Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

kazi nzuri wakuu......Mimi naomba kama anaweza kujua majina ya hawa vijana walioshika hilo bakuli ambalo mwalimu anachanganya mchanga huo na bado wako hai?mbona sijawahi kusikia wakikumbukwa.......pia hao akina mama kushoto ni akina nani na huyo mzee kushoto anaepiga makofi......

attachment.php


Huyo mzee anaepiga makofi kushoto ni chifu petro itosi marealle (marehemu). Alikuwa ana represent machifu wa tanzania.
 
FMES,

..Hussein Tindwa hakuwa mshambuliaji.

..nadhani Hussein Tindwa ndiye mrithi wa Omar Chogo.

..halafu Mohamed Bakari "Tall" alikuja kumrithi Tindwa[r.i.p].

..Baada ya Omar Mahadhi alifuata Athumani Mambosasa.

..sina uhakika kama Moses Mkandawile alicheza kabla au baada ya Iddi Pazi.

..nina uhakika Iddi Pazi hakucheza na Mohamed Kajole. Pazi amecheza miaka ya kina Raphael Paul, Mussa Kiwelu, na Lila Shomari.

..Halafu Willy Mwaijibe,Abdalah Mwinyimkuu, na Ezekiel Greyson "juju man," walicheza miaka ipi?

IDDY PAZI NDIYE GOLKIPA ALIYEMRITHI OMAR MAHADHI BIN JABIRI WAKATI MAMBO SASA NDIYE ALIYEIPELEKA SIMBA NUSU FAINALI,TINDWA NI KWELI ALIMRITHI CHOGO NA BAADA KUFA KWA TINDWA NDIPO MOHAMED BAKARY TALL ALIPORITHI MIKOBA AKIWA NA BRUCE LEE DAUD SALUM,BAADA YA PAZI KUTIMKIA ELHILAL SUDAN 82-3 NDIPO MOSSES MKANDAWILE ALIPOBEBA JUKUMU HILO MPAKA 87 PALE ILIPOZALIWA SIMBA YA JABIR SIKAMKONO NA WACHEZAJI WAKE AKINA JUMA SHAMTE WAKATI HUO NDIO YULE TAJIRI RUWEIHY NA MZEE SSB WALIPOITOSA SIMBA BAADA YA GOLBACHEV JIMMY DAVID NGONYA KUINGIA MADARAKANI NA AKINA EMANUEL MAKAIDI (HUYU MPINZANI MABAGA SIKU HIZI), KAMA MTAKUMBUKA 1987-1989 SIMBA WALIKWAMA SANA HUSUSAN 1988 NA 89 MAANA HATA JEZI ILIKUWA MOJA TU ILE SALAMA TRAVEL, NI KIPINDI KIBAYA SANA KWA SSC AMBACHO NAAMINI BADO KINATUTESA SISI MANAZI WAKE INGAWAJE BY THEN NDIO TULIKUWA WADOGO ILA ILIKUWA NI HUZUNI SANA KILA UKISIKIA MADUNDO MTAMBO NA RELI YAKE BASI TUNASALI TU INGAWAJE DUA ZETU ZILIISHIA MAJONZI, NAMKUMBUKA MPUMBAVU (ninakusifu kwa jinsi ulivyotunyima raha ktk gazeti lako la mfanyakazi)MMOJA JAMES NHENDE ALIWAHI ANDIKA ETI UKITAKA KUIONA SIMBA KTK MSIMAMO WA LIGI BASI UNALAZIMIKA KUGEUZA GAZETI MIGUU JUU KICHWA CHINI MAANA ALWAYS TULIKUWA KTK DANGER ZONE, 87-88-89 SIMBA ILIKUWA NWAZALENDO HAWA-ASTON PARDON, MOHAMED NYAUBA, ADAM SELEMAN, IDDY SELEMAN, JUMA LIMONGA, EDWARD CHUMILA,JUMA SHAMTE,TWAHA HAMIDU,JOHN MAKELELE NA MTAALAAM DAN MUHOJA WENGINE WAKUU ENDELEENI ILA BAADA YA KUNG'ARA KWA MKANDAWILE LICHA YA KUFUNGWAFUNGWA KWAKE NA YANGA KILA MARA 90s SIMBA TULIMPATA MRUNDI MACKENZIE RAMADHANI ALIYENGARA SANA MSIMU HUO HUKU AKITUHUMIWA HAKUWAHI KUBADILI JEZI ALIYOIVAA MPAKA SIMBA INAUBEBA UBINGWA WA BARA, KUMBUKENI PIA BAADA YA TALL-DAUD SALUMU NA KIDOGO SHABAN MUSSA SIMBA WALIBAHATIKA KUPATA KIJANA TOKA DOM- TWALIB HILARY AMBAYE ALILETA TAFRAN 84-5 KTK MECHI YA SIMBA NA YANGA, NI SIMBA PIA ILIYOBAHATIKA KUMPATA KIJANA WA KINDAMBA OCD DEO NJOHOLE(mungu mlaani Abbasy Gulamali kwa kumharibia maisha kijana huyu kwa kumlaghai), Mmenikumbusha mbali wakuu maana hayo muyasemayo ni utoto wangu primary hasa, mzee akiwa na ile 277 ya mbao wacha kabisa, It was more than fantastic,comrades,Thank you very much
 
1. Kama ninakumbuka vizuri ni kwamba Yanga ilichukua wachezaji wawili toka Mlimani, nao ni Leodgar Tenga, na Edward Hizza, wote walikuwa benchi kwa sababu Tenga, alikuwa akimsaidia Hassan Gobbos, Hizza hakuweza hata kucheza mechi kubwa,

However, Yanga wakiwa wanajitayarisha kwa safari ya Brazil, Tenga na Hizza, waliitwa kwenye timu ya Mlimani, ili kuiwakilisha kwenye michezo ya Vyuo Vikuu iliyokuwa inafanyika Mexico, hivyo wote wawili wakashindwa kwenda Brazil na Yanga,

2. kwa sababu ninakumbuka vizuri sana kwamba baada tu ya mechi ya Nyamagana, ambapo Sunday na Sembuli waliifunga Simba, timu hizi ziilirudiana tena kwenye Uwanja Wa Tartan wa Zanzibar, kwenye finali ya Kombe la Ubingwa wa East and Central Afrika, ambako kwa mara nyingine tena Yanga waliishinda Simba kwa magoli mawili kwa moja, yaliyofungwa na wale wale Sunday Manara na Sembuli na this time Tenga alikuwemo ndani ya ile mechi upande wa Yanga, mechi mabayo kwa mara ya kwanza katika historia ya michezo bongo ilichezwa usiku.

Kipindi kati ya cha mechi ya Nyamagana na Zanzibar, kilikuwa ni kifupi sana kwamba Tenga ndio alijiunga na kuweza kucheza mechi kubwa namna ile, lakini I colud be wrong pia.

3. Wachezaji waliojiunga na Yanga kutokea Morogoro, baada ya kombe la Taifa, kwenye ngwe ya kwanza alikuwa ni Sembuli peke yake,

Ngwe iliyofuatia walikuwa ni kipa Patric Nyaga, Juma shaabani, Jella Mtagwa, na Juma Matokeo, Muhaji Mukhi, naamini alitokea timu ya mkoa wa Kigoma kama Makumbi Juma.

Ngwe ya mwisho ya wachezaji wa Morogoro kuingia Yanga, ilimalizwa na Ahmed Jongo na Omar Hussein. Otherwise, wakuu heshima mbele kwa historia na marekebisho, nia na madhumuni ni kuelimishana.



...Wakuu, Heshima zenu. Haya, tuendelee kukumbushana na kurekebisha panapofaa kurekebisha. kumbukumbu zangu mimi zinasimama pale pa kwamba

Gibson Sembuli alijiunga na Yanga baada ya kombe la Taifa la mwaka 1973 ndio akasajiliwa na Yanga mwishoni mwa mwaka huo kwa maana hiyo alikuwa kwenye kikosi cha Yanga kilichokuwa kikitafuta Ubingwa mwaka 1974 na kuutwaa kule Nyamagana Julai/August mwaka huo kwa kuiangusha Simba.

Mwezi uliofuata, yaani September/October kombe la Taifa likachezwa na baada tu ya kumalizika karibuni NUSU ya kikosi chote cha timu ya Mkoa wa Morogoro kikahamia Yanga ndio hao akina Patrick Nyaga, Juma Shabaan, Juma Matokeo, Jellah Mtagwa. Huyu Muhaji Mohamed Mukhi sina hakika kama ni mzaliwa wa Kigoma lakini alijiunga na Yanga akitokea Morogoro.

Wote hao wakajiunga na kikosi cha Yanga kilichokuwa kambini chini ya Tambwe Leya kikijiandaa na mashindano ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki yaliyofanyika miezi mitatu baadaye, yaani January 1975 ambapo kama ulivyosema Yanga waliitungua tena Simba kwa mabao yale yale na wafungaji walewale 2-1, Sunday Manara na Gibson Sembuli.

Ni katika michuano hiyo ambapo wakongwe wa Yanga akina kipa Elias Michael na Muhidin, mabeki Selemani Said sanga, Hassan Gobbos walianza kukosa namba na kuwaachia 'vijana' akina Jellah Mtagwa, Juma Matokeo, Patrick Nyagah,leodgaard Tenga ambao mashindano hayo 'yaliwatoa' sana!

Ni baada ya kipigo hiki ndio purukushani zikaanza kwanza kwa upande wa Simba zilizoishia kwa kuzawaliwa kwa timu ya NYOTA NYEKUNDU/RED STAR mwezi May/June 1975 iliyoanza na akina Haidar Abeid'Muchacho'. mdogo wake Khalid Abeid, Kessy Manangu na wengineo.

Yanga nao baada ya kipigo cha Enugu Rangers mambo yakaanza kuharibika na mwishoni mwa mwaka huo kukazuka makundi ya Raizon na Kandambili yaliyosababisha mwaka 1976 wachezaji wote wa kikosi cha kwanza cha Yanga
kutimuliwa Yanga na kujinga na kuchezea NYOTA AFRIKA ya Morogoro na wakawa wakiishi Dar na kwenda kuichezea siku za mechi mjini Morogoro!

Hata hivyo, walifaulu kuibeba timu hiyo hadi ikafika fainali ya klabu bingwa ya Tanzania 1976 ambapo walikutana na Simba kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha ambapo Simba walitwaa ubingwa kwa kuilaza Nyota (Raizon) bao 1-0.

Baada ya kutoka Arusha wachezaji wote mastaa wa Yanga mwezi September/Oltober 1976 wakajiunga na timu ndogo ya Zamalek ya Kariakoo ambayo ikabadilishwa jina na kuwa PAN AFRICA!

...Tunaendelea...
 
Mwalimu,

Mambosasa na Mahadhi walipokezana hata baada ya Mahadhi kuanza kuachia ngazi.

Mkandawire na Pazi walipokezana pamoja na Nemes (Khadija Kopa).

Yanga nayokumbuka ni ile ya Bernard Madale, kisha akaja Dunia Adonis, kisha kuja nafikiri Hamisi Kinye. Kama sikosei, hata Steven Nemes alidakia Yanga kwa muda mfupi na alipomrithi Pazi, ndipo tulipoanza kumuita Khadija Kopa.

Pondamali alikuja mrithi Kinye, kisha akaja yule kipa kutoka Pamba, i am not sure kama alikuwa ni Lubigisa, but a cycle ya makipa wazuri walikuja Yanga huku Mwameja akishikilia usukani Simba kwa muda (possibly the longest Simba GK)

Je mwamkumbuka Paul Ssali wa KCC na Uganda Cranes?


Rev. Kishoka, hapo pa Hamis Kinye umemsahau kipa aliyepata kuwa miongoni mwa makipa wazuri Yanga iliyowahi kuwa nao ambaye alikuwa akishindana na Hamisi Kinye...Joseph Fungo!!
 
Mkuu uko sawa-

1. Willy Mwaijibe - alikuwepo Mwanza, lakini akielekea ukingoni kwa sababu hata Chitete alikuwepo Nyamgana lakini ndio waliokuwa wakielkea mwishoni mwa career zao.

Ni kweli Idd Pazi "Father" Alikuwa hajaingia hapa ananikumbusha mbali sana huyu mkulu, ambaye niliwahi kucheza naye mpira utotoni, na mpaka leo ni jirani yangu kule Kinyerezi, maana huyu alikuwa kile kitu kinaitwa multi-talented, originally alikuwa mshambuliaji akitumia mguu wa kushoto nilicheza naye timu moja ya mabaharia Jangwani ya Muungano Sports Club,

Baadaye nilicheza naye tena kwenye timu ya kiwanda cha nguo cha Sungura-Tex, ambako mara kwa mara tulikuwa tukipambana na Kurugenzi ya Kisarawe timu ya Ezekieli Greyson "Jujuman", kabla hajachukuliwa na Simba. Nilipoamua seriously ku-stick na ubaharia, Idd Pazi na wachezaji wengine niliocheza nao pale kama Hamzuruni, na Makobe, wao walienda Nyota ya Mtwara, baadaye Idd alichukuliwa na Simba, Hamzuruni alichukuliwa na Yanga, Makobe naye alikuja Ummangani kwenye Meli.

Sasa hivi Idd ambaye ninawasiliana naye mara kwa mara, yupo Thailand ambako ni mfanya biashara mkubwa sana. wadogo zake Idd yaani Omar na Muhidini, nao pia waliwahi kuchezea Simba na Yanga, lakini hawakuwa na talent kama ya kaka yao Idd, the guy was just phenominal ninakumbuka kuna wakati wa mechi zetu za utotoni timu za adui zilikuwa zikimkataa kabisa kushiriki kwa sababu akiwa mdogo sana tayari alikuwa akichukuliwa kucheza timu za watu wazima, kwa hiyo maadui walidai kuwa asiruhusiwe kushiriki, off course sasa it sound like a joke, lakini I wish ungewepo uone how serious hii ishu ilikuwa.

2. Abdallah Mwinyimkuu "Carlos" na Ezekiel Greyson "Jujuman", hawa walikuwemo katika miaka ya kati kati ya 70s, kwa sababu nakumbuka sana ile mechi ya Simba na AS Vita ya Zaire, pale Uwanja wa Taifa, hawa wawili walikuwemo na kwenye lists ya zamani aliyekuwemo siku ile alikuwa ni Kibadeni,

Maana hizi zilikuwa enzi za kina Daudi Salum "Bruce Lee", unakumbuka Simba walikuwa na huyu mchezaji aliyetokea Tabora?


...kabla ya kujiunga na Simba Ezekiel Greyson 'Jujuman' alijinga kwanza na Yanga mwishoni mwa mwaka 1975 akiwa miongoni mwa wachezaji wenye umri mdogo wa timu hiyo. Ni Yanga ndio waliompa jina la Jujuman wakifananisha uchezaji wake na upigaji gitaa la Rithim wa mzaire Vata Mombassa 'Jujuman' wa Orch Lipua Lipua iliyokuwa ikitamba miaka hiyo na mipigo ya kavasha. Alikuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichotunguliwa 6-0 na Mnyama akiwa na akina Yanga Bwanga, Benard Madale, Boniface Makomole,Selemani Jongo, Ayoub Shabaan, Mwinda Ramadhani na wengineo. mwishoni mwa mwaka huo 1977 ndio akajiunga na Simba.
 
Rev. Kishoka, hapo pa Hamis Kinye umemsahau kipa aliyepata kuwa miongoni mwa makipa wazuri Yanga iliyowahi kuwa nao ambaye alikuwa akishindana na Hamisi Kinye...Joseph Fungo!!

Mkuu mbona umemsahau Golikipa saafi sana wa Yanga, Isega Isindani kutoka Mbeya, au?
 
1.
IDDY PAZI NDIYE GOLKIPA ALIYEMRITHI OMAR MAHADHI BIN JABIRI WAKATI MAMBO SASA NDIYE ALIYEIPELEKA SIMBA NUSU FAINALI,

Sawa sawa mkuu, kwa hiyo ilikuwa hivi Athuman Mambosasa/Omar Mahadhi/Idd Pazi/Moses Mkandawile, au?.

2.
TINDWA NI KWELI ALIMRITHI CHOGO NA BAADA KUFA KWA TINDWA NDIPO MOHAMED BAKARY TALL ALIPORITHI MIKOBA AKIWA NA BRUCE LEE DAUD SALUM,

Katika hiki kipindi Simba iliwahi kuwa na mabeki kama Omar Choggo/Aloo Mwitu/Isihaka Mwitu/Athumani Juma/Mohamed Bakari "Tall"/Nico Njohole/Daudi Salum/Shabaan Baraza/Kajole Machela/Malota Soma/Raphael Paul, au?

3.
BAADA YA PAZI KUTIMKIA ELHILAL SUDAN 82-3 NDIPO MOSSES MKANDAWILE ALIPOBEBA JUKUMU HILO MPAKA 87

Sawa sawa 100%.

10.
NI SIMBA PIA ILIYOBAHATIKA KUMPATA KIJANA WA KINDAMBA OCD DEO NJOHOLE(mungu mlaani Abbasy Gulamali kwa kumharibia maisha kijana huyu kwa kumlaghai), Mmenikumbusha mbali wakuu maana hayo muyasemayo ni utoto wangu primary hasa, mzee akiwa na ile 277 ya mbao wacha kabisa, It was more than fantastic,comrades,Thank you very much

Mkuu inaoneakana ulikuwa hukosi mipirani, heshima mbele!
 
1.
kabla ya kujiunga na Simba Ezekiel Greyson 'Jujuman' alijinga kwanza na Yanga mwishoni mwa mwaka 1975 akiwa miongoni mwa wachezaji wenye umri mdogo wa timu hiyo. Ni Yanga ndio waliompa jina la Jujuman wakifananisha uchezaji wake na upigaji gitaa la Rithim wa mzaire Vata Mombassa 'Jujuman' wa Orch Lipua Lipua iliyokuwa ikitamba miaka hiyo na mipigo ya kavasha.

1. Ni kweli mkuu Ezekiel Greyson, akiwa Kurugenzi ya Kisarawe, alichaguliwa kuichezea timu ya mkoa wa Pwani kwenye Taifa Cup,ambako alinga'ara sana na kuchukuliwa na Yanga,

2. Huko nako alisifika sana na kuitwa "Jujuman", lakini akajitoa na kuingia Simba baada ya kushawishiwa sana na wa nyumbani mwenzake, aliyekuwa katibu wa Simba, Mkulu David Ngonya.

2.
Alikuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichotunguliwa 6-0 na Mnyama akiwa na akina Yanga Bwanga, Benard Madale, Boniface Makomole,Selemani Jongo, Ayoub Shabaan, Mwinda Ramadhani na wengineo. mwishoni mwa mwaka huo 1977 ndio akajiunga na Simba.

1. Baada ya mechi na Enugu Rangers, ilidaiwa kuwa Kitwana "Popat" Manara, alihongwa hela na Wa-Nigeria, ili asifunge kabisaa, na hasa alipokosa goli la wazi dakika za mwisho ndipo hiyo theory ikathibitishwa,

2. Yanga ikapata viongozi wapya kina Mohamed Misanga na David Mwambungu, ambao walidhani kuwa Le` Grande Mangara Tabu Mangara, aliyekuwa Supreme Leader wa Yanga then, ndiye aliyekuwa chanzo cha kina Kitwana kutokuwa na nidhamu, inasemekana hawa walikuwa wametumwa na baadhi ya viongozi wakuu wa serikali waliokuwa wapenzi wa Yanga, kwenda Yanga kurekebisha mambo hasa ya nidhamu,

3. Lakini wakagonga mwamba pale wachezaji, ambao wengi walikuwa Royal kwa Mangara, walipokataa kukubali sheria zao mpya, viongozi hao wakaamua kutumia ubabe kwa kuwapa conditions mpya wachezaji hao na wasipokubali watakuwa wamejifukuza wenyewe kwenye team, Wachezaji wakagoma na ndipo ikaundwa Pan Afrika (Panya), na wengine wakajiunga na timu ya kampuni ya Sigara, lakini huko mbele ya safari wote walijiunga na Pan.

a. Baadhi ya wachezaji hao walioenda Pan moja kwa moja, ni pamoja na Jella Mtagwa, Juma Matokeo, Juma Shaaban, Sunday Manara, Kitwana Manara, Patric Nyaga, Maulid Dilunga, Omar Kapera, James Mwalusako, na wengineo.

b. Walioenda Sigara ni pamoja na Juma Pondamali, Hussein Mkweche, Jafari Abdulrahaman, Rashid Idd "Chama", Adolf Rishad, Mohamed Yahaya "Tostao", Kassim Manara, na Gordian Mapango, chini ya kocha Saaban Marijan.

c. Lakini baadaye wote walijiunga na Pan, ingawa Sunday na Kassim, walienda Holland kucheza pro-ball, baadaye pia Nico Njohole naye aliondoka, huku kina Haidari Abeid, Bakari Tall, Jummane Masuminti, Ahmed Amasha, Isihaka Kaungu, Aluu Ally, nao wakazamia Uarabuni kucheza Pro.

d. Shaaban Katwila, George "Best" Kulagwa, Isaack Mwakatika, wakahamia Burundi kucheza Pro pia, kwenye timu ya soka ya rais wa huko Bagaza, kwa jina Intele au (International)
 
Kasi ya picha imepungua!!!

Heshima mbele mkuu,

Kama unazo picha zaidi sio vibaya ukiziweka hapa, otherwise tunakula picha na mazungumzo, sasa hivi tunajadili picha za mcezo wa mpira wa miguu zilizowekwa kwa mara ya mwisho na Mkulu Kichuguu,

Hii historia pia ni muhimu sana kwa taifa letu, kwa sababu ukiona jinsi tunavyocheksha sasa hivi na michezo, kuna wasi wasi kwa mwananchi asiyeelewa kudhani kuwa toka tupate uhuru, as a nation tumekuwa sindikiza wengine tu na kuvuta mkia,

Hapana mkuu, kuna wakati Tanzania tulikuwa tunasifikia sana kwa michezo, Filbert Bay alikuwa bingwa wa dunia meter 1,500 kwenye kukimbia, Suleman Nyambui, Juma ikangaa walikuwa mabingwa wa marathon wa dunia, Titus Simba alikuwa bingwa wa ngumi zisizo za kulipwa, Yanga na Simba walikuwa wakipokezana kombe la East and Central Afrika, Maulid Dilunga na Leodgar Tenga walichaguliwa na kushiriki kwenye timu ya mpira ya bara la Afrika kwenye mashindano ya mabara ya dunia kule Mexico, Emmanuel Mlundwa aliwahi kuwa bingwa wa dunia ngumi zisizo za kulipwa,

Kama una picha mkuu naomba uziweke hapa kama ni siasa au za michezo, hapa hakuna haraka wala hatuna mashidano, tunakula historia pole pole picha zipo zinakuja, tena bado kabisaa mkuu.

Ahsante na karibu sana mkuu!
 
1.

Katika hiki kipindi Simba iliwahi kuwa na mabeki kama Omar Choggo/Aloo Mwitu/Isihaka Mwitu/Athumani Juma/Mohamed Bakari "Tall"/Nico Njohole/Daudi Salum/Shabaan Baraza/Kajole Machela/Malota Soma/Raphael Paul, au?
Mkuu FMES na wote,

Shukurani sana kwa kutukumbusha historia hii ya kabumbu ... nasikitika kuwapa taarifa kwamba kwamba Nico Njohole ni mgonjwa sana .. yuko Uingereza. Nitawapa taarifa zaidi kadri hali yake itakavyokuwa inaendelea.
 
Kasi ya picha imepungua!!!

...Pata hizo za historia ya Zanzibar, beware, some are Graphic!;

...mapinduzi daima...
View attachment 2161
...Gwaride, majeshi ya serikali ya Shamte(?)
View attachment 2162
...watawala, Jumba hili sasa ni la Aga Khan Foundation, kazi za sanaa za mikono nk zinafanyika hapo...kwa mbaali kule nyuma ndio bandari ya Unguja, mpaka sasa.
View attachment 2163
...uhuru wa Zanzibar December! huh!?...
View attachment 2164

...YOU HAVE BEEN WARNED!!!, ...GRAPHIC PICTURES!!!...maiti zimetapakaa kila mahala...
View attachment 2165
 
Shukurani sana kwa kutukumbusha historia hii ya kabumbu ... nasikitika kuwapa taarifa kwamba kwamba Nico Njohole ni mgonjwa sana .. yuko Uingereza. Nitawapa taarifa zaidi kadri hali yake itakavyokuwa inaendelea.

Mkuu Kipunguni,

Heshima mbele, najua kwamba mara ya mwisho Nico Njohole, alienda UK kucheza kwa kulipwa, kwanza tunashuruku sana kwa habari hizi tunaomba habari zake zaidi mkuu kama utakavyozipta na tutamuombea kwa Mwenyezi Mungu amponyeshe haraka, lakini ahsante mkuu kwa kutuhabarisha.

Vipi mkuu anasumbuliwa na nini hasa?

Salute!
 
Mkuu Mchongoma,

Heshima mbele mkuu, eti huyu aliyekaa kulia kwa Karume kwenye picha na kina Thabit Kombo, naona kama ni Major General Mirisho Sarakikya,

Yaani kati kati ya Kombo na Karume, aliyevaa nguo za JWTZ, ukiangalia kwenye kofia yake utaona ngao ya JWTZ, au?

Otherwise, heshima kubwa sana mkuu na hizi picha za Zanzibar, yaani salaaam kutoka kila kona ya dunia wananchi wakitoa hesima zao kwa hii thread, na wachangiaji wote duh, saafi sana!
 
Mchongoma,

..FMES umepatia 100%. aliyekaa kati ya Karume na Thabit Kombo ni aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Maj.Gen.Sam Mirisho Sarakikya.

..huyo askari mwenye miwani ndiye nani? je aliyemuua Karume ni mmoja kati ya walinzi wake?

..maskini Okello, naona hata sanduku lake liko ndani ya karandinga!!

..baada ya Karume kuwa Raisi, Okello alipewa wadhifa gani?

NB:

..Mkapa alimpandisha cheo Sarakikya kuwa Generali[4 star] kamili.

..Sarakikya anaingia kwenye kundi moja na Twalipo[r.i.p],Musuguri,Kyaro,Kiwelu,Mboma,Waitara, na Mwamunyange.

..Tumainieli Kiwelu ndiye 4-star General pekee ambaye haja-serve kama Mkuu wa Majeshi.
 
..huyo askari mwenye miwani ndiye nani? je aliyemuua Karume ni mmoja kati ya walinzi wake?

Mkuu eti ni kweli nasikia kuwa aliyemuuwa Karume, alikuwa ni mmoja wa linzi wake ambaye Karume aliwahi kumuuwa baba yake, ni kweli au?
 
Back
Top Bottom