Tuseme: Makonda, Haya hapa Majina ya Wauzaji Madawa ya Kulevya wakubwa

Akiungwa mkono anaweza hii vita ni kubwa sana sio kama tunavyofikiri akamuulize Duterte ugumu wake kikubwa aache usanii wa kutajataja majina ya wasanii wanotumia huku dealers anawakwepa huwezi kukomesha biashara hii kwa kumkamata Chid Benz au wema sepetu....
 
Makonda ni mtu mdogo sana kupigana hii vita. Amina yupo wapi? Aliwataja wauza unga akamsahau mumewe adhabu yao wote tunajuwa. Dunian kote hii ni vita nzito na kama hamjuw tz ni pepo yao sasa huyu bwana makonda hata maziwa ya mama hayajaisha harufu mwilin mwake aweze? Huu utakuwa muujiza mbaya zaid ameanza vibaya. Hajafuwata logistic za kimafia what do we expect? Nduguzanguni hapa ndipo vijana tunaonekana hamna kitu.
Muda utatujuza ila end ya makonda sio nzuri why anacheza mpira mwanzo wa goli nakumaliza mwisho wa Goli what u expct
Uwenda ametoa siri ambayo hakupaswa toa na huo ndio mwisho wake.


Acha maneno tumpe hongera kijana mwenzetu amefanya kitu cha kuonekana na kusikika, ameanza na hao ambao ndio wanaoyaeneza mitaani kwa maana ya kukata mikono hlf atarudi tu kukata miguu inayoleta, cha msingi AUNGWE MKONO na sisi wananchi na hata president wetu kudeclare alichokianzisha kijana kiongozi shupavu.
 
Habari wana JF!


Toka Jana mchana baada ya RC Makonda ku release majina ya watu waliokamatwa na wanaoshutumiwa kwa uuzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya kumezuka mjadala mkubwa sana kwenye media na social media kuna wanaompongeza na wanaombeza , lengo la uzi huu ni kujikita zaidi kwa wanaombeza Makonda! Nimesoma kwenye social media kwa upande wanaombeza wamejikita katika mambo makuu;

1.Wanasema mbona kawataja dagaa na mapapa amewaacha.
2.Wengine wanasema anajaribu kuzuia mijadala inayoendelea ya matokea ya kidato cha NNE baada ya shule za serikali kufanya vibaya na anataka kucreate attention kwenye suala lake. N.k

Binafsi ningependa kumpongeza RC Makonda kwa hatua hii hatupaswi kumbeza zaidi anapaswa kuungwa mkono. Tunaoishia kuandika kwenye social media majina ya wauza madawa ya kulevya tunayo bado haisaidii zaidi kama kweli tunayo nia RC Makonda kila MTU mkazi wa DSM ofisi yake anaijua na sidhani kama ni kuna vizuizi vya kwenda kuonana, nenda mwambie mh. Majina mengine haya hapa! Hao tutakuwa tumemsaidia sana na unaweza ukakaa na kuandika negative kama majina uliyomtajia hatayashughulikia.

Tusifanye kila jambo liwe la kisiasa, wengine wameenda mbali huko nyumba 2015 kwenye uchaguzi wakimcheka wema sana maana alikuwa mstari Wa mbele kwenye kampeni za CCM. Wenye wanaodhani Makonda alichokifanya ni kidogo basi naomba twende mbele zaidi tuwe naye kwahili jambo ili baadaye akishindwa twende kwenye media na social media tumbeze.

Mwisho vita hii aliyoianzisha Makonda si ndogo kama tufikiriavyo, hawa watu ni kifupi ukiwatikisa umetikisa nchi, umetikisa uchumi wa nchi.
 
Screenshot_2017-02-03-14-03-12.png
 
Kuna mtu anaitwa Tiko mtoto wa magomeni bishow moja hivi amefuga rasta...Sasa huyo ndio dealer mkubwa apo bongo..alafu yeye pia kang'oka tokea last year December nafikiri yupo ndani
 
Na kuna chafu yenyewe ipo gerezani sasa hivi kama miezi 6 hivi..anaitwa shkuba..!!huyo ndio big pin Africa nzimaaa...alikuwa wanted mpka south Africa
 
Kuna watu wadis makonda kutaja watumiaji...mbona kuna namba chafu wapo maisha mabovu...sema huu mtandao ni mkubwa. .
 
Kuna mtu anaitwa Tiko mtoto wa magomeni bishow moja hivi amefuga rasta...Sasa huyo ndio dealer mkubwa apo bongo..alafu yeye pia kang'oka tokea last year December nafikiri yupo ndani
Yupo ndan kitambo
 
Miaka ya 80 mwishoni na 90 mkoa wa Mbeya kulikuwa na Jambazi mmoja maarufu sana alikuwa anafahamika kwa jina la Jombi. Alikuwa maarufu na tajiri. Yeye alikuwa na mtandao mkubwa sana na inasemekana Polisi wengi wakubwa walikuwa kwnye payroll yake kwa njia moja au nyingine pamoja na wanasiasa. Huyu bwana alikuwa akiiba magari TZ anaenda kuuza SA au Zambia na akiiba huko analeta TZ.

Pia alikuwa akifanya Ujambazi mwingine wa humu humu ndani kwa umakini mkubwa sana. Ilikuwa ikitokea anatakiwa akamatwe kuhojiwa anapigiwa simu aende kituoni au anaambiwa kesho kuna vijana wanakuja. So anajiandaa anavyojua. Siku mbili tatu mnamwona mtaani anadunda kama kawaida. Ni Mkapa alikuja kumkamata huyu mweshimiwa Jambazi.

Nimerudia habari hiyo kwa kufananisha na kile kinachoendelea hapa nchini. Kusema wauza madawa wa kulevya wakubwa hawafahamiki ni uongo mkubwa na utatupeleka motoni. Wanafahamika sana wengine ni watoto wa viongozi na viongoz wenyewe, wengine ni wabunge na makada wa vyama vyetu, wengine ni wafadhili wakubwa wa vyama na timu zetu, wafadhili wa wanamuziki, wasanii na wenye kufadhili hata maisha ya watu flan flan hapa mjini.

Wanafahamika sana. Nenda Kinondoni kuna himaya za watu hawa. Nenda Mbezi, nenda kaangalie watoto wanaosoma chuo cha diplomasia wanavyoharibika kwa madawa haya.

Kama Makonda ameamua kupambana na madawa ya kulevya atoe namba yake ya simu apewe majina. Lakini hilo si issue sana anaweza enda omba kwa ndugu Kikwete, yeye anayo list ambayo alisema hadi viongozi wa dini wapo na watu wengine wengine aliosema ni wazito. Yaani walikuwa wanaogopwa kuliko serikali. Hayo majina sidhan kama Kikwete atamnyima.

Lakini ikiwa Kikwete hatotaka kumpa basi sisi vijana tunaweza msaidia akipewa hayo majina hatusemi aje atangaze. Hapana tunaomba afanye uchunguzi ili tusije nasi wengine tukawa tumewasingizia. Awakabidhi polisi kitengo husika, polisi waadilifu wachunguze na kuwakamata wahusika.

Wanafahamika wala si siri. Wengine bado ni wabunge na wengine wanajihusisha na music, usanii au ufadhili wa vyama vyetu.

Makonda tupatie namba yako ndugu, tukusaidie kukutajia wahusika wakuu ukiacha hawa uliowataka waje kukuona ofisini. Sisemi waachwe ila nashangaa kwa nini ulipendelea waje kukona wewe ofisini? Ili iweje? Si ungesema wakamatwe? Wapelekwe polisi? Na halafu mahakamani?

Watanzania tusimung'unye maneno. Tusipepese macho, tusing'ate kucha na kutizama chini.

Tuseme Makonda haya hapa majina ya wauza madawa ya kulevya ili Mungu alinusuru Taifa hili na madhambi yanayolizunguka.
Ila Jombi mwisho wake haukuwa mzuri pia kaka. Kapunga Rice Farm alishambuliwa vibaya sana na askari waliochoka na shughuli zake.
 
Back
Top Bottom