Steve nyerere huyu si Kuna muigizaji fulani ameigiza naye movie fulani Hao wanawake wanauza madawa na yeye alipewa akalewa maunga Kwa hiyo labda Hawa wasanii wanaonyesha movie za maisha yao wanafanya vijana wapende maisha ya uteja. Asee nimewashtukia bongo movie baadhi labda itakuwa ma drug dealer mapunda kila siku nje ya NchiTuanze kwa kutaja wauzaji.
1. Idd Azzan
2. Steve Nyerere
........ Endelea.
Anaishia kutaja nicknames tu TID,Chiz,Makomeo,Wile ... halafu watu wanampongezaasipambane na matawi akate mizizi
Ni sawa na kuwakamata wanywa gongo, huku ukiwaacha atengeneza gongo wakiendelea na kuongezeka.U hav a Point...
Hii vita si ya kinyonge kama watu wanavyofikiri.
Mwisho wa siku wakaishia ku deal na hawa hawa wadogo alaf wale majambaka wenyewe wanakula bata na dada zetu.
Tufike hatua ya kujua na kuiga mfano wa mkuu wa UfilipinoMimi nilikuwa nawaza hivi
Kwakuwa rais wetu ni msema kweli na ana nia ya dhati ya kuondoa maovu mbalimbali nchini basi amuunge mkono makonda katika hili, ili hii vita iwe ya KITAIFA
Rais atoe tamko kila mwananchi mwenye jina la mtu anayeshukiwa kujihusisha na hii biashara alipeleke ikulu na rais mwenyewe awe anayapokea
Mwisho wa siku majina yote yaliyopelekwa yatangazwe hadharani na waende kuripoti kituo cha kati na watamkuta rais huko
Scuba sio muuzaji mkubwa mkuu ila waanzilishi wa hiyo biashara. yani kati ya wauzaji wa siku nyingi nae yumo.Makonda anatuletea utoto wafadhiri wake ndio wafanyabiaahara wakubwa hao wana uwezo wa kuingiza kilo 50 ya pure cocaineMuuzaji mkubwa tanzania ambaye ni shkuba Yuko jela lindi!ila bado nje Kuna Mtandao wake
Unaendelea....
List aliyoitaja makonda Kuna wauzaji na Kuna wasanii wauzaji MADAWA na wasanii watumiaji madawa...
Kikubwa acha tuone mwisho itakuwaje maana Kuna wengine aliyowataja wapo kitambo kwenye game walishakamatwa na kuachiwa..
Kuhusu polisi ambao wanashirikiana na wauzaji kwa kutoa taarifa kwa wauzaji na kuchukua pesa hao maskari kitambo tu walikuwa wanakula hela na wauzaji wadogo na wa kati....
Ova
Basi mie nikadhani umeitaja orodha ya hao watuMiaka ya 80 mwishoni na 90 mkoa wa Mbeya kulikuwa na Jambazi mmoja maarufu sana alikuwa anafahamika kwa jina la Jombi. Alikuwa maarufu na tajiri. Yeye alikuwa na mtandao mkubwa sana na inasemekana Polisi wengi wakubwa walikuwa kwnye payroll yake kwa njia moja au nyingine pamoja na wanasiasa. Huyu bwana alikuwa akiiba magari TZ anaenda kuuza SA au Zambia na akiiba huko analeta TZ.
Pia alikuwa akifanya Ujambazi mwingine wa humu humu ndani kwa umakini mkubwa sana. Ilikuwa ikitokea anatakiwa akamatwe kuhojiwa anapigiwa simu aende kituoni au anaambiwa kesho kuna vijana wanakuja. So anajiandaa anavyojua. Siku mbili tatu mnamwona mtaani anadunda kama kawaida. Ni Mkapa alikuja kumkamata huyu mweshimiwa Jambazi.
Nimerudia habari hiyo kwa kufananisha na kile kinachoendelea hapa nchini. Kusema wauza madawa wa kulevya wakubwa hawafahamiki ni uongo mkubwa na utatupeleka motoni. Wanafahamika sana wengine ni watoto wa viongozi na viongoz wenyewe, wengine ni wabunge na makada wa vyama vyetu, wengine ni wafadhili wakubwa wa vyama na timu zetu, wafadhili wa wanamuziki, wasanii na wenye kufadhili hata maisha ya watu flan flan hapa mjini.
Wanafahamika sana. Nenda Kinondoni kuna himaya za watu hawa. Nenda Mbezi, nenda kaangalie watoto wanaosoma chuo cha diplomasia wanavyoharibika kwa madawa haya.
Kama Makonda ameamua kupambana na madawa ya kulevya atoe namba yake ya simu apewe majina. Lakini hilo si issue sana anaweza enda omba kwa ndugu Kikwete, yeye anayo list ambayo alisema hadi viongozi wa dini wapo na watu wengine wengine aliosema ni wazito. Yaani walikuwa wanaogopwa kuliko serikali. Hayo majina sidhan kama Kikwete atamnyima.
Lakini ikiwa Kikwete hatotaka kumpa basi sisi vijana tunaweza msaidia akipewa hayo majina hatusemi aje atangaze. Hapana tunaomba afanye uchunguzi ili tusije nasi wengine tukawa tumewasingizia. Awakabidhi polisi kitengo husika, polisi waadilifu wachunguze na kuwakamata wahusika.
Wanafahamika wala si siri. Wengine bado ni wabunge na wengine wanajihusisha na music, usanii au ufadhili wa vyama vyetu.
Makonda tupatie namba yako ndugu, tukusaidie kukutajia wahusika wakuu ukiacha hawa uliowataka waje kukuona ofisini. Sisemi waachwe ila nashangaa kwa nini ulipendelea waje kukona wewe ofisini? Ili iweje? Si ungesema wakamatwe? Wapelekwe polisi? Na halafu mahakamani?
Watanzania tusimung'unye maneno. Tusipepese macho, tusing'ate kucha na kutizama chini.
Tuseme Makonda haya hapa majina ya wauza madawa ya kulevya ili Mungu alinusuru Taifa hili na madhambi yanayolizunguka.