna vijana wanakuja. So anajiandaa anavyojua. Siku mbili tatu mnamwona mtaani anadunda kama kawaida. Ni Mkapa alikuja kumkamata huyu mweshimiwa Jambazi.

Nimerudia habari hiyo kwa kufananisha na kile kinachoendelea hapa nchini. Kusema wauza madawa wa kulevya wakubwa hawafahamiki ni uongo mkubwa na utatupeleka motoni. Wanafahamika sana wengine ni watoto wa viongozi na viongoz wenyewe, wengine ni wabunge na makada wa vyama vyetu, wengine ni wafadhili wakubwa wa vyama na timu zetu, wafadhili wa wanamuziki, wasanii na wenye kufadhili hata maisha ya watu flan flan hapa mjini.

Wanafahamika sana. Nenda Kinondoni kuna himaya za watu hawa. Nenda Mbezi, nenda kaangalie watoto wanaosoma chuo cha diplomasia wanavyoharibika kwa madawa haya.

Kama Makonda ameamua kupambana na madawa ya kulevya atoe namba yake ya simu apewe majina. Lakini hilo si issue sana anaweza enda omba kwa ndugu Kikwete, yeye anayo list ambayo alisema hadi viongozi wa dini wapo na watu wengine wengine aliosema ni wazito. Yaani walikuwa wanaogopwa kuliko serikali. Hayo majina sidhan kama Kikwete atamnyima.

Lakini ikiwa Kikwete hatotaka kumpa basi sisi vijana tunaweza msaidia akipewa hayo majina hatusemi aje atangaze. Hapana tunaomba afanye uchunguzi ili tusije nasi wengine tukawa tumewasingizia. Awakabidhi polisi kitengo husika, polisi waadilifu wachunguze na kuwakamata wahusika.

Wanafahamika wala si siri. Wengine bado ni wabunge na wengine wanajihusisha na music, usanii au ufadhili wa vyama vyetu.

Makonda tupatie namba yako ndugu, tukusaidie kukutajia wahusika wakuu ukiacha hawa uliowataka waje kukuona ofisini. Sisemi waachwe ila nashangaa kwa nini ulipendelea waje kukona wewe ofisini? Ili iweje? Si ungesema wakamatwe? Wapelekwe polisi? Na halafu mahakamani?

Watanzania tusimung'unye maneno. Tusipepese macho, tusing'ate kucha na kutizama chini.

Tuseme Makonda haya hapa majina ya wauza madawa ya kulevya ili Mungu alinusuru Taifa hili na madhambi yanayolizunguka.
Aloo, nahisi hausaki tonge kama "slow slow"
 
Ninavyojua mtu kama Chid Benz hana athari yoyote hata akifikishwa mahakamani kwani ni lofa tu,biashara ya mihadarati ni ya watu matajiri tena si tajiri uchwara hao wanaoimbwa na Ngwasuma sijui kupaishwa na Twanga hao ni wataka sifa tu .Matajiri wa kuuza unga wanaweza hata kujenga mahospitali,mashule na wakachangia hata vyama vya kisiasa na hata kupiga picha na wakubwa ,sasa cha kujiuliza wewe unadhani mtu tajiri achangie mamilioni ili iweje,mimi najua wachangiaji mamilioni yasio na miwaa ni wale wenye mfuko au taasisi kama kama akina Billy Gate,Soros,Mengi,hawa wengine wengi wao ni matapeli wa kimataifa na hata sote tunayajua,wanakwepa kodi ,wanabadili majina ya kampuni zao.Huwezi kumuona Bakhresa na utajiri wote alionao akimwaga fedha eti za kufadhili miradi na akajitangaza kutwa nzima.
 
hiyo kazi ilishawashinda polisi, miaka yote ni kulialia tu, unga unaingilia njia wanazolinda wenyewe, kazi yao ni ipi sasa? kwa hiyo nina mashaka nao,
Hii kazi wakabidhiwe jeshi uone, mwezi tu, hakutakuwa hata kile wanachokiita ukucha mmoja!!
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana hapo kwa Jombi.
Mwaka 98 tukiwa wadogo sana nakumbuka aliiba gari ya broh Zambia, kwa kua alikua anafahamika ni yeye broh alimfuata hadi Mbeya lakini kilichompata broh imebaki simanzi na history isiyofutika maishani mwetu.
 
Aiseee, kweli nimeamini kupambana na wauza madawa ya kulevya ni kazi ngumu kweli, inahitaji nguvu ya ziada vinginevyo hata makonda anaweza shindwa inaonekana biashara hii imeshaota mizizi.
 
Miaka ya 80 mwishoni na 90 mkoa wa Mbeya kulikuwa na Jambazi mmoja maarufu sana alikuwa anafahamika kwa jina la Jombi. Alikuwa maarufu na tajiri. Yeye alikuwa na mtandao mkubwa sana na inasemekana Polisi wengi wakubwa walikuwa kwnye payroll yake kwa njia moja au nyingine pamoja na wanasiasa. Huyu bwana alikuwa akiiba magari TZ anaenda kuuza SA au Zambia na akiiba huko analeta TZ.

Pia alikuwa akifanya Ujambazi mwingine wa humu humu ndani kwa umakini mkubwa sana. Ilikuwa ikitokea anatakiwa akamatwe kuhojiwa anapigiwa simu aende kituoni au anaambiwa kesho kuna vijana wanakuja. So anajiandaa anavyojua. Siku mbili tatu mnamwona mtaani anadunda kama kawaida. Ni Mkapa alikuja kumkamata huyu mweshimiwa Jambazi.

Nimerudia habari hiyo kwa kufananisha na kile kinachoendelea hapa nchini. Kusema wauza madawa wa kulevya wakubwa hawafahamiki ni uongo mkubwa na utatupeleka motoni. Wanafahamika sana wengine ni watoto wa viongozi na viongoz wenyewe, wengine ni wabunge na makada wa vyama vyetu, wengine ni wafadhili wakubwa wa vyama na timu zetu, wafadhili wa wanamuziki, wasanii na wenye kufadhili hata maisha ya watu flan flan hapa mjini.

Wanafahamika sana. Nenda Kinondoni kuna himaya za watu hawa. Nenda Mbezi, nenda kaangalie watoto wanaosoma chuo cha diplomasia wanavyoharibika kwa madawa haya.

Kama Makonda ameamua kupambana na madawa ya kulevya atoe namba yake ya simu apewe majina. Lakini hilo si issue sana anaweza enda omba kwa ndugu Kikwete, yeye anayo list ambayo alisema hadi viongozi wa dini wapo na watu wengine wengine aliosema ni wazito. Yaani walikuwa wanaogopwa kuliko serikali. Hayo majina sidhan kama Kikwete atamnyima.

Lakini ikiwa Kikwete hatotaka kumpa basi sisi vijana tunaweza msaidia akipewa hayo majina hatusemi aje atangaze. Hapana tunaomba afanye uchunguzi ili tusije nasi wengine tukawa tumewasingizia. Awakabidhi polisi kitengo husika, polisi waadilifu wachunguze na kuwakamata wahusika.

Wanafahamika wala si siri. Wengine bado ni wabunge na wengine wanajihusisha na music, usanii au ufadhili wa vyama vyetu.

Makonda tupatie namba yako ndugu, tukusaidie kukutajia wahusika wakuu ukiacha hawa uliowataka waje kukuona ofisini. Sisemi waachwe ila nashangaa kwa nini ulipendelea waje kukona wewe ofisini? Ili iweje? Si ungesema wakamatwe? Wapelekwe polisi? Na halafu mahakamani?

Watanzania tusimung'unye maneno. Tusipepese macho, tusing'ate kucha na kutizama chini.

Tuseme Makonda haya hapa majina ya wauza madawa ya kulevya ili Mungu alinusuru Taifa hili na madhambi yanayolizunguka.
Kwa hiyo makonda leo ana uwezo Gani wa kukabidhiwa majina ya wauza unga na wakati waziri wa wizara husika yupo, DPP yupo na yule wa ikulu yupo.
 
Back
Top Bottom